Kadi bandia za CHADEMA zaiumbua CCM Mbeya

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
SIKU moja baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbusho kutamba mbele ya viongozi wa juu wa CCM Taifa kuwa wanachama 497 wa Chadema akiwamo diwani wa Kata ya Nzovwe hapa, Hezron Mwakalobo,wamejiunga na chama hicho,ameibuka na kukana madai hayo. Mbali Diwani huyo, Uongozi wa Chadema mkoani hapa umedai kuwa mwanachama aliyekihama chama hicho ambaye wanamtambua ni mmoja na kwamba kadi 497 zilizopokelewa na CCM si za wanachama wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwakalobo alikana madai yaliyotolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya kuwa amejiondoa katika Chadema na kwamba madai hayo yalilenga kuudanganya umma wa Watanzania. “Mimi ni diwani wa Kata ya Nzovwe kupitia tiketi ya Chadema na nimechaguliwa na wananchi ambao wameniamini na kunipa nafasi ya uongozi” alisema na kuongeza kuwa hana nia na wala hajafikiria kujiunga na CCM.

Kwa upande wake Katibu wa Chadema, Mkoa wa Mbeya, Eddo Makata alisema kati ya wanachama 497 waliotangazwa na CCM kuwa wamekihama chama hicho ni mmoja tu, Walen Kaminyoge ambaye ni Katibu wa Jimbo la Mbozi Mashariki ndiye aliyekihama chama hicho. Alisema kadi zilizopokelewa na Viongozi wa CCM si za wanachama wa Chadema. “Hivi karibuni Kaminyoge alienda Makao Makuu Dar es Salaam na kuomba apewe kadi 100 kwa ajili ya wanachama wapya, hakuwapa wanachama na ndio hizo kawapa viongozi wa CCM” alisema.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbusho, kabla ya kumkaribisha Nape kuzungumza katika mkutano huo wa hadhara, alimueleza kuwa wanachama 497 wa Chadema wamejiunga na CCM pamoja na wanafunzi 330 kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani Mbeya.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete alipokea kadi zaidi ya 3,000 zilizodaiwa ni za wanachama wa chadema wa Jimbo la Mbeya vijijini waliojiunga CCM, hata hivyo ilikuja kudaiwa kuwa kadi hizo zilikuwa si halali.

Akizungumza jana katika viwanja vya Ruanda Nzovwe, Katibu wa Itiadi na ueneza wa CCM Taifa, Nape Nnauye aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kujiunga na chama hicho kwa kuwa ni sawa na nyoka wa shaba, ambapo mtu akiumwa na nyoka wa kawaida akimtazama nyoka huyo atapona.

Mwananchi
 
Mwamalala alisema kitendo cha waanzilishi hao wa CCJ kusimama na kuanza kuikosoa serikali yao kwa maelezo kwamba imeshindwa kusimamia vema sekta ya umeme na dhana ya kujivua gamba, ni wazi kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao hivyo wanaiunga mkono CHADEMA.
"Ninadhani hawa watu wana ajenda ya siri…hata mchezo uliofanyika ndani ya CCM kununua kadi za chama chetu kutoka kwa wanaowaita wafuasi wa CHADEMA tunaufahamu na tayari mmoja kati ya waliotumiwa kutimiza azma hiyo tumemkamata na yuko polisi Mbozi," alisema Mwamalala.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Jeremia Mwakatumbula mkazi wa Mbozi aliyekutwa na kadi 10 za CHADEMA ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kuzinunua kadi hizo kwa sh 10,000 kila moja.
 
Haya Nape na genge lako mnazidi kuvuna mnacho kipanda .Umafya hauwezi kuiokoa CCM na matumizi ya pesa si jibu kwa shida za watanzania ambao wana taabika mno chini ya CCM .
 
Japokuwa mbinu za kisiasa ni nyingi, na njia za kupata wanchama ni jinsi unavyocheza kalata, lakini UONGO huwa unamadhara makubwa kwani inafika mahali, huwezi kudanganya tena! Wananchi wakishagundua hili, atapoteza imani zaidi na zaidi!....
 
Wanatumia hela nyingi kuhalalisha uongo badala ya kukaa chini kutatua matatizo ya chama. Its up to them if they don't wanna change.
 
Yaani haya majamaa yanazidi kutumia hela ya walipa kodi kununua kadi za chadema?

Unajua ccm imejaa waganga njaa tupu, usiyaone yamevaa manguo ya kijani ukidhani yamekusanywa bure ni lazima uyalipe tena pesa nyingi. Hamna mtu anayekubali kuvaa nguo ya kijani siku hizi bila kulipwa pesa!


Hizi mbinu za viongozi wa chini wa ccm kuwandanganya viongozi wa juu i kwa swala la utendaji ni sugu sana. Wanafanya hivyo ilikuonekana wamefanya kazi na hivyo kujustify matumizi ya pesa za chama.

CCM ni ufisadi mpaka chini, sijui watamvua gamba nani na wamache nanai maana kila kajitu ccm ni kaiizi kwa level yake.

Kashifa hii lazima cdm waipeleke kwa nguvu ya umma ili ccm izidi kupolomoka maana ufisadi bado una waumbua mpaka ngazi za chini hata vikatibu vya ccm vya mikoa,wilaya,vijiji vyote vinakula kodi za watanzania kwa kununua wananchama feki.
 
Wakati unaendelea kutafakari CCM na Viongozi wake; NIPASHE waliripoti hivi

Wanafunzi walalamika kulazimishwa kuhudhuria maandamano ya CCM leo


Na Emmanuel Lengwa 16th July 2011

Wanafunzi wa shule za Sangu, Meta na Ivumwe zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi mkoani Mbeya, wamelalamikia hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa kuwalazimisha kuhudhuria maandamano ya chama hicho yanayotarajiwa kufanyika leo jijini Mbeya.
Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina yao, wanafunzi hao wamedai kuwa viongozi wa CCM wamekwenda kwenye shule zao na kuwaamuru walimu wawashinikize wanafunzi kuhudhuria maandamano hayo.

Walisema viongozi hao wa CCM wameahidi kuwapelekea magari yatakayowabeba kutoka kwenye shule zao kwenda mahali pa kuanzia maandamano na kisha kuwarejesha shuleni baada ya maandamano kumalizika.

Walisema kitendo hicho cha kuwalazimisha sio kizuri kwa kuwa na wao wanayo hiyari ya kwenda au kutokwenda kwenye maandamano hayo.
"Pamoja na kwamba hizi shule za wazazi zinamilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ambayo ipo chini ya CCM, lakini watambue kuwa na sisi tunazo itikadi zetu za kisiasa ambazo zinapaswa kuheshimiwa," alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Mwanafunzi huyo ambaye alionekana kuwa kiongozi wa kundi kubwa la wanafunzi waliofika katika ofisi za gazeti hili kulalamika, alisema wao hawako tayari kuhudhuria maandamano hayo kwa kuwa wanayo kazi moja tu ya kujisomea.

"Wao kama wanataka wanafunzi waongeze idadi ya watu kwenye maandamano yao, wawachukue wale wa O- level, lakini sisi kwanza ni watu wazima wenye maamuzi yetu na pia tunajiandaa na mitihani kwani sisi tunaona kama muda hautututoshi," alisema.

Mwalimu mmoja wa shule ya Sekondari Meta ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alithibitisha kuombwa na viongozi wa CCM ili wawaruhusu wanafunzi wa shule hiyo kuhudhuria maandamano hayo.

"Ni kweli viongozi wa CCM wamefika hapa na kutuomba wanafunzi waende kwenye maandamano yao, kwa kuwa wao ndio wamiliki wa shule hizi na ndio waajiri wetu, sisi hatuna uwezo wa kuwakatalia, lakini pia sioni ubaya wowote kwa wanafunzi kwenda kwenye maandamano hasa ukizingatia kuwa kesho (leo) sio siku ya masomo," alisema.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbusho, alisema suala hilo sio la kwake na kama lipo wanaopaswa kuulizwa ni walimu wa wanafunzi hao au viongozi wa Jumuiya ya Wazazi.

"Hilo mimi halinihusu, kawaulize walimu wao na kama hutaridhika waone viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kwa sababu wao ndio wamiliki wa shule hizo," alisema Shumbusho.

Maandamano cha CCM yanayotarajiwa kufanyika leo yamepangwa kuanzia eneo la Mafiati na kuishia viwanya vya Rwandanzovwe.


CHANZO: NIPASHE


Hii ndio CCM inayoangaika kudhihirisha ulimwengu kuwa "wanapendwa" na wananchi wao!
 
Napenda wanapo nunua kad za cdm kwni wana ongeza income ndani ya chama. Lakn watz wa sasa sidhani kama wana danganyika kiurahis kama ivo.
 
Kuna michezo michafu katika siasa ila huu ni mchezo wa kujicgafu wenyewe magamba,kwani mbeya hakuna wanachama wa vyama vingine isipokuwa cdm tu?kila kadi zininazorudishwa ni za cdm tu,magamba yanahofia cdm kweli muda wao umekwisha.
 
Mimi ninachosema kwa ccm na watanzania kwa ujumla....raha ya siasa ni maendeleo na ndipo siasa itaendeshwa kiulaini sana...sasa huku kufurahia kadi feki za wapinzania wakati nchi ni giza ni sawa na kubeba panga la kukuangamiza wewe mwenyewe. Watanzania ni lazima tuwe na mawazo pevu ya kulilia mabadiliko na kisiasa na maendeleo ya haraka kulingana na wakati tuliopo...mungu atubariki sana ...
 
Taksi zililipwa 10000, Bajaj na pikipiki 8000 kila moja na wafanyakazi wa Shule zote za Jumuia ya wazazi Mbeya walipewa 5000/= kila mmoja. Ilikuwa ukisahfika uwanjani baada ya maandamano unamwona cashier anakupa haki yako. Kazi ipo
 
Mmmhh CCM sasa sijui niwafananishe na nini............nisaidieni
 
Back
Top Bottom