John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Mie sina tatizo kabisa na aliyechaguliwa kama taratibu zimefuatwa.
Ni kweli kuwa CDM walienda kuchukua taarifa za mtu kutoka vodacom MPESA? kama ni hivyo, basi huku ni kuingilia privacy ya mtu na sina hakika kama wanaruhusiwa kufanya hivyo. Privacy inakoma kuwa privacy kama kuna public interests na kazi hiyo huhitaji kibali maalum. Wao walipewa kibali hicho na nani?

Aah kwa hiyo hapa issue ni kibali, na sio rushwa sio?
 
Mie sina tatizo kabisa na aliyechaguliwa kama taratibu zimefuatwa.
Ni kweli kuwa CDM walienda kuchukua taarifa za mtu kutoka vodacom MPESA? kama ni hivyo, basi huku ni kuingilia privacy ya mtu na sina hakika kama wanaruhusiwa kufanya hivyo. Privacy inakoma kuwa privacy kama kuna public interests na kazi hiyo huhitaji kibali maalum. Wao walipewa kibali hicho na nani?

hayo yalishapita tume sahau kabisa
 
Ndugu zangu wanaJF,

Nilikuwa nafuatilia mchakato wa uchaguzi uliokuwa ukiendelea ndani ya Baraza la Vijana Chadema Taifa, nimeshtushwa sana na kauli na maneno ya baadhi ya makada wa CCM, CUF, NCCR, UPDP,UDP ect. za kutaka baadhi ya vijana wawe viongozi.

Napingana na hawa wanasiasa uchwara ambao wana kazi ya kupandikiza viongozi ndani ya CDM kwa maslahi yao binafsi. Ukikuta CCM au chama kingine cha upinzani kinamshabikia sana kiongozi fulani ndani ya CDM au anagombea nafasi ya uongozi ujue kuna mawili, kwanza ni ama huyo anayemtaka awe kiongozi ni kipandikizi chake/mamluki au ana uwezo mdogo wa akili/ hana msimamo.
Nashukuru viongozi wetu wa CDM hasa Mwenyeki na Katibu wake hili wanalifahamu vizuri. Tunakumbuka uchaguzi wa Bavicha uliopita, tumeona Kafulila ambaye walikuwa wakimpigia debe eti ndio kiongozi mzuri leo yuko wapi? hana msimamo.

Kumbuka wakati tunataka Dr. Slaa agombee urais walijitokeza watu wengi sana wakitaka asigombee, kwa sababu gani? Ukifuatilia jibu liko wazi na walikuwa wanajua atashinda na atawashughulikia. Hata sasa bado wanamuogopa sana huyu bwana.

Kumbuka wakati Zitto anachukua fomu za kugombea umwenyekiti jinsi walivyompigia debe eti anafaa, ukiangalia na kitu alichokifanya mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kafanya nini, mnashindwa nini hapa? swala ni kwamba CCM hawakotayari kuona CDM inapata viongozi waadilifu na wenye misimamo ya kweli ya kuwatetea wananchi.

Juzi kwenye kuiunda kambi ya upinzani bungeni eti CCM wanashabikia Mbowe asiwe Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, lengo ni nini, wanajua kuwa mbowe ana msimamo wa weli.

Hadi juzi kuna wadau humu JF na kwenye media zingine nawaona wakijaribu kuwabeba na kuwachafua baadhi ya wagombea.

Kitu ambacho nawashauri wana CDM ni kuwa makini sana pale wanapokuta CCM, CUF, UDP, NCCR, UPDP, etc wanawaunga mkono baadhi ya viogozi au wagombea ndani ya CDM, ikiwezekana kufanyika kwa uchunguzi mkali kwa hao wanaoungwa mkono na wapinzani wao kisiasa.
 
Wana Magamba kinachowauma nini? Heche ndio hivyo keshachaguliwa kama atauua umoja wa vijana mbona poa tu, mbona Riz1 aliwavuruga UVCCM watu tulinyamaza hebu tulieni msijifanye mna uchungu sana na CDM.
 
Naanza kwa kumshukuru sana Mwenyekiti na Katibu wake kwa jambo jema kutimiza jukumu lao la kutuletea kijana mzarendo kuongoza vijana wa Taifa hili.

Pia nawapongeza wagombea wote kwanza kupata nafasi ya kugombea na pia kwa kuaminiwa na chama kupeperusha Bendera ya chama kama Bavicha,ila tu ni kwamba alihitajika apatikane mmoja kati ya nyote,na katika siasa hamna droo,ivo tulitegema tungempata wa kuongoza jumuiya yetu kama vijana,nawapongeza.

Kwa namna ya pekee nampongeza ndugu Heche kwa kukubali kuongoza mapambano tukielekea kwenye ushindi 2015. Kushinda kwako si kuwa wewe ndo mtukuka,ni tu kwamba demokrasia ya kura imekunasa wewe,ivo kuwa bega kwa bega na wote bila makundi.

Uongozi ni mateso,hongera kwa kukubali mateso ayo. Nawatakia wanacdm maendeleo kwa kuwa mmeonesha ukomavu wa pekee ktk siasa. Tupo pamoja kuelekea 2015,hapo ndo cdm itakuwa inachukua mzigo wa kuijenga nchi mpya ya Watanzania.

Hongera sana.

Gsana.
 
Mie sina tatizo kabisa na aliyechaguliwa kama taratibu zimefuatwa.
Ni kweli kuwa CDM walienda kuchukua taarifa za mtu kutoka vodacom MPESA? kama ni hivyo, basi huku ni kuingilia privacy ya mtu na sina hakika kama wanaruhusiwa kufanya hivyo. Privacy inakoma kuwa privacy kama kuna public interests na kazi hiyo huhitaji kibali maalum. Wao walipewa kibali hicho na nani?

ndugu ktk principle of confidentiality kuna vipengele vya except. Moja inasema except if required by the law or where there substantial public interest. Ukidefine public interest kwa upande wa stakeholders,ni wazi inaweza ikawa muhimu kufanya ivo. Kabla ya kufuata data zozote ktk network service operator. Utakaa na mhusika/mteja pamoja na anayehitaji evidence mbele ya mwanasheria wa network operator. Sasa kama kila kitu kimezingatiwa kisheria,kelele zinatoka wapi? Kama cdm wameamua kufanya kisheria tatizo li wapi?
 
Khaa!! jamani, hoja ijibiwe hapa,sio mnajaza sredi kwa post za ng.uruwe pori tu,mwenye details amwage tuone!!coz naona kama kuna hoja hapa!!

Hoja iliyopo ni kwamba chama cha magamba waliingiza mamluki wao kugombea nafasi za uongozi bavicha ili baadae walete mifarakano ndani ya chama. Wameshindwa sasa wanaleta habari za umbeya na chuki za makusudi ili kuwapaka matope wanamapinduzi wazalendo
 
Ben hongera sana kufikia hatua kama hiyo still hayo ni mafanikio kuthubutu kugombea na kukubali kuenguliwa, mambo mengine ni zaidi ya ubinadamu biblia inatuambia maandalizi ya moyo ni ya mwanadamu lakini jawabu latoka kwa bwana. And in other place inasema all things happens together for gud for those who love God and are called accordimg to his will. Juzi mimi nilipewa jina usingizini kuwa John Heche atakuwa mshindi lakini I have to admit mimi wewe ndiye ulikuwa chaguo langu, kwani nimesoma sana post zako humu nami nilitokea kuwa convinced u fit the post most. Acha tuone what will come thru kama Heche atashinda please mpe ushirikiano its more than what we can see from human eyes! Be blessed!

Glory and honour be unto our God almighty!

Mimi huyo Heche hata sura siifahamu na wala sijawahi bahatika kusoma post yake hata moja hapa JF kwa jina lake. Lakini as a preacher nataka kuwaambia kwamba wakati mwingine tuelewe kuwa if the favour of God is not on your side there is nothing you can do to get whatver you want to. Utashangaa unaweza kuwa na uwezo; unapendwa na una kila sababu ya kupata nafasi lakini mazingira yanakataa. Mine choice was Ben Saanane nimekuwa nikifuatilia sana post zake hapa JF na kwakweli nilitokea kumkubali kwani alionyesha kwangu anaweza akawa kiongozi. Wagombea wengine siwafahamu kabisa na pengine wako hapo kwa ID za tofauti so let us agree kuwa '...maandalizi ya moyo ni kazi ya mwanadamu lakini jawabu la toka kwa Mungu....'

Wagombea wote please mpeni ushirikiano Heche kwani as a Prince and an evangelist nawausia kuwa his time has come na Mungu ameruhusu yeye kuwa mwenyekiti. Mkimpa ushirikiano you are humbling yourself into Godly decision na pengine kwenu ninyi this is your training (in christianity we call 'safari ya jangwani kuelekea nchi ya ahadi; Your destiny') time to go to other levels.

The way God works is whoever humbles him/herself the order is s/he should be exaulted. Mkienda against some of you are going to delay your success! This is my wor to you as a preacher and a prince; ukitaka you can take my words ukiona ni upuuzi yenyewe yatabaki yenye nguvu na mwisho wa siku penda usipenda utayakuta yanakusubiri kuku kumbusha that I once adviced you! Best wishes to all contenders....Prince Ame in the Kingdom of Heaven!
 
ChademaTarime200810131.jpg



 
Nani anajua kwa undani kwamba CDM walienda Vodacom M-PESA kuchukua taarifa za mtu? Au tunajadili majungu? Kama walipewa ina maana taratibu husika zilifuatwa. Kama kuna mtu ameingiliwa faragha yake basi alalamike mahakamani. Mashaka yako yatajibiwa huko.
 
CHADEMA is going to another level those who believe should take my words wabishi tutawakuta tukishafika kule tunapotaka.

Baada ya hapa mapigo UVCCM-mafisadi watakayo ipata Mungu mwenyewe ni shahidi. Vijana wengi sana will join CHADEMA kiasi cha kufanya watu kuikana hadharani kuwa waliwahi kuwa na association na mafisadi.

I told you I never do things kwa hisia I know what am talking for what I say is a command kwani as I say the environment has to obey ninachokiambia hasa kama nimepewa kukisema na baba yangu...CCM-mafisadi are on fire and there is no way they can escape this wangojee tu doomsday yao si mbali from now!
 
Wakuu,

Wakati tunampongeza Bwana Heche, hebu niambieni. Alliance ya wagombea ni nini? kwa nani? ina maana gani?
 
Wakuu,

Wakati tunampongeza Bwana Heche, hebu niambieni. Alliance ya wagombea ni nini? kwa nani? ina maana gani?
Soma hizi posts
Ben Saanane wewe ni mnafiki,maana unajua kabisa wewe ni usalama wa taifa,hukuwa na lengo la kuijenga chadema bali kuiiua bavicha,,,,
Tuhuma hizi si mimi peke yangu,Grayson na mwampamba ambao tulikuwa tuungane,tuhuma hizi zilimwangukia na kuondolewa katika uchaguzi.Anyway,alliance ni kosa?kila mmoja alikuwa tayari kuacha kugombea uenyekiti kwa masharti ya kuangalia hoja za wagombea na kuziunganisha ili tuelekeze nguvu kwa mgombea mmoja kwa maslahi ya BAVICHA.Sasa hili sitaki kulijadili saa hizi

Kuna mgombea mwingine John Heche naye inasemekana alikuwa na tuhuma lakini za kwake ikasemekana hazikuwa na ushahidi na nyingine ambazo zilionekana ni nyepesi kwa hiyo ikabidi apewe Onyo,aendeleee na uchaguzi wakati huo huo atakuwa anachunguzwa tuhuma zake.
Kwa sababu tulifanya alliance na Grayson,hili likaonekana ni kosa kubwa.Ndiyo nakubali nilifanya alliance na kuunganisha ajenda zetu.Sasa hii hofu na kosa liko wapi?
Nilituhumiwa kupokea wajumbe kutoka Zanzibar-Hizi ni tuhuma za kupika
Nilituhumiwa mara 2 kupiga kampeni kabla ya muda-Hapa hapana ukweli
Nilituhumiwa kufanya vikao vya siri mara 8-Huu ni uzushi,tuhuma za kupika
Nilituhumiwa kuwagawa vijana-Hii sio sahihi,sijui msingi na mantiki ya tuhuma hii

Nakubali inapotokea kwamba nimekiuka kanuni ni lazima niwajibishwe,hatuwezi kuwa na demokrasia bila kanuni.Vijana wanaelewa ni kitu gani kinaendelea.Kinachohitajika sasa ni kuhakikisha kwamba uchaguzi hauvurugiki kwa maslahi ya chama chetu.Asanteni nitarudi tena
 
Dah,hii picha ina nikumbusha home enzi hizo nauza ndizi kwenye stendi hii hii,...
God is good!

Tarime stendi kuu

heche.jpg
 
hongera sana Heche, tunakuamini tunakupenda.

amini kwamba umechaguliwa na vijana wakitarajia na kutegemea kitu chema kutoka kwako.

ziko changamoto nyingi utakazo kutananazo kama kiongozi isikuvunje moyo, nasi tunakuombea kwa mungu akulinde

Shirikiana na viongozi wenzako, kubali kukosolewa.

usikubali kila ushauri unaopewa, fanya uchambuzi wa kina ndio uufanyie kazi.

HONGERA SANA JOHN HECHE KWA USHINDI, HONGERA SANA WAZEE WETU WA CHADEMA KWA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI CHADEMA
 
Back
Top Bottom