Jumuiya ya Waswahili Kariakoo wampa onyo Makinda na wenzake

Umenena vema Mkandara.

Kwanza kabisa huyu mwanzisha mada ametaka kulikuza sana hili jambo! Spika hakuwatukana watu wa kariakoo hata kidogo!
Kwamba watu wasifanye kama wako kariakoo, ni msemo tu. Nani asiyejua sokoni kulivyo na makele - soko lolote lile lina kelele.Kariakoo ni soko kubwa na kelele zake zinajulikana.Sasa huyu anayeleta hii mada kutaka kugombanisha watu kwa UDINI na UKABILA sidhani ni muungwana.

JF istumiwe vibaya kuzalisha chuki miongoni mwa watu.ACHENI HIZO TAFUTENI JINGINE MAANA KARIBUNI MMEJITAHIDI SANA KUWAVUNJIA HESHIMA VIONGOZI NA HASA WALIOTANGULIA KAMA MWALIMU NYERERE N.K. KWANI MKISHACHONGANISHA WANANCHI NA KUCHOCHEA CHUKI MTAFAIDIKA NINI?

Kinachompoza madam spika ni hili jina la ANNA, lakini angekuwa anaitwa Sikuzani au sikitu au Mwazani au Sikujuwa, porojo za hawa waswahili usingezisikia. Ndio maana Ditopile ndio binadamu wa kwanza Tanzania hii kupewa dhamana na mahakama zetu huku akiwa na kesi ya mauwaji.
 
Kwa sababu wengi wao ni waislamu wao ni cuf na ccm tu. Waache watukanwe mpaka kwenye misuli.
Mkuu, tunashukuru sana kwa kutujuza tulikuwa hatufahamu, kumbe Chadema ni chama cha Wakiristo
 
Leo nimeona humu kwa mara ya kwanza MAGWANDA kamsifia MAGAMBA. siasa za bongo bwana
 
Cant blame the man for expressing his opinion

I might not agree with him but he is entitled to have some

That said, I think Makinda like most of our politicians has a tendency of looking down on people...the difference ni kuwa sasa watu wanayo platform ya kulalamika
 
Cant blame the man for expressing his opinion

I might not agree with him but he is entitled to have some

That said, I think Makinda like most of our politicians has a tendency of looking down on people...the difference ni kuwa sasa watu wanayo platform ya kulalamika

Granted that the man who started the thread is entitled to his opinion, then Madam Speaker is equally entitled to express her self the way she did.

I wouldnt like to believe that the Speaker intended to belittle Kariakoo people but rather she was trying to bring a point home as regards how the august house should be. The House is almost turning into a market place - Kariakoo!..Nani anabisha kuwa "Kariakoo" kwa watu wengi siyo sokoni?Wengi hawaangalii kuwa Kariakoo ni zaidi ya soko.
 
aliyeanza kudharau watu wa kariakoo ni mkuu wa operesheni wa polisi...kamishna paul chagonja.....alipokuwa akielezea kukamatwa kwa mbowe....alisema ..."mbowe kama kiongozi mkuu wa upinzani anatakiwa kuwa na busara na sio kufanya kama watu wa kariakoo""".....nafikiri viongozi wetu wanapoteza muelekeo
 
mashado we ni kiboko. nimejifunza mengi kutoka hii historia fupi, lakini makini.....thanks.
am not sure kama ukimuuliza meya wa jiji kama anajua yote haya...nitacopy hii story na kuiweka.

mashado- kama una historia zaidi ya kariakoo, na hata jiji zima tafadhali.
many thanks.
 
Tena huyu mama katukosea vibaya sana. Anashangaza! Khaa, haoni haya wala hajui vibaya!

Mengi kayasema Mashado, mimi sina zaidi ila namuandikia barua rasmi huko huko bungeni atuombe radhi.

Haaaah haaah Faiza huyu mama si magamba mwenzako?!
 
mashado we ni kiboko. nimejifunza mengi kutoka hii historia fupi, lakini makini.....thanks.
am not sure kama ukimuuliza meya wa jiji kama anajua yote haya...nitacopy hii story na kuiweka.

mashado- kama una historia zaidi ya kariakoo, na hata jiji zima tafadhali.
many thanks.

Mkuu sio Meya tu hata Mkulu mwenyewe atakua hajui kitu hapa!lada bwagamoyo!
 
Granted that the man who started the thread is entitled to his opinion, then Madam Speaker is equally entitled to express her self the way she did.

I wouldnt like to believe that the Speaker intended to belittle Kariakoo people but rather she was trying to bring a point home as regards how the august house should be. The House is almost turning into a market place - Kariakoo!..Nani anabisha kuwa "Kariakoo" kwa watu wengi siyo sokoni?Wengi hawaangalii kuwa Kariakoo ni zaidi ya soko.

The problem is we have a divide and the real divide in modern Tanzania is no longer between the main political parties (CCM& CHADEMA), but between the Political Class and the rest of WALALAHOI and this means that the Political Class of Makinda et al is not merely separated from the ordinary people … it is actively hostile and Kariakoo isn't just a name being thrown around.

Makinda, Chami and the rest of our political elites live in a sealed world - like NASA astronauts on an alien planet, moving along their airlocked passages between a series of domes such as their wapambes, parliament, govt , media, all within the giant dome of our politics. Furthermore theyve formed a self-admiring, self-promoting coteries.

In this case, Anne Makinda liike all inhabitants of a sealed world, behave very oddly and her latest comments on Kariakoo and its inhabitants says alot about her character as politician in a powerful post such as hers
 
Mbona aliomba msamaha baadaye? Tena alisema hakuwa na lengo la kuwa-offend watu wa kariakoo bali alikuwa anamaanisha wabunge waache kupiga kelele kama zinazopigwa pale sokoni kariakoo.
 
dar-es-salaam-tanzania-inside-the-kariakoo-market.jpg


Katika hali isiyo ya kawaida Jumuiya ya wa Swahili Tanzania imemjia juu Spika Anne Makinda juu ya kauli yake ya kuwakebehi watu wa Kariakoo ambako wengi wao wana asili ya Kiswahili.

Tamko rasmi la Jumuiya ya waswahili limekuja baada ya kauli ya makinda iliyojaa dharau na kebehi kwa wabunge kuwa wasiwe kama watu wa Kariakoo. Klabu ya Saigon nayo imesema itatoa tamko lao rasmi kesho juu ya haya matamshi machafu na ya dharau ya spika Anna Makinda.

Anne Makinda labda alitakiwa kurudi darasani na akapigwe brash kuhusu umuhimu wa Kariakoo na watu waliowahi kuishi kariakoo na Makinda should know better than most kuwa hicho chama kilichomweka kwenye hicho kiti alichokalia kilizaliwa Kariakoo na na kusema ukweli ni kuwa dharau aliyoitoa Anna Makinda kwa kariakoo itakuwa si kwa wafanya bishara ndogo ndogo walipo pale bali ni pamoja na waswahili wengine kama akina Mwinjuma Mwinyikambi, Kiyate Mshume, Jumbe Tambaza, Sheikh Hassan bin Amir and Sheikh Suleiman Takadir ambao walikuwa ni wakaazi wa Kariakoo.

Labda Makinda angeongea na wenzie wakampeleka maeneo ya makuu 4 yaliyoifanya kariakoo :

1.Kariakoo

2.Gerezani

3.Kisutu

4.Mission Quarter.

Spika Anna angejua watu wa Katiakoo wameshiri vipi kwenye kwenye uhuru wa nchi hii asingeweza kuwatukana wabunge kwa dharau kama alivyofanya leo.

Najua Makinda hawezi kumwomba ZUNGU au wabunge wengine wa Dar lakini sitoshangaa kuwa huyu mama akawa hajui hata hiyo TAA ilikuwa na makao makuu wapi na sacrifice zipi mzee Bin Sudi aliziingia kutoa lile jengo mwaka 1930!

Anna kama ulijuwa hujui basi ujue kuwa jengo hili ndio TANU ilizaliwa na mpaka leo lipo pale mtaa wa kariakoo na Mtaa Mpya ulipoungana


Kama ulikuwa hujui basi upande wa Magharibi wa Kariakoondiko ilikokuwa Mission Quarter (NYUMA YA TBL) na eneo hili lilitengwa maalim kwa ajili ya kuwalinda wahamiaji na waswahili waliokuwa wengi kariakoo na ambao waliishhi kwa amani na utulivu kwa miaka zaidi ya 70 mpaka leo hii ambako Pspika wa Bunge unatoa kauli zenye nia ya kuvunja amani na utulivu baina ya watu wa kariakoo

Kwa kuonyesha kuwa Waswahili wa Kariakoo walikuwa hawana kinyongo ndio maana majina ya mitaa imebaki vile vile kama vile mtaa wa Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda, Muheza , Magila na sasa hivi mmetuletea jina la mpuuzi wenu yule (MAKAMBA) na mkampa mtaa jina ili hali hana lolote la maana linalomsabahisha na Kariakoo (when time will come TUTALIONDOA)

Lakini wana JAMII FORUM msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.

Watu wengine maarudu ambao walikuwa ni wana Kariakoo walikuwa wakazi wa MISSION QUATER ni babu yangu bwana THOMAS PLANTAN ambaye alikuwa ni rais wa African Association na al Marhum mzee JOHN RUPIA ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana enzi zile.

Anna Makinda kama hujui basi kwa taarifa yako tuu ni kuwa nyumba ya Al Marhum John Rupia ilikuwa mtaa wa Likoma na Magila, nyumba hii mpaka leo ipo na ndiko African Association ilianzishwa mwaka 1929. Nyumba hii mpaka leo ipo japi si katika hali yake ya zamani.

Lakini pia nataka nikujulishe kuwa Mission Quarter ndiko kulikokuwepo kiwanda cha kuchapisha cha mwafrica wa kwanza ambacho kilikuwa cha mzee wangu MASHADO PLANTAN ambaye alikuwa ni mtu wa kusini na alikuwa anachapisha JAMII FORUM ya enzi hizo ilikuwa ikiitwa ZUHURA ambayo Nyerere alikuwa analitumia sana kupiga debe dhidi ya wakoloni!

Lakini yote hayo Makinda kwako unaona ni upuuzi tuu kwani kariakoo pia ina eneo linaitwa GEREZANI ambako ilikuwa ni nyumbani kwa Omari Londo, Ally Sykes, Zuberi Mtemvu, Mashado Plantan, Muhsin Mende and Dossa Aziz. Hawa walikuwa ni majabali na wazalendo waliokutana na Nyerere baadae. Kwa kuonyesha tuu kuwa sisi si wafuata bendera, ZUBERI MTEMVU, MUHSIN MENDE na MASHADO PLANTAN waliamua kujiondoa TANU na kuanzisha chama kingine cha upinzani kwa jina la TANGNYIKA AFRICAN CONGRESS na hapo ndiko zilianza tofauti kubwa na baba yako Nyerere.

Anna makinda unaposema waBunge wasiwe kama watu wa kariakoo unamaana hutaki wawe INDEPENDENT THINKERS kama akina Mzee Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faizi, Idd Tosiri, Bantu Kasella Bantu, Abdulwahid Sykes and Dossa Aziz?

Kwa kuendelea kukuambia tuu umuhimu wa kariakoo ni kuwa ile open space inayotazamana na viwanja vya Mnazi Mmoja ilikuwa ni plot ya JOHN RUPIA ambayo aliitoa kama zawadi kwa TANU ili wajenge ile centre. Of course kwa sababu ya serikali yako ilivyokuwa haithamini historia na heritage ili nyumba ilivynjwa wamejenga gorofa pale bila kuzingatia au kuweka kumbukumbu yoyote ile, na huyo baba yenu Nyeree mnaye sema kuwa mnahifadhi ujumbe wake historia kaye nyingi iliyokuwa mle ndani iliishia kutupwa bila mazingatio yoyote yale ya kuhifadhi yaliyokuwa mle.

Sehemu nyingine ambayo leo hii umeitukana ni Soko la kariakoo ambalo Nyerere alikuwa haishi kwenda pale....bila kusahau kuwa hata shirika la masoko kariakoo lilikuwa linatoa SCHOLARSHIP kuwasomesha watu mpaka University of Dar.

Leo Hii spika wa Bunge umeamua kuwatukana :

WASHOMVI ambao walikuwa wanafanya baishara ya samaki

WAZARAMO ambao walikuwa wanafanya baishara ya nazi

WANYAMWEZI (wanawake) ambao walikuwa wanafanya baishara ya tumbaku kavu huku wanaume wakifanya biashara ya viazi ziliskukuwa zinalimwa Kigamboni

WALUGURU walikuwa wanafanya biashara za machungwa na mboga za majani

WAARABU walikukuwa wanafanya biashara ya ngano, mabucha ya nyama, na viungo mbali mbali

WAHINDI walikuwa wanashindana sana na WAARABU kwenye biashara mbali mbali


Je Anna Makinda unajua kama Nyerere aliwahi kufanya kazi soko la kariakoo kama Market Master? Je unajua kama ofisi yake ilikuwa kwenye junction ya mtaa wa Tandamti ( siku hizi mnauita mtaa wa Mshume Kiyate) na mtaa wa Swahili?

Matusi uliyowatukana wana Kariakoo leo ni matusi ambayo umewatukana wa Swahili wa Mwembe Togwa (siku hizi mnapaita Fire), Umewatukana wakari wa Ronald Cameroon Road ( sikuhizi United Nations Road) na wengineo wengi...lakini wansiasa wenye calibre za wewe Anna Makinda ndio hao hao mlioamua kuquestion maamuzi ya mzee Kitwana Kondo alipokuwa meya mwaka 1995 alipoa mua kubadili jina la mtaa wa Tandamti na kuita mtaa wa Mshume Kiyate ...tena mlipiga makelele mkisaidiwa na waandishi wa habari ambao hawaijui historia ya kariakoo kwa kuuliza huyu Mshume Kiyate ni nani? Nyie nyie ndio mlilalamika mitaa mingine ya kariakoo ilipobadilishwa na kupewa majina ya Tatu Binti Mzee, Max Mbwana, Omari Londo halafu leo hii unathubutu kututukana sisi wana Kariakoo!

Onyo kwa Anna Makinda na wanasiasa wenye tabia za kudharau watu wa kariakoo kama Cyrill Chami na wengineo, Wana Kariakoo na Waswahili wa zama hizi hatutonyamaza kwani vyombo vya kulalama tunavyo na haki zetu tunazijua na mkiendelea na dharau zenu basi mjue kuwa pamoja kuwa waswahili hatutonyamaza na kama ikiwezekana tujibu mapigo basi tutaangalia namna bora zaidi za kuwajibu lakini hatutokaa kimya...maana leo mmeanza na waswahili na watu wa kariakoo kesho tunajua mtahamia kwa wa chagga na watu wa Moshi kesho kutwa mtahamia kwa nyakyusa na watu wa Mbeya na Iringa

Tofauti ni kuwa sasa tumelimika na tunaouwezo wa kuona mnapoanza kutuletea dharau bila kujali wakazi na watu wa kariakoo nao ni wapiga kura kama watu wa kwenu


Sijui kama humu hawa Wahindi na Waarabu wanakubalika katika kuheshimika kama wananchi halisi, kutokana na maelezo ya mara nyingi humu nahisi mushkeli.
 
dar-es-salaam-tanzania-inside-the-kariakoo-market.jpg



Kama kwa picha iliyopostiwa ndio reflection ya jamii ya waswahili, basi ni heri Mama Makinda wala asithubutu kuomba radhi.
Yaani mnataka Bunge liwe na marap rap ya kiswahili kama hayo?
kuwa mstaarabu,mbona kijijini kwenu wanaishi maisha mabaya kuliko hao jamaa hapo. hivi unajua kuwa kijijini kwenu wanajua kuwa nyerere bado hajafa?
cool down man acha dharau yule bi kidude aliteleza kweli
 
Tena huyu mama katukosea vibaya sana. Anashangaza! Khaa, haoni haya wala hajui vibaya!

Mengi kayasema Mashado, mimi sina zaidi ila namuandikia barua rasmi huko huko bungeni atuombe radhi.

Tuuuu!
Dada siamini macho yangu kuwa leo unampinga mtu wa magamba!
 
Tena huyu mama katukosea vibaya sana. Anashangaza! Khaa, haoni haya wala hajui vibaya!

Mengi kayasema Mashado, mimi sina zaidi ila namuandikia barua rasmi huko huko bungeni atuombe radhi.

Mhhhh! sikutegemea hata siku moja uandike chochote hapa jamvini kuipinga kauli ya kingunge yeyote ndani ya chama cha magamba hata kama kauli hiyo haiungwi mkono na Watanzania walio wengi. Si mwanzo mbaya labda si ajabu siku za karibuni tutakusoma pia ukiunga mkono kauli za viongozi wa CHADEMA ambazo zina mashiko au kuungwa mkono na Watanzania walio wengi. Hongera zako FF!
 
Granted that the man who started the thread is entitled to his opinion, then Madam Speaker is equally entitled to express her self the way she did.

I wouldnt like to believe that the Speaker intended to belittle Kariakoo people but rather she was trying to bring a point home as regards how the august house should be. The House is almost turning into a market place - Kariakoo!..Nani anabisha kuwa "Kariakoo" kwa watu wengi siyo sokoni?Wengi hawaangalii kuwa Kariakoo ni zaidi ya soko.

Hapo ndipo tofauti ya lugha iwepo baina ya kiongozi na mtu wa kawaida.

Hata Kama watu wote wanafahamu Kariakoo inamaanisha sokoni, kiongozi hapaswi kutumia assumption hiyo kwa vile kuna watu wana asili na Kariakoo na inaweza kuleta maana mbaya kwao.

Juzi Mkandara aliuliza kwanini wanachadema wanadharau Waislam kwa kutumia neno 'madrasa'...wakati kimsingi 'madrasa' ni neno zuri tu na pia ni character ambayo waislam wanatakuwa kuwa nayo (elimu ya madras)

Kabla ya hapo tuliwahi kujadiliana kuwa ni dharau kuwaita Wahindi 'wadosi' japokuwa dosti linamaana njema.

Kwa hiyo tunatarajia kiongozi asitumie maneno Kama "biashara ya umachinga" na mengineyo kama "anapenda pesa kama Mchagga/Mpemba" na kadhalika
 
dar-es-salaam-tanzania-inside-the-kariakoo-market.jpg



Kama kwa picha iliyopostiwa ndio reflection ya jamii ya waswahili, basi ni heri Mama Makinda wala asithubutu kuomba radhi.
Yaani mnataka Bunge liwe na marap rap ya kiswahili kama hayo?

ukitazama picha..hiyo ndiyo kariakoo anayoidhania spika Makinda lakini kwa mtazamo wa Mashado(nami namuunga mkono), kariakoo ni zaidi ya huo mtazamo finyu wa spika Makinda, na alichokieleza Mashado ndiyo maana pana ya kariakoo.

Asante sana Mashado....bahati mbaya sana kwa nchi yetu, historia ni kitu cha kupuuzwa(si unaona hata ile sikukuu ya mashujaa walishaifuta!)

Kwa spika Makinda ni aibu kwake kuongea bila kufikiri au kwa lugha ya sasa kuropoka(ukipenda kukurupuka)...ulitegemea asiwe ni mtu wa hivyo lakini ndiyo chaguo letu, tutafanyaje, vinginevyo tungempinga na sasa asingekuwa pale.

Mi nadhani wakubwa wajifunze kufikiri kabla ya kuongea, zile zama za UMC(msema chochote) zimepita, kila kauli itaangaliwa na kupimwa katika 3D, wengi wataangushwa kwa kauli tu na wakati utathibitisha.

Nawakilisha!
 
Back
Top Bottom