Joyce Kiria ana upeo mdogo kuhusu haki, aache kupotosha jamii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
JOYCE KIRIA ANAUPEO MDOGO KUHUSU HAKI, AACHE KUPOTOSHA JAMII.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Baada ya kuishiwa kifurushi nikajikuta nipo Channel 10, huko nilikutana na mwanamama aitwaye Joyce Kiria ambaye kwa mazungumzo yake ni dhahiri anapotosha jamii.

Joyce Kiria elewa kuwa kwenye nchi hii sheria zetu kwa kiasi kikubwa zinampendelea zaidi Mwanamke kuliko mwanaume. Hasa sheria za Ndoa. Sheria za kifursa na kiuchumi, Mwanamke na mwanaume wapo Sawa kabisa. Kisiasa, Sheria inampa upendeleo zaidi Mwanamke.

Joyce Kiria lazima aelewe kuwa sheria za nchi yetu hazina tatizo lolote kuhusu Haki za Wanawake.
Hakuna sehemu hata moja kwenye sheria zetu zinazomnyima Mwanamke haki ya Kusoma, kufanya kazi, kumiliki Mali, kufanya maisha yake pasipo kuvunja sheria. Hakuna.

Ndio maana wapo Wanawake waliosoma, wanaomiliki mali, wenye vyeo vikubwa hata kabla ya harakati za kutetea hao wanawake hapa nchini. Yaani miaka ya sabini wapo wanawake kibao wenye shahada, wapo madaktari, waalimu, wanasheria, wahasibu n.k.

Suala la ukatili wa kijinsia au ukatili wa aina yoyote lipo kisheria. Sheria zipo na adhabu zipo.
Kumpiga mtu yeyote bila kujali jinsia yake ni kosa kisheria na unaweza kufungwa. Kumchapa mtoto wako uliyemzaa kupitiliza ni kosa kisheria. Mwalimu kumchapa mtoto kinyume na sheria ni kosa kisheria.

Kumtolea maneno machafu mtu iwe kwa kumtukana, kumdhihaki, kumbagaza ni kosa kisheria na adhabu zipo.
Joyce Kiria hujui mambo yote haya? Kwa nini unailaumu serikali wakati sheria tayari zipo? Ishu ni utekelezaji wake unaoathiriwa na wahusika wenyewe.

Ni wanawake wangapi au wanaume wangapi wanafanyiwa ukatili lakini hawaendi kushtaki wanamaliza kifamilia? Sasa hapo kosa nila nani?

Unataka itungwe sheria ya haki Sawa. Hivi hujui sheria ya Haki sawa itamkandiza zaidi Mwanamke kuliko ilivyo sasa ambapo Mwanamke anapendelewa?

Lazima ieleweke kuwa kinachoisumbua jamii yetu ni hulka ya Utegemezi wa wanawake ambapo ndio hupelekea ukandamizaji wa baadhi ya haki zao kwa. Kupenda wenyewe.

Ukiwa tegemezi lazima uhuru wako uwe mashakani. Hilo Joyce Kiria lazima uwape elimu wanaokusikiliza na sio kuipa elimu Serikali ambayo inawatu wenye elimu, vyeo, uzoefu na Exposure mara kumi kukushinda.

Unasema hakuna Haki za wanawake au wanawake wanakandamizwa Ilihali kuna mamilioni ya wanawake ni wasomi, viongozi wa makampuni, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa n.k.

Unasema wanawake wanakandamizwa wakati Rais wa nchi hii ni Mwanamke, Spika ni mwanamke, angalia wapo wabunge na mawaziri ni wanawake. Nenda Muhimbili utakuta Madaktari na wahudumu wa afya wanawake, nenda vyuoni huko ukaone wanawake wenzako wakifanya kazi. Nenda mahakamani, nenda umoja wa mataifa. Hao wamesoma miaka hiyo, miaka ya giza nchi ikiwa changa.

Kila mtu atapewa heshima yake kwa Haki aliyonayo. Iwe ni mwanaume au mwanamke. Kila mtu anaheshimika jinsi inavyostahili.

Wewe kama hukusoma tafuta mwenzako ambaye hajasoma. Mtaheshimiana. Wewe kama huna hela tafuta mwenzako ambaye hana hela mtaheshimiana.

Tatizo lenu Wanawake mnapenda vitu ambavyo sio stahiki zenu. Unakuta mwanaume mwanamke hujaenda shule, umetoka familia duni. Alafu unataka kuolewa kwenye familia zenye hadhi ya juu kukushinda. Hapo lazima moto uwake. Lazima unyanyasaji, ukandamizaji, udhalilishaji na dharau ziwepo.

Wanawake wengi mnapenda sana heshima ambayo hamna kwa kigezo cha sijui kuzaa. Umezaa watoto wako tuu. Hujazaa wengine. Watakaokuheshimu ni wale wanaokustahili. Sio unataka uheshimike kwenye jamii kama kwenye familia yako wakati hauna mchango wowote. Umelogwa nini?

Heshima inakuja na gharama. Heshima inakuja kwa Tija. Kama huna Tija yoyote kwenye jamii Nani akuheshimu Ndugu yangu, labda familia yako kwa sababu huko ndio unatija.

Achaneni na maneno ya kinafikinafiki kuwa sijui heshimu kila mtu. Hiyo haipo. Kinachoheshimiwa ni kile kinachostahili. Chenye tija. Heshima ipo kwenye HAKI.

Joyce Kiria hamasisha Wanawake wasome zaidi na zaidi. Wafanyekazi na kuzalisha mali. Kazi zipo nyingi. Kuwa fundi nguo, kuwa mamantilie, kuwa mfugaji, fanya kazi.

Kulea watoto wako sio kazi ya kutaka heshima kwa Watu wengine. Hao ni watoto wako mjinga wewe. Watu watakupa heshima kwa utumishi wako kwao na sio kwa mambo yako mwenyewe. Kulea watoto utapata heshima kwa hao watoto wako. Watoto ndio watakuheshimu kwa sababu unatija kwao. Na ikiwa hao watoto wakawa na tija kwenye jamii basi jamii itakuheshimu kupitia watoto wako.

Unataka kugawana mali 50/50 na mumeo wakati wewe ulikuwa hauzalishi chochote. Hivi hiyo ni haki ukitazama. Wewe mumeo hafanyi kazi, yupo nyumbani analea watoto alafu atake mgawane mali inakuingia akilini.

Wanawake wapewe ari, mtazamo mpya kuhusu maisha, shauku ya kujitegemea ili wasiteseke wala kunyanyaswa au kunyanyasika.

Kasumba ya Mwanamke kuhudumiwa iondolewe ndani ya jamii. Masuala sijui ya kutolewa mahari yote yaondolewe kwenye jamii kwa sababu hiyo yote ni kumkandamiza na kumnyanyasa Mwanamke. Jambo ambalo Watibeli hilo tulishamalizana nalo zamani sana.

Sio wanawake wanaonyanyasika pekee kwenye jamii zetu. Yapo makundi mengi ikiwemo hata wanaume wapo wanaonyanyasika. Sheria zipo. Sema Watu wetu bado ni waoga mno. Hawawezi kujitetea kwa sababu akili zao ni tegemezi. Mpaka wapate msaada wa mtu mwingine wasiyemjua na asiye na wajibu na maisha yao wenyewe.

Somesha watoto wako alafu uone kama kuna Kima atawafanyia ujingaujinga. Husikii wanaume wengi hawataki kuoa wanawake waliosoma, sababu kubwa ni suala la Haki. Na bahati nzuri kwenye haki kila mmoja ni sawa kwa mwingine ingawaje hawalingani.

Nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
JOYCE KIRIA ANAUPEO MDOGO KUHUSU HAKI, AACHE KUPOTOSHA JAMII.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Baada ya kuishiwa kifurushi nikajikuta nipo Channel 10, huko nilikutana na mwanamama aitwaye Joyce Kiria ambaye kwa mazungumzo yake ni dhahiri anapotosha jamii.

Joyce Kiria elewa kuwa kwenye nchi hii sheria zetu kwa kiasi kikubwa zinampendelea zaidi Mwanamke kuliko mwanaume. Hasa sheria za Ndoa.
Sheria za kifursa na kiuchumi, Mwanamke na mwanaume wapo Sawa kabisa.
Kisiasa, Sheria inampa upendeleo zaidi Mwanamke.

Joyce Kiria lazima aelewe kuwa sheria za nchi yetu hazina tatizo lolote kuhusu Haki za Wanawake.
Hakuna sehemu hata moja kwenye sheria zetu zinazomnyima Mwanamke haki ya Kusoma, kufanya kazi, kumiliki Mali, kufanya maisha yake pasipo kuvunja sheria. Hakuna.

Ndio maana wapo Wanawake waliosoma, wanaomiliki mali, wenye vyeo vikubwa hata kabla ya harakati za kutetea hao wanawake hapa nchini. Yaani miaka ya sabini wapo wanawake kibao wenye shahada, wapo madaktari, waalimu, wanasheria, wahasibu n.k.

Suala la ukatili wa kijinsia au ukatili wa aina yoyote lipo kisheria. Sheria zipo na adhabu zipo.
Kumpiga mtu yeyote bila kujali jinsia yake ni kosa kisheria na unaweza kufungwa.
Kumchapa mtoto wako uliyemzaa kupitiliza ni kosa kisheria. Mwalimu kumchapa mtoto kinyume na sheria ni kosa kisheria.

Kumtolea maneno machafu mtu iwe kwa kumtukana, kumdhihaki, kumbagaza ni kosa kisheria na adhabu zipo.
Joyce Kiria hujui mambo yote haya?
Kwa nini unailaumu serikali wakati sheria tayari zipo? Ishu ni utekelezaji wake unaoathiriwa na wahusika wenyewe.

Ni wanawake wangapi au wanaume wangapi wanafanyiwa ukatili lakini hawaendi kushtaki wanamaliza kifamilia? Sasa hapo kosa nila nani?

Unataka itungwe sheria ya haki Sawa. Hivi hujui sheria ya Haki sawa itamkandiza zaidi Mwanamke kuliko ilivyo sasa ambapo Mwanamke anapendelewa?

Lazima ieleweke kuwa kinachoisumbua jamii yetu ni hulka ya Utegemezi wa wanawake ambapo ndio hupelekea ukandamizaji wa baadhi ya haki zao kwa. Kupenda wenyewe.

Ukiwa tegemezi lazima uhuru wako uwe mashakani. Hilo Joyce Kiria lazima uwape elimu wanaokusikiliza na sio kuipa elimu Serikali ambayo inawatu wenye elimu, vyeo, uzoefu na Exposure mara kumi kukushinda.

Unasema hakuna Haki za wanawake au wanawake wanakandamizwa Ilihali kuna mamilioni ya wanawake ni wasomi, viongozi wa makampuni, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa n.k.

Unasema wanawake wanakandamizwa wakati Rais wa nchi hii ni Mwanamke, Spika ni mwanamke, angalia wapo wabunge na mawaziri ni wanawake. Nenda Muhimbili utakuta Madaktari na wahudumu wa afya wanawake, nenda vyuoni huko ukaone wanawake wenzako wakifanya kazi. Nenda mahakamani, nenda umoja wa mataifa.
Hao wamesoma miaka hiyo, miaka ya giza nchi ikiwa changa.

Kila mtu atapewa heshima yake kwa Haki aliyonayo. Iwe ni mwanaume au mwanamke. Kila mtu anaheshimika jinsi inavyostahili.
Wewe kama hukusoma tafuta mwenzako ambaye hajasoma. Mtaheshimiana. Wewe kama huna hela tafuta mwenzako ambaye hana hela mtaheshimiana.

Tatizo lenu Wanawake mnapenda vitu ambavyo sio stahiki zenu. Unakuta mwanaume mwanamke hujaenda shule, umetoka familia duni. Alafu unataka kuolewa kwenye familia zenye hadhi ya juu kukushinda. Hapo lazima moto uwake. Lazima unyanyasaji, ukandamizaji, udhalilishaji na dharau ziwepo.

Wanawake wengi mnapenda sana heshima ambayo hamna kwa kigezo cha sijui kuzaa. Umezaa watoto wako tuu. Hujazaa wengine. Watakaokuheshimu ni wale wanaokustahili. Sio unataka uheshimike kwenye jamii kama kwenye familia yako wakati hauna mchango wowote. Umelogwa nini?
Heshima inakuja na gharama. Heshima inakuja kwa Tija. Kama huna Tija yoyote kwenye jamii Nani akuheshimu Ndugu yangu, labda familia yako kwa sababu huko ndio unatija.

Achaneni na maneno ya kinafikinafiki kuwa sijui heshimu kila mtu. Hiyo haipo. Kinachoheshimiwa ni kile kinachostahili. Chenye tija. Heshima ipo kwenye HAKI.

Joyce Kiria hamasisha Wanawake wasome zaidi na zaidi. Wafanyekazi na kuzalisha mali. Kazi zipo nyingi. Kuwa fundi nguo, kuwa mamantilie, kuwa mfugaji, fanya kazi.

Kulea watoto wako sio kazi ya kutaka heshima kwa Watu wengine. Hao ni watoto wako mjinga wewe. Watu watakupa heshima kwa utumishi wako kwao na sio kwa mambo yako mwenyewe. Kulea watoto utapata heshima kwa hao watoto wako. Watoto ndio watakuheshimu kwa sababu unatija kwao. Na ikiwa hao watoto wakawa na tija kwenye jamii basi jamii itakuheshimu kupitia watoto wako.

Unataka kugawana mali 50/50 na mumeo wakati wewe ulikuwa hauzalishi chochote. Hivi hiyo ni haki ukitazama. Wewe mumeo hafanyi kazi, yupo nyumbani analea watoto alafu atake mgawane mali inakuingia akilini.

Wanawake wapewe ari, mtazamo mpya kuhusu maisha, shauku ya kujitegemea ili wasiteseke wala kunyanyaswa au kunyanyasika.

Kasumba ya Mwanamke kuhudumiwa iondolewe ndani ya jamii. Masuala sijui ya kutolewa mahari yote yaondolewe kwenye jamii kwa sababu hiyo yote ni kumkandamiza na kumnyanyasa Mwanamke. Jambo ambalo Watibeli hilo tulishamalizana nalo zamani sana.

Sio wanawake wanaonyanyasika pekee kwenye jamii zetu. Yapo makundi mengi ikiwemo hata wanaume wapo wanaonyanyasika.
Sheria zipo. Sema Watu wetu bado ni waoga mno. Hawawezi kujitetea kwa sababu akili zao ni tegemezi. Mpaka wapate msaada wa mtu mwingine wasiyemjua na asiye na wajibu na maisha yao wenyewe.

Kumbe uwezekano wa kuongea pumba kwa kujipiga kifua na kujinadi upoooo. Pamoja na paragraf nyingi lakini hakuna hoja ya maana hapo.

Hiz ishu za mfumo wa maisha inabidi ziangliwe kisayansi sio mhemko. Kuna quantity na frequency unavyoangalia rate ya unyanyas ngazi zote. Kuna vitu mtibeli unapuyanga
 
huyo alishawai kuwa house girl kabla ajafika hapo.usimlaumu

Vizuri.
Historia yake alipaswa aitumie kuhamasisha wanawake wengine kuwa nao wanaweza kuanzia chini mpaka kutimiza malengo yao.

Kuhusu ukatili ni ishu ya yeye kutengeneza foundation ya kuwasaidia wahanga wa ukatili kisheria kwa sababu sheria tayari zipo.
 
Kumbe uwezekano wa kuongea pumba kwa kujipiga kifua na kujinadi upoooo. Pamoja na paragraf nyingi lakini hakuna hoja ya maana hapo.

Hiz ishu za mfumo wa maisha inabidi ziangliwe kisayansi sio mhemko. Kuna quantity na frequency unavyoangalia rate ya unyanyas ngazi zote. Kuna vitu mtibeli unapuyanga

Ukiwa tegemezi lazima unyanyasaji uwepo. Kipi hauelewi Mkuu.
Unyanyasaji ni sehemu ya dharau kwa jambo lisilo na tija.

Hata wewe mwanaume kama huna Tija lazimaa unyanyaswe. Hivyo sio ishu ya Wanawake tuu
 
Unajua utegemez unaletwa na nn? Nan anapenda kuwa tegemezi?

Nini PENDEKEZO lako hapo ili unyanyas uishe?. Wanawake wasiwe tegemezi au unaamin nn?
 
Mtu yeyote asiwe tegemezi kama hataki unyanyasaji. Hiyo ipo wazi.

Ukipenda utegemezi inamaanisha unapenda kunyanyaswa.
Wanawake wengi wanapenda utegemezi.
 
JOYCE KIRIA ANAUPEO MDOGO KUHUSU HAKI, AACHE KUPOTOSHA JAMII.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Baada ya kuishiwa kifurushi nikajikuta nipo Channel 10, huko nilikutana na mwanamama aitwaye Joyce Kiria ambaye kwa mazungumzo yake ni dhahiri anapotosha jamii.

Joyce Kiria elewa kuwa kwenye nchi hii sheria zetu kwa kiasi kikubwa zinampendelea zaidi Mwanamke kuliko mwanaume. Hasa sheria za Ndoa.
Sheria za kifursa na kiuchumi, Mwanamke na mwanaume wapo Sawa kabisa.
Kisiasa, Sheria inampa upendeleo zaidi Mwanamke.

Joyce Kiria lazima aelewe kuwa sheria za nchi yetu hazina tatizo lolote kuhusu Haki za Wanawake.
Hakuna sehemu hata moja kwenye sheria zetu zinazomnyima Mwanamke haki ya Kusoma, kufanya kazi, kumiliki Mali, kufanya maisha yake pasipo kuvunja sheria. Hakuna.

Ndio maana wapo Wanawake waliosoma, wanaomiliki mali, wenye vyeo vikubwa hata kabla ya harakati za kutetea hao wanawake hapa nchini. Yaani miaka ya sabini wapo wanawake kibao wenye shahada, wapo madaktari, waalimu, wanasheria, wahasibu n.k.

Suala la ukatili wa kijinsia au ukatili wa aina yoyote lipo kisheria. Sheria zipo na adhabu zipo.
Kumpiga mtu yeyote bila kujali jinsia yake ni kosa kisheria na unaweza kufungwa.
Kumchapa mtoto wako uliyemzaa kupitiliza ni kosa kisheria. Mwalimu kumchapa mtoto kinyume na sheria ni kosa kisheria.

Kumtolea maneno machafu mtu iwe kwa kumtukana, kumdhihaki, kumbagaza ni kosa kisheria na adhabu zipo.
Joyce Kiria hujui mambo yote haya?
Kwa nini unailaumu serikali wakati sheria tayari zipo? Ishu ni utekelezaji wake unaoathiriwa na wahusika wenyewe.

Ni wanawake wangapi au wanaume wangapi wanafanyiwa ukatili lakini hawaendi kushtaki wanamaliza kifamilia? Sasa hapo kosa nila nani?

Unataka itungwe sheria ya haki Sawa. Hivi hujui sheria ya Haki sawa itamkandiza zaidi Mwanamke kuliko ilivyo sasa ambapo Mwanamke anapendelewa?

Lazima ieleweke kuwa kinachoisumbua jamii yetu ni hulka ya Utegemezi wa wanawake ambapo ndio hupelekea ukandamizaji wa baadhi ya haki zao kwa. Kupenda wenyewe.

Ukiwa tegemezi lazima uhuru wako uwe mashakani. Hilo Joyce Kiria lazima uwape elimu wanaokusikiliza na sio kuipa elimu Serikali ambayo inawatu wenye elimu, vyeo, uzoefu na Exposure mara kumi kukushinda.

Unasema hakuna Haki za wanawake au wanawake wanakandamizwa Ilihali kuna mamilioni ya wanawake ni wasomi, viongozi wa makampuni, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa n.k.

Unasema wanawake wanakandamizwa wakati Rais wa nchi hii ni Mwanamke, Spika ni mwanamke, angalia wapo wabunge na mawaziri ni wanawake. Nenda Muhimbili utakuta Madaktari na wahudumu wa afya wanawake, nenda vyuoni huko ukaone wanawake wenzako wakifanya kazi. Nenda mahakamani, nenda umoja wa mataifa.
Hao wamesoma miaka hiyo, miaka ya giza nchi ikiwa changa.

Kila mtu atapewa heshima yake kwa Haki aliyonayo. Iwe ni mwanaume au mwanamke. Kila mtu anaheshimika jinsi inavyostahili.

Wewe kama hukusoma tafuta mwenzako ambaye hajasoma. Mtaheshimiana. Wewe kama huna hela tafuta mwenzako ambaye hana hela mtaheshimiana.

Tatizo lenu Wanawake mnapenda vitu ambavyo sio stahiki zenu. Unakuta mwanaume mwanamke hujaenda shule, umetoka familia duni. Alafu unataka kuolewa kwenye familia zenye hadhi ya juu kukushinda. Hapo lazima moto uwake. Lazima unyanyasaji, ukandamizaji, udhalilishaji na dharau ziwepo.

Wanawake wengi mnapenda sana heshima ambayo hamna kwa kigezo cha sijui kuzaa. Umezaa watoto wako tuu. Hujazaa wengine. Watakaokuheshimu ni wale wanaokustahili. Sio unataka uheshimike kwenye jamii kama kwenye familia yako wakati hauna mchango wowote. Umelogwa nini?

Heshima inakuja na gharama. Heshima inakuja kwa Tija. Kama huna Tija yoyote kwenye jamii Nani akuheshimu Ndugu yangu, labda familia yako kwa sababu huko ndio unatija.

Achaneni na maneno ya kinafikinafiki kuwa sijui heshimu kila mtu. Hiyo haipo. Kinachoheshimiwa ni kile kinachostahili. Chenye tija. Heshima ipo kwenye HAKI.

Joyce Kiria hamasisha Wanawake wasome zaidi na zaidi. Wafanyekazi na kuzalisha mali. Kazi zipo nyingi. Kuwa fundi nguo, kuwa mamantilie, kuwa mfugaji, fanya kazi.

Kulea watoto wako sio kazi ya kutaka heshima kwa Watu wengine. Hao ni watoto wako mjinga wewe. Watu watakupa heshima kwa utumishi wako kwao na sio kwa mambo yako mwenyewe. Kulea watoto utapata heshima kwa hao watoto wako. Watoto ndio watakuheshimu kwa sababu unatija kwao. Na ikiwa hao watoto wakawa na tija kwenye jamii basi jamii itakuheshimu kupitia watoto wako.

Unataka kugawana mali 50/50 na mumeo wakati wewe ulikuwa hauzalishi chochote. Hivi hiyo ni haki ukitazama. Wewe mumeo hafanyi kazi, yupo nyumbani analea watoto alafu atake mgawane mali inakuingia akilini.

Wanawake wapewe ari, mtazamo mpya kuhusu maisha, shauku ya kujitegemea ili wasiteseke wala kunyanyaswa au kunyanyasika.

Kasumba ya Mwanamke kuhudumiwa iondolewe ndani ya jamii. Masuala sijui ya kutolewa mahari yote yaondolewe kwenye jamii kwa sababu hiyo yote ni kumkandamiza na kumnyanyasa Mwanamke. Jambo ambalo Watibeli hilo tulishamalizana nalo zamani sana.

Sio wanawake wanaonyanyasika pekee kwenye jamii zetu. Yapo makundi mengi ikiwemo hata wanaume wapo wanaonyanyasika.
Sheria zipo. Sema Watu wetu bado ni waoga mno. Hawawezi kujitetea kwa sababu akili zao ni tegemezi. Mpaka wapate msaada wa mtu mwingine wasiyemjua na asiye na wajibu na maisha yao wenyewe.

Somesha watoto wako alafu uone kama kuna Kima atawafanyia ujingaujinga. Husikii wanaume wengi hawataki kuoa wanawake waliosoma, sababu kubwa ni suala la Haki. Na bahati nzuri kwenye haki kila mmoja ni sawa kwa mwingine ingawaje hawalingani.

Nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuna haja gani sisi kukaa na kupoteza muda kumjadili house girl asiyetaka kujiendeleza kielimu?
 
Yule Si Mwandishi Wa Habari Mwenye Muda Mrefu Ila Sasa Anajiona Mwanasheria.

Heri Aende Shule Akaongeze Elimu Ya Upande Huo
 
Mbona upeo wenu ni mmoja. Kama ungekuwa na upeo mkubwa, usingemtegemea binti kimoso akulishe, akuvalishe na kukutunza we kibenten chake huku unazugia na uandishi wa vitabu vya hadithi za uongo. Hivi mkuu huoni aibu kutunzwa na mwanamke? Hivi unauwezo wa kuuza hata nakala 10 za vitabu vyako kweli kwa mwaka mzima?😀😃😄
 
Atakuwa ni single mother aliyeachika.Wengi wao wamekuwa wakipotoshana sana na kujilinganisha na wanaume.Wanawake wa aina hiyo ni janga kwenye taifa tena wanatumia vibaya vyombo vya habari kuwapotosha wanawake wenzako.
Ila pia wanawake wa kaskazini ni wajuwaji sana ndiyo maana wengi wanaachika.
 
  • Thanks
Reactions: FWC
Kati ya watu ambao hawana akili wa kwanza ni wana harakati wa haki za binadamu na watetezi wa haki za binadamu.

Ni sawa na watu wako Dsm wanalalamika wamasai kuondolewa maporini kwenda kuishi kwenye nyumba zenye hadhi ya ubinadamu
 
Back
Top Bottom