Stories of Change - 2023 Competition

jayboy

Member
May 26, 2023
19
15
Makala hii ni muhimu katika kuangazia mienendo mbalimbali ya nchi zinazofuata na kuongozwa na demokrasia na katiba guru Kati ya watawala na watawaliwa, pia makala hii inasisitiza upatikanaji wa demokrasia kupitia misingi iliyowekwa ya haki na usawa kwa wote, Uhuru wa vyombo vya habari ushirikibwa vyama vya siasa katika kampeni za uchaguzi,vile vile ushiriki wa vyama vya siasa katika kampeni za uchaguzi, lakini ushirikishwaji wa wananchi wote katika kutoa maoni, uamuzi na ushauri juu ya uendeshwaji wa shughuli mbalimbali za serikali.

Pia makala hii inaonesha namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za siasa katika kufikia misingi imara ya siasa safi nchini Tanzania Kama vile rushwa ,ubaguzi wa kisiasa ,ukosefu wa ukweli na uwazi ,kuteka nyara za taasisi za kisiasa,ukatili wa kijinsia au kisiasa Kama vile vurugu za uchaguzi na mauaji ya wanasiasa, kufungiwa kwa vyombo vya habari Kama vile magazeti ,redio na televisheni pindi wanapoonekana wanakosoa tabaka utawala,pia upendeleo wa kisiasa,rushwa na ufisadi,umasikini na migogoro ya ardhi.

Pia makala hii inaonesha namna ya kulinda nakudai masilahi ya pamoja kupitia ushawishi na ukombozi wa kifikra kutoka vyama vya upinzani katika kuwahamasisha wananchi kudai mabadiliko mbalimbali yanayotakiwa kufanyika ili kuboresha siasa safi ya Tanzania kwa kudai mabadiliko ya haraka yatakayoweza kukidhi mahitaji ya siasa safi nchini Tanzania kwa manufaa ya watu wote siyo kwa mtu mmoja mmoja Kupitia kuheshimu haki na usawa wa kila raia ili kulinda Uhuru wa watu katika jamii kupitia kutoa maoni mbalimbali takayo kubaliwa na kila mtu bila ya kuangaliwa yanatoka upande gani wa siasa au chama, pia ukweli na uwazi wa viongozi wa serikalini katika kutimiza majukumu yako ya kila siku na kuwachukulia hata za kisheri na nidhamu pindi wanapo kiuka haki za binadamu.

Siasa safi ni miongoni mwa mambo muhimu katika maendeleo ya Taifa lolote duniani.

Siasa safi inayozingatia uwajibikaji na utawala bora inajenga misingi imara ya kuleta maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii pia.

Nchini Tanzania ,kumekuwa na changamoto nyingi katika kuhakikisha siasa safi inasimamiwa kwa kuzingatia uwajibikaji na utawala bora, hivyo makala hii inalenga kuangazia misingi ya upatikanaji wa siasa safi nchini Tanzania na mabadiliko yanayotakiwa kufanyika katika uwajibikaji na utawala bora katika siasa safi ya Tanzania.

Misingi ya siasa safi nchini Tanzania Kama ifuatavyo:

Katiba:
Ni mkusanyiko wa sheria ,kanuni na taratibu zote zinazo elezea jinsi gani nchi itakavyoongozwa na jinsi ya mfumo wa utawala utakavyo Fanya kazi.

Katiba inaelezea haki na wajibu wa raia, madaraka ya serikali na kuongoza namna tume zinavyofanya kazi.

Katiba pia inaelezea namna mamlaka ya serikali za kitaifa na eneo zinavyofanya kubaliana na taasisi za kidini ,kijamii na kiuchumi.

Katiba ni msingi wa utawala bora na demokrasia, inahakikisha kuwa haki usawa na Uhuru wa raia inaheshimiwa na kulindwa dhidi ya dhuluma na ubaguzi, pia inatoa utaratibu wa kusuluhisha na kutatua matatizo kwa njia ya utulivu na amani.

Katiba inaweza kuwa na sehemu mbalimbali pamoja na kuelezea muundo wa serikali, uchaguzi, haki za binadamu, Uhuru wa vyombo vya habari na kutoa ufafanuzi kuhusu muundo wa mahakama na namna sheria zinavyotungwa na kutekelezwa.

Pia inaweza kuelezea mchakato wa kubadilisha katiba yenyewe ili kuweza kikidhi mahitaji ya wananchi.

Katiba ni muhimu katika kuhakikisha utawala bora, amani na utulivu katika nchi, hivyo basi inasaidia kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu na kusimamia Uhuru wa raia, vilevile inasimamia uwajibikaji wa serikali na kudhibiti mamlaka yake katika kuhakikisha wananchi wake wanapaza sauti na kupata haki ya kushiriki katika maamuzi ya serikali yako.Kwa ujumla, katiba ni msingi muhimu wa nchi yoyote inayoendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia na haki za binadamu, katiba ni chanzo cha mamlaka ya kisiasa nchini Tanzania inapoendelea kuimarishwa kukuza ustawi wa demokrasia safi na uongozi bora.

Vyama vya siasa:vyama hivi huundwa na watu wenye mawazo na maoni yanayofanana kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa,kijamii na kiuchumi.

Lengo la vyama vya siasa ni kuwakilisha masilahi ya wanachama wake na kufanya kampeni za kuwania viti vya uongozi katika serikali za kikanda, kitaifa na kimataifa.

Vyama vya kisiasa pia hutumika Kama jukwaa la kushiriki katika mijadala ya kisiasa, kutoa Sera na maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi na kutoa ushauri kwa serikali na taasisi nyingine za kisiasa.

Vyama vya siasa vinaweza kuwa na msimamo wa kushoto,wakati au wa kulia kulingana na Sera na maoni yao.

Kuna aina mbili za vyama vya siasa ambazo ni vyama vya siasa viwakilishi na vyama vya siasa visit how a kilos hi.

Vyama vya siasa viwakilishi ni vile vinavyo shiriki katika uchaguzi na vinapata viti katika serikali, kwa mfano vyama Kama Chama cha Mapinduzi (CCM),Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Civic United Front (CUF) lakini vyama visivyowakilishi ni vile ambavyo havishiriki katika uchaguzi na havina viti katika serikali kwa mfano Jumuiya ya Umma wa Kiislamu(JUKI).

Misingi na malengo ya vyama vya siasa inatofautiana kutoka chama hadi chama,lakini kwa ujumla kuna malengo ambayo yanashikiliwa na vyama vya vingi.Malengo haya ni pamoja na kuunda Sera na mipango ya serikali, kuhakikisha wananchi,kuhamasisha wananchi,kushiriki katika uchaguzi wa serikali,kusimamia demokrasia, Kuendeleza umoja na ushirikiano wa kitaifa ,kuimarisha utawala wa kisheria,kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kudumisha utamaduni wa kisiasa, amani na utulivu.

Uhuru wa vyombo vya habari:

vyombo vya habari nchini Tanzania vinahitajika kufanya kazi kwa Uhuru na uwajibikaji ili kupata taarifa kwa umma.Ni muhimu kwa vyombo vya habari kufanya kazi kwa uwazi na kuzingatia maadili ya kazi yao.

Vyombo vya habari Kama vile magazeti,redio na televisheni ni muhimu katika kuhakikisha demokrasia inaimarika Tanzania .Wanasiasa wanaotaka kupata kura za wananchi wanatumia Sana vyombo vya habari ili kufikisha ujumbe wao kwa umma,kwa hiyo ni muhimu kwa vyombo vya habari kuhakikisha habari wanazo chapisha au kursha za kweli ni za Kweli na zinazingatia maslahi ya umma, vilevile wanapaswa kuwa na uwezo wa kufikisha habari kwa umma kwa njia ya uwazi yenye uwazi ,Uhuru na haki.

Vyama vya siasa vinapaswa kuwa na uhuru wa kutoa taarifa na kufanya kazi zao bila kuingiliwa na serikali au viongozi wa kisiasa ilikuwafikishia wananchi taarifa sahihi na za kweli.

Utawala wa sheria:
Unakakikisha kuwa hakuna mtu ,hata mwanasiasa huko juu ya sheria na kwamba kila mtu anachukua jukumu lake katika kufuata sheria na utaratibu za kisheria.Katika utawala wa sheria,hakuna mtu yeyote anayebaguliwa kwa sababu ya hadhi yake au cheo chake,na kila mtu bila kujali nafasi yake katika jamii,anaweza kishitakiwa na kupewa adhabu akiwa amevunja sheria.

Kwa hiyo wanasiasa pia wanapaswa kufuata sheria na kuhakikisha kuwa wana wanawawakilisha wapiga kura zao kwa heshima na uadilifu kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye demokrasia, wanasiasa wanapata mamlaka kupitia mfumo wa kura za maoni za kidemokrasia,lakini hapaswi kutumia madaraka yao kupindukia au kufanya mambo yasiyokuwa na akili.

Haki na usawa:
Haki na usawa ni msingi muhimu wa siasa safi nchini Tanzania na katika nchi nyingine yoyote duniani, haki na usawa humwezesha kila mtu kupata fursa sawa za maendeleo na kutimiza ndoto zake bila ubaguzi au upendeleo kwa sababu ya jinsia, rangi, dini, kabila na hali ya kiuchumi. Ni muhimu kuwa na mfumo wa kidemokrasia ambao unaweka misingi ya haki na usawa kwa kila raia. Hii inaweza kuwakilishwa katika mfumo wa upigaji kura Uhuru nawa hiari, utawala wa sheria ambao unahakikisha raia yeyote anapata haki sawa mbele ya sheria na Uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani bila hofu ya kulipizwa kisasi.

Pia ni muhimu kwa wanasiasa kuwa na uwezo wa kuongoza kwa mtazamo wa mbali ,kutambua mahitaji ya wananchi katika siku zijazo.

Viongozi wanapaswa kuwa na uwezo wa kuna changamoto zinazowakabili watu wao na kuzitafutia suluhisho bila kujali masilahi yao binafsi au kisiasa.

Ukweli na uwazi:
Ukweli na uwazi ni vitu muhimu Sana katika siasa safi Tanzania, katika uchaguzi ni muhimu kwa vyama vya siasa na wagombea kutokana na Sera na ahadi zao, pia kujitokeza kweli katika kutatua shida mbalimbali za wananchi wao kupitia utekelezaji wa vitendo wa sera na ahadi mbalimbali walizo wasilisha kipindi cha kampeni, sambamba na uwajibikaji ni muhimu katika utendaji wa serkali. Kuweka taarifa zinazo zinazohusiana na matumizi ya fedha za umma na maamuzi sahihi kuhusu nchi Inawezesha wananchi kufuatilia maendeleo na kufanya maamuzi sahihi kuhusu utawala. Hali hii inasaidia kupunguza ufisadi, migogoro ya kisiasa na matumizi mabaya ya fedha za umma kwani serikali itakuwa inawajibu mkubwa Sana kwa watu wake, kwa hiyo ni muhimu sana kwa serikali kuwa wazi katika kufanya maamuzi, kutangaza Sera na kukabiliana na matatizo wanayokabiliana na watu wake.

Mbali na misingi ya siasa safi nchini Tanzania kuna faida mbalimbali zinazopatikana kutoka na kuwepo kwa siasa safi nchini , miongoni mwa faida hizo ni kumairika kwa demokrasia katika kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa njia ya Uhuru na haki, pia wanasiasa wanachaguliwa kwa misingi ya uwezo wao na Sera zao,kuleta amani na utulivu, kukuza uchumi kwa kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, hivyo kukuza uchumi na kutoa ajira kwa wananchi wa Tanzania kwa kuwa siasa safi inaondoa ukiritimba na ufisadi Inakuwa rahisi kwa watu wenye uwezobwa kiuchumi kuwekeza na kuchangia katika ukuaji wa kiuchumi, Pia kuleta usawa na uwajibikaji katika serikali, hii imesaidia Sana kuwepo kwa viongozi walio na utayari wa kushughulikia changamoto za wananchi na kusimamia vizuri rasilimali za nchi,vilevile uwajibikaji unaosiamamiwa na siasa safi unahamasisha uwazi,uwadilifu na utawala bora katika taasisi za serikali na kuimarisha demokrasia, haki za binadamu, amani na utulivu.
Katika kuimarisha siasa safi ya Tanzania kuna njia mbalimbali za kuongeza uwajibikaji na utawala bora katika masuala ya siasa hususani siasa ya Tanzania, miongoni mwa njia hizo Kama ifuatavyo:

Kuimarisha mfumo wa sheria na utawala wa sheria
;
Kuimarisha mfumo wa sheria na utawala wa sheria ni jambo muhimu Sana katika kuhakikisha uwajibikaji na utawala bora katika siasa. Hii inaweza kusaidia au kuharakisha kuwepo kwa Uhuru wa mahakama na sheria zilizopo zinaheshimiwa na kutekelezwa kwa usawa.

Kuweka mikakati ya kupambana na rushwa pamoja na ufisadi; uwajibikaji na utawala bora katika siasa safi inaweza kufanyika kwa kutekelezwa mikakati ya kupambana na rushwa pamoja na ufisadi, mikakati huu unaweza kufanikiwa kwa kuhakikisha kuwa kuna sheria zinazosimamia na kuadhibu vitendo vya rushwa Katika siasa na kuhakikisha kuwa taasisi husika zinapaswa Kuimarishwa na kuwezeshwa vyema ili kusimamia suala la rushwa.

Kuimarisha ukweli na uwazi
; siasa safi nchini inahitaji ukweli na uwazi katika kufichua matatizo mbalimbali ya sekta za serikali ili kuweza kutafutia suluhisho mbalimbali za matatizo hayo ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za kijamii Kama vile maji, umeme, elimu,cafya na miundombinu. Kwa kuweka wazi taarifa mbalimbali za wtumishi wa umma, taasisi au wizara kunasaidia kuboresha utendaji kazi mzuri hasa pale kiongozi anapotakiwa kutoa taarifa za kweli kuhusu taasisi yake, hivyo basi hana kutoa taarifa za uongo hali hii inachochoea hali ya uwajibikaji kwa viongozi katika jamii.

Kuongeza ushiriki wa wananchi; siasa safi inahitaji kushirikisha wananchi moja kwa moja katika maamuzi yanayohusu maendeleo ya nchi, hali hii inasaidia kutoa nafasi kwa wananchi katika kushiriki katika michakato ya kijamii na kisiasa Kama vile kupiga kura, kuandika maoni yao kuhusu Sera na mapendekezo ya Sera na kushiriki katika mikutano ya umma.

Kuhimiza kuwepo kwa katiba guru;katiba Uhuru ni katiba ambayo imeandaliwa na kupitishwa kwa kuzingatia mamlaka na Uhuru wa taasisi za kisheria na zisizo za kisheria, bila kuingiliwa na mtu au kikundi chochote cha kisiasa au kifedha.Katiba Uhuru inaruhusu wananchi kumiliki na kusimamia serikali yao kwa njia ya kidemokrasia na inaweza kubadilishwa kwa njia ya amani na sheria, kwa kuzingatia matakwa ya wananchi na katiba yenyewe, katiba huru ni chombo muhimu cha kuongoza na kuendesha serikali kwa lengo la kuimarisha demokrasia ,haki za binadamu na utawala bora na uwajibikaji.

Kuulind uhuru wa mahakama
; uwajibikaji na utawala bora inasaidia Sana katika kulinda misingi ya siasa safi Tanzania kwa sababu uhuru wa mahakama ni kanuni ambyo inalinda na kuhakikisha kuwa kuwa mamlaka ya mahakama inafanyakazi yake bila kuingiliwa na mtu yeyote au kitu chochote .Uhuru wa mahakama ni sehemu ya misingi ya utawala wa sheria na hupatikana kwa njia ya kujitolea kwa mahakama kufanya kazi yake kwa uhuru bila shininikizo kutoka kwab serikali, chama cha siasa, watawala au vyombo vya habari.

Hivyo basi hata ya serikali katika kulinda uhuru wa mahakama nchini imesaidia Sana kuwepo kwa misingi mizuri ya sheria nchini dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki na sawa na hivyo kufikia hata nzuri ya uwajibikaji na utawala bora nchini mbapo ni matokea ya misingi ya siasa safi nchini Tanzania.

Kuunda tume uhuru ya uchaguzi; pia kunawezab kuongeza uwajibikaji na utawala bora kupitia kuunda tume uhuru ya uchaguzi, Tume huru ya uchaguzi (THU)ni chombo maalumu ambacho kimeundwa na kukusudiwa kuwa huru,ni chombo ambacho haki na upande wala mtu binafsi ambaye anaweza kuathiri utendaji wake .Tume huru ya uchaguzi ni chombo kinachosimamia na kuratibu uchaguzi wa haki na huru kwa kuwa inauwezo wa kufanya kazi bila kuingiliwa na mtu yeyote, iwe serikali au chama chochote cha siasa.

Tume huru ya uchaguzi inachangia kuwepo kwa misingi bora ya uwajibikaji na utawala bora amabayo husaidia sana katika kuimarisha siasa safi ya Tanzania.

Kuchochea mchakato wa katiba mpya; pia mbinu nyingine ya kuongeza uwajibikaji na utawala bora katika siasa za Tanzania ni kupitia kutoa mapendekezo ya kudai mabadiliko mapya ya katiba ambayo itakidhi mahitaji ya wanajamii.

Mchakato wa katiba mpya ni juhudi za kuanda katiba mpya kwa kufanyiwa mageuzi katiba iliyopo ya nchi, katiba ya nchi ni waraka muhimu wa kisheria ambao kuelezea mamlaka na majukumu ya serikali, wananchi na makundi mbalimbali ya kijamii.

Kuunda katiba mpya ni mchakato wa kidemokrasia ambao huangalia upya katiba iliyopo na kutoa mapendekezo ya mageuzi na mabadiliko, mchakato huu inahitaji ushiriki wa wananchi, viongozi ,wadau wengine katika kujadili na kutoa maoni yao kuhusu hati ya katiba iliyopo na mabadiliko yanayotakiwa.

Hata hivyo ili nchi iweze Kuendeleza inahitaji vitu vikuu vinne ;siasa safi,watu,uongozi bora na ardhi,katika hali halisi nchi nyingi duniani zinashindwa kuendelea kutokana na kuwa na sifa mbaya ambazo hazifuati misingi ya kidemokrasia katika masuala ya utawala bora na uwajibikaji, hivyo basi hakuna budi nchi ya Tanzania kulinda na kuhifadhi amani na utulivu, haki na usawa pamoja na kuheshimu misingi yote ya siasa safi ili kukuza demokrasia yetu.
 
sawa sawa
Siasa safi ni msingi mkuu wa maendeleo nchini ambao inatakiwa kulindwa na kuheshimiwa Sana kwani nchini isiyokuwa na siasa safi IPO hatarini katika kudumia kimaendeleo kwani siasa ndiyo inaamua mstakabali mzima wa maisha ya baadae
 
Back
Top Bottom