John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Wakuu,

Habari ndio hiyo Heche amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Taifa wa Bavicha baada ya kupata 53% ya kura zote, akiwaacha kwa mbali wagombea wengine 5,, uchaguzi umeisha alfajiri hii

uchaguzi-bavicha.jpg

Dr. Slaa katika mkutano wa uchaguzi

uchaguzi-bavicha2.jpg

Wajumbe katika mkutano wa uchaguzi
 
Wakuu
Habari ndio hiyo Heche amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Taifa wa Bavicha baada ya kupata 53% ya kura zote,akiwaacha kwa mbali wagombea wengine 5,,uchaguzi umeisha alfajiri hii

Duh,ameshinda jamaa aisee!
Haya bana,ngoja tu tumpe ushirikiano kwa manufaa ya chama!
Tarime haitaenda chadema tena,kama heche kashinda
He will always bring conflict na ccm wata nufaika na minyukano ya chadema kule
 
mtakoma huko mlikofikiri mtapandia. na huyo kibaraka wenu mwambieni wenye mapenzi mema na nchi hii wanaripoti huko huko na ndo kimbilio la watoto wao maana hatuna ardhi nyingine zaidi ya hii. hata ikulu inawezekana pia kuripoti CDM.

sio wote wanafikiri na kufanya simply for stomach.

Habari ndo hio, hapa mmeingia choo cha kike. tangulie kwenye magamba kule.
 
Wakuu
Habari ndio hiyo Heche amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Taifa wa Bavicha baada ya kupata 53% ya kura zote,akiwaacha kwa mbali wagombea wengine 5,,uchaguzi umeisha alfajiri hii
Hongera sana Heche nakujua wewe ni jasiri huogopi vitisho vya magamba, magamba walifanya juu chini ili usiwe mwenyekiti wa Bavicha lakini Mungu ni mkuu hongera sana wazee wa Chadema, wajumbe na viongozi wote wa Chadema hakika mmetupa mtu atakayekuwa msaada na nguzo kuu ya Chadema.
 
Khaa!! jamani, hoja ijibiwe hapa,sio mnajaza sredi kwa post za ng.uruwe pori tu,mwenye details amwage tuone!!coz naona kama kuna hoja hapa!!
 
Wakuu
Habari ndio hiyo Heche amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Taifa wa Bavicha baada ya kupata 53% ya kura zote,akiwaacha kwa mbali wagombea wengine 5,,uchaguzi umeisha alfajiri hii
Tunakushukuru Mwana Mapambano kwa kuktujuza hilo sisi kama wanachama na wapenzi wa CHADEMA tunamuahidi ushirikiano yeye apige kazi tu sisi tuko pamoja naye siku zote. Hongera sana Hechee!!!
 
Hongera Heche!!Uongozi si lelemama,wamekuamini,tunakuamini,una kazi kubwa na ngumu mbeleni,uimara wako ndio nguvu kubwa ya mafanikoi bavicha. Hatutaki majibizano yasiyo na tija kama UVccm!!
All the best in ur new Carrier
 
Hongera sana mkuu,

Sikujui hata kwa sura, sijui ilikuwa na title gani lakini ujasiri wako unanipa kila sababu ya kuamini utakuwa mwiba kwa magamba na wale wanafiki ambao tumbo linawaongoza.

Tuendeleze mapambano.
 
Duh,ameshinda jamaa aisee!
Haya bana,ngoja tu tumpe ushirikiano kwa manufaa ya chama!
Tarime haitaenda chadema tena,kama heche kashinda
He will always bring conflict na ccm wata nufaika na minyukano ya chadema kule

Duh, inamaana ndo anawachaguliaga wanatarime mbunge?
 
makamu wake nani,katibu na naibu katibu na je wajumbe mwenye uwezo wa kutupa hilo plz then naombeni hoja zile za ukabila udini zifutike kabisa kwani hazitatujenga kabisa
 
magamba walifanya juu chini ili usiwe mwenyekiti wa Bavicha lakini Mungu ni mkuu hongera sana wazee wa Chadema, wajumbe na viongozi wote wa Chadema hakika mmetupa mtu atakayekuwa msaada na nguzo kuu ya Chadema.

Ingetosha tu kusema una imani na Heche, haya mengine ya CCM kufanya juu chini ili Heche asisinde as if wagombea wengine wa Uenyekiti walikuwa mamluki wa CCM ni hoja ya hovyo kabisa.

By the way wamuogope kwa nini hasa?binafsi naamini pia kuwa Heche kwa kutojua atainufaisha sana CCM Tarime 2015, wait and see!!
 
Duh, inamaana ndo anawachaguliaga wanatarime mbunge?

Nope,anapenda sana madaraka!
Alivo shindwa kwenye kura za maoni hakusaidia chochote
chadema kushinda,hasira zake ilikua za manufaa kwa ccm!
No wonder 2015 ataenda kugombea tena,waitara atataka nae pia,
mnyukano ule ule,mwisho wa siku atakae shindwa kura za maoni hata saidia mwenzake kwenye kampeni!

Hakuna ubishi kwamba Heche ana nguvu kubwa tarime,na kama angepitishwa yeye angeshinda
ila,kwa upande wa uongozi wa chama tarime,hana nguvu na hapo ndipo waitara anapo mshindia!

So far,tusahau hayo na tuangalie mbele kuna nini
 
Hongera sana Heche nakujua wewe ni jasiri huogopi vitisho vya magamba, magamba walifanya juu chini ili usiwe mwenyekiti wa Bavicha lakini Mungu ni mkuu hongera sana wazee wa Chadema, wajumbe na viongozi wote wa Chadema hakika mmetupa mtu atakayekuwa msaada na nguzo kuu ya Chadema.

Mbona Heche huyohuyo ndio analalamikiwa na wana CHADEMA kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kulipoteza jimbo la Tarime kwa CCM,na wengine wanadiriki kusema kwamba kuchaguliwa kwake kutapelekea jimbo la Tarime liendelee kushikiliwa na CCM mwaka 2015?.....

Wape hongera wajumbe wa BAVICHA walioshiriki na kufanya uchaguzi badala ya hao wazee wa CHADEMA na Viongozi wa CHADEMA,kuwapa hongera hao wazee na viongozi kutawafanya baadhi ya watu wahisi kwamba John Heche kachaguliwa na wazee wa CHADEMA na viongozi wa CHADEMA kitu ambacho si kweli...

Mwisho naomba kumpongeza sana John Heche kwa kuchaguliwa,cha msingi apewe tu ushirikiano,ni kiongozi mzuri sana huyu.
 
Hongera sana JOHN HECHE kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bavicha,kazi yako kubwa ni kuleta mshikamano kwa vijana wote wa Chadema nchi nzima,pia kuhakikisha kuwa jimbo la Tarime uchaguzi ujao linarudi Chadema.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Chadema,Mungu ibariki Bavicha.
 
Wanajamvi...hii ndio safu ya uongozi wa bavicha taifa,John Heche mwenyekiti,Makamu mwenyekiti bara Juliana Shonza na visiwani Sharifa..
 
Mbona Heche huyohuyo ndio analalamikiwa na wana CHADEMA kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kulipoteza jimbo la Tarime kwa CCM,na wengine wanadiriki kusema kwamba kuchaguliwa kwake kutapelekea jimbo la Tarime liendelee kushikiliwa na CCM mwaka 2015?.....

Wape hongera wajumbe wa BAVICHA walioshiriki na kufanya uchaguzi badala ya hao wazee wa CHADEMA na Viongozi wa CHADEMA,kuwapa hongera hao wazee na viongozi kutawafanya baadhi ya watu wahisi kwamba John Heche kachaguliwa na wazee wa CHADEMA na viongozi wa CHADEMA kitu ambacho si kweli...

Mwisho naomba kumpongeza sana John Heche kwa kuchaguliwa,cha msingi apewe tu ushirikiano,ni kiongozi mzuri sana huyu.
Wazee lazima wapongezwe kwa kusimamia uchaguzi vizuri bila kuharibika hilo la Heche kuchangia kulipoteza jimbo waachie wanachadema wenyewe ndio wamemuona anafaa wamemchagua hayo mengine ni maneno ya wafa maji tumeyazoea.
 
Heche ni mzuri, moyo wake wote uko CDM matatizo madogo madogo ambayo aliwahi kutajwa kuwa nayo atabadilika naamini. kuna vijitabia mtu/binadamu anafanya but kadiri umri unavoenda anaimarika na kubadilika. hakuna binadamu aliye kamili. tumtakie heri na kumpa ushirikiano
 
Back
Top Bottom