Joseph Selasini, a Square peg in a Round hole?

Shule za kata hazikuanza 2005; wazo la shule za kata liliainishwa katika mpango wa national poverty strategy wa mwaka 1998. Hizo shule zilianza kujengwa kipindi cha rais Mkapa.

Zoezi hilo liliongezwa nguvu na ujio wa serikali ya awamu ya nne ambapo PM Lowassa alilifanya moja ya mipango yake na shule za kata zikaanza kujengwa kwa wingi. Kati ya shule za kata zilizopo sasa, karibu asilimia 25 zilianza kabla ya mwaka 2006.

Mkuu wengi ni watoto wadogo akili zao wamezipata miaka hiyo2005,hawajuhi lolote la nyuma ya hapo
 
Gurudumu,

Nimezungumza nae. Amekanusha hayo yote uliyoandika. Sijaona Hansard. Unaweza kunisaidia taarifa zaidi kuthibitisha maneno yako? Kama mwanachama wa CDM nina haki ya kulalamika dhidi ya kauli kama hizo na hatua zitachukuliwa. Ni makosa makubwa kama tutabaki kushutumu viongozi wetu wholesale bila kujua ukweli na sababu za misimamo yao.

Napinga sana fikra kwamba CDM is a whole mass and each has to think in the same way. That isnt right!

Mkuu Alberto, nilikaa kimya kukusubiri ufute hii kauli yako lakini pengine hujapata nafasi.

Ngoja nikuulize maswali mapana kidogo. Hivi katika chama chenu mna utaratibu wa ku-monitor wabunge na viongozi wenu watamka nini hadharani? Je huwa mnachambua hizo kauli katika muktadha wa maono na malengo ya chama? Je kazi ya party whip wenu ni nini kule bungeni?

Hivi unajua kwamba wabunge wa ccm wengi wanatofautiana na itikadi ya chama chao? Kwamba wanajua ukweli kwamba chama kimeshindwa kutawala nchi. Kwamba wengi hawaridhiki na maamuzi ya ngazi za juu ya chama chao? Ukiongea nao one to one utagundua hilo lakini wakiwa mbele ya vyombo vya habari wanatetea itikadi na misingi ya chama chao. Tena wote wanateteana hadi utadhani ni wapumbavu.

Kama itikadi, misingi ya chama, maamuzi ya chama, hayatasimamiwa na kutetewa na wabunge wa chama nani atafanya hiyo kazi. Na kama makada wa chama, Kama Msando, watatetea upungufu Kama huo wa Shibuda na Selasini?
 
Shule za kata hazikuanza 2005; wazo la shule za kata liliainishwa katika mpango wa national poverty strategy wa mwaka 1998. Hizo shule zilianza kujengwa kipindi cha rais Mkapa.

Zoezi hilo liliongezwa nguvu na ujio wa serikali ya awamu ya nne ambapo PM Lowassa alilifanya moja ya mipango yake na shule za kata zikaanza kujengwa kwa wingi. Kati ya shule za kata zilizopo sasa, karibu asilimia 25 zilianza kabla ya mwaka 2006.
Du Mkulima ni kweli kabisa Shule za Kata zilianza hata kabla ya hapo kwani kwa Mkoa wa Kilimanjaro zilikuwepo na zilifaulisha sana. Na huko Rombo ni kila kijiji hivyo Selasini ana haki ya kutetea, pia nimemwona ni mtu wa msimamo na ukweli kwa anayoyaona na kuyasikia.
Unajua ili ushinde Ubunge katika Jimbo ni lazima uangalie upepo upo wapi? Walipokuwa NCCR na Masumbuko, Mrema, Nswazugwako, Marando na wengineo walchukiwa sana lakini mpaka leo wanahitajika na Watanzania hivyo hata wakienda Chama chochote watapewa Ubunge tu
 
Nataka niwape CV ya Mheshimiwa Joseph Selasini. 1976- 1979 Elimu ya Sekondari (kaengesa Seminari), 1980-82 Alihitimu kidato cha sita Itaga Seminari. Baada ya hapo alisoma elimu ya seminari kuu kwa ajili ya kuwa padri wa kanisa katoliki lakini alifukuzwa na hakuendelea tena na masomo. Kati ya mwaka 1987- 1993 alifanya kazi Benki ya Nyumba (THB) kama afisa Usafirishaji baada ya kupewa kazi na Urassa aliyekuwa Mkurugenzi mkuu kwa wakati huo. Alliba gari ya Benki ya Nyumba na kuliuza na kwa vile Urassa alikuwa ndugu yake hakamchukulia hatua. Kimsingi Joseph Selasini si msafi bali anapotaka kitu chake anaweza kumsaliti yeyote hata baba yake mzazi. Wakati wa mtafaruku wa NCCR kati ya Mbatia na Masumbuko Lamwai aliweza kumsaliti kaka yake kwa kueleza udhaifu wa makuzi ya utotoni alioufahamu ili tu kujipendekeza kwa James Mbatia. Kwa hiyo si ajabu kuona leo hii bungeni anajipendekeza kuisifia CCM kwa mafanikio ambayo hayapo. Kwa hiyo wana CDM hiyo ni WAKE UP CALL, kajionyesha mapema huyo
 
Mkuu mbona kama umekwenda personal zaidi?
 
mkuu ngongo.... kinachonifurahisha sana ni hii trade mark ya font type unayoitumia ..... unless otherwise ... business as usual

Huo ndio mwandiko wake jamani, na ukweli amesema Ngongo na mimi tunashangaa sana jinsi mnavyowasema kina Kafulila wengine mara ohh wameangishwa kwenye uenyekiti wa kamati ilhali hata kugombea hawajagombea!!!!
 
Hapa jamvini lazima tukubali kuwachambua wabunge wetu ili wajue kuwa sisi wananchi tunakwenda kwa mtindo wa digitali zaidi kama alivyosema Hon.Mdee leo.Huyu mbunge aliyetoa mchango hovyo hovyo lazima tumjadili kwa kina ili ajue kuwa hajawatendea haki CDM.

Kama tuliweza kumchambua Hon.Zitto kwa muda wa wiki kadhaa na hatimaye alijitokeza yeye Zitto na kutoa ufafanuzi kwa maswali yote magumu yaliyotusumbua wakati ule.Vivyo hivyo huyu selasini lazima tumchambue kwa kina.Maana yeye ni kioo cha jamii inayofuata demokrasia.
CDM tuache kubeba wabunge wabovu tukiwasema sana watapata nafasi ya kujirekebishe.TUENDELEE KUMCHAMBUA SELASINI HADI AJITOKEZE ATOE UFAFANUZI
 
Mkuu Alberto, nilikaa kimya kukusubiri ufute hii kauli yako lakini pengine hujapata nafasi.

Ngoja nikuulize maswali mapana kidogo. Hivi katika chama chenu mna utaratibu wa ku-monitor wabunge na viongozi wenu watamka nini hadharani? Je huwa mnachambua hizo kauli katika muktadha wa maono na malengo ya chama? Je kazi ya party whip wenu ni nini kule bungeni?

Hivi unajua kwamba wabunge wa ccm wengi wanatofautiana na itikadi ya chama chao? Kwamba wanajua ukweli kwamba chama kimeshindwa kutawala nchi. Kwamba wengi hawaridhiki na maamuzi ya ngazi za juu ya chama chao? Ukiongea nao one to one utagundua hilo lakini wakiwa mbele ya vyombo vya habari wanatetea itikadi na misingi ya chama chao. Tena wote wanateteana hadi utadhani ni wapumbavu.

Kama itikadi, misingi ya chama, maamuzi ya chama, hayatasimamiwa na kutetewa na wabunge wa chama nani atafanya hiyo kazi. Na kama makada wa chama, Kama Msando, watatetea upungufu Kama huo wa Shibuda na Selasini?

Unajua huku JF uzuri wenu mmekaa kupinga chochote kinachosifia serikali.....Mimi najua hii serikali imeshindwa kuendesha nchi inavyotakiwa, lakini pia kuna mafanikio madogo madogo ambayo yamepatikana kutokana na sera hizi hizi za hii serikali, wote tunajua how good on paper hizi sera zilivyo, tatizo huwa utekelezaji, na huo utekelezaji unatofautiana kwa levels mbali mbali. Sio kwamba shule zote za kata zimefeli...hapana. Jambo jingine Kilimanjaro watu wanavyochukulia elimu kwa uzito wake ni tofauti na maeneo mengine, wazazi wanazi-support hizo shule, kuna sehemu wanajitolea watu kufundisha wanafunzi, wanafunzi wenyewe wanajituma. Hivyo kama mtu akisifia lengo la kuanzisha shule za kata tusianze kupinga tu kiupofu upofu. Mfano, yeye katumwa na wananchi wa Rombo, kama wameona mafanikio ya hizo shule, wakasema akazisifie, wewe utapinga nini???
 
Hapa jamvini lazima tukubali kuwachambua wabunge wetu ili wajue kuwa sisi wananchi tunakwenda kwa mtindo wa digitali zaidi kama alivyosema Hon.Mdee leo.Huyu mbunge aliyetoa mchango hovyo hovyo lazima tumjadili kwa kina ili ajue kuwa hajawatendea haki CDM.

Kama tuliweza kumchambua Hon.Zitto kwa muda wa wiki kadhaa na hatimaye alijitokeza yeye Zitto na kutoa ufafanuzi kwa maswali yote magumu yaliyotusumbua wakati ule.Vivyo hivyo huyu selasini lazima tumchambue kwa kina.Maana yeye ni kioo cha jamii inayofuata demokrasia.
CDM tuache kubeba wabunge wabovu tukiwasema sana watapata nafasi ya kujirekebishe.TUENDELEE KUMCHAMBUA SELASINI HADI AJITOKEZE ATOE UFAFANUZI

Kwani yeye ni Mbunge wa digitali? Angekuwa wa digitali angekuwa ameshajitokeza tangu hii thread ilipoanzishwa. Hilo ni jambo lingine la CDM kuchuja
 
Unajua huku JF uzuri wenu mmekaa kupinga chochote kinachosifia serikali.....Mimi najua hii serikali imeshindwa kuendesha nchi inavyotakiwa, lakini pia kuna mafanikio madogo madogo ambayo yamepatikana kutokana na sera hizi hizi za hii serikali, wote tunajua how good on paper hizi sera zilivyo, tatizo huwa utekelezaji, na huo utekelezaji unatofautiana kwa levels mbali mbali. Sio kwamba shule zote za kata zimefeli...hapana. Jambo jingine Kilimanjaro watu wanavyochukulia elimu kwa uzito wake ni tofauti na maeneo mengine, wazazi wanazi-support hizo shule, kuna sehemu wanajitolea watu kufundisha wanafunzi, wanafunzi wenyewe wanajituma. Hivyo kama mtu akisifia lengo la kuanzisha shule za kata tusianze kupinga tu kiupofu upofu. Mfano, yeye katumwa na wananchi wa Rombo, kama wameona mafanikio ya hizo shule, wakasema akazisifie, wewe utapinga nini???

Mkuu hoja yako ingemeremeta zaidi kama ungetuwekea data za shule za kata za Rombo kwamba zimefanya vizuri na kuthibitishia kwamba wapiga kura wake walimtuma aende bungeni kuzisifu, au vipi mkuu?
 
Mkuu,
Ni jukumu la wanaomshutumu waje hapa na evidence kwamba anasema uongo. Not mimi. Kuhusu kutumwa na wananchi kusema hilo nimesema kama mfano, so sina haja ya kuweka data yoyote.

Anyway kuhusu shule za kata, hebu tazama hizi:
http://www.matokeo.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/s0979.htm
http://www.matokeo.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/s0510.htm
http://www.matokeo.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/s0818.htm
 
yote aliozungumza selasini shauri yake lakini hila na wanafunzi wa kata kufika chuo kikuu ndo limeniumiza, kwani shule hizi zimeanza 2005 hvyo 2009 product ya kwanza ikatoka sasa toka 2009 mpaka mwaka huu kweli wamefika chuo kikuu lini?? hata kama wamefika chuo kikuu basi ni asilimia robo tu ya wanafunzi wote je? hawa wengine selasin anajua walipoishia???

Huyu mbunge kadanganya bungeni inabidi achukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa muongozo!!:twitch:
 
Mkuu,
Ni jukumu la wanaomshutumu waje hapa na evidence kwamba anasema uongo. Not mimi. Kuhusu kutumwa na wananchi kusema hilo nimesema kama mfano, so sina haja ya kuweka data yoyote.

Anyway kuhusu shule za kata, hebu tazama hizi:
http://www.matokeo.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/s0979.htm
http://www.matokeo.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/s0510.htm
http://www.matokeo.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/s0818.htm

Mkuu hoja yangu ilikuwa kuhusu msimamo wa Chadema kwamba shule za kata ni sera mbovu halafu mbunge wa Chadema anazisifia hadharani.
 
Unajua huku JF uzuri wenu mmekaa kupinga chochote kinachosifia serikali.....Mimi najua hii serikali imeshindwa kuendesha nchi inavyotakiwa, lakini pia kuna mafanikio madogo madogo ambayo yamepatikana kutokana na sera hizi hizi za hii serikali, wote tunajua how good on paper hizi sera zilivyo, tatizo huwa utekelezaji, na huo utekelezaji unatofautiana kwa levels mbali mbali. Sio kwamba shule zote za kata zimefeli...hapana. Jambo jingine Kilimanjaro watu wanavyochukulia elimu kwa uzito wake ni tofauti na maeneo mengine, wazazi wanazi-support hizo shule, kuna sehemu wanajitolea watu kufundisha wanafunzi, wanafunzi wenyewe wanajituma. Hivyo kama mtu akisifia lengo la kuanzisha shule za kata tusianze kupinga tu kiupofu upofu. Mfano, yeye katumwa na wananchi wa Rombo, kama wameona mafanikio ya hizo shule, wakasema akazisifie, wewe utapinga nini???

Nadhani kuna tatizo la kuchanganya data hapa. Neno "Shule za Kata" limeibuka kutokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya nne, chini ya aliyekuwa waziri mkuu Lowasa. lakini shule za kata kama shule za kata zimekuwepo siku nyingi. na wazo lenyewe ni zuri tu. tatizo linakuja katika huu mkakati wa injinia Lowasa. kama yalivyo matatizo mengine mengi tu katika nchi yetu, wanasiasa wanapotumia mpango fulani kwa maslahi ya kisiasa, ambapo mara nyingi hutekeleza baadhi ya vipengele vya mradi huo, kwa kulazimisha matokeo ya haraka ili mtu ajichukulie sifa.

Kwa kuwa mradi ni halali na ni mzuri, lazima kutakuwa na mjadala mkali hapo. na ndio mtego wenyewe, kwamba kuna wengi wataona ni kitu kizuri, tatizo ni dogo tu la utekelezaji. kwa kweli tatizo sio dogo, maana kwa utekelezaji wa ujenzi wa shule za kata huko nyuma, angalau mambo ya msingi katika shule yalikuwa yanazingatiwa. lakini SHULE ZA KATA za Lowasa zimekuja kama Tsunami. tunasahau kwamba shule sio jengo tu, kuna vitu vingi vinatakiwa viangaliwe (mfano walimu, vifaa, maabara, visheni au falsafa ya shule, nk.). Badala ya shule, tunaweza kujikuta tunajenga viwanda vya kutengeneza waharibu nchi, sio wajenga nchi. ni kama ugonjwa wa kansa. ni zile zile cells za mwili, ila zinakua bila mpangilio unaotakiwa. hapo mtu anakuwa na kansa. SHULE ZA KATA za Lowasa sio shule, NI KANSA.
 
Haya sasa, leo amelalamika bungeni katika swali lake la msingi kwa Wizara ya Elimu kwamba kiwango cha kusoma na kuandika kimeshuka kutoka asilimia 89.4 miaka ya themanini hadi 69 mwaka 2010. Is he consistent?
 
Niko na wazee na vijana kijiweni Dar, kuna watu wa ROMBO wanalalamika watu wa kwao kumchagua Selasini. Wanasema hajafanya chochote na anataka posho iongezwe.

Yeyote anaejua mazuri ya mh huyu anipe niwaelimishe coz wanasema bora Mramba
 
Back
Top Bottom