John Shibuda na mgogoro wa Kauli ya kuisifia CCM; Kauli za wana CHADEMA

Mbunge wa maswa mashariki (Chadema) Mh. Magale Shibuda amewapa siku 3 bavicha wamtake radhi yeye na wapiga kura wake kuhusu kutoa kauli kwenye NEC ya ccm kugombea urais anasema wana fikra hasi na kusahau kuwa yeye ni mjumbe wa APRM mpango wa kujitathimini africa kwa hiyo alikuwa anatoa mada kwenye NEC.

Mada yenyewe ni Kugombea urais siyo!!!!!!!!!!!! Huyu ndiyo anaelekea mwisho..
 
OPEN MINDEDNESS IS WHAT IS REQUIRED

Mimi sielewi na sitoelewa kwa nini Mheshimiwa Shibuda ashupaliwe kama vile amefanya ufisadi. Alichofanya Mheshimiwa Shibuda ni kitendo kinachoonyesha kuwa amekomaa kisiasa na hana kinyongo. Amewataka BAVICHA kumuomba radhi kwa kuwa wanathitaji kufahamu siasa; sio chuko, Sio uhuni bali ni uungwana na kuwa open minded.

BAVICHA na wao kama ni waungwana na wanajua siasa, watajua la kufanya na sio kulumbana na Mheshimiwa Shibuda. Tena Shibuda anapaswa apewe nafasi ya kugombea Urais 2015 na CDM.
 
amegundua kuwa anaogelea kwenye maji ya kaskazini wakati yeye ni wa magharibi.amegundua kuwa aliingia choo cha kike
 
Shibuda anaposema BAVICHA imuombe radhi anafikiri BAVICHA ni Heche na wenzake tu jambo ambalo anajidanganya maana BAVICHA si wakina Heche tu bali na sisi vijana wote wa CDM so huyu mzee ni sawa na MALAYA wa kisiasa na sisi BAVICHA hatuwezi kumuomba msamaha hata kidogo.
CHADEMA MNASUBIRIA NINI? PIGENI CHINI HUYU LOFA MAANA SI WA KUCHEKEWA HATA KIDOGO HUYU MALAYA WA KISIASA. MJINGA SANA.......... Katuboa sana huyu shibuda.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO- CHADEMA-
MKOA WA SINGIDA​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA BARAZA LA VIJANA CHADEMA MKOA WA SINGIDA.

Taarifa kwa Vyombo vya habari na Umma wa watanzania.
Waheshimiwa waandishi wa habari, na watanzania wote kwa ujuma.
Tumewaiteni hapa leo mchana, kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wetu wa Baraza la vijana wa CHADEMA- Taifa.
Watanzania wamehangaika miaka mingi, wanajua shida walizopata, wanajua jinsi Chama cha Mapinduzi ambavyo hakikuwasaidia, wananchi wamebaki katika maisha magumu siku zote, shida mbalimbali, zikiwemo manyanyaso yanayotokana na serikali ya chama cha mapinduzi. Tunasisitiza kuwa ni kweli mabadiliko yanahitajika kwa sasa, watanzania wanahitaji mabadiliko na mabadiliko ni lazima.
Kama alivyosema Baba wa Taifa, Tumeonewa kiasi cha kutosha; tumenyonywa kiasi cha kutosha; tumenyanyaswa (tumetumikishwa) kiasi cha kutosha; na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Ni unyonge wetu uliotufanya tuonewe, tunyonywe, tunyanyaswe na tupuuzwe. Sasa tunataka mapinduzi ili tusionewe, tusinyanyaswe na tusipuuzwe tena. Huo ndio unapaswa kuwa msimamo wa watanzania wanaotaka mabadiliko ya sasa ambayo kweli tutake tusitake tunayahitaji kwa nguvu zote.
Hivyo Baraza la vijana Mkoa wa Singida, kama ilivyo kwa Baraza la vijana kitaifa ni kuwa hatuko tayari kuvumilia Kiongozi yeyote wa CHADEMA, au Mbunge yeyote wa CHADEMA anayesaliti harakati za mapambano kuelekea mabadiliko na Uhuru wa kweli unaohitajika kwa watanzania, na kwa manufaa ya watanzania. Nasisitiza kuwa Vijana wa CHADEMA, Tuseme ukweli ili Taifa la Tanzania linufaike liendelee kudumu. Wabunge wanaoona kuwa CHADEMA, ambacho ndicho chama pekee cha Upinzani nchini hakifai, na ambao wapo CHADEMA waende kule wanapona kunafaa tena haraka, kuliko kudhalilishana kwa misingi isiyo kidhi haja za kisiasa, kielimu wala hazina mantiki zinapotafakariwa na watu wenye akili timamu. BAVICHA tunasisitiza kuwa wabunge wa CHADEMA ambao wanashiriki vikao au kuomba makada wa CCM kuwasaidia kufanya mabadiliko, hasa viongozi wa CCM walioifisadi nchi yetu, wabunge hao ni wasaliti, na iwe mchana, gizani, au usiku. Chini, pembeni, juu au kando kando HATUWAUNGI MKONO, na hawafai kwa safari yetu ya mabadiliko. Shibuda ametudhalilisha kama Chama, kwenda kutangaza nia ya kugombea Urais kwenye Kikao cha CCM, na kumwomba Kikwete ambaye Chama chetu kwa niaba ya watanzania kinamtuhumu kwa ufisadi kuwa Meneja wa Kamepni, Hivyo tunasisitiza kuwa tunaunga mkono tamko la BAVICHA TAIFA.Ikiwezekana achukuliwe hatua za kinidhamu ndani ya CHAMA

Josephat Isango
MWENYEKITI-BAVICHA MKOA
SINGIDA.

kwani isango we ni nani hasa,una ujanja gani wa kufukuza wanachama???umeingiza wangapi hadi uweze kufukuza,au njaa ndio inakutuma kusema kinachokuwa karibu na mdomo kwa hulipii
 
shibuda ametuvua nguo wanacdm.
Mlimkaribisha wenyewe na mkampa kadi ya uanachama kwa mbwembwe.
Hamkujua mmeingiza nini, sasa tunasubiri sakata la "civil warfare" ndani ya CDM, mimi natafuta popcorn na kuvuta stuli, nishaagiza bia baaardi!
 
kwani isango we ni nani hasa,una ujanja gani wa kufukuza wanachama???umeingiza wangapi hadi uweze kufukuza,au njaa ndio inakutuma kusema kinachokuwa karibu na mdomo kwa hulipii

jiangalie sana bwana mdogo TAMUCHUNGU ikiwezekana kapime akili hauko sawa kama baba shibuda
Kwanza ilikua lazima uquote maandishi yote hayo kisa uandika pumba zako?ninamasha na uwezo wako wa ubongo
 
Last edited by a moderator:
Mlimkaribisha wenyewe na mkampa kadi ya uanachama kwa mbwembwe.
Hamkujua mmeingiza nini, sasa tunasubiri sakata la "civil warfare" ndani ya CDM, mimi natafuta popcorn na kuvuta stuli, nishaagiza bia baaardi!
Usiifananishe chadema na CUF....ingekuwa chedema watu wa kukurupuka shibuda angesha ondolewa siku nyingi sana lakini angalia wanavyoenda nae... hata madiwani chadema haikukurupuka leo wako wapi?.....
 
Mkuu Shardcole,shibuda haijui maana halisi ya nguv ya umma sasa wakati umemfika, kilio chake kimefika kwenye kiti chetu cha kunesanesa si alizani sisi ni kalunguyeye kama alipotoka!
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA kama chama makini tunachokitegemea kushika dola na kuwawajibisha mafisadi wote sasa mbona mnatuangusha? Tunasikia tu BAVICHA peke yao ndio wanatoa tamko lakini nyie mtaifa mmekaa kimya sasa sijui mnamuogopa shibuda? Kwa hali hii basi huu utakuwa ni mwanzo mpya wa kuyumbishwa na virusi kwa maana Viongozi wetu taifa mna ugonjwa wa kuogopa, yaani mnakomaa na visangara na vidagaa na mnashindwa kukoma na mapapa! Shame on CDM kama hali ndio hii kwani haiwezekani siku ya 3 sasa nyie mmekaa kimya tu alafu sisi ndo huwa tunawashtumu CCM kwa kuwalea mafisadi huku nyie wenyewe bado mnalea virus CDM, sasa sisi BAVICHA tufanye nn na wakati nyie uongozi wa taifa mmekuwa majoka vibisa.
 
Shibuda anataka kutuvuruga ametumwa na mabosi wake, hawezi kuombwa radhi kwa upuuzi wake akitaka arudi CCM hatumtaki, very stupid
 
CHADEMA kama chama makini tunachokitegemea kushika dola na kuwawajibisha mafisadi wote sasa mbona mnatuangusha? Tunasikia tu BAVICHA peke yao ndio wanatoa tamko lakini nyie mtaifa mmekaa kimya sasa sijui mnamuogopa shibuda? Kwa hali hii basi huu utakuwa ni mwanzo mpya wa kuyumbishwa na virusi kwa maana Viongozi wetu taifa mna ugonjwa wa kuogopa, yaani mnakomaa na visangara na vidagaa na mnashindwa kukoma na mapapa! Shame on CDM kama hali ndio hii kwani haiwezekani siku ya 3 sasa nyie mmekaa kimya tu alafu sisi ndo huwa tunawashtumu CCM kwa kuwalea mafisadi huku nyie wenyewe bado mnalea virus CDM, sasa sisi BAVICHA tufanye nn na wakati nyie uongozi wa taifa mmekuwa majoka vibisa.

Tulia Kamanda,
CHADEMA hawakurupuki. wakitoka wanatoka na tamko la uhakika.
 
Mlimkaribisha wenyewe na mkampa kadi ya uanachama kwa mbwembwe.
Hamkujua mmeingiza nini, sasa tunasubiri sakata la "civil warfare" ndani ya CDM, mimi natafuta popcorn na kuvuta stuli, nishaagiza bia baaardi!

malaya kama hawa wapo wengi Shiverz.
 
Back
Top Bottom