John Shibuda na mgogoro wa Kauli ya kuisifia CCM; Kauli za wana CHADEMA

Taarifa imepokelewa!
Kwa kuwa imekwishafahamika, mpango wao umeshafeli.
Wataishia kupiga makelele kama beberu.
Mukama alipotoa mapendekezo ya kuinusu ccm, mwenyekiti akamzawadia ukatibu mkuu. Ameshindwa kufanya lolote na wana ccm wanamkumbuka makamba sinia.
Huyu benson bana naye mwisho wake uu karibu sana.
 
shibuda anawaumiza akili ?????????????????, ooooh noo, you must be kidding , the whole situation is under control , tulieni , tulie , kwani hamjui stori ya humpty dumpty , JUST WAIT FOR THE GREAT FALL, Viongozi wa CDM Ni watu makini, na SHIBUDA ni sisimizi tu , kuna kitu kina mpa jeuri , na soon atakitopeza , Then utamwisho wa stori za huyu kirusi
 
Mkuu taarifa yako imepokelewa tunashukuru,ila ingelifaa zaidi kama ungetoa source,ama kama chanzo ni wewe basi tuweke wazi zaidi badala ya kuwaambia viongozi waifanyie kazi taarifa hii,nijuavyo mimi kama wewe ni mpenda mabadiliko na unakubali kuwa CDM ni chama kinacholeta mabadiliko na kitaleta mabadiliko tunayoyapigania na hasa kuchukua dola,nigekushauri na wewe kama taarifa zako ni za kweli na unaamini chanzo chako basi nenda makao makuu ukutane na Dr Slaa umweleze mkanda wote jinsi ulivyosukwa,kama Dr atakuwa hayupo au yuko bussy sana basi omba ukutane na Mh Mnyika umweleze picha yote ilivyo na mwisho utapata nafasi ya kushauri the way forward.
Nadhani kama ni issue sensitive sana si busara sana kuwahi kwenye jukwaa hili zaidi ya kulifikisha mahali husika hasa kwa kuwa huenda una taarifa sahihi za uzandiki huu.
Lakini hata na wapenda maendeleo kama kweli tunachukizwa na ufisadi wote unaofanywa na CCM,ugumu wa maisha unaosababishwa na watu kupora fedha za walipa kodi,uzembe na madudu mengine yote basi natoa rai tusiruhusu njama za aina yoyote kwa ushawishi wa fedha au hata ahadi ya vyeo.ni dhambi mbaya sana tutakuwa tuna-commit.na hata hivyo tusidhani uongozi wa taifa umekaa kimya kwa kumuogopa shibuda,na wala msidhani viongozi wa kitaifa hawana taarifa zozote wala hawakerwi na baadhi ya juhudi za kutaka kukiangusha chama,wanajua ila ni vema kuendelea kuwashauri na kuwataarifu pale tunapokuwa na taarif sahii juu ya mipango miovu ya kudhoofisha chama.
Nawasihi wapenda mabadiliko,wapenda maendeleo,wanachama wa CDM na watu wote wenye mapenzi mema tuwe na subira na tuwe na moyo thabiti wa uvumilivu.
PAMOJA TUTASHINDA DHIDI YA WALAFI WA PESA,WALAFI WA MADARAKA,MAFISADI,MAGAMBA NA KILA AINA YA UOVU,KUMBUKENI MUNGU HAJA LALA!
 
kama wengine walivyoshauari, Shibuda ni wa ku-ignore tu. Hata kule magambani walikuwa wakim-ignore ndio maana alikimbia. Hata hivyo CDM hawawezi kupoteza mda na mwendawazimu, atajiropokea na mwishowe atasepa.
 
shibuda anawaumiza akili ?????????????????, ooooh noo, you must be kidding , the whole situation is under control , tulieni , tulie , kwani hamjui stori ya humpty dumpty , JUST WAIT FOR THE GREAT FALL, Viongozi wa CDM Ni watu makini, na SHIBUDA ni sisimizi tu , kuna kitu kina mpa jeuri , na soon atakitopeza , Then utamwisho wa stori za huyu kirusi
Seen....
 
ilijulikana toka mwanzo kuwa kanunuliwa,uzuri wetu watanzania espacially tunaotaka ukombozi wa nchi hii,kwa hali zote,hatuwezi kuyumbishwa na shuda,cha maana; tunapaswa kuwa tayari kwa lolote ambalo litakuja kuharibu harakari hizi za ukombozi.shibuda; amezoea maisha ya kununuliwa,siku zijazo atajiuza hata mwili wake maana soko la uchochezi limefikia mwisho.
kama tunavyosema,nguvu ya uma ndo iliyochangia chadema kufuka hapa ilipo,hiyo hiyo nguvu ya uma itamtia adabu huyo kibalaka asiye na utu hata wa kuwajali wapiga kura wake.

together we can, and naamini Mungu yupo upande wetu kwa dua na sala zinazofanywa na watanzania wenye nia njema na nchi yao.
 
Wana JF na wanaokipenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA,

Napenda kuchukua fursa hii adhimu kuwataka Uongozi wa juu CHADEMA kuwa makini sana na kauli tata ambazo zimetolewa na Mhe. Steven Wassira - MB wa Bunda kupitia tiketi ya CCM na Mhe. John Shibuda-MB wa Maswa Magh. kupitia tiketi ya CHADEMA. Nasema ni kauli tata kwa sababu kwanza zinafanana madhui yake na pili zinalenga kuibomoa CHADEMA kwa kila hali.

Kauli ya Mhe. Wassira al-maarfu kama Tyson imedai kuwa CHADEMA ni kampuni binafsi ya Bwana Edwin Mtei iliyojaa ukabila na dini hivyo CHADEMA haipashwi kupewa kushika dola(utawala). Bwana Tyson akaendelea kusema kuwa Watanzania wategemee kuona matatizo makubwa sana yakikikumba chama hicho na katika miaka michache ijayo kabla ya Uchaguzi wa 2015 CHADEMA itakuwa imekufa kabisa!!!Kwa kauli hii ambayo imetolewa na kiongozi wa Serikali ya CCM ambaye ni MB na Waziri anayeshughulikia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Mahusiano ya Jamii inaleta maswali mengi sana kuliko majibu.

Wassira huyuhuyu tulimsikia kwenye kampeni za Arumeru East akidai kuwa, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991. Baada ya taarifa hizo KANISA Katoliki nchini lilimtaka Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.Madai hayo yalitolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi. Sina hakika kama Wassira alitekeleza agizo hilo la Kanisa Katoliki.

Juzi Bwana John Madale Shibuda aliibukia kwenye Mkutano wa NEC Dodoma akiomba kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2015 kwa kupitia tiketi ya CHADEMA lakini kampeni zake zifanywe na Rais Kikwete aliyeko madarakani sasa. Kauli hii imewaacha Watanzania wengi midomo wazi na hasa Viongozi wa CHADEMA na wale wa CCM! Kwa mazingira ya kawaida haiwezekani Mbunge wa chama pinzani akaomba kugombea nafasi kwa ngazi fulani lakini kwa kuomba afanyiwe kampeni na Chama Tawala. Haingii akilini asilan! Shinuda huyuhuyu amekuwa kipingana na Sera za chama chake-CHADEMA kila leo. Alipinga wazo la CDM kukataa Wabunge kulipwa posho akaungana na Wabunge wa CCM kutaka posho hizo zisifutwe! Sasa basi kwa kuangalia kauli hizi za Bwana Wassira na Bwana Shibuda zinaonekana kufanana kwa kila hali.

Kwamba lengo la hawa jamaa 2 ni kuivuruga CHADEMA na hatimaye iweze kusambaratika kabla ya 2015 na hivyo basi kuacha nafasi kwa CCM kushinda kirahisi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015. Ikumbukwe kwamba Shibuda alitokea CCM baada ya kuenguliwa kwenye kura za maoni akaamua kutimkia CHADEMA. Yaelekea hapa kulikuwa na mchezo ukichezwa makusdi na CCM ili iweze KUPANDIKIZA MAMLUKI wake ndani ya CDM na hatimaye waweze kufanya kazi yao kwa urahisi kuibomoa CHADEMA. Kwa hiyo basi Wassira na Shibuda wana agenda moja tu,kuisambaratisha CHADEMA, chama kinachoonekana kuwa tishio kwa CCM mapema na haraka iwezekanavyo kabla ya 2015.

Hii game inachezwa kwa utaalamu wa hali ya juu kati ya CCM na Shibuda. Watu na hasa viongozi wa CDM lazima walione hili na wachukue hatua za MAKSUDI kuinusuru CHADEMA. Kwa sasa vita ya kuisambaratisha CDM inapigwa nje na ndani ili kuimaliza CDM! Kauli za Wassira na Shibuda ziko dhahiri kabisa. Kwa hiyo mimi kama Mtanzania mwenye uchungu na nji hii napenda kuwaomba viongozi wa CDM kwa ujumla wao washikane pamoja na waanze kupambana na umafia,uhuni na upuuzi huu wa CCM wa kutaka kuingilia vyama vya upinzani kwa kupandikiza vibaraka na mashushu ili kuua upinzani.

Jambo la kwanza kabisa kuhusiana na kauli hizi tete za Shibuda ni kumweka kikao na ahojiwe aeleze nini nia na madhumuni yake na hatimaye atimuliwe ndani ya Chama kwa kufutiwa uanachama. Lakini pia kwa kauli za Wassira ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Jamii) ashtakiwe Mahakamani kwanza kwa kuwakashfu viongozi wa CHADEMA na pili kwa kusema UONGO kutoa KAULI ZA UCHOCHEZI na kati ya Kanisa, CHADEMA na Wananchi.

Msajili wa Vyama John Tendwa ameisajili CHADEMA kama Chama cha siasa na siyo Kampuni binafsi ya Edwin Mtei. Kama Wassira ana uthibitisho huo aupeleke Mahakamani vinginevo akae kimya na apelekwe kwa Pilato afungwe au apigwe faini kwa uzushi. Waasira yuko Ofisi ya Rais kama Waziri kwa kazi Maalumu ya KUUA upinzani na ndiyo maana Kiwete kamwacha maksudi pale hata baada ya mabadiliko ya Baraza Jipya la Mawaziri.

Kila Mtaznania anajua kazi ya Wassira Bungeni ni KULALA NA KUKOROMA wakti wote wa vikao. Hana mchango wowote ziadi ya KUPINGANA NA VIONGOZI WA UPINZANI.

Naomba kuwasilisha.
 
Hivi mpaka leo hii bado kuna Mtanzani mwenye akili timamu aliyebahatika kupata hata hako ka-elimu ka ngumbaru anayefurahia vyama vya upinzani vihujumiwe na Chama Cha Mafisadi? Ama kweli ishu ya ukombozi ni ngumu hasa kwa kuwa wale wanaokombolewa wanapanga mbinu pori kuhakikisha utumwa wao unabaki kuwa wa kudumu! Shibuda kwani ni nani mpaka apate dakika za kujadiliwa? Pengine angeweza kufaulu ikiwa angewahi kuja na hatua yake hiyo ya kiusaliti. Lakini too late kuudhibiti moto wa CDM ambao umeshakolea katika majani makavu ya nyika kubwa Tanzania. Too late, traitor!!!!
 
Jinsi CHADEMA watakavyo handle hii ishu, ni kipimo kikubwa sana kwao. So far BAVICHA wamekurupuka. na kwa bahati mbaya badala ya kusikiliza upande wa pili wa shilingi watu wameshamhukumu Shibuda. ukiwauliza HIVI SHIBUDA ALISEMA NINI EXACTLY HAWAJUI!!!. Zaidi ya kusikiliza na kusoma propaganda machine zenye kuziandama "Sauti huru" ndani ya Chadema, hakuna kingine wanachosikiliza. IFAHAMIKE, ILIKUWEPO SAUTI HURU YA CHACHA WANGWE!- PROPAGANDA MACHINE ILIMUANDAMA VILIVYO, IKAJA SAUTI HURU YA ZITTO KABWE- MACHINE HII HAILALI , UTANI WA KISIASA WA SHIBUDA- MACHINE HII INAONA KAMA "THIS IS TOO MUCH". lakini ndani ya Chadema zishatolewa kauli mbaya sana zaidi ya "Jk kuwa campaign manager wa Shibuda". Zishatolewa kauli za (1) Masanduku ya Kura kutoka South Africa (2) Zishatolewa kauli za Uasi na uhaini dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Mbunge wa Chadema Nasari (3) Zishatolewa Kauli za "Waislamu ni wengi kwenye tume ya Katiba" Kauli zote hizi PROPAGANDA MACHINE YA CHADEMA IKO KIMYA KWA MAANA WANAOZITOA WAKO UPANDE WA "WASTAHIKI". KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA CHADEMA HAIWEZI KUTHRIVE NA KUWA CHAMA CHENYE KUTOA PICHA NA ISHARA YA KURIDHISHA MBELE YA WANANCHI!.
 
Wakati wenzao wa CCM wakionyesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa hata kufikia kuwakaribisha wapinzani wao wakuu katika vikao na shughuli zao, CHADEMA wao wako busy kufanya character assasination dhidi ya watu wao wenyewe. haihitaji kuwa mtaalamu wa nyklia kujua kwamba kuna campaign ya chini chini ya kuwaharibia/kuwafunika ZITTO na SHIBUDA ndani ya CHADEMA. Propaganda machine iliyofunguliwa kwa kasi ya kutisha dhidi ya ZITTO miezi kadhaa iliyopita naona kwa sasa imeelekezwa kwa shibuda. hii haijengi chama, bali inakibomoa. KAMA CHADEMA WANASHINDWA KUONA ASSET NDANI YA UWEZO WA KUJENGA HOJA WA ZITTO, na pia WANASHINDWA KUTOFAUTISHA SENSE OF HUMOR YA MHESHIMIWA SHIBUDA na USERIOUSNESS WA ISSUES je chama hiki kinaweza kusimama na kujidai kwamba kimekomaa?. Kauli ya kukibomoa chama wala haikutolewa na SHIBUDA- Kauli ya kukibomoa chama ilitolewa na Mzee Mtei, Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema na Muasisi juu ya kuwemo kwa Waislamu wengi katika tume ya Katiba. KAULI HII AMBAYO MZEE MTEI HAJAIKANUSHA WALA KUOMBA RADHI NDIYO KAULI ILIYOIHARIBIA CHADEMA KWA KIWANGO KISICHOELEZEKA KULIKO KAULI YA "UJIRA WA MWIHA" AU "KUMUOMBA JK AMFANYIE CAMPAIGN SHIBUDA". Tulitegemea Chama makini kimuhoji mzee Mtei na kumlazimisha kuwaomba msamaha watanzania kwa kauli divisive, ya chuki, ya udini na YA KUKIHARIBIA CHAMA MBELE YA UMMA!.Mnamlaumu Shibuda eti amekiharibia chama mbele ya umma kwa kuunga mkono Posho bungeni- JE NI NINI KILICHO BORA, KUWA MUWAZI KWAMBA UNAZIUNGA MKONO POSHO AU KUJIFANYA UNAPINGA HUKU UKIZICHUKUA?. NI NANI MNAFIKI HAPO?.Kiufupi ni kwamba BAVICHA WAMECHEMSHA, na siasa siyo ugomvi wala vita. MATAMKO HAYA YA BAVICHA YANAISAIDIA CCM ZAIDI kuliko CHADEMA. yanawafanya CCM waproject "Cool" image mbele ya wananchi, kwa kuonekana kwamba ni chama chenye kuweza kupingana na wapinzani bila kupigana, KITENDO CHA CCM KUWAKARIBISHA NA KUWAPA JUKWAA WAPINZANI WAO WAKALI KAMA MREMA NA SHIBUDA kunaisaidia CCM ionekane chama kilichokomaa mbele ya Umma.Wakati CCM wakiproject "cool" image mbele ya wananchi CHADEMA wao wanaproject "Reactionary" image mbele ya umma. SIAMINI KWELI CHADEMA HAWAJUI TOFAUTI YA UTANI WA KISIASA NA SIASA YENYEWE. hivi kweli Shibuda kutamka JK awe campaign manager wake ni serious issue ya kutumia wino na karatasi pesa za walipa kodi(Ruzuku) hivi hivi?.KITU KINGINE NI KWAMBA BAVICHA WANAMLAUMU SHIBUDA BILA KUTOA QUOTE NZIMA YA SHIBUDA ALITAMKA NINI, JE HUU SIYO UONEVU?- IWAPO WALIMCHUKUA OUT OF CONTEXT JE WATAREPAIR VIPI DAMAGE WALIYOIFANYA?.Mwisho namshauri Shibuda awashitaki hawa Bavicha katika vikao vikuu vya Chama, kama haki isipopatikana basi awashitaki kwa Wanachama. na WATANZANIA WANAELEWA PUMBA NA MCHELE NI UPI

Kwenye bviTa wanatanianaga!!!
 
Kwa wakuu wote wa chadema na wapenda mabadiliko
kwa taarifa za uhakika tulizo nazo Shibuda na wenzake 27 waliopenyezwa ama kujipenyeza ndani ya chadema wamekubali kutumika kuimaliza kwa gharama ya Mil150 peke yake
tunasikia wamepewa kazi ya kuleta mvurugano ndani ya chama kwa kusudi moja tu nalo ni kuifanya chadema ianze kazi ya kutatua migogoro ndani ya chama na ccm iweze kutumia nafasi hiyo kijipanga,Bwana Benson Bana ndiye aliyekuja na idea na kupata nguvu kwa kuungwa mkono na VIONGOZI WA JUU wa ccm,chadema hiyo taarifa ifanyieni kazi haraka sana
Slaa na timu yake ni watu makini na kama wameweza kukachero na kupata habari nyeti na za siri kubwa kubwa basi hii nayo kama ipo basi tayari watakuwa nayo na inafanyiwa kazi.
 
Ndugu wana jamii forum, wanachadema,wapenda madiliko.na wapenda maendeleo
salaaaam..... napenda kuupa pole uongozi mzima wa chadema.
kwani mgogoro huu si mdogo kama ambavyo watu wengi wanaweza kuutazama
haraharaka. jamani kwa tunaomfahamu shibuda huyu ni mtu hatari sana
na huu ndio muda muafaka kwake kufanya alichoagizwa, ushawishi wa shibuda maeneo anayotoka ni mkubwa mno.
na huu ndo mtego mkubwa kwa chadema. kwani anchokifanya shibuda kutaka kuigawa
chadema kikanda na hivyo kupoteza nguvu. naamini chadema mlimpokea huyun mtu bila kumjua
ushauri tiba ya haraka iinahitajika ili chadema ibaki salama.
 
nadhani watanzania sio watu wakushawishiwa tena,pia wingi wa maneno ya shibuda sio sababu ya yeye kukubalika.
kama anaona anayo mambo ya msingi apande jukwaani na awaambie wananchi.
pia penye wengi hapakosi migongano hata katika utendaji,lakini tunatazama migongano hii inaathari gani kwa wananchi na taifa kwa ujumla:? kama matatizo yake shibuda ni kati yake na uongozi nadhani hiyo ni juu yake. kama chama,hatuna haja ya kutumia mda mwingi kushambuliana na shibuda,tunazo kanuni na taratibu za chama,naomba zitumike kulimaliza hili.
nape alipoongelea mgombea binafsi alimaanisaha kumtumia shibuda kuharibu cdm.na wakifanikiwa tu,utasikia mgombea binafsi haruhusiwi.
 
kwa bahati mbaya, ccm wamechelewa kuianzisha hii move, nadhani chadema waendelee kumshukuru mungu kuwepo Kwa uhuru wa vyombo vya habari, mitandao na pia wanaharakati, wao ccm muda si mrefu watapoteana, tusubiri. tunajua kuwa pesa itatumika kuiangamiza CDM, Ila pesa haina nafasi kwa wanamageuzi
 
Ndugu wana jamii forum, wanachadema,wapenda madiliko.na wapenda maendeleo
salaaaam..... napenda kuupa pole uongozi mzima wa chadema.
kwani mgogoro huu si mdogo kama ambavyo watu wengi wanaweza kuutazama
haraharaka. jamani kwa tunaomfahamu shibuda huyu ni mtu hatari sana
na huu ndio muda muafaka kwake kufanya alichoagizwa, ushawishi wa shibuda maeneo anayotoka ni mkubwa mno.
na huu ndo mtego mkubwa kwa chadema. kwani anchokifanya shibuda kutaka kuigawa
chadema kikanda na hivyo kupoteza nguvu. naamini chadema mlimpokea huyun mtu bila kumjua
ushauri tiba ya haraka iinahitajika ili chadema ibaki salama.

Huu sio wakati wa usanii wa maneno matamu ya ghilba au mikwala mbuzi tena! Watu wa kanda tajwa watamfuata huyo shibuda kwa kuwaletea maendeleo na sio ngonjera zake ambazo hazileti sembe!
 
Good analysis makoye2009

Binafsi nina imani nyingi sana na viongozi wa ngazi ya juu wa chadema hususani KAMANDA MBOWE na DR SLAA. Kamanda mbowe alishawai kudhungumza kwamba yupo ktk siasa za upinzani (chadema) zaidi ya miaka 20 sasa, matunda yake yameanza kuonekana sasa (chadema kuaminiwa na watanzania), kwa hiyo hatoruhusu either kirusi, mamluki, pandikizi kutaka kuivuluga chadema, KASEMA HATORUHUSU HILO LITOKEE, Big up M/kiti Mbowe.

chadema long live
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom