Joseph Selasini, a Square peg in a Round hole?

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Mbunge huyu wa chadema apingana na sera za chadema bungeni. Amesema;

1. Shule za kata ni nzuri kwa sababu kuna vijana wake wamefika chuo kikuu kupitia shule za kata (hajali wamejifunza nini)

2. Amepongeza serikali kwamba imefanya mambo mengi sana kuleta maendeleo ya nchi hii

3. Asema uchaguzi ulikuwa huru na haki

4. Asema wanafunzi wa vyuo vikuu wasijihusishe na siasa, wakati Chadema ina mkakati wa kujiuza vyuo vikuu na wameanzia Makumira

(Maana ya "square peg in a round hole" kwa mujibu wa Oxford Advanced Learner's Dictionary sixth edition ni, "a person who does not feel happy or comfortable in a particular situation, or who is not suitable for it")
Mimi ni mwana Rombo na mkereketwa wa maendeleo ya wilaya ya Rombo na taifa zima kwa ujumla hasa katika sekta nyeti ya ELIMU. Mbunge wangu Josephy Selasini kimya kimezidi hatukusikii ukiendesha harakati za maendeleo.

Pengine unaziendeleza ila huweki wazi katika vyombo vya habari maana wengine hatupo jimboni, tupo sehemu mbalimali za Tanzanaia na dunia kwa ujumla. Tuna mawazo mengi sana chanya ambayo tungekushirikisha wewe kama mbunge yangesukuma mbele gurudumu hili la maendeleo. Tupo vijana wasomi wa fani mbalimbali ambao tunaweza kushirikiana na wewe katika kubuni mbinu mbalimbali za kuboresha na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni mwetu. Ushauri wangu ni huu mheshimiwa.

Andaa mkutano wa wana Rombo wote waishio Dar es salaam na sehemu nyingine kwa lengo la kuwaleta watu pamoja ili tuweze kutafakari na kubuni ni kwa namna gani maendeleo ya Rombo yanaweza yakaboreshwa haraka iwezekanavyo.

Mwisho nakutakia maendeleo mazuri katika shughuli zako.
 
hANA jipya huyu.
HAta anapoongea hana mvuto na hayuko bold, maana anajua wazi anaongea mambo ambayo aidha si kweli, au ameyakariri kwa nguvu!
 
hANA jipya huyu.
HAta anapoongea hana mvuto na hayuko bold, maana anajua wazi anaongea mambo ambayo aidha si kweli, au ameyakariri kwa nguvu!

hili nalo nimeliona kwamba alikuwa anaongea hajiamini na kama hajajiandaa
 
Ndo faida ya kuchukua yoyote kumpa ubunge.

Yaani? Alikuwa anapigiwa makofi na wabunge wa ccm kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kwani historia yake ya vyama ikoje, alikuwa chama gani kabla?
 
yote aliozungumza selasini shauri yake lakini hila na wanafunzi wa kata kufika chuo kikuu ndo limeniumiza, kwani shule hizi zimeanza 2005 hvyo 2009 product ya kwanza ikatoka sasa toka 2009 mpaka mwaka huu kweli wamefika chuo kikuu lini?? hata kama wamefika chuo kikuu basi ni asilimia robo tu ya wanafunzi wote je? hawa wengine selasin anajua walipoishia???
 
Nafikiri ni wa CHADEMA?tumezoea bogus wako CCM,sasa ilikuwaje?:laugh::laugh:

Heshima kwako Dyslexia,

Hapana huyu si mbunge wa CHADEMA atakuwa ni mbunge wa NCCR Mageuzi hapana labda ni wa UDP kwa Bwana Mapesa au inawezekana anawakilisha TLP siunajua tena kile chama kina watu wehu kama mwenyekiti wao.Siku zote wabunge na Viongozi wa CHADEMA wako right hawezi kuongea upupu kama wa Selasini ebo nachoka mwaka huu tutaona mengi.

Halafu wewe dada mbona jina lako gumu hivi linatamkwaje ?.
 
Ni wa CHADEMA,,yapo ma-bogus huko mi nayamezea tu,watayaona wenyewe!!naona ilikuwa bora yeyote mradi si Mramba,wakachukua huyo jamaa,na ni CCM mzuri ni vile tu walimnyima gombea akaenda CHADEMA kama alivyo Shibuda,kazi ipo kubwa sana,bado hatujaona!!!:laugh::laugh:
 
hapo sisiem ndo wajiulize inakuwaje mgombea wao anashindwa na mtu bogus, either mgombea wao ni bogus zaidi au watu wamechoka wapo tayari kuchagua jiwe kuliko sisiem
 
Mbona haujaniambia asili ya jina lako linatamkwaje ?.Unajua nimelipenda.

hapo sisiem ndo wajiulize inakuwaje mgombea wao anashindwa na mtu bogus, either mgombea wao ni bogus zaidi au watu wamechoka wapo tayari kuchagua jiwe kuliko sisiem

Tuhuma za rushwa mkuu,watu wamechoka,ofcoz CCM wajifunze kutokana na hili kosa!kazi kwa warombo!
 
Nafikiri ni wa CHADEMA?tumezoea bogus wako CCM,sasa ilikuwaje?:laugh::laugh:

Huyu ndio alimng'oa Mramba kule Rombo.

Wananchi walimpigia kura za HASIRA baada ya Mramba kuwatukana kina mama wa Rombo.

Sasa yupi afadhali, huyu au Mramba?
 
Back
Top Bottom