John Mnyika ana elimu gani? Uwezo wake wakujibu hoja unatokana na mafunzo ya maprofesa wa bongo au akili za kuzaliwa?

Kosa lake kuu ni kusaini barua ya kina Mdee na baadae kukana kuwa sio yeye
Acha kutufanya wapumbavu. J.J Mnyika aliwezaje aliwezaje kupeleka list ya majina ikiwa na jina moja la Mwanachama aliyekuwa Gerezani?? Na je ni nani aliyetoa kibali cha kumuondoa usiku Mwanachama yule Gerezani kisha kumuwahisha Dom kwenda kuapishwa??
 
Kwani alisema katiba kuruhusu rais kuwa dictator alisema kama sifa au udhaifu wa hiyo katiba? Sisi wengine sio waumini wa katiba hii, hivyo ni haki yetu kuwapinga wanaotumia udhaifi wa katiba hii kuleta ulevi wa madaraka.
Bado ,unakosea mkuu ,huwezi kuwapinga wanaosimamia katiba na katiba inawaruhusu wafanye hivyo , naweza ungana nawewe ukisema tunatakiwa kuikataa katiba iliyopo inayosimamiwa na viongozi

Narudia ,kikwete alitoa hisani kwa vyama vya upinzani na wao wakabweteka ,hivyo nitabakia kumshukuru maguguli kutuonesha palipokuwa panavuja na panapoendelea kuvunja
 
Katika interview ambazo zilikuwa na maswali marahisi kwa mtu neutral lakini maswali magumu kwa mwanasiasa ni interview ya juzi Clouds kati ya Mnyika na wanahabari wa chombo hiki.

Lakini kati ya story zote zilizojitokeza unamwona Mnyika akichambua na kujibu maswali na hoja zote kiuhalisia bila kuzua mjadala kuhusu uhalali wa majibu yako. Hakuna majibu yakupika

Lakini eneo la pili anaonekana wazi siyo mwanasiasa bali ni binadamu mwenye uwezo na ufahamu sahihi kuhusu mahitaji ya Dunia kabla,sasa na baadaye. Anatambua wazi kwamba CHADEMA siyo nchi bali ni chama cha siasa kilichoundwa kukidhi matakwa ya mfumo wa kisiasa na kwamba kupitia taasisi hii upo uwezekano mkubwa wa binadamu waliopo ndani kupishana kimtazamo.

Mfano mzuri ni pale alipokiri kwamba yeye binafsi alikataa kumpokea Lowasa, lakini mwisho akaona kiu ya kisiasa ya kuiondoa CCM madarakani iliyokuwa ndani ya watu walio wengi na hapo ndipo alikubali kuendelea kutokukubaliana na msimamo wa chama kuhusu aina ya mgombea wao lakini akaamua kuunga mkono maono ya wananchi ya kuiondoa CCM madarakani.

Tafsiri kubwa hapa anatuambia si chadema wala CCM wanaoweza kuitoa nchi hapa ilipokwama isipokuwa watanzania kuamua kuunda mfumo wa kikatiba unaotoa haki na unaosimamia nidhamu ya kisiasa na serikali. Incase tukipata mfumo sahihi wa kikatiba may be tunaweza kufuata mfumo wa Kenya ambapo ikifika uchaguzi zinaundwa pande mbili let say UPANDE YANGA NA UPANDE WA SIMBA AU NG'OMBE NA MBUZI AU KUSHOTO NA KULIA THEN MNAUZA SERA WANANCHI WANACHAGUA.

Maono ya Mnyika yanatufumbua macho kwamba tuache imani kwa chama tubaki na imani ya nchi. Kenya wanapiga hatua kwa sababu hakuna akili zinazosubiri kuwa chawa zipewe nafasi....kila nafasi inamgumo wa ushindani.

Lakini jambo la mwisho kuhusu John Mnyika ni uwezo wake wakusimama kama Katibu mkuu na chama kubaki imara kipindi cha JPM. Kusimama imara kutetea chama dhidi ya waovu wa tume ya uchaguzi ambao walifikia hatua yakughushi nyaraka na kuzipeleka Bungeni.......Mnyika amesema wazi kwamba Tume ya Uchaguzi haijawahi kuonyesha popote barua yakuwapitsha akina Mdee iliyodaiwa kutolewa na Chadema. Maana yake anakiri kwamba pamoja na mawimbi mazito alisimama kama katibu mkuu na itoshe kusema kwamba huyu ndiye katibu mkuu bora kuwahi kutokea baada ya Mzee Kinana na Dr. Slaa. Katika mazingira ya kawaida, Mbowe alifahamu msimamo wa Mnyika dhidi ya Lowasa lakini alidiriki kumpendekeza kuwa katibu mkuu jambo ambalo siyo dogo. Uvumilivu wake ungekuwa mdogo angeungana na Slaa na matokeo yake angekuwa ameshapoteza dira kisiasa au ni DC kama walivyo akina Nassary, Mashinji nk

Natamani atunukiwe nishani ya utumishi uliotukuka
Mnyika kichwa kile ,
Tanzania one ya zamani ile
 
Bado ,unakosea mkuu ,huwezi kuwapinga wanaosimamia katiba na katiba inawaruhusu wafanye hivyo , naweza ungana nawewe ukisema tunatakiwa kuikataa katiba iliyopo inayosimamiwa na viongozi

Narudia ,kikwete alitoa hisani kwa vyama vya upinzani na wao wakabweteka ,hivyo nitabakia kumshukuru maguguli kutuonesha palipokuwa panavuja na panapoendelea kuvunja
Ni wapi wapinzani wameikubali katiba hii Hadi useme nakosea? Katiba hii kuendelea kuwepo sio kuwa inakubalika.
 
Katika interview ambazo zilikuwa na maswali marahisi kwa mtu neutral lakini maswali magumu kwa mwanasiasa ni interview ya juzi Clouds kati ya Mnyika na wanahabari wa chombo hiki.

Lakini kati ya story zote zilizojitokeza unamwona Mnyika akichambua na kujibu maswali na hoja zote kiuhalisia bila kuzua mjadala kuhusu uhalali wa majibu yako. Hakuna majibu yakupika

Lakini eneo la pili anaonekana wazi siyo mwanasiasa bali ni binadamu mwenye uwezo na ufahamu sahihi kuhusu mahitaji ya Dunia kabla,sasa na baadaye. Anatambua wazi kwamba CHADEMA siyo nchi bali ni chama cha siasa kilichoundwa kukidhi matakwa ya mfumo wa kisiasa na kwamba kupitia taasisi hii upo uwezekano mkubwa wa binadamu waliopo ndani kupishana kimtazamo.

Mfano mzuri ni pale alipokiri kwamba yeye binafsi alikataa kumpokea Lowasa, lakini mwisho akaona kiu ya kisiasa ya kuiondoa CCM madarakani iliyokuwa ndani ya watu walio wengi na hapo ndipo alikubali kuendelea kutokukubaliana na msimamo wa chama kuhusu aina ya mgombea wao lakini akaamua kuunga mkono maono ya wananchi ya kuiondoa CCM madarakani.

Tafsiri kubwa hapa anatuambia si chadema wala CCM wanaoweza kuitoa nchi hapa ilipokwama isipokuwa watanzania kuamua kuunda mfumo wa kikatiba unaotoa haki na unaosimamia nidhamu ya kisiasa na serikali. Incase tukipata mfumo sahihi wa kikatiba may be tunaweza kufuata mfumo wa Kenya ambapo ikifika uchaguzi zinaundwa pande mbili let say UPANDE YANGA NA UPANDE WA SIMBA AU NG'OMBE NA MBUZI AU KUSHOTO NA KULIA THEN MNAUZA SERA WANANCHI WANACHAGUA.

Maono ya Mnyika yanatufumbua macho kwamba tuache imani kwa chama tubaki na imani ya nchi. Kenya wanapiga hatua kwa sababu hakuna akili zinazosubiri kuwa chawa zipewe nafasi....kila nafasi inamgumo wa ushindani.

Lakini jambo la mwisho kuhusu John Mnyika ni uwezo wake wakusimama kama Katibu mkuu na chama kubaki imara kipindi cha JPM. Kusimama imara kutetea chama dhidi ya waovu wa tume ya uchaguzi ambao walifikia hatua yakughushi nyaraka na kuzipeleka Bungeni.......Mnyika amesema wazi kwamba Tume ya Uchaguzi haijawahi kuonyesha popote barua yakuwapitsha akina Mdee iliyodaiwa kutolewa na Chadema. Maana yake anakiri kwamba pamoja na mawimbi mazito alisimama kama katibu mkuu na itoshe kusema kwamba huyu ndiye katibu mkuu bora kuwahi kutokea baada ya Mzee Kinana na Dr. Slaa. Katika mazingira ya kawaida, Mbowe alifahamu msimamo wa Mnyika dhidi ya Lowasa lakini alidiriki kumpendekeza kuwa katibu mkuu jambo ambalo siyo dogo. Uvumilivu wake ungekuwa mdogo angeungana na Slaa na matokeo yake angekuwa ameshapoteza dira kisiasa au ni DC kama walivyo akina Nassary, Mashinji nk

Natamani atunukiwe nishani ya utumishi uliotukuka
Nakubaliana na tathimini yako
 
Baada ya kusema hayo alipaswa aulizwe kuwa kughushi ni kosa la jinai, baada ya yeye kugundua hao wabunge 19 wameingia Bungeni kwa barua ya kughushi alipaswa afanye nini?. Ofisi yoyote haipaswi kuonyesha nyaraka yoyote ya kiofisi kwa yeyote, hao NEC wamuonyeshe Mnyika barua ya kutoka Chadema kama nani?.

Chadema na Mnyika walichopaswa kufanya baada ya kugundua kuna forgery
1. Kuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike.
2. Uchaguzi ungethibitisha jinai ya forgery
3. Baada ya jinai ya forgery kuthitishwa, NEC wange withdrawal zile barua za uteuzi
4. Bunge lingewafuta ubunge
5. Nafasi 19 za viti maalum Chadema zingetangazwa kuwa wazi.
6. Chadema waligoma kupeleka majina ya wabunge wake wa viti maalum kwa hoja ya hawayatambui matokeo ya uchaguzi, hawamtambui mshindi na hawalitambui Bunge!.
7. Baada ya maridhiano, walikubaliana kugawana kitu kinachoitwa nusu mkate, hivyo sasa wanayatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020, wanamtambua rais wa JMT na wanalitambua Bunge na wanapokea ruzuku yao toka ofisi ya Msajili wa vyama.

The Best Way Forward
Kutoendelea na kesi, kuwasamehe hao 19, kujipanga kwa uchaguzi wa 2025 kama walivyo shauriwa hapa CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

P
Kumbe kuna kipindi huwa unajizima data kwa maksudi eeeeh???
 
Wakati mwingine kuwa objective katika mambo ni tatizo kwa sababu we are always surrounded by many trappings. Mfano, mtu usiyemtakia mafanikio hata akifanikiwa utaona hajafakiwa kama ambavyo wewe ungetaka. Na wengi wetu tunabaki katika level hii ya judgement. We have no good judgement on many things ana we are not ethical as well. So, our way of looking at things is often negative and we hardly affirm the good we see in other people. Ingawa binafsi napenda criticisms kwa sababu zimenisaidia sana ku'improve' katika maisha yangu binafsi, siyo watu wote wanaopenda kuwa criticised. Nilipoanza maisha nilikuwa sina vitu vingi sana na kwa nature ya kazi yangu, niliona niwe na mimi jioni naenda viti virefu kidogo. Mara habari hizo zikatoka. "Ha, mtu mwenye hana ABC, halafu karibu kila jioni utamuona akiwa amekalia kiti kirefu." Mfanyakazi wa ndani aliamua kumwaga mboga. Nilivyosikia nilikasirika sana, nitakataka kumfukuza kwa "kutoa siri nje". Lakini katika kujitafakari nikafikiri amenisaidia kwa sababu amesema vitu ambavyo sina. Nilichofanya nilichukua notebook yangu na kuorodhesha hivyo vitu ambavyo vilitupwa mtaani hata nikawa gumzo mtaani. Nilipomaliza, nikanyamaza. Kila nikipata fedha nanunua kitu kimojawapo na thank God baada ya muda fulani nikawa nime'exhaust' orodha yote na nikaendelea kunyamaza bila kusema kitu. Siku nilipohama eneo lile, likaje gari moja hivi, dereza alivyoona vitu akanishauri kwamba gari lake ni dogo sana, nitafute kubwa. Likaje kubwa, vitu vikapakiwa hata kulazimisha vienee. Wale waliokuwa wakinicheka baadaye nilisikia habari habari zao wakisema: "kumbe yule jamaa alikuwa na akili sana. Watu walimcheka, lakini yeye alijua alichokuwa akikifanya. Alikuwa na vitu vingi sana, hata vile walivyosema hana alikuwa navyo." Hili limebaki kuwa somo kwangu. Watu wakisema kitu fulani negative kinachokuhusu "note it down". Tafakari kama walichosema ni kweli au la. Kama ni kweli kifanyie kazi bila kujitangaza ili watu wenyewe ndiyo waanze kukutangaza wenyewe (wakati huo wewe kimya). This is how we should behave. Wanasiasa wetu hawataki kukosolewa, sisi wenyewe hatutaki kukosolewa, viongozi wetu hawataki kukosolewa, kinachofuata nini? Ni sifa za uwongo/flattery na kwa bahati mbaya wanasiasa wanapenda flattery, sisi tunapenda flattery na viongozi wetu wanapenda flattery. Therefore, flattery everywhere!
Mtu anakuhukumu kwa kile ulichofanya, sio unachoweza kufanya. Ukifanya unachoweza inakuwa ni surprise kwake.
 
Mtu anakuhukumu kwa kile ulichofanya, sio unachoweza kufanya. Ukifanya unachoweza inakuwa ni surprise kwake.
Kuna watu wanahukumu hata kwa kufikiri tu kwamba unaweza kufanya hivi na hata kama hufikirii hivyo, wao wameshaona utafiri hivyo. Ujue kuna watu wanaona wao ni watakatifu tangu kuzaliwa kwao na wanawaona wengine kama wakosefu tangu kuzaliwa kwao.
 
Back
Top Bottom