Tumain
JF-Expert Member
- Jun 28, 2009
- 3,154
- 70
- Thread starter
- #61
Hakuna ubishi kwamba udhaifu wa vyama vya upinzani dhidi ya CCM uko wazi. Lakini mimi ningependa pia tuangalie juhudi za dhahiri za baadhi ya wapinzani ambazo zimetoa changamoto si kwa CCM tu bali hata kwetu wa-Tanzania wengine. Sitaki kurudia kutaja yaliyo wazi hasa kuhusu matendo ya ufisadi uliolazimisha Serikali (hatimaye) kukiri na kudai kuchukua hatua.
HATA KAMA BADO JUHUDI HIZO ZIMESHINDWA KUBADILI STATUS QUO BASI SIDHANI KAMA NI VYEMA KUWABEZA HAO WACHACHE WALIOAMUA KUBEBA BANGO LA UPINZANI KWA DHATI (These people are not a monolithic block, by the way).
Kama ni udhaifu wa upinzani, mtazamo wangu mimi, tatizo ni sisi wa-Tanzania wote. Inakuwaje katikati ya utendaji mbovu ikiwa ni pamoja na unyanyasaji unaoendelezwa katika mfumo wa ukiritimba wa chama kimoja (virtually) tunashindwa kujitoa kuimarisha uongozi na kuunga mkono chama/vyama mbadala (upinzani imara) na tunaendelea kutoa zawadi ya ushindi wa kishindo kwa chama kimoja (CCM) kwa ama kukipigia kura nyingi au kutoshiriki uchaguzi kwa tusioridhika na status quo.
Kujaribu kulinganisha upinzani (siasa) na Kakobe (dini) ni kwenda nje ya mantiki.
Wahenga walisema ukishajua tatizo uko karibu kupata suluhisho, tukishafahamu kwamba hatuna viongozi katika upinzani wenye guts kama kakobe tumekaribia kupata solution..tukiendelea kuamini kwamba slaa ni godfather, wakati hawezi hata kuaminiwa na watu 10 kwenye department yake then hatutafika mahali
Wananchi hawana makosa yoyote wanamsubiri mwalimu anaweza kuwafundisha somo la siasa..hasa za upinzani..tutafute mandela na raila wetu..tusipumbazwe na watu waio na uwezo kama walioko sasa.