Nduka
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 8,552
- 2,360
Kwa matukio yanayoendelea bungeni, natamani:-
1. Mtu kama profesa Baregu anahusika vipi au nafasi yake ipo vipi, ikumbukwe yeye ni mmoja wa wazee wa CDM na ni msomi mahiri wa sayansi ya siasa. Namfahamu binafsi kwa kuwa tuliwahi kufanya naye kazi kama member wa bodi wa taasisi fulani, alikuwa ni msema ukweli, mshauri na mkosoaji mkubwa. Natamani kujua yanayofanywa na akina Lema yanamfurahisha au yanamkaraisha kuwa yeye ni sehemu ya wanachofanya.
2. Kitila Mkumbo, ni kijana msomi naweza kusema sijawahi kuelewa msimamo wake kwenye jambo lolote, amekuwa kama analinda baadhi ya maslahi yake hivyo misimamo yake inaishia moyoni, hapa JF watu walijaribu kumchimba kuhusu kinachotokea Arusha akaruka futi laki saba. Naamini pia ni sehemu ya washauri wa CDM kwa hiyo yanayoendelea kutokea huko pia yana mkono wake, natamani kujua kama anajisikiaje kuwa sehemu ya haya.
3. Mzee Mwanakijiji, jamaa ni msemaji wa kile anachokiamini, huwa naamini kuwa hanakuremba kwenye anachokiamini, amewahi kuwapinga CDM na CCM kwa ukali ulio sawa. Naamini yeye sio sehemu ya kinachofanywa huko Dodoma na akina Lema lakini natamani kujua safari hii atawachana akina nani.