OCD Bunda fuatilia utendaji kazi wa baadhi ya mgambo wanaokusaidia kazi wengi wanashirikiana na vibaka

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
202
436
Naandika andiko hili kwa uchungu sana!Kwanza ni jambo zuri sana Kwa jeshi la polisi kushirikiana na jeshi la akiba maarufu kama Mgambo katika kulinda usalama wa raia na mali zao.Ni jambo la kupongezwa na Kila mtu anayelitakia mema Taifa lake!

Mkuu pasipo kuficha kitu hawa Mgambo wanaosaidiana na askari polisi wana maslahi na Vibaka.Fanya uchunguzi wa kina utalibaini hili.Nimeshuhudia zaidi ya mara tatu Mgambo wanavamia maeneo ya vibaka lakini wanapowakamata,kibaka mwenye chochote mfukoni huachiwa hapo hapo na wasio na chochote hufikishwa kituoni.Unategemea uhalifu utaisha Kwa staili hii?

Bahati mbaya zaidi asilimia kubwa ya Mgambo wanaosaidiana na polisi hawajapitia mafunzo ya Mgambo kwa hiyo hawana kabisa ethics za masuala ya ulinzi na usalama.Haishangazi kuona jeshi la polisi mnapanga mipango ya kuvamia kambi za wahalifu mfano maeneo ya wacheza kamari,wavuta bangi,wakabaji ila hata kabla hamjaondoka wahalifu tayari wanakuwa washapata taarifa.Hawa Mgambo wanalipaka matope jeshi la polisi!

Pia kuna Yule Mgambo mfupi mliyempa mamlaka ya kutembea na pingu muda wote.Huyu sasa kazi yake ni kutumia hizo pingu kwa maslahi yake binafsi.Fuatilia pia hili upate ukweli wote.Anapokutana na vibaka ni kuomba pesa huku akionyesha pingu zake kama Kinga.Hapa utegemee uhalifu kuisha kweli?

Kuna kundi la vijana wanaotapeli watu kwa kuwauzia dhahabu feki na kuwarushia maburungutu ya pesa.Fikiria kwa nini hawa matapeli wanajiamini sana kwenye mission zao,kuna chain ya vijana wako wasio waaminifu wanapata percent kadhaa toka kwa hawa vijana!Na nikueleze tu palipo na hawa vijana Mgambo pia huwa wapo na baadhi ya maaskari wako wasio waaminifu huwa attention kusubiri mgao.

Haya siyo majungu mkuu chunguza Kwa intellijensia utabaini ukweli wote.
Uchunguzi wa kipekee ufanye pia kwa Mgambo aitwae s****l.Huyu ndio partner haswaa na hao vijana wapigaji!
Uchunguzi wa kipekee pia uelekeze kwa askari wako mmoja ajulikanae kwa jina maarufu la Man 'Z'.Huyu ni askari corrupt sana!Kumwelezea hapa inaweza kujaza pages za kutosha.Ila Kwa kifupi mfanyie tu uchunguzi wa kina ujiridhishe,isionekane ni majungu!Kuna mengi utajifunza!

Jukumu la ulinzi na usalama ni la kila raia,tutashirikiana vyema na jeshi la polisi katika masuala ya ulinzi na usalama ila pia hatutasita kutoa taarifa Kwa mamlaka kuhusu askari na Mgambo waovu wanaolipaka matope jeshi la polisi!
 
Back
Top Bottom