Daydream
Member
- Oct 26, 2023
- 58
- 328
Nakumbuka mwaka 2012 nilifungua biashara ndogo iliyonipelekea kukodi frem itakayonisaidia kufanya biashara yangu.
Kwakua biashara ilikua bado changa nikaona ngoja niende Kariakoo nikanunue Radio (Subwoofer) ya Tshs 150k.
Nilifanikiwa kununua ile Radio kwa Tshs 150k na nikatoka Kariakoo nakurudi nayo nyumbani salama kabisa.
Nilipofika nyumbani nikasema ngoja niifanyie testing ile Radio nikaona haina shida ila tu kwenye upande wa bass ilikua inanichanganya kidogo jinsi ya kufanya setting.
Baada ya kuona setting ya bass inanichanganya nikaona bora nirudi kule Kariakoo kwenye lile duka nililouziwa wakanielekeze kwakua nilipokua naishi na Kariakoo sio mbali sana ni kama dakika 30 kwa daladala.
Nilifika dukani wakanifanyia testing na kunielekeza jinsi ya kuongeza au kupunguza bass ingawa uongezaji wake na upunguzaji ulikua complicated kidogo.
Baada kumaliza testing walinifungia tena kwenye boksi nikaiweka begani ili nielekee kituoni.
Kwakua nilikua nimechoka na ule mzunguko wa nenda rudi kimoyomoyo nikasama nikiona kijana anaebeba mzigo basi nitamlipa ili anibebee hadi stand ya daladala.
Nilipomaliza tu kushuka zile ngazi za duka akatokea kijana mmoja akanambia broh lete nikubee unipoze kidogo, nikamuuliza bei gani akanambia Tshs 300.Nikaona sio mbaya kwani nikimpatia hiyo Tshs 300 nitakua nimepungukiwa nini.
Balaa likaanza nilivyomtwika tu ule mzigo tukaanza kutembea kuelekea kituo cha daladala cha Msimbazi.
Nadhani hakuna asiejua msongamo wa eneo lile la Kariakoo, watu ni wengi sana na kama mko wawili ukijichanganya kidogotu ujue mnapotezana.
Wakati tunatembea kuelekea kituo cha daladala na yule kijana mimi nilikua nyuma yeye mbele na lengo la kukaa nyuma yake ni ili asinipotee machoni (close monitoring) mana simjui.
Wakati tumeongozana akajifanya kama amesimama kidogo kupisha watu sasa mimi nikawa kama hatua tatu mbele yake, ile nageuka tu nyuma sioni mtu aliebeba boksi.
Nikajaribu kutupia jicho kona zote sikumuona na baada ya kama dakika 10 nikakubali tu matokeo kwamba nimeibiwa
Unaweza kujiuliza kwanini nilienda tena Kariakoo ili wakanielekeze jinsi ya kufanya setting ya bass wakati kwenye boksi kulikua na User Manual
Kwakua nilikua na mambo mengi kichwani nikaona kukaa kusoma User Manual itanipotezea tu muda mana nilihisi huenda ile Radio ina shida ndio maana nilifunga tena safari hadi Kariakoo.
Nilikua nasikia tu kwamba Kariakoo watu wanaibiwa sana na siku hiyo ndo ilikua mara yangu ya kwanza kuibiwa eneo lile.
Hakuna sehemu naiheshimu kama Kariakoo na mpaka leo nikienda eneo lile basi nachukua tahadhari kubwa sana, watu wanaibiwa sana.
Je wewe mdau wa JF uliwahi kutapeliwa na ilikua kwa namna gani ?
Karibu