Joseph shamba vengu wa orijino komedi

si huyu mtu yupo muhimbili niliona mmoja ya magazeti ya udaku akiwa anapewa pole na mzee wakaya..
 
Mkuu pale yeye ni vengu(usanii) na si joseph shamba(halisi) hawezi kumzihaki akiwa kama joseph lakini akiwa kama vengu ni rahisi kufanya usanii wa maigizo

No wonder ufumaniwa utasingizia ni shetani tu alikupitia, na sio wewe.

Stupid excuse.
 
Ugua pole ndugu yangu mungu akujalie neema upone mapema amani iwe kwako!!
 
jamaaa anumwa hoi yuko muhimbilina amekaaa ICU kwa mwezi mzima nw ameshatoka yuko wodi za kawaida xaxa....tumuombeeni apone hata kama alikuwa mlevi sana......
 
get well soon 5.jpg

Kila la kheri Mkuu wetu.
 
Wana Jukwaa!!! Hivi yule selebu maarufu wa kundi la vichekesho la ORIJINO KOMEDI, JOSEPH SHAMBA yu wapi siku hizi? Maana ni muda mrefu nafuatilia vipindi vya komedians hao na simuoni. Pia hata katika ziara zao za mikoani pia haambatani na kundi hilo mahiri



Selebu Vengu anaumwa, alikuwa amelazwa Muhi2.
Tumuombee apate kupona haraka ili aendelee na shughuli zake.
 
Jamani acheni mzaha huyu ndio Vengu anaumwa saana hata mheshimiwa alienda kumjulia hali lakini ninyi masharobaro mnakuja na comment za ajabuuu!! Mpeni pol basi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1 Get well soon Jembee!!


IMG_0650.jpg
 
Kuna thread ilikuwa inamuelezea huyu jamaa kuwa ni mgonjwa sana amelazwa Muhimbili so nadhani hiyo ndiyo hali halisi
 
Mmh Nimaamini kweli wa Baadhi ya WaTanzania tumejaliwa na maneno ya Uzushi tena wa hali ya juu kama ni kiwango basi ni asiliama100.99.
Joseph AKA Vengu yu hoiii Muhimbili karibu mwezi wa tatu sasa.Hadi mheshimiwa JK alikwenda kumjulia khali.
Alilazwa ICu kwa takribani miezi 2.Anasumbuliwa na ugonjwa wa kichwa na ndo sababu alikuwa anazimika zimika ovyoo mitaani.
Tena Tunawahamasisha wa TZ na haswa wapenzi wa ze coooomeee dddd waweze kumchangia kwa hali na mali na yeye aende kutibiwa kama waheshimiwa kuleee kwenye hosp zao Bombayyyy.
Nawasilisha mada .Tafakari kabla ya kuchangia mda.usikurupuke tafuta vyanzi vya habari.
 
Ngongo msaidieni kijana huyu wa home....., mko karibu na waamuzi acha kupendekeza simamia utekelezaji....
 
Na Sifael Paul
AFYA ya staa wa Orijino Komedi ‘OK', Joseph Shamba ‘Vengu' (pichani) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na ugonjwa unaodaiwa kushambulia sehemu ya kichwa, imeibua majonzi na vilio kwa mashabiki wake, wadau wa sanaa na Watanzania kwa jumla.

Baada ya gazeti pacha na hili, Ijumaa Wikienda Jumatatu wiki hii kuripoti habari ya Vengu kukaa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa takribani miezi miwili, Ijumaa lilipokea simu na meseji nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakipeleka vilio vyao kwa wadau wa sanaa na serikali kuwa ufanyike utaratibu wa staa huyo kupelekwa India kwa ajili ya matibabu kama ilivyo kwa wanasiasa.

"Ukweli habari ya afya ya Vengu inaumiza sana. Nani asiyejua mchango wa Vengu? Hapa inahitajika nguvu ya pamoja ya hali na mali ili akatibiwe nje, apone na aendelee na harakati za kuitumikia jamii kwa vichekesho vyake vilivyojaa mafunzo," zilisomeka baadhi ya meseji za wasomaji wa habari hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alikwenda kumjulia hali Vengu ambaye alikuwa ametolewa ICU na kuwekwa wodi namba moja katika Jengo la Mwaisela alipolazwa hadi sasa.

KUTOKA IJUMAA
Sisi sote ni ndugu, watoto wa baba mmoja. Vengu ni mwenzetu tena ni mfano wa kuigwa na vijana watafutaji. Mwenzetu anahitaji sala na dua zetu. Tunaamini wadau wa sanaa na serikali yetu sikivu watafanya jitihada za kumsaidia.
 
he! Jamani this is very sad! Huyu jamaa anaumwa aisee! Imenigusa sana picha iliyowekwa humu! he! Yamefika hapo?
 
Back
Top Bottom