JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Nondo aliyekuwa anatetea kiti hicho ameibuka kidedea baada ya kupata kura 66 sawa na asilimia 55.4 ya kura zote, akifuatiwa na Julius Masabo aliyepata kura 45 sawa na asilimia 37.8 ya kura zote, nafasi ya tatu ikienda kwa Mhandisi Ndolezi Petro aliyepata kura saba (7) sawa na asilimia 5.8 ya kura zote, huku Ruqayya Nassir akipata kura moja (1) sawa na asilimia 0.8 ya kura zote.
Katika uchaguzi huo idadi ya wapiga kura ilikuwa ni 120 ambapo kura halali zilikuwa ni 119 na kura moja (1) imeharibika.