Kakobe: Hatuchagui malaika bali Rais; afuta Ibada za FGBF siku ya uchaguzi

Ngoja twende Wizara ya Mambo ya Ndani tu-check kama ame-reniew usajili wa kanisa lake. Mwaka ule alipotishiwa usajili alijirekebisha, sasa anaanza chokochoko, ataipata.
 
kama mtu anataka kupiga kura anaweza tuu, KKKT na RC wana misa nyingi sana (tatu nakuendelea) na kila misa haichukui zaidi ya masaa 2 na zinaanza 12 asubuhi, so kusali sio kigezo labda kwa hao wanaosali asubuhi mpaka jioni

.
Nampongeza sana Kakobe kwani ameonyesha ukomavu mkubwa sana wa utatuzi wa matatizo yanaowakabili waTz wengi hasa umaskini. Kimsingi kakobe anatoka kwenye makanisa ya kipentekoste ambayo yana vikundi visivyoamini katika kupigia kura. Na wachungaji wao huwashikilia hao waumini ndani ya nyumba za ibada kuanzia saa moja asubuhi hata saa 12. Hudai kuwa hao viongozi wa kisiasa hawana mchango wowote katika maisha yao ikiwa ni ufukara au utajiri. Utastajabia watu wa aina hii wanapokuwa wamepitia ugumu fulani wa maisha hupewa msaada na mtu fulani hivi mwenye busara na bidii katika kazi, basi watamshukuru Mungu kwa kusikia kilio chao na kuwaondolea tatizo lililokuwa linawakabili pasina kujua kwamba wao wenyewe ni sehemu ya tatizo lililokuwa linawakabili. Ni sehemu ya tatizo kwa maana kwamba kama wangeshiriki kwa mkono wao na kwa kura yao kumleta kiongozi muadilifu na mwenye kuwajali kwa kusimamia tunu za taifa kwa haki wasingelikua ombaomba ndani ya nchi yao wenyewe, huku wageni waliopanga kwao wakiwa na ziada katika mahitaji yao. Usipopiga kura basi jua hakika kama elimu, afya, maji, umeme vimekugeuka kuwa kama anasa kwako na jamii inayokuzunguka basi umesababisha wewe na mbele za Mungu uu mbaya kuliko asie amini. Hivyo basi nawaomba viongozi wa kiroho wafahamu fika kuwa hawawezi kuhudumia roho tu nje ya mwili kwani ni hakika kabisa kuwa mwili unapoelemewa na maumivu hutengana na roho ambayo hawawezi kamwe kuwa na mahusiano nayo tena. Mahusiano na hizo roho ni kwa sababu ya uwepo wa mwili kinyume chake ni 'Hakuna kitu'
 
Excellent kakobe. I think elimu ya uraia aliyotoa kila Mtanzania anaihitaji. So wito kwangu kwa makasisi ni kuwa Toeni elimu hiyo bila woga. Msiogope kuwa mkitoa elimu vizuri mtafutwa...
 
Nadhani kuna watu wanafurahi Wakristo wengi wasipige kura, safari hii tumefanya juhudi nyingi; lakini NEC imeng'ang'ania, na hatuwezi kuacha kwenda kupiga kura kwani tunaweza kuchaguliwa kiongozi asiyefaa tukajutia kwa miaka mitano.

"Hivyo natangaza rasmi siku hiyo ya uchaguzi hakutakuwa na ibada katika makanisa yote ya FGBF, milango ya makanisa hayo siku hiyo ifungwe na ibada ya siku hiyo ifanyike siku ya Jumamosi," alisema askofu huyo.

Ni uamuzi mzuri kwani kazi ni moja tu siku hiyo, kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kweli TZ.
 
Nimefurahi kuona sasa uchaguzi unaanza kupewa umuhimu unaostahili. Ingekuwa vema kila mtu akapige kura yake maana tumedharau sana hilo zoezi, hasa wasomi na wakazi wa mijini, halafu siasa zikileta balaa ndio wa kwanza kulalamika. This time hatutakuwa na wakumlaumu kama hatutaenda kupiga kura zetu.
 
Ubarikiwe askofu Kakobe kwa kuona umuhimu wa waumini kushiriki kikamilifu katika kupiga kura.
 
Mwanzo mzuri wa kutowachagua mafisadi..................hureeee kakobe
 
Nimesoma kwenye gazeti la mwananchi leo kuwa Kakobe ametoa elimu ya uraia kali kabisa na kuna lines zimenifurahisha. Pia amefuta ibada za Jumapili ya tarehe 31 October kuwapa waumini wake nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu

Ukiangalia mahubiri hayo aliyoyaita elimu ya uraia, yanampigia kampeni mgombea wa Chadema. My advise kwa chadema, watumieni waumini wa Kakobe kuwa mawakala kwenye maeneo korofi ambayo ccm inataka kushinda kwa njia yoyote. Hao waumini wa Kakobe hawali rushwa hao. Sound funny lakini kwa jinsi ninavyosikia CCM wametenga billions of shillings kuwahonga mawakala wa upinzani vituoni ili kuchakachua kura. I think waumini wa kakobe ndio wanaweza kusimamia vizuri bila kuingilika kwa rushwa--Chekeni sana but ndivyo ninavyoona

I totally agree with you...not a lot of people will think this makes sense though.
 
Sawa ila aliwahamasisha kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura?
 
Jamani si mnamwingiza kakobe vitani na ccm baada ya muda tutasikia kakobe anaambiwa na serikali kuwa amejenga kanisa barabarani kwa hiyo livunjwe na watakuwa tayari hata kwenda mahakamani..................sidhani km kakobe kamaanisha moja kwa moja kiasi hicho labda ni tafsiri tu ya watu
i totally agree with you...not a lot of people will think this makes sense though.
 
Mwaka huu thithiem mmeze wembe, tutajitokeza kupiga kura za kutaka mabadiliko!
 
Hamna lolote hapa.....

Ila namsifu kuwa ni Msomi wa kweli na anaona mbaali sana.

Kashasoma alama ukutani na kafahamu kuwa UKUTA WA BERLINI UTAANGUKA soon.

Bado akina Mhando, IPPMedia na wengine hawajaliona. Akina kaka Michuzi bado wanatangatanga.....

Nina imani kama ilivyokuwa USA, dakika za mwisho wakiona ukweli ulivyo, na wao watabadilika.
 
Kitendo cha Kakobe nakitafsiri kama ongezeko la uelewa wa haki za msingi za watanzania na umuhimu wa kupiga kura, i think Tanzania is not very far from the turning point whether for good or worse.
 
Back
Top Bottom