Jumuiya ya Waswahili Kariakoo wampa onyo Makinda na wenzake

Lakini wana JAMII FORUM isije msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.

Unaposema huyu mama anafuata nyayo za Baba yakeMwalimu Nyerere una maana gani? haya ni matusi makubwa na nadhani kuna haja ya wewe kuwaomba wana JF msamaha..


 
Mimi sioni kosa la Anna Makinda, kwa sababu ushaidi upo, vibaka wote wapo kariakoo, watu wa porojo wasio na kazi za kufanya wapo kariakoo, nyumba mbovu na duni zipo kariakoo, mashoga wapo kariakoo.
Sasa aombe radhi ya nini? au kwa sababu ni mkristo? mbona ikulu kule kuna wavuta bange wa kumwaga tu kwenye eneo la feri ambapo ni opposite na makao ya Rais?
Nasisitiza Spika ni mtu mkubwa hawezi kushinikizwa na kikundi cha wanywa kahawa kama huyu alieleta mada hii.
 
nampongeza mh.spika kwa kuwadiss hawa wanacarrier corps,waliipigia kura nyingi sana ccm wakati wa uchaguzi..na bado
 
Ni kiashiria kuwa hafai kuwa kiongozi.heshima na nidhamu haipimwi kwa kuomba msamaha ila mwenye heshima na nidhamu anajizuia kufanya makosa ambayo yatamtaka aombe samahamani.maneno kama haya hatukuyaona wakati wa uongozi wa Mr. 6
 
Mimi sioni kosa la Anna Makinda, kwa sababu ushaidi upo, vibaka wote wapo kariakoo, watu wa porojo wasio na kazi za kufanya wapo kariakoo, nyumba mbovu na duni zipo kariakoo, mashoga wapo kariakoo.
Sasa aombe radhi ya nini? au kwa sababu ni mkristo? mbona ikulu kule kuna wavuta bange wa kumwaga tu kwenye eneo la feri ambapo ni opposite na makao ya Rais?
Nasisitiza Spika ni mtu mkubwa hawezi kushinikizwa na kikundi cha wanywa kahawa kama huyu alieleta mada hii.
Mkuu samahani ningerudisha matusi mazito lakini hapa sii mahala pake. Nyie wepesi sana kutukana watu lakini dhahiri matendo yenu ndio yale Yesu alisema anajiona msafi awe wa kwanza kurusha jiwe..
Kwa uhakika hukuyajua yote haya uloyasema pasipo wewe mwenyewe kuwa mshiriki..
 
Ni kiashiria kuwa hafai kuwa kiongozi.heshima na nidhamu haipimwi kwa kuomba msamaha ila mwenye heshima na nidhamu anajizuia kufanya makosa ambayo yatamtaka aombe samahamani.maneno kama haya hatukuyaona wakati wa uongozi wa Mr. 6

Nasisitiza sioni kosa la spika alichozungumza ndio ukweli wenyewe. anaetaka kuthibisha ukweli huu basi aende sokoni kariakoo, alafu atapata jibu.
 
Lakini wana JAMII FORUM isije msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.

Unaposema huyu mama anafuata nyayo za Baba yakeMwalimu Nyerere una maana gani? haya ni matusi makubwa na nadhani kuna haja ya wewe kuwaomba wana JF msamaha..




Nyerere aliwadharau alafu akaruhusu Soko la kariako lijengwe hapo. Ebu jaribu kuonyesha busara zako katika kuandika. Mi nadhani kauli yake sio nzur lakini mnaikuza na kufanya exagaration out of proportion. Mbona tunawaita watu "wamachinga"

Jamani mbona watu wengine kama wanakuwa sawa a huyo A na makinda. Hili neno sio sahihi lakini siyo la ajabu sana kiasi hicho.
 
Lakini wana JAMII FORUM isije msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.

Unaposema huyu mama anafuata nyayo za Baba yakeMwalimu Nyerere una maana gani? haya ni matusi makubwa na nadhani kuna haja ya wewe kuwaomba wana JF msamaha..



Mkuu, watu utawajua kwa maneno yatokayo midomoni mwao.

Swala lilikuwa dogo tu la kumwambia aombe radhi!!
Sasa matokeo yake hadi mitaa ya kariakoo na nyumba za akina Sykes zimeingizwa kwenye ugomvi.

Kuna mambo ya kitaifa yanapitishwa bungeni kwa hoja za mdioooo!! lakini hakuna anayekuja kusema kama Sykes and Co wangekuwepo leo na kuona hili!!!
Yani watu wanaona hoja ni majina ya mitaa tu!!! na historia ambayo hainipunguzii bei ya gas wala petrol!!
Wakati mwingine unaweza ukatukana mtu!
 
Mimi nadhan mama spika alimanisha kariakoo kwa maana ya soko, harakati zinazofanyika sokoni, kelele zile, labda angetumia neno msiwe kama watu wa sokoni pengine kusingekuwa na malumbano yote haya, lakini yote kwa yote sioni kosa kubwa kihivyo mpaka watu wanatuletea stori ndefu na kejeli nyingi kwa spika pamoja na baba wa taifa.
 
Mkuu matusi uliyoandika ni mengi sana yaani kwa maneno msiwe kama watu wa kariakoo ndo yanakutoka yote hayo kweli?

Basi kama kariakoo ndo mko hivyo basi mama hajakosea na hatutaki wabunge wenye maneno mengi yasiokuwa na maana na matusi mengi kama nyie.
 
Mtoa maada inaoneka ni fundi wa kuchanganya uongo na ukweli ili kudanganya watu.
Hoja imepoteza maana na ndio sababu kaandika mineno miingi kuficha tabia yake ya unafiki na uzushi!
 
dar-es-salaam-tanzania-inside-the-kariakoo-market.jpg
Katika hali isiyo ya kawaida Jumuiya ya wa Swahili Tanzania imemjia juu Spika Anne Makinda juu ya kauli yake ya kuwakebehi watu wa Kariakoo ambako wengi wao wana asili ya Kiswahili.Tamko rasmi la Jumuiya ya waswahili limekuja baada ya kauli ya makinda iliyojaa dharau na kebehi kwa wabunge kuwa wasiwe kama watu wa Kariakoo. Klabu ya Saigon nayo imesema itatoa tamko lao rasmi kesho juu ya haya matamshi machafu na ya dharau ya spika Anna Makinda.Anne Makinda labda alitakiwa kurudi darasani na akapigwe brash kuhusu umuhimu wa Kariakoo na watu waliowahi kuishi kariakoo na Makinda should know better than most kuwa hicho chama kilichomweka kwenye hicho kiti alichokalia kilizaliwa Kariakoo na na kusema ukweli ni kuwa dharau aliyoitoa Anna Makinda kwa kariakoo itakuwa si kwa wafanya bishara ndogo ndogo walipo pale bali ni pamoja na waswahili wengine kama akina Mwinjuma Mwinyikambi, Kiyate Mshume, Jumbe Tambaza, Sheikh Hassan bin Amir and Sheikh Suleiman Takadir ambao walikuwa ni wakaazi wa Kariakoo.Labda Makinda angeongea na wenzie wakampeleka maeneo ya makuu 4 yaliyoifanya kariakoo : 1.Kariakoo 2.Gerezani 3.Kisutu 4.Mission Quarter. Spika Anna angejua watu wa Katiakoo wameshiri vipi kwenye kwenye uhuru wa nchi hii asingeweza kuwatukana wabunge kwa dharau kama alivyofanya leo. Najua Makinda hawezi kumwomba ZUNGU au wabunge wengine wa Dar lakini sitoshangaa kuwa huyu mama akawa hajui hata hiyo TAA ilikuwa na makao makuu wapi na sacrifice zipi mzee Bin Sudi aliziingia kutoa lile jengo mwaka 1930!Anna kama ulijuwa hujui basi ujue kuwa jengo hili ndio TANU ilizaliwa na mpaka leo lipo pale mtaa wa kariakoo na Mtaa Mpya ulipoungana Kama ulikuwa hujui basi upande wa Magharibi wa Kariakoondiko ilikokuwa Mission Quarter (NYUMA YA TBL) na eneo hili lilitengwa maalim kwa ajili ya kuwalinda wahamiaji na waswahili waliokuwa wengi kariakoo na ambao waliishhi kwa amani na utulivu kwa miaka zaidi ya 70 mpaka leo hii ambako Pspika wa Bunge unatoa kauli zenye nia ya kuvunja amani na utulivu baina ya watu wa kariakoo Kwa kuonyesha kuwa Waswahili wa Kariakoo walikuwa hawana kinyongo ndio maana majina ya mitaa imebaki vile vile kama vile mtaa wa Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda, Muheza , Magila na sasa hivi mmetuletea jina la mpuuzi wenu yule (MAKAMBA) na mkampa mtaa jina ili hali hana lolote la maana linalomsabahisha na Kariakoo (when time will come TUTALIONDOA)Lakini wana JAMII FORUM msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.Watu wengine maarudu ambao walikuwa ni wana Kariakoo walikuwa wakazi wa MISSION QUATER ni babu yangu bwana THOMAS PLANTAN ambaye alikuwa ni rais wa African Association na al Marhum mzee JOHN RUPIA ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana enzi zile.Anna Makinda kama hujui basi kwa taarifa yako tuu ni kuwa nyumba ya Al Marhum John Rupia ilikuwa mtaa wa Likoma na Magila, nyumba hii mpaka leo ipo na ndiko African Association ilianzishwa mwaka 1929. Nyumba hii mpaka leo ipo japi si katika hali yake ya zamani.Lakini pia nataka nikujulishe kuwa Mission Quarter ndiko kulikokuwepo kiwanda cha kuchapisha cha mwafrica wa kwanza ambacho kilikuwa cha mzee wangu MASHADO PLANTAN ambaye alikuwa ni mtu wa kusini na alikuwa anachapisha JAMII FORUM ya enzi hizo ilikuwa ikiitwa ZUHURA ambayo Nyerere alikuwa analitumia sana kupiga debe dhidi ya wakoloni!Lakini yote hayo Makinda kwako unaona ni upuuzi tuu kwani kariakoo pia ina eneo linaitwa GEREZANI ambako ilikuwa ni nyumbani kwa Omari Londo, Ally Sykes, Zuberi Mtemvu, Mashado Plantan, Muhsin Mende and Dossa Aziz. Hawa walikuwa ni majabali na wazalendo waliokutana na Nyerere baadae. Kwa kuonyesha tuu kuwa sisi si wafuata bendera, ZUBERI MTEMVU, MUHSIN MENDE na MASHADO PLANTAN waliamua kujiondoa TANU na kuanzisha chama kingine cha upinzani kwa jina la TANGNYIKA AFRICAN CONGRESS na hapo ndiko zilianza tofauti kubwa na baba yako Nyerere.Anna makinda unaposema waBunge wasiwe kama watu wa kariakoo unamaana hutaki wawe INDEPENDENT THINKERS kama akina Mzee Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faizi, Idd Tosiri, Bantu Kasella Bantu, Abdulwahid Sykes and Dossa Aziz?Kwa kuendelea kukuambia tuu umuhimu wa kariakoo ni kuwa ile open space inayotazamana na viwanja vya Mnazi Mmoja ilikuwa ni plot ya JOHN RUPIA ambayo aliitoa kama zawadi kwa TANU ili wajenge ile centre. Of course kwa sababu ya serikali yako ilivyokuwa haithamini historia na heritage ili nyumba ilivynjwa wamejenga gorofa pale bila kuzingatia au kuweka kumbukumbu yoyote ile, na huyo baba yenu Nyeree mnaye sema kuwa mnahifadhi ujumbe wake historia kaye nyingi iliyokuwa mle ndani iliishia kutupwa bila mazingatio yoyote yale ya kuhifadhi yaliyokuwa mle.Sehemu nyingine ambayo leo hii umeitukana ni Soko la kariakoo ambalo Nyerere alikuwa haishi kwenda pale....bila kusahau kuwa hata shirika la masoko kariakoo lilikuwa linatoa SCHOLARSHIP kuwasomesha watu mpaka University of Dar.Leo Hii spika wa Bunge umeamua kuwatukana :WASHOMVI ambao walikuwa wanafanya baishara ya samakiWAZARAMO ambao walikuwa wanafanya baishara ya naziWANYAMWEZI (wanawake) ambao walikuwa wanafanya baishara ya tumbaku kavu huku wanaume wakifanya biashara ya viazi ziliskukuwa zinalimwa KigamboniWALUGURU walikuwa wanafanya biashara za machungwa na mboga za majani WAARABU walikukuwa wanafanya biashara ya ngano, mabucha ya nyama, na viungo mbali mbaliWAHINDI walikuwa wanashindana sana na WAARABU kwenye biashara mbali mbaliJe Anna Makinda unajua kama Nyerere aliwahi kufanya kazi soko la kariakoo kama Market Master? Je unajua kama ofisi yake ilikuwa kwenye junction ya mtaa wa Tandamti ( siku hizi mnauita mtaa wa Mshume Kiyate) na mtaa wa Swahili?Matusi uliyowatukana wana Kariakoo leo ni matusi ambayo umewatukana wa Swahili wa Mwembe Togwa (siku hizi mnapaita Fire), Umewatukana wakari wa Ronald Cameroon Road ( sikuhizi United Nations Road) na wengineo wengi...lakini wansiasa wenye calibre za wewe Anna Makinda ndio hao hao mlioamua kuquestion maamuzi ya mzee Kitwana Kondo alipokuwa meya mwaka 1995 alipoa mua kubadili jina la mtaa wa Tandamti na kuita mtaa wa Mshume Kiyate ...tena mlipiga makelele mkisaidiwa na waandishi wa habari ambao hawaijui historia ya kariakoo kwa kuuliza huyu Mshume Kiyate ni nani? Nyie nyie ndio mlilalamika mitaa mingine ya kariakoo ilipobadilishwa na kupewa majina ya Tatu Binti Mzee, Max Mbwana, Omari Londo halafu leo hii unathubutu kututukana sisi wana Kariakoo!Onyo kwa Anna Makinda na wanasiasa wenye tabia za kudharau watu wa kariakoo kama Cyrill Chami na wengineo, Wana Kariakoo na Waswahili wa zama hizi hatutonyamaza kwani vyombo vya kulalama tunavyo na haki zetu tunazijua na mkiendelea na dharau zenu basi mjue kuwa pamoja kuwa waswahili hatutonyamaza na kama ikiwezekana tujibu mapigo basi tutaangalia namna bora zaidi za kuwajibu lakini hatutokaa kimya...maana leo mmeanza na waswahili na watu wa kariakoo kesho tunajua mtahamia kwa wa chagga na watu wa Moshi kesho kutwa mtahamia kwa nyakyusa na watu wa Mbeya na IringaTofauti ni kuwa sasa tumelimika na tunaouwezo wa kuona mnapoanza kutuletea dharau bila kujali wakazi na watu wa kariakoo nao ni wapiga kura kama watu wa kwenu
Uache tabia za shetani, kujifanya malaika! Ilhali umejaa hila ovu ktk hoja yako.
 
Kitendo cha huyu mama kukubali kuwekwa kwa interest za watu fulani nilijua tu japo amekubali lakini kazi haiwezi na virtually amejipunguzia miaka kadhaa ya kuishi bila yeye kujijua ...yaani kama angetakiwa kuishi miaka 20 kabla ya kuwa supika basi ni wazi kwamba baada ya usupika wa kuchongewa ataishi 11 hivi au 10, bila kuwa na adui phisically....
 
dar-es-salaam-tanzania-inside-the-kariakoo-market.jpg



Matusi uliyowatukana wana Kariakoo leo ni matusi ambayo umewatukana wa Swahili wa Mwembe Togwa (siku hizi mnapaita Fire), Umewatukana wakari wa Ronald Cameroon Road ( sikuhizi United Nations Road) na wengineo wengi...lakini wansiasa wenye calibre za wewe Anna Makinda ndio hao hao mlioamua kuquestion maamuzi ya mzee Kitwana Kondo alipokuwa meya mwaka 1995 alipoa mua kubadili jina la mtaa wa Tandamti na kuita mtaa wa Mshume Kiyate ...tena mlipiga makelele mkisaidiwa na waandishi wa habari ambao hawaijui historia ya kariakoo kwa kuuliza huyu Mshume Kiyate ni nani? Nyie nyie ndio mlilalamika mitaa mingine ya kariakoo ilipobadilishwa na kupewa majina ya Tatu Binti Mzee, Max Mbwana, Omari Londo halafu leo hii unathubutu kututukana sisi wana Kariakoo!

Onyo kwa Anna Makinda na wanasiasa wenye tabia za kudharau watu wa kariakoo kama Cyrill Chami na wengineo, Wana Kariakoo na Waswahili wa zama hizi hatutonyamaza kwani vyombo vya kulalama tunavyo na haki zetu tunazijua na mkiendelea na dharau zenu basi mjue kuwa pamoja kuwa waswahili hatutonyamaza na kama ikiwezekana tujibu mapigo basi tutaangalia namna bora zaidi za kuwajibu lakini hatutokaa kimya...maana leo mmeanza na waswahili na watu wa kariakoo kesho tunajua mtahamia kwa wa chagga na watu wa Moshi kesho kutwa mtahamia kwa nyakyusa na watu wa Mbeya na Iringa

Tofauti ni kuwa sasa tumelimika na tunaouwezo wa kuona mnapoanza kutuletea dharau bila kujali wakazi na watu wa kariakoo nao ni wapiga kura kama watu wa kwenu

Duh!

kaka japo si kila mtu atafurahia post yako kwani issue yenyewe imegusa senstivities za watu.

lakini more importantly umeleta issues za heritage na history na kama mwanakariakoo na kama mswahili naona you had to put your points across

je Cyrill Chami anahusika vipi au naye keshawahi kuwatukana watu wa Kariakoo?
 
Huku Makinda juzi juzi kaziba barabara watu wa kawaida wasipite

she doesn't care about anyone let alone hao waswahili wa Kariakoo

lakini nimefurahi mwandishi kuleta historia ya kariakoo ambayo imeelezea kuwa kariakoo si kwa watu washenzi na wahuni na wasio na akili kama ambavyo Spika amejaribu kuwafanya wabunge

Regardless of political allegiance, its not ana excuse kutukana wananchi ambao wanalipa kodi na kosa lao ni kuishi kariakoo

shows how out of touch wanasiasa wetu walivyo
 
Lakini wana JAMII FORUM isije msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.

Unaposema huyu mama anafuata nyayo za Baba yakeMwalimu Nyerere una maana gani? haya ni matusi makubwa na nadhani kuna haja ya wewe kuwaomba wana JF msamaha..



Umenena vema Mkandara.

Kwanza kabisa huyu mwanzisha mada ametaka kulikuza sana hili jambo! Spika hakuwatukana watu wa kariakoo hata kidogo!
Kwamba watu wasifanye kama wako kariakoo, ni msemo tu. Nani asiyejua sokoni kulivyo na makele - soko lolote lile lina kelele.Kariakoo ni soko kubwa na kelele zake zinajulikana.Sasa huyu anayeleta hii mada kutaka kugombanisha watu kwa UDINI na UKABILA sidhani ni muungwana!

JF istumiwe vibaya kuzalisha chuki miongoni mwa watu.ACHENI HIZO TAFUTENI JINGINE MAANA KARIBUNI MMEJITAHIDI SANA KUWAVUNJIA HESHIMA VIONGOZI NA HASA WALIOTANGULIA KAMA MWALIMU NYERERE N.K. KWANI MKISHACHONGANISHA WANANCHI NA KUCHOCHEA CHUKI MTAFAIDIKA NINI?
 
Mkuu samahani ningerudisha matusi mazito lakini hapa sii mahala pake. Nyie wepesi sana kutukana watu lakini dhahiri matendo yenu ndio yale Yesu alisema anajiona msafi awe wa kwanza kurusha jiwe..
Kwa uhakika hukuyajua yote haya uloyasema pasipo wewe mwenyewe kuwa mshiriki..

Mkuu usije na majibu ya rejareja, nilichotukana mimi hapo ni nini? hayo niliyoyasema sio sehemu ya sifa za kariakoo?
 
Tena huyu mama katukosea vibaya sana. Anashangaza! Khaa, haoni haya wala hajui vibaya!Mengi kayasema Mashado, mimi sina zaidi ila namuandikia barua rasmi huko huko bungeni atuombe radhi.
kumbe wajua kukasirika!sie twalala twasubir mapya yajayo,kuki guruwe tamu bana binadamu iko chungu bana iko sikia nisaah.kwani kakufanya vibaya,mwanzo tu utazoea.malipo n hapa dunian na bado
 
Back
Top Bottom