Kakobe: Hatuchagui malaika bali Rais; afuta Ibada za FGBF siku ya uchaguzi

Sadaka na zaka zote anazopata anapeleka Chadema...kwa hivyo hii ni kutimiza ahadi yake ya kwamba watamjua yeye ni nani baada ya kupigwa mkwara na Ngeleja kuhusu nguzo za Tanesco... Nadhani alisahau ile ya kaisari mpe kaisari :lol:
 
Siamini kama hili ni swala la kutafuta umaarufu. alichokifanya ni sahihi sababu waumini wa makanisa yake wataamka wakijua siku hiyo kazi ni moja tu ya kupiga kura. kuliko wangetakiwa kuchagua waanze kipi kati ya kwenda kanisani na kwenda kituoni kupiga kura
Ndugu zangu napenda kuunga hoja ya Mheshimiwa Baba Askofu KAkobe kwani ni vyema mtukutumia haki yake ya kupiga kura amefanya vizuri kuwatangazia watu wa dhehebu lake kufanya ibada jumamosi maana nayo ni siku ambayo ni yya mapumziko hata mimi nilifikiri nifanye ipi kwanza maana wametuingilia kwenye siku ambayo ndio wakristo au waamini wa Kristo ndio wanakutana kumuomba Mungu wao hii ukiangalia kuna hila ndani yake kwani nini hakufanya jumatatu au siku za kazi au Ijumaa?lakini waamini na watanzania tupige kura na tuwachague wale wanaoweza kutuletea Maendeleo kuanzia maendeleo ya mtu wa chini hadi taifa kwa ujumla hatutaki wanaojiletea maendeleo ya watu wachache tu kama wanavyofanya viongozi wanotawala wa cCM hata baba wa taifa alionyesha Uwezo mzuri wa kiongozi bora anayejali taifa na si nafsi yake na ndio akatoa mfano wa rais wa marekani Kenedy alipochaguliwa aliwauliza watu usiseme Tanzania itakufanyia nini bali sisi Viongozi na Watanzania wote tuifanyie nini Tanzania kwa ajili ya maendeleo. Mungu ibariki Tanzania
 
“Kwenye uchaguzi mkuu hatuchagui malaika wa kutupeleka mbinguni bali kiongozi wa kuliongoza taifa... tuchague kwa kufuata kanuni na taratibu za katiba, kwa kuwa viongozi wote wana sifa, kinachotakiwa ni kuangalia nani ana kipaji cha uongozi,” alisema Kakobe.

hii imekaa vizuri sana sana wadau
 
Nimesoma kwenye gazeti la mwananchi leo kuwa Kakobe ametoa elimu ya uraia kali kabisa na kuna lines zimenifurahisha. Pia amefuta ibada za Jumapili ya tarehe 31 October kuwapa waumini wake nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu

Ukiangalia mahubiri hayo aliyoyaita elimu ya uraia, yanampigia kampeni mgombea wa Chadema. My advise kwa chadema, watumieni waumini wa Kakobe kuwa mawakala kwenye maeneo korofi ambayo ccm inataka kushinda kwa njia yoyote. Hao waumini wa Kakobe hawali rushwa hao. Sound funny lakini kwa jinsi ninavyosikia CCM wametenga billions of shillings kuwahonga mawakala wa upinzani vituoni ili kuchakachua kura. I think waumini wa kakobe ndio wanaweza kusimamia vizuri bila kuingilika kwa rushwa--Chekeni sana but ndivyo ninavyoona
 
Kakobe anazidi kuzihirisha kuwa ni askofu mwenye karama ya mfalme suleimani. Nakumbuka kile kisa cha wanawake wawili ambao mmoja wao alifiwa na mtoto. Kakobe anawafuasi kama 2M tanzania nzima najua watu hawatakubaliana na mimi!
Si wafuasi tu usiwasahau ndugu zao ni sawa na wafanyakazi laki 3 na nusu Kikwete alisahau kuwa wana watu wanaowategemea.
 
safi sana baba askofu kakobe

huyu tuko nae chama kimoja cha chadema
Siyo kuwa mpo naye chadema ila kwa mtu yeyote mpenda nchi yake atafanya hivyo!
TATIZO NIKUWA UKIZUNGUMZIA UFISADI MEANS UNAZUNGUMZIA CCM!??
 
Wachagga walimharibia Mrema mwaka 1995 kwa kutaka kuchagua Rais wa kabila lao. Makanisa nayo yakijionyesha kwa staili hii ya Kakobe yatamharibia Dr Slaa. Ni vizuri Dr Slaa akalikemea hili. Nakumbuka hata Obama kuna mchungaji mmoja waliekuwa wanafahamiana vizuri alitaka kumtibulia. Obama alizikana kauli za mchungaji yule.
 
Wachagga walimharibia Mrema mwaka 1995 kwa kutaka kuchagua Rais wa kabila lao. Makanisa nayo yakijionyesha kwa staili hii ya Kakobe yatamharibia Dr Slaa. Ni vizuri Dr Slaa akalikemea hili. Nakumbuka hata Obama kuna mchungaji mmoja waliekuwa wanafahamiana vizuri alitaka kumtibulia. Obama alizikana kauli za mchungaji yule.
Tofautisha kauli ya Jeremiah Wright na ya Kakobe, Wright alikuwa anamchafua Obama.
 
safi sana baba askofu kakobe

huyu tuko nae chama kimoja cha chadema
Sijui nina Imani haba?? Au nimeweka mawazo yangu kusiko?? Ninachoamini mimi Mgombea yeyote wa upinzani akishaanza kupigiwa mapambio ya sifa na Mtumishi huyu wa Bwana, ni kama anamtia GUNDU. Atapigwa gap refuuuuuuuuuu na mgombea wa CHAMA CHA MAJIZI hadi tushangae!!!!!
 
Huo ni msisitizo wa Askofu wao, na waumini wake wote Tanzania nzima wameshajua nani wa kumchagua - kazi ipo mwaka huu.
 
Mchungaji Kakobe gunning for Mchungaji Slaa. Who is surprised? and shamelessly injecting udini along the way. If you can fool waumini wako and collect their money effortlessly, sio kwa wote WaTanzania.
 
Keep it up Reverend Zacharia Kakobe, wahimize na akina Mwingira wa Efatha na wale wa Agape Life Church and kina Ngrurumo ya Upako, i.e wale ambao wana waamini wengi bila kusahau zile kuu kama RC na KKKT wafanye ibada zao Jumamosi na wahamasishe waamini wao wapige kura siku hiyo. Ni lazima mabadiliko yatokee and the only preciuous time and opportunity is this one, please, do not temper with the available golden moment in our Lilfe. Let us make a change, the change is with you, use it!!
 
Hili suala la Kakobe kuwaruhusu waumini wake wakapige kura ni la maana sana hasa ukizingatia haki ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa. Lakini kwa Kakobe kujifanya anampigia debe mgombea fulani ni tatizo. Kwanza si kwamba waumini wake woote wanaamini katika mgombea anayetaka kuwachagulia. Akumbuke anaongoza watu wa Itikadi tofauti. Lakini pia undumi la kuwili wa JF ndio unaonekana hapa. Mwaka 2005, baadhi ya makanisa yalidiriki kusema kuwa JK ni chagua la Mungu, hili limeonekana tatizo miaka yoote hii mitano na mjadala juu ya hili umekuwa ukiendelea. Lakini pia licha ya kuwa endorsed km chagua la Mungu leo hii wengi wamekuwa wakilalama kuwa hakukidhi mahitaji ya Watanzania walio wengi. Kwahiyo wakati fulani haya madebe ya hawa wanaojiita watumishi wa Mungu yana walakini.
Pamoja na hayo, kwakuwa Kakobe ameanza lazima counter attacks zitafuata kutoka kwa viongozi wa dini nyingine. Haki za Kiraia wakati wa Uchaguzi???? Hii ni kampeni.
 
Jamaa anamatatizo yule, akisahaulika anatafuta popularity faster, amekaa kibiashara zaidi....
kama huelewi ni vema ukatafuta kujifunza; jee unaoujasiri wa kumunyoshea kidole mtumishi wa Mungu! Kama unao ujasiri fahamu unamnyooshea kidole Mungu aliyekuumba na kukupa uhai mpaka sasa. Ninakushauri ujirekebishe.
Msingi hapa ni kwamba Huyu Masihi wa Bwana amefundisha somo chini ya kichwa "MKRISTO NA UCHAGUZI" na katika maarifa hayo hajatajwa mgombea yoyote wa kuchaguliwa sasa unanishangaza jumla ya wote waliorespond message hii ni wewe peke yako upo aggressive.

JARIBU KUFUATILIA SOMO HILI KATIKA CHANNEL 10 SIKU YA IJUMAA NA JUMAMOSI KUANZIA SAA TATU USIKU NA ALHAMISI STAR TV SAA NNE USIKU WIKI HILI kisha kama unakomenti nizipate toka kwako baada ya hapo.
 
Mara hii mpaka kieleweka baba!!! Na bado. Siku hiyo makanisa yote yanafungwa. Tumeshtukia Mbinu zenu baba.


Mwaka huu wataisoma na Mlinzi wao Maalum.................

Tunaweza kumchagua mbunge yeyote................

Lakini linapokua suala la Rais.........Tumechoka na Mzee wa Maigizo na kampeni zake za Nyasi kwa Nyasi
 
hili suala la kakobe kuwaruhusu waumini wake wakapige kura ni la maana sana hasa ukizingatia haki ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa. Lakini kwa kakobe kujifanya anampigia debe mgombea fulani ni tatizo. Kwanza si kwamba waumini wake woote wanaamini katika mgombea anayetaka kuwachagulia. Akumbuke anaongoza watu wa itikadi tofauti. Lakini pia undumi la kuwili wa jf ndio unaonekana hapa. Mwaka 2005, baadhi ya makanisa yalidiriki kusema kuwa jk ni chagua la mungu, hili limeonekana tatizo miaka yoote hii mitano na mjadala juu ya hili umekuwa ukiendelea. Lakini pia licha ya kuwa endorsed km chagua la mungu leo hii wengi wamekuwa wakilalama kuwa hakukidhi mahitaji ya watanzania walio wengi. Kwahiyo wakati fulani haya madebe ya hawa wanaojiita watumishi wa mungu yana walakini.
Pamoja na hayo, kwakuwa kakobe ameanza lazima counter attacks zitafuata kutoka kwa viongozi wa dini nyingine. Haki za kiraia wakati wa uchaguzi???? Hii ni kampeni.

utajijua!!
 
Mchungaji Kakobe gunning for Mchungaji Slaa. Who is surprised? and shamelessly injecting udini along the way. If you can fool waumini wako and collect their money effortlessly, sio kwa wote WaTanzania.

Ni serikali gani iliyowezesha haya yote yajitokeze?!
 
Back
Top Bottom