Athari za 50/50 katika jamii

Pesanyingi

JF-Expert Member
Apr 15, 2023
400
666
Dhana hii ya 50/50 ni dhana iliyoletwa hapa duniani na watu wenye nia ovu .Si kwamba nawadharau wanawake hapana, kiasili, kiutamaduni na hata kiimani hakuna sehemu kunako sisitiza usawa kati ya mwanamke na mwanaume.

Niishairu jamii irudi katika misingi yetu Mwanamke aongozwe na mwanaume na tutashudia jamii ikiwa katika hali ya ustawi chanya tunaotegemea.

Leo hii mwanaume hapewi tena kipaumbele kama hapo awali jambo ambalo linatishia mustakabali wa jamii kwa ujumla na tukilifumbia macho swala hili kwa kufuata umagharibi kuna siku katika Dunia hii tutashuhudia mwanaume akipambana kupata haki yake au usawa na hapo tutakuwa tumechelewa sana.Kwenye nafasi zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii mwanamke anapaswa kuongozwa.

Miongoni mwa athari za mfumo huu tunazidi kuziona kila siku mfano,

Ongezeko la single mama hawa hujiona ni wanaume na nusu.

Mmomonyoko wa maadili.

Watoto wa kiume kutokupewa kipaumbele kwa nafasi mbali mbali katika jamii.

Vifo kwa wanaume,hapa sababu ni msongo wa mawazo.

Waafrika turudi kwenye asili yetu mwanaume ni kiongozi, muongoza njia na mwenye maono mapana.

Unaweza ongezea athari zingine.
 
Kwanza tukumbuke,dhambi iliingia duniani kupitia mwanamke,baadhi ya watu [ktk historia]na hata wafalme,walipotoshwa na hata kufikwa na umauti kwasababu ya mwanamke [mf.Samsoni,Yohana mbatizaji n.k/Mfalme Suleiman n.k].

Shetani alishaigundua njia nzuri na rahisi kwake ya kuikamata na hata kuitawala dunia ni mwanamke,sasa anataka dunia/ulimwengu umwabudu yeye, ili afanikishe azma yake hiyo, anamtumia mwanamke kwa kumpa nguvu kisiasa na kiuchumi dhidi ya mwanaume [kiongozi aliye jisahau].

Kiufupi,anawatumia mawakala wake na vyama vyao vya siri pamoja na taasisi kubwa kama UN,WHO, World Economic Forum n.k. pamoja na upapa kuvuruga ulimwengu/dunia kwa maovu mengi ikwemo ushoga n.k.ili watimize ajenda zao kuelekea New World Order. Muda hautoshi,ila tafuta [Google]UN agenda 2021-2030 Goals.
 
Hakuna wakati [ktk historia ya ulimwengu] ambao Mwenyezi MUNGU aliwahi kumfanya mwanamke kuwa kiongozi/mtawala wa taifa lolote duniani.Hii dhambi tuliyoifanya Tanzania ambayo tunaishangilia na kuisifia kila leo,italigharimu Taifa.
 
Tunapokwenda hali itazidi kuwa mbaya kwetu na vizazi vyetu,na tushingae wakidai mwanamke naye ni kichwa cha familia kwasababu ya dhana 50/50.
Jamii sasahiv inamtazama mtoto wa kike kwa hicho la tatu na likimpa tumaini kuliko wa kiume.Watoto wa kiume wakipuuziwa hadi wengine kujiingiza kwenye ushoga na kuonekana ni jambo dogo TU.
 
Back
Top Bottom