Kaka yangu anatembea na mama mkwe wangu

Naishi dar, brother wangu mkubwa ambaye ni mstaafu kaja kufuatilia madai yake.
Nyumbani kwangu anaishi pia mama wa mke wangu.
Juzi nlipotoka kwenye mizunguko na kurudi nyumbani mida ya saa tano asubuhi niliwakuta live wakilimega tunda.
Kwa kweli kaka yangu ni mtu mzima ambaye kwa umri kamzidi hata mkwe wangu.
Lakini hii siielewi, matokeo yake nimejikuta mi ndo naona aibu hata kuwaangalia.

Mh.....,!!!!! Kweli hawakukosea waliosema ishi uyaone na nyumba hizi kweli zinaficha mengi.
 
waache wale tunda kaka, au ulitaka kula wewe?

hayo ndiyo maisha kaka, sahau yaishe... Halafu kumbuka kuwa huwezi mwambia wife kwanza ni aibu pili italeta mgongano ndani ya nyumba.. Hayo ndiyo yale utakayoishi nayo milele kama siri moyoni mwako.
 
pole dogo,kaa na bro mtete.
Je, bro naye ni mjane?
Wewe je umeoa au ndio kusaidiana maisha?
Sipati picha ya mama mkwe kuwa mdogo kuliko bro wako!
 
Hahahahahahaaaa.......Hii mada sina hakika kama ni ya ukweli ila kwa hizi comments tu ...u guyz have made my day.......Very Laughable...

Braza Kuwa Baba Mkwe????????????
 
Sipati picha ya mama mkwe kuwa mdogo kuliko bro wako!

Hii inawezekana koz mi kuna mshikaji wao dingi yake ana wake wanne....so braza wake mkubwa ryt now yupo kwenye 50's na ana wajukuu tayari....na huyo mshikaji wangu ni 2nd last........
 
kesi Hipo,
kwa sababu huyo Kakake sasa atakuwa ni Babamkwe wake, na Watoto wa Kakake sasa watakuwa mashemeji zake, Na Mkewe anamwita huyo kaka ya Mmewe kuwa ni Babayake na watoto wa wa huyo shemeji yake watakuwa wadogo zake
Kaaaaaazi kwelikweli

mie naona huu ni mzunguruko tu wacha wasuuze roho as long as wote wapo single.mama mkwe raha jipe mwenyeweeeeeeeeee!
BTW: lazima nikiri kuwa hii kali na hutokea mara chache kwa miaka.LOLs
 
mama anamvunjia heshima mwanae, among all men aje awe huyo shemeji?? wote hawana adabu hata kidogo
 
ni jambo la aibu!
wote kuoa sehemu moja!
kwa vile umemzoea kaka yako,huyo ndio uongee naye..
mwambie jinsi lilivyo jambo la aibu na mkeo akijua jinsi atakavyoghafilika,...

au ongea na mkeo aongee na mama yake..,
wasiwaibishe kama ni ukame wakatafute wapenzi huko nje!
mijitu mingine sijui ikoje...haina aibu!
Hapa Fab naona na meno uliuma wakati una-type kuonyesha msisitizo:teeth:
 
Huyo blaza lazima tu amesha wahi kumgonga hausigeli wake
Kujibuji kuna akina mama hawataki kuzeeka ati, unafanya mchezo? Unawezakuta jamaa aliitwa chumba kuombwa msaada wa kuuwa mende
hapo. Ukiingia tu basi utajua mweneywe kama wewe ni Yusufu au Nanihii .........hahah
 
Naishi dar, brother wangu mkubwa ambaye ni mstaafu kaja kufuatilia madai yake.
Nyumbani kwangu anaishi pia mama wa mke wangu.
Juzi nlipotoka kwenye mizunguko na kurudi nyumbani mida ya saa tano asubuhi niliwakuta live wakilimega tunda.
Kwa kweli kaka yangu ni mtu mzima ambaye kwa umri kamzidi hata mkwe wangu.
Lakini hii siielewi, matokeo yake nimejikuta mi ndo naona aibu hata kuwaangalia.

hahaha naona kiranja mkuu unamuonea huruma braza na pensheni yake.
ndio tuu leiti, naona braza mafao atayaacha dar na kurudi kijijini
mikono mitupu.
 
hahaha naona kiranja mkuu unamuonea huruma braza na pensheni yake.
ndio tuu leiti, naona braza mafao atayaacha dar na kurudi kijijini
mikono mitupu.
Hahahh anarudi na furaha ya dakika tano................... kama nyuki dume anavyofia hewani baada ya kumpata malkia
 
Mama mkwe amezidiwa ndo mana,haja 'do' cku nyingi ndo mana, ni vzr wamesaidiana, mama mkwe anampenda bro wako,nawe wampenda mwanae basi upendo mpaka baasi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom