Jumuiya ya wazazi (CCM)Kilimanjaro yapigwa pini, ni kuhusu ujenzi wa bwalo la chakula Kibo Sekondari

Jun 20, 2023
62
73
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kupitia ofisi ya Udhibiti wa uborq wa shule Manispaa ya Moshi ,imeagiza kusitishwa mara moja ujenzi wa bwalo la chakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kibo.

Hatua hii inakuja kufuatia malalamiko ya wazazi/walezi wa wanafunzi wa shule ya Msingi Kiboshant kudai kukosa eneo la maegesho ya Magari wakati wa kuwapeleka na kuwarudisha watoto wao nyumbani.

Hivi karibuni Jumuiya hiyo ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro iliingia kwenye mgogoro na mwekezaji Community Project Promotion wanaoendesha shule ya msingi ya Kiboshant kufuatia hatua yake ya kuanzisha ujenzi wa bwalo la chakula kwenye eneo la maegesho ya Magari ya wazazi.

Maagizo hayo yako kwenye barua ya Apirl 12 Mwaka huu kutoka ofisi ya Udhibiti ubora wa shule Manispaa ya Moshi kwenda mdhibiti Mkuu wa shule Kanda ya kaskazini mashariki (nakala tunayo)

TAARIFA YA UFUATILIAJI WA MGOGO MGOGORO KATIKA SHULE YA KIBO SEKONDARI NA KIBOSHANT.

1.1 UTANGULIZI.
Ofisi ya Udhibiti Ubora wa shule Manispaa ya Moshi ilifanya ufuatiliaji wa malalamiko yaliyowasilishwa na wazazi kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao kuhusu ujenzi unaoendelea Katika eneo la jumuiya ya wazazi Kilimanjaro lenye shule ya Kibo Selondari inayoendeshwa na St.Thomas Aquinas na Kiboshant inayoendeshwa na wawekezaji Community Polroject Promotion zilizopo Kata ya Longuo ,Ufuatiliaji huu umefanyika 9/4/2024.

1.2 CHANZO CHA MGOGORO.
Malalamiko ya mgogoro yametokana na ujenzi wa bwalo la Kibo Selondari katika mpaka wa shule ya Kiboshant ambapo utasababisha mwingiliano wa sauti Katika ufundishaji na ujifunzaji kwa shule ya Kiboshant.

1 .3 HADIDU ZA REJEA....... ........ ..

1.4. MBINU ZILIZOTUMIKA..................

1.5 MATOKEO YA UFUATILIAJI.
1. Tulibaini hakuna mikataba Kati mmiliki wa eneo na wawekezaji wa shule zote mbili ni makubaliano tu lakini hakuna mkataba rasmi ulio katika maandishi (written document(.

2. Tulijionea ujenzi ukiendelea na nguzo zilijengwa kama mpaka kati ya shule ya sekondari Kibo na shule ya msingi Kiboshant hali iliyozua taharuki kwa wazazi/walezi wa shule ya msingi Kiboshant kushindwa kupata eneo la kupaki Magari yao wanapowafuata wanafunzi na kuwachukua na kusema ujenzi unaoendelea utakuwa karibu na madarasa ya shule ya msingi hivyo kuhofia kutokusikilizana pale wanafunzi watakapokuwa madarasani ,ukaribu huo sio salama kwa wanafunzi hao .

3 Wanafunzi ni wadogo kuchangamana na wanafunzi wa kidato cha V & VI sio salama.

1.6 MAONI NA MAPENDEKEZO.

Mmiliki wa eneo(jumuiya)anashauriwa kusitisha ujenzi wa bwalo na kujenga eneo jingine kwani ana eneo kubwa la kutosha (zaidi ya ekari kumi) ili kuepusha muingiliano wa shughuli za pande zote mbili na kuwepo utulivu wakati wa ujifunzaji na ufundishaji.

Wawekezaji wa Kiboshant waslmeshauriwa kuwa na geti lao na eneo lao la kupaki Magari ili kuepusha mgogoro baina ya pande zote mbili .
Mmiliki wa eneo anaagizwa kujenga ukuta ili kutenganisha shule ya sekondari na msingi kuepusha muingiliano .

Mwekezaji wa Kibo sekondari alishauriwa kufuata taratibu za usajili wa shule kwani anawafunzi wa masomo ya ziada kwa maandalizi ya kidato cha Tano bila kibali cha kulaza wanafunzi hao kutoka kwa mamishina wa Elimu .

Mmiliki wa Kibo sekondari anapaswa kuomba kibali cha kubadilisha meneja kwani kwa Sasa meneja ni St.Thomas Aquinas ambaye ni meneja/mwekezaji mpya.
 
Kuvuja kwa ripoti ya uchunguzi juu ya mgogoro kati ya shule ya sekondari ya Kibo na shule ya msingi ya Kiboshant uliofanywa na ofisi ya mdhibiti ubora wa shule Manispaa ya Moshi ,kumewaweka matatani maofisa wa ofisi hiyo..

Hii inatokana na kuchapishwa kwa Taarifa hiyo kwenye Jukwaa hili jumapili April 28 Mwaka huu ambako ofisi hiyo baada ya uchunguzi wake ikaja na maoni pamoja na MAPENDEKEZO ya kumaliza mgogoro huo unaozihusu shule hizo ambazo zinaendeshwa na wawekeza wawili tofauti .

Shule ya Kibo sekondari inaendeshwa na mwekezaji St Thomas Aquinas wakati shule ya msingi Kiboshant inaendeshwa na wawekezaji Community Project Promotion.
Mgagoro huo unatokana na hatua ya Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (ccm)mkoa wa Kilimanjaro ambao ndiyo wamiliki wa shule hizo kuanza ujenzi wa bwalo la chakula kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari na kuziba kabisa eneo la maegesho ya Magari kwa ajili ya wazazi wa shule ya msingi na kuzua malalamiko kutoka kwa wazazi/walezi wa wanafunzi hao

Baada ya taarifa hiyo kuchapishwa na kusambaa kwenye mitandao ya Kijamii ,baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo wameanza kutishwa na kutakiwa kuandika maelezo kwa nini ripoti hiyo imevuja..

Mmoja wa watumishi hao (jina tunalo)amesema kuwa habari hizo zimewaweka kwenye wakati mgumu sana kwani wameanza kufuatiliwa na kutakiwa kuandika maelezo..

"Umesababisha taharuki kwa ofisi hasa tulioandika taarifa nakuomba tu uitoe JF maana tumeanza kufuatiliwa na kutakiwa kuandika maelezo".

"Ujue umetuharibia sana na ujue umetuweka kwenye wakati mgumu "amesema mtumishi huyo bila kufafanua zaidi.

Kwa faida ya wasomaji wetu na Kwa wale ambao pengine hawakuweza kuiona na kuisoma naomba kuirejea ili mtoe maoni yenu kama ilistahili kuondolewa ama la..

Lakini swali ni je taarifa hiyo ni sahihi au si sahihi na kama ni sahihi walitaka kificha nini na Kwa faida ya nani?
Naomba kuwasilisha.

HII HAPO CHINI ISOME

Back
Top Bottom