Kaka yangu hamtaki mchumba wangu. Nifanye nini?

mamamzungu

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
2,374
3,887
Anasema ikitokea tumeoana hatutoboi miaka 5. Namnukuu “ Mkitoboa miaka 5 niko pale uniite mbwa”

Ni kaka yangu mtoto wa mama yangu mdogo alielelewa nyumbani kwetu… yeye tayari ana familia yake mke na watoto yuko under 30 .. Ni kaka ambaye tumekuwa tukishirikishana mambo ya mahusiano yetu mpk sasa..

Sikujua kuwa mpenzi wangu anafahamiana na kaka yangu mpk siku nilipompost status nikimuwish happy birthday.

Kaka yangu alinifungukia kuwa wanafahamiana na wamepiga kozi wote kiufupi wanafanya kazi zinazofanana na wanajuana mpk vyumba wanavyoishi japo hawana urafiki ni ile wakikutana ndio wanakuwa marafiki..

Mpk Kaka yangu anakuja kufahamu nina mahusiano nae ilichukua mwaka mzima kumfahamu na sikumwambia kuwa tuna mahusiano nilimwambia tu marafiki

Kwa sasa tunaelekea hatua nzuri kaka yangu amenishikia king’ora kwamba huyo mwanaume hanifai niachane nae simuwezi.. ninapomuuliza sababu haniambii nikazielewa

Sababu mpk sasa nilioiona kubwa aliyoniambia ni kuwa:
  • kabila la watu wa mwisho wa dunia sio kabila la kuolewa nao (yeye ameishi sana huko so ana wafahamu)
  • Ni washirikinaa sanaa (anaamini kwamba huyu mpnz wangu kanipata kwa madawa) alinipa kielelezo Kuna rafiki yake mwingine wa kabila hilo alimpata mwanamke kwa madawa matokeo wamezaa watoto wawili mwanamke akili imefunguka kakimbiaa
Kubwa la Leo ambalo limenifanya niombe ushaurii ni hili

Amesema kuwa huyu mpzn wangu alishawahi kutoa posa mahali halafu akahairisha kuoa.. na alimpa ujauzito huyo mwanamke ila aliukataa akasema atoe ujauzito,, mwanamke alipokataa kutoa mimba alimtumia hawara yake ampelekee Zawadi ya juice kumbe ndani ya juice kaweka dawa ya kutoa mimba

Hiyo story bro anadai kahadithiwa na ex wa mpnz wangu

Kiukweli nimeshindwa kuelewa nifanye nini.. Kijana nampenda na amekuwa mtu mwema kwangu mpk sasa tuna miaka 2 ya mahusiano sijaona bays kwake

Ushaurii wenu wakuu
 
Sikiliza wakubwa, wakikwambia acha acha kweli, usishupaze shingo
 
Kama katoka huku mkunduni mwa dunia kimbia... Kusini sio pa kupashadadia. Kama sio yeye ndugu zake watakupa shida sana. Sio lazima uchawi hata maelewno tu wao kwa wao kama familia ni mbinde.
 
Msikilize kaka yako maana ni mwanaume sisi wanaume tunajuana na huwa tunawatakiwa mema sana dada zetu.
 
Kama katoka huku mkunduni mwa dunia kimbia... Kusini sio pa kupashadadia. Kama sio yeye ndugu zake watakupa shida sana. Sio lazima uchawi hata maelewno tu wao kwa wao kama familia ni mbinde

Hapana ni kule kwa kina brother K
 
Kata pua, uunge wajihi..

We kama unaona anakufaa olewa, mengine mbele ya safari.

Akwambiacho kaka yako ni kweli ilapala umeleta huku means hujamuelewa kaka yako.

Hapo ni
Moyo vs akili.
 
Kata pua, uunge wajihi..

We kama unaona anakufaa olewa, mengine mbele ya safari.

Akwambiacho kaka yako ni kweli ilapala umeleta huku means hujamuelewa kaka yako.

Hapo ni
Moyo vs akili.

Kweli simuelewi
 
Kuna kitu kinaendelea humu nilipost kukushauri naikatokea sa hv naona wameifuta wehu wa PAW
 
Mskilize Kaka.

Sisi wanaume tunafahamiana vzr sana.

Mie hakuna rafiki yangu atakayeweza kumuoa Dada yangu. ni waharibifu vby mno.
 
Back
Top Bottom