Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
- Thread starter
- #21
Nakubaliana nawewe ila kipengele kimoja tu, kwamba kwavile huoni kitisho chakuvamiwa na Wareno na SA unahisi jeshi halinakazi tena ya ulinzi na badala yake unataka jeshi lifanye shughuli nyengine, hapa kwa mtazamo wangu hauko sawa, jeshi linakiwa kuwa active muda wote kwani adui hakuletei barua.
Nadhani umenielewa vibaya; kitu ambacho tulitakiwa kufanya kwanza kama taifa (jeshi) ni threat analysis. Je tishio la usalama wa Tanzania liko upande gani hasa na ni lipi more realistic? Tukishapata jibu hilo tunatakiwa kufanya review of our current military policies kuziona zinaendana vipi na tishio hilo au matishio hayo.
Sasa tukishafanya hiyo review itatupasa tu-update au upgrade hiyo policies na pamoja nayo kumodify jeshi hilo liendane na uhalisia huo mpya. Nilichokisema hapo juu kuwa jeshi letu mwanzoni kabisa lilikuwa kwa ajili ya kulinda the existence of a young nation from threats from abroad na kutoka nje. Ndio maana utaona kuwa baada ya maasi ya 1964 tulitengeneza mfumo uliozuia vitu vikubwa viwili kutokea jeshini - mapinduzi ya kijeshi na uasi mwingine. Matokeo yake karibu mara tatu mapinduzi yalizuiwa na hakuna wakati wowote ambapo wanajeshi wametishia kuweza kuasi na sasa hivi jeshi letu limejengwa kiasi kwamba hivyo vitu haviwezi kutokea.. mtu anaweza kufikiria kupanga na kujaribu lakini haiwezekani kutokea.
Lakini pia lilikuwa linatishiwa na vurugu za kutoka mipaka yetu hivyo utaona hata vikosi vyetu vimepangwa kuwa karibu na mipaka yetu sana, silaha zikiwekwa mbalimbali n.k Tatizo moja ni kuwa mfumo wa sasa unafanya JWTZ iwe jeshi zito kumove in case of immediate threat kwani ni lazima kwanza kumobilize resources zilizotawanyika nchi nzima lakini hilo ni kwa sababu ya our then perceived threat.
So katika ulimwengu wa leo tishio letu ni nini hasa? Sidhani kama ni Afrika ya Kusini au nchi ya nje!