CCM45: Chama cha Mapinduzi chavisihi na kuviomba vyama vya siasa nchini kuendeleza umoja wa kitaifa, kuthamini na kukuza ustawi wa demokrasia iliyopo

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
May 27, 2020
1,450
799
photo_2022-02-05_04-55-32.jpg

====

Tarehe 5 Novemba, 1976 Mkutano wa pamoja wa Halmashauri Kuu za Taifa wa vyama vya TANU na ASP uliofanyika mjini Zanzibar, uliamua kuvivunja vyama hivyo ili kuunda chama kipya, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Vyama hivyo vya ukombozi vilivunjwa kwa heshima na taadhima kubwa, si kwa sababu vilishindwa kutimiza malengo yao, bali ni kwa nia ya kutaka kupata Chama kimoja kipya, kilicho imara na madhubuti kukabiliana na changamoto za kudumisha umoja wa taifa letu na kuleta maendeleo ya watu wa Tanzania.

Lengo kuu la Chama Cha Mapinduzi kilichozaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na ridhaa ya wanachama wa vyama vyetu viwili, kwa ajili hiyo, lilikuwa ni kuongoza Watanzania katika mapambano magumu ya kudumisha na kuimarisha uhuru wa nchi yetu na wa kila Mtanzania.

Kadhalika, CCM ilikuwa na jukumu kubwa la kulitoa Taifa na watu wake kutoka kwenye unyonge na umaskini na kuwa nyuma kimaendeleo. Bahati nzuri kwa muda wote wananchi wameonesha imani kubwa kwa Chama chetu kwa kuendelea kukichagua na kukipa heshima ya kuliongoza taifa letu.

Katika kipindi cha miaka 45 ya uhai wake, Chama cha Mapinduzi kimefanya mambo mengi mazuri. Kama ilivyokuwa kwa TANU na ASP, CCM imeendelea kuwaongoza Watanzania siyo tu katika kulinda uhuru wa nchi yao, bali pia katika harakati za kujiletea maendeleo yao. Mafanikio ya dhahiri yanaonekana, kupitia utekelezaji wa sera zake mbalimbali Chama cha Mapinduzi kimeendelea kujijengea uhalali wa kuongoza nchi yetu katika dunia ya sasa yenye mazingira yanayobadilika kila mara.

Moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ni kudumu na kuimarika kwa muungano wetu. Katika kipindi cha miaka 45 ilyopita Muungano wetu umezidi kuimarika kutokana na juhudi za makusudi za chama chetu za kuhakikisha kuwa muungano wetu unadumu milele.

Tumefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali ziliyojitokeza katika muungano wetu. Pia, tumeweza kufanya mambo kadhaa mapya ambayo yamefanya mambo yaende vizuri zaidi. Kitendo cha kuungana kwa TANU na ASP ndiyo kilichozaa chombo kilichokuwa na nguvu na uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na changamoto za Muungano wetu.

Changamoto zilizoshughulikiwa kwa wepesi na uharaka zaidi. Imepunguza manung’uniko na kuimarisha upendo na mshikamano baina ya watu na Serikali za nchi zetu. Leo muungano wetu ni mfano bora wa kuigwa siyo tu barani Afrika bali duniani kote. Watanzania tumeudhihirishia ulimwengu kuwa dhamira yetu ya kuungana ni imara na haitetereki.
Tutaendelea kuimarisha muungano wetu kwa faida ya nchi yetu na watu wetu. Tunafanya hivyo kwa kutambua faida kubwa na nyingi zinazotokana na muungano wetu ambazo kila mmoja wetu anazitambua.

Hivyo tunapokuwa tunayo kila sababu kutumia maadhimisho haya ya miaka 45 kuwaenzi waasisi wa muungano wetu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume na leo tunaendelea kuwahakikishia watanzania kuwa Muungano wetu uko katika mikono salama chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Chama chetu pia kimeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha umoja wa taifa letu. Kama ilivokuwa kwa vyama vya TANU na Afro Shiraz sera za CCM zimeendelea kulenga katika kuwaunganisha Watanzania na kujenga taifa moja imara lenye watu wamoja.

Leo watu wetu wanathamini umoja wa taifa letu zaidi pengine kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Licha ya tofauti za kisiasa, rangi, dini au kabila, kila mmoja wetu anajivunia na kuona faraja kuwa Mtanzania. Watanzania tumeutanguliza utaifa wetu mbele kabla ya tofauti zetu. Hii ndiyo inayotujengea amani, utulivu na mshikamano, mambo ambayo baadhi ya wenzetu Afrika na hata duniani ni bidhaa adimu sana.

Tumeweza kufanikiwa kubaki kuwa na taifa lenye umoja na utulivu, licha ya nchi yetu kupitia katika kipindi kigumu cha mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na kuingia katika mfumo wa vyama vingi na uchumi wa soko huria. Licha ya umoja wetu hata ukomavu wa kisiasa wa wananchi wetu nao pia umeuimarika sana.

Watanzania ni watu wasioyumba wala kubabaishwa. Ni watu makini, wachambuzi na watambuzi mahiri. Haya ni mafanikio makubwa na ni jambo la kujivunia. Lakini pia ni sifa kubwa kwa chama chetu ambacho ndicho kiliongoza mageuzi hayo hapa nchini. Wahenga wamesema usione vinaelea vimeundwa. CCM itaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kudumisha na kuendeleza umoja, amani na utulivu wa taifa letu. Ikiwa ni msingi mkuu wa kupatikana kwa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Katika kipindi cha miaka 45 ya uhai wa Chama Cha Mapinduzi, taifa letu limepiga hatua kubwa na kupata mafanikio mbalimbali katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Hali ya maisha ya Watanzania ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka 45 iliyopita.
Pamoja na kuwa bado nchi yetu ni maskini, lakini hali za watu wetu ni bora zaidi sasa kuliko ilivyokuwa mwaka 1977. Watu wengi wana kipato kikubwa, wanaishi katika nyumba bora zaidi, wanavaa vizuri na wanakula vizuri.

Utoaji wa huduma za elimu, huduma za afya, maji, barabara, umeme zimeimarika kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Haya yote yanatokana na sera sahihi na mipango mizuri ya Chama cha Mapinduzi.

Miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi imekuwa Mwalimu wa Demokrasia nchini na mataifa jirani, hakika Chini ya Utawala wa Chama Cha Mapinduzi Madarakani imeweza Kusimamia na kuongoza nchi kufanya uchaguzi, wananchi kutumia mamlaka na haki zao za kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka kwa Amani na Utulivu.

Hata hivyo uongozi wa CCM ndani ya miaka 45 tumefanikiwa kusimamia muundo wa sera zetu , mikakati na aina ya siasa inayohitajika katika nyakati tulizonanzo jambo ambalo limesaidia sana kulinda kwa kwa nguvu zote na kusimamia usalama wa taifa letu na watu wake ili kudumisha amani , umoja na kujivunia Uhuru wake .

Kazi kubwa ya utekelezaji wa sera kwa miaka yote ya utawala wa CCM madarakani ni kuhakikisha umoja wa kitaifa unadumu na kubaki, tukipinga siasa chafu za ukabila, rangi, dini au ukanda badala yake sera zake zimekuwa zilihimiza umoja na mshikamano hali ambayo imelifanya Taifa letu kuwa lenye utulivu, upendo na ushirikiano .

Katika nyakati zote kila mwananchi amekuwa mlinzi wa Taifa lake, askari wa mstari wa mbele anayehakikisha hatokei adui akayejivisha koti la kuwa kibaraka au wakala badala yake mapambano yameelezwa dhidi ya maadui Ujinga , Umasikini na Maradhi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka yote 45 kimekuwa kuwa mstari wa mbele kuendeleza na kudumisha ujirani mwema ili kujenga haiba ya maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi sambamba na kudumisha mahusiano mema na kuendeleza ushirikiano na vyama vingine rafiki na vya kidugu duniani ikiwemo kanda ya Afrika Mashariki na duniani kote.

Kuwa muda wote wa utawala CCM kimeendeleza mahusiano hayo na kushirikiana na vyama vingine ili kuhakikisha ujirani mwema unadumu, unaendelezwa na kuwaletea manufaa wananchi kwenye taifa letu na mataifa mengine. CCM katika kipindi cha miaka 45 kimekuwa chachu ya kuanzishwa kwa kamati ya nchi tano zilizo mstari wa mbele kusini mwa Afrika ambapo kwa wakati ule mataifa kadhaa yalikuwa bado hayajapata uhuru wake.

Kwa kushirikiana na vyama vingine vya ukombozi, CCM kimekuwa na mchango mkubwa kwa mataifa hayo kashamirisha juhudi za ukombozi hadi mataifa hayo yalipopata uhuru na kujitawala wenyewe. Dhana ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni kutanuka kwa wigo wa demokrasia shirikishi , ushindani wa sera kwa sera, ujenzi wa hoja kwa nguvu ya hoja.

Kwa kipindi chote cha miaka 45 CCM kimeendelea kuwa Chama sikivu na makini sana tena kwa nyakati zote. Kinapenda na kujali dhima ya majadiliano kwa njia za kiungwana kuliko kuandamwa na vitisho, kebehi, ubabe au kushuritishwa.
CCM kiko tayari wakati wote kupokea maoni, ushauri na rai hatimaye kufikia kwa maafikiano yanayoheshimu njia za kiungwana na kistaarabu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Wakati tukiadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi wito wetu kwa watanzania ni kuendeleza Umoja na Mshikamno wa taifa. Pia tunaendelea kuvisihi na kuviomba vyama vyote vya siasa nchini tuendeleze umoja wetu wa kitaifa, kuthamini na kukuza ustawi wa demokrasia iliopo nchini kwetu. Yapo mataifa mengi duniani hivi sasa yanatamani yafanane na Tanzania lakini kwa bahati mbaya kwao haiwezekani baada ya baadhi ya wanasiasa wao kuvuruga amani yao.

Mafanikio haya yamekuwa ndio msukumo mkubwa wa ujenzi wa imani kwa wananchi wa Taifa letu na Imani hiyo itaendelea kulindwa na kuheshimiwa kwa utiifu Mkubwa; Pamoja na baadhi ya mafanikio niliyoainisha bado kazi iliyo mbele yetu ni kubwa na nzito.

Kwa namna ya pekee Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyojipambanua tokea amechukua hatamu ya uongozi wa kuliongoza Taifa letu kwani ameonesha uwezo, juhudi na jinsi alivyodhamiria kukabiliana na changamoto mbali mbali za kiuchumi kijamii na kisiasa katika kusukuma mbele maendeleo endelevu ya nchi yetu.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi


SHAKA HAMDU SHAKA
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
04 FEBRUARI, 2022.
 
Hongereni sanaa kumbe mmezeeka ndio maanaaa?!
45 years,bado tunaongelea matundu ya choo,madarasa ya nyasi,elimu mbovu, barabara chini ya kiwango..
Mimi nadhani imefika muda wenu wa kupumzika,mmekula vya kutosha na mmezeeka sasaaa.
 
Kwa namna ya pekee Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyojipambanua tokea amechukua hatamu ya uongozi wa kuliongoza Taifa letu kwani ameonesha uwezo, juhudi na jinsi alivyodhamiria kukabiliana na changamoto mbali mbali za kiuchumi kijamii na kisiasa katika kusukuma mbele maendeleo endelevu ya nchi yetu.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wakati tukiadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi wito wetu kwa watanzania ni kuendeleza Umoja na Mshikamno wa taifa. Pia tunaendelea kuvisihi na kuviomba vyama vyote vya siasa nchini tuendeleze umoja wetu wa kitaifa, kuthamini na kukuza ustawi wa demokrasia iliopo nchini kwetu. Yapo mataifa mengi duniani hivi sasa yanatamani yafanane na Tanzania lakini kwa bahati mbaya kwao haiwezekani baada ya baadhi ya wanasiasa wao kuvuruga amani yao
 
Utoaji wa huduma za elimu, huduma za afya, maji, barabara, umeme zimeimarika kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Haya yote yanatokana na sera sahihi na mipango mizuri ya Chama cha Mapinduzi.
 
Ati ccm kiongozi wa demokrasia wakati anasurvive kt madaraka kwa wizi wa kura.

Mijizi kama nini tena jizi namba moja ni li dikteta JPM, Mungu alitie kabisa ktk moto wa milele uko lilipo liungue liwe kama mshikaki.

Nilimchukia sana yule mshenz na katili JPM.
pombe
 
Hili li makala lirefu hivi kuhusu CCM unategemea watu walisome?
 
Vyama vingine mnamengi ya kujifunza toka Chama Changu Cha Mapinduzi,

Tangu mwaka 1992 hadi sasa ni miaka 30,

Sio kweli kwamba vyama vyenu ni vichanga ila wengi wenu hammaanishi,

Asante sana Crde Shaka Hamdu Shaka hazina ya CCM-Tanzania
 
Bila CCM, Tanzania itayumba ukweli ndio huo tunataka hatutaki ,

Someni hiyo hotuba neno kwa neno,
Hotuba imejaa tambo na majisifu Tu. Ukichukua hotuba kama ilivyo, CCM haina kasoro, haina madhaifu.
Hivi kweli;
CCM inakuza demokrasia?
CCM inataka ushirikiano na Wapinzani wake wa kweli?
CCM inajali maisha ya maskini wa nchi hii?
 
Hotuba imejaa tambo na majisifu Tu. Ukichukua hotuba kama ilivyo, CCM haina kasoro, haina madhaifu.
Hivi kweli;
CCM inakuza demokrasia?
CCM inataka ushirikiano na Wapinzani wake wa kweli?
CCM inajali maisha ya maskini wa nchi hii?
Kuhusu Sisi kukuza demokrasia,

Kama hujui waliotaka vyama vingi walikuwa 20%

Lakini CCM ikawapa Ushindi,

CCM inataka ushirikiano na vyama vyote ndio maana Zanzibar tunaongoza na Wapinzani,

Kwa taarifa kila unachokiona hapa kwenye uso wa nchi ya Tanzania kimeletwa na CCM,

HOSPITALI ZOTE NI ZAO LA CCM,
SHULE ZOTE NI ZAO LA CCM
BARABARA ZOTE NI ZAO LA CCM
 
Back
Top Bottom