JWTZ na Mahusiano ya Kujenga Uchumi wa Kisasa: Maswali yasiyojibiwa

Nakubaliana nawewe ila kipengele kimoja tu, kwamba kwavile huoni kitisho chakuvamiwa na Wareno na SA unahisi jeshi halinakazi tena ya ulinzi na badala yake unataka jeshi lifanye shughuli nyengine, hapa kwa mtazamo wangu hauko sawa, jeshi linakiwa kuwa active muda wote kwani adui hakuletei barua.

Nadhani umenielewa vibaya; kitu ambacho tulitakiwa kufanya kwanza kama taifa (jeshi) ni threat analysis. Je tishio la usalama wa Tanzania liko upande gani hasa na ni lipi more realistic? Tukishapata jibu hilo tunatakiwa kufanya review of our current military policies kuziona zinaendana vipi na tishio hilo au matishio hayo.

Sasa tukishafanya hiyo review itatupasa tu-update au upgrade hiyo policies na pamoja nayo kumodify jeshi hilo liendane na uhalisia huo mpya. Nilichokisema hapo juu kuwa jeshi letu mwanzoni kabisa lilikuwa kwa ajili ya kulinda the existence of a young nation from threats from abroad na kutoka nje. Ndio maana utaona kuwa baada ya maasi ya 1964 tulitengeneza mfumo uliozuia vitu vikubwa viwili kutokea jeshini - mapinduzi ya kijeshi na uasi mwingine. Matokeo yake karibu mara tatu mapinduzi yalizuiwa na hakuna wakati wowote ambapo wanajeshi wametishia kuweza kuasi na sasa hivi jeshi letu limejengwa kiasi kwamba hivyo vitu haviwezi kutokea.. mtu anaweza kufikiria kupanga na kujaribu lakini haiwezekani kutokea.

Lakini pia lilikuwa linatishiwa na vurugu za kutoka mipaka yetu hivyo utaona hata vikosi vyetu vimepangwa kuwa karibu na mipaka yetu sana, silaha zikiwekwa mbalimbali n.k Tatizo moja ni kuwa mfumo wa sasa unafanya JWTZ iwe jeshi zito kumove in case of immediate threat kwani ni lazima kwanza kumobilize resources zilizotawanyika nchi nzima lakini hilo ni kwa sababu ya our then perceived threat.

So katika ulimwengu wa leo tishio letu ni nini hasa? Sidhani kama ni Afrika ya Kusini au nchi ya nje!
 



Mkuu Gogomoka,

Hoja yako ni nzuri sana nakuunga mkono ila kuna sehemu umependekeza vyama vyetu vya upinzani esp CUF&CDM kujaribu kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa Jeshi letu hili, ndio ni vizuri ila tatizo lililopo ni kuwa wana jeshi walio wa chini kabisa ndio wana uhusiano na vyama vya upinzani ila wakubwa zao wamemezwa na ufisadi wa CCM kwa kuleweshwa na pesa za umma hapo kuna tatizo ni kubwa inatubidi kufanya nguvu ya ziada kwa hilo na kupata utaalamu wa kupenetrate
Jethro... Gogomoka kaiweka vizuri (he is a great asset)

Amezungumzia upcoming potentials, na hilo ndilo tulitakalo, hawa recent ex-monduli, ambao bado tupo nao kwenye social networks, young and energetic, wapo walio frustrated na wengine tayari wanahisi unfairness in an existing system

IT IS A GREAT IDEA FROM GOGOMOKA, AND AN IMPLEMENTABLE ONE
 
Yaani nimefurahia sana michango yenu. I hope some of our ruling elite are inspired by them. People are real deep in this one.
 
...Tuendele pale ambapo sasa kumbe utakuta hata Makampuni makubwa ya Ulinzi na kuuza silaha ndani ya nchni yatakuwa mali ya Jeshi na idara ya Usalama wa taifa kwa sura ama ya JKT au shirika jipya, na hivyo ungekuta Jeshi kupitia makampuni yake ya ulinzi ndio yameshika lindo katika migodi yote mikubwa ya madini, viwanya vya ndege vikubwa, bandari nk hii inatowa fursa mbili kwa taifa kwanza kama biashara ya kuuza ulinzi imara kwa makampuni husika lakini kubwa ni kujuwa na kuwa na uhakika kuwa kila kinachofanyika ndani ya hayo makampuni yana maslahi ya Taifa letu na hamna hujuma yoyote tunayofanyiwa. Nikupe tu taarifa Mkuu wangu ni kuwa hakuna kampuni yoyote itawekeza leo katika nchni za Magharibi na hata uchina husiajiri wanajeshi ama kwa kujuwa ama kwa kuto kujuwa!

Hii ina maana kumbe wale twiga wasinge ondoka hapa nchni maana Jeshi imara na lenye kulinda maslahi na uchumi wa Tanzania ndio wangekuwa wameshika lindo sehemu zote muhimu za nchni hii na hata KIA na ndani ya Mbuga zote za Utalii na siyo KK Security na Group 4 Security.

Kama nilivyokwisha kusema mashamba ya JK badala ya kubadilishwa kuwa mali binafsi ya Mwamunyange yalipaswa sasa kutafuta soko la mazao ya chakula nje ya mipaka yetu na ndio wangekuwa mfano wa kuigwa kwa kuuza vyakula raw na vya kusindikwa ndani na nje ya nchni.
 
Mi pia hua nabakia na maswali mengi sana kuhusu TISS.
Hivi vijana wanaoingizwa kule wanajua maana ya usalama wa taifa kweli au ni just kwa vile baba zao au wakwe zao walikua kwenye system nao wanapatiwa hizo nafasi?? Siku hizi kazi yao imekua ni kuwa black mail wale wanao criticise seikali badala ya kufuatilia external threats!!.
Kuna wengine wamekua wakitumia title za usalama kuwatisha wakuu wa taasisi zao ili wapewe rushwa na pia hao hao kwenye hizo taasisi walizokua attached ndo mafisadi na wala rushwa wakuu.....sitaki niwataje kwa majina na vithibitisho vyao ila makosa siyo yao ila ya system inayowateua na kuwapa madaraka wasiyojua maana yake.
 
Jethro,

Nakubaliana na wewe, sasa changamoto ni kwa uongozi wa Chadema kutafuta mbinu mbadala za kuweka mahusiano na upcoming officers.
 
Mwanakijiji,

Kabla sijaenda mbali, mkuu siku zote unaonyesha maturity na passion ambayo kama Watanzania wachache wakiwa nayo surely Tanzania itabadilika positively.Mkuu mabadiliko siku zote yaanzishwa na mtu mmoja, nakusihi usikate tamaa kuweka maswali magumu mezani. Inapowezekana nitajitahidi kuchangia.
Natumaini wapo wenzetu walio kwenye fence wakiwa na beneficial knowledge lakini wewe uongozi wako unatupa inspiration to join the bandwagon.

Kujaribu kuchangia kwenye maswali yaliyofuata; Binafsi tunaamini kuwa wanajeshi ni Watanzania na binadamu kama sisi, wanashiriki shughuli za kijamii kama wengineo. Changamoto ni namna ya kufahamu jeshi kama institution. Kwa kuanzia viongozi kama Dr Slaa/Kabwe/Lissu inabidi kuanza kujenga mahusiano binafsi ili kuweka informal lines of communications, huo ndio mwanzo wa yote. Baada ya hapo kwa kupitia njia za wazi na mahusiano waliyowekuwa nayo inakuwa rahisi kuandaa internal (inhouse) workshop kwa maofisa wa jeshi kuelezea policy ya Chama chao (CDM) Hiyo inatoa nafasi kwa wao kuchangia/kuboresha policy kuhusiana na suala la ulinzi na usalama wa nchi. Yaani hao wanajeshi wachangie ground up approach katika kuandaa policy hiyo. Wakifanya hivyo ni somehow itawafanya wawe at ease kujua hawa sio vibaraka wa UK/USA kama vile MDC wanavyokuwa perceived kule Zimbabwe. Naamini hilo halitashindikana kama likiandaliwa na kutekelezwa strategically na professionally. Kila kitu kinawezekana hali mradi na jinsi unatengeneza approach yako.

NB: Hiyo strategy inabidi ipo applicable kwenye security organs zote. Polisi na TISS naona ndio rahis zaidi kuliko jeshini.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom