Kama mbunge analipwa mshahara kama watumishi wengine kwanini mbunge akistaafu anapewa pesa zote huku watumishi wengine ni 33%?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Huwa natamani kuelewa vizuri. Sijajua vizuri kama Mbunge analipwa mshahara kila mwezi kwa miaka mitano, lakini ninachofahamu ni kuwa bunge likivunjwa baada ya miaka mitano huwa wanapewa hela nyingi sana, zaidi ya milioni 200 kwamba hiki ni kiinua mgongo.

Natamni kujua ni kigezo gani kilitumika kumpa Mbunge huyu milioni zote hizo kwa miaka mitano. Kwamba yawezekana hatarudi bungeni? Kama ni hivyo kwa nini mtumishi wa umma akiacha kazi asipewe hela zake zote za hifadhi ya jamii?

Lakini pia ni kigezo gani kilitumika kwa mtumishi wa umma kupewa 33% ya fedha zake za hifadhi ya jamii na kwa nini isiwe 50%?

Wastani wa maisha ya Mtanzania ni miaka 66, ni kigezo gani kimetumika kumfanya mtumishi wa umma akae kazini mpaka miaka 60 na apewe 33% ya fedha zake za hifadhin ya jamii wakati kiuhalisi bado ana mika 6 tuu ya kuishi duniani? Hata LOWASA ameishi miaka 70 tu na siyo 72 au 82?

Serikali yetu haina budi kuliangalia swala hili kwa jicho la tatu na kuwahurumia watumishi wa umma ambao kiuhalisia wanaishi maisha magumu tofauti na mfanyabishara. Bidha zikapanda mitaani, mshahara haupandi kila mwezi.

Mtumishi wa umma ni kukamuliwa tu PAYE, NSSF (ampapo akistaafu atapewa 33%), kodi mitaani kwa kila atakachonunua. Ndiyo unakuta mtumishi wa umma anastaafu hata nyumba hana maana yeye aliishi maisha ya kukamuliwa tu!
 
huwa natamani kuelewa vizuri. Sijajua vizuri kama mbunge analipwa mshahara kila mwezi kwa miaka mitano.lakini ninajofahamu ni kuwa bunge lilivunjwa baada ya miaka mitano huwa wanapewa hela nyingi sana zaidi ya milioni 200 kwamba hiki ni kiinua mgongo.

natamni kujua ni kigezo gani kilitumika kumpa mbunge huyu milioni zote hizo kwa miaka mitano .kwamba yawezekana hatarudi bungeni? kama ni hivyo kwa nini mtumi wa umma akiacha kazi asipewe hela zake zote za hifadhi ya jamii?

lakini pia ni kigezo gani kilitumika kwa mtumishi wa umma kupewa 33% ya fedha zake za hifadhi ya jamii na kwa nini isiwe 50% ?

wastani wa maisha ya mtanzania ni miaka 66 , ni kigezo gani kimetumika kumfanya mtumishi wa umma akae kazini mpaka miaka 60 na apewe 33% ya fedha zake za hifadhin ya jamii wakati kiuhalisi bado ana mika 6 tuu ya kuishi duniani?Hata LOWASA ameishi miaka 70 tu na siyo 72 au 82?

serikali yetu haina budi kuliangalia swala hili kwa jicho la tatu na kuwahurumia watumishi wa umma ambao kiuhalisia wanaishi maisha magumu tofauti na mfanyabishara.bidha zikapanda mitaani ,mshahara haupandi kila mwezi.mtumishi wa umma ni kukamliwa tu PAYE , NSSF ( ampapo akistaafu atapewa 33%) ,makodi mitaani kwa kila atakachonunua.Ndiyo ,unakuta mtumishi wa umma anastafu hata nyumba hana maana yeye aliishi maisha ya kukamliwa tu.hahahahahah

Why mtumishi wa umma ana staafu after miaka 30+ and Mbunge anastaafu kila after 5 years?
 
Cha kujiuliza hapohapo,huyo mtumishi wa umma pamoja na kupewa kiasi hicho kwa namna hiyo,lakini huweza kumchangia MAMA pesa ya kuchukulia fomu ya UONGOZI.
Haya no ma haha(in Lowasa's voice).
 
huwa natamani kuelewa vizuri. Sijajua vizuri kama mbunge analipwa mshahara kila mwezi kwa miaka mitano.lakini ninajofahamu ni kuwa bunge lilivunjwa baada ya miaka mitano huwa wanapewa hela nyingi sana zaidi ya milioni 200 kwamba hiki ni kiinua mgongo.

natamni kujua ni kigezo gani kilitumika kumpa mbunge huyu milioni zote hizo kwa miaka mitano .kwamba yawezekana hatarudi bungeni? kama ni hivyo kwa nini mtumi wa umma akiacha kazi asipewe hela zake zote za hifadhi ya jamii?

lakini pia ni kigezo gani kilitumika kwa mtumishi wa umma kupewa 33% ya fedha zake za hifadhi ya jamii na kwa nini isiwe 50% ?

wastani wa maisha ya mtanzania ni miaka 66 , ni kigezo gani kimetumika kumfanya mtumishi wa umma akae kazini mpaka miaka 60 na apewe 33% ya fedha zake za hifadhin ya jamii wakati kiuhalisi bado ana mika 6 tuu ya kuishi duniani?Hata LOWASA ameishi miaka 70 tu na siyo 72 au 82?

serikali yetu haina budi kuliangalia swala hili kwa jicho la tatu na kuwahurumia watumishi wa umma ambao kiuhalisia wanaishi maisha magumu tofauti na mfanyabishara.bidha zikapanda mitaani ,mshahara haupandi kila mwezi.mtumishi wa umma ni kukamliwa tu PAYE , NSSF ( ampapo akistaafu atapewa 33%) ,makodi mitaani kwa kila atakachonunua.Ndiyo ,unakuta mtumishi wa umma anastafu hata nyumba hana maana yeye aliishi maisha ya kukamliwa tu.hahahahahah
Kwa sababu wabunge ndo wanaotunga sheria.
Lazima wajipendelee
 
Chukua hii.

1. Viongozi wakuu wa nchi, viongozi wakuu wa vyombo vya usalama na maafisa wakuu hupata 80% ya mishahara yao wakistaafu na stahiki 80% za aliyeko madarakani.

Pension zao za mkupuo ni mzigo wa maana Toka hazina. Mzito hasa.

NB. Mtumishi wa kundi hili alifariki mwenza anahudumuwa Hadi Umauti.

2. Viongozi wa kisiasa, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na madiwani. Hupata 40% ya jumla ya mishahara yao. Muda wao ukiidha au utenguzi, anapewa Hela yake.

Mfano mbunge analipwa 12,000,000 *60*04 jibu unalopata ndo anapata.

Hataendelea na malipo yoyote.

Ndiyo maana Hawa ni machawa hasa, kila sentensi mama amesema na ukunguni wote.

3. Kundi la watumishi wa umma.
Kuna formula yenu. Mtapata 33%. Na utaendelea kupata malipo Kwa miaka 12½ Toka ustaafu. Unashauriwa ustaafu ikiwa na 60.

Ukifa kabla, mwenzi wako ataliopwa Kwa miaka mitatu mfululizo, atahudumiwa na nhif, na kama una mtoto mnufaika wa nhif pia atahudumiwa Hadi afikishe 18 yrs.

4. Watumishi wa sekta binafsi ni kama na3 hapo juu isipokuwa bima.

Mnaopindea kikokotoo wengi ni watumishi wenye miaka 50+ au watoto wao Kwa kuwa wamejazwa taarifa zisizo sahihi.

Serikali iwaelimishe.
 
Huwa natamani kuelewa vizuri. Sijajua vizuri kama Mbunge analipwa mshahara kila mwezi kwa miaka mitano, lakini ninachofahamu ni kuwa bunge likivunjwa baada ya miaka mitano huwa wanapewa hela nyingi sana, zaidi ya milioni 200 kwamba hiki ni kiinua mgongo.

Natamni kujua ni kigezo gani kilitumika kumpa Mbunge huyu milioni zote hizo kwa miaka mitano. Kwamba yawezekana hatarudi bungeni? Kama ni hivyo kwa nini mtumishi wa umma akiacha kazi asipewe hela zake zote za hifadhi ya jamii?

Lakini pia ni kigezo gani kilitumika kwa mtumishi wa umma kupewa 33% ya fedha zake za hifadhi ya jamii na kwa nini isiwe 50%?

Wastani wa maisha ya Mtanzania ni miaka 66, ni kigezo gani kimetumika kumfanya mtumishi wa umma akae kazini mpaka miaka 60 na apewe 33% ya fedha zake za hifadhin ya jamii wakati kiuhalisi bado ana mika 6 tuu ya kuishi duniani? Hata LOWASA ameishi miaka 70 tu na siyo 72 au 82?

Serikali yetu haina budi kuliangalia swala hili kwa jicho la tatu na kuwahurumia watumishi wa umma ambao kiuhalisia wanaishi maisha magumu tofauti na mfanyabishara. Bidha zikapanda mitaani, mshahara haupandi kila mwezi.

Mtumishi wa umma ni kukamuliwa tu PAYE, NSSF (ampapo akistaafu atapewa 33%), kodi mitaani kwa kila atakachonunua. Ndiyo unakuta mtumishi wa umma anastaafu hata nyumba hana maana yeye aliishi maisha ya kukamuliwa tu!
Kwanini mbunge anastafu Kila baada ya miaka mitano vipi na wewe tukikwambia ustafu baada ya miaka mitano uchukue chako utakubali?
 
Jenista Mhagama aliulizwa hilo swali na Magufuli akajiumauma tu ipo haja wabunge wote wasirudi bungeni mwakani tupate wale wenye akili wanaojitambua
 
Kazi ya mbunge ni ya mkataba wa miaka mitano, sio 'permanent and pensionable'. Pia viwango vya pensheni havifanani, kuna watu wao ni makundi maalamu, au tuseme wameamua kujiweka wawe makundi maalumu. Hao wabunge ni miongoni mwao. Mshahara wao ni wa kawaida tu, kama milioni nne hivi, lakini wamejiwekea posho ya karibu milioni kumi na moja isiyokatwa kodi!! Alafu wakimaliza muda wao wanapewa hayo mafedha yote kwa mkupuo.

Hoja ya msingi ni wafanyakazi wote wa mikataba walitakiwa kupewa chao na mifuko ya hifadhi za jamii baada ya mikataba yao kuisha kama wanavyofanya kwa wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya N.K

Na sio kuletewa sarakasi za sijui thibitisha kuwa hauna kazi, mara tutakuba moja ya tatu hiyo nyongine mpaka ufikishe miaka 60. Ni wizi na upumbavu kabisa.
 
Watanzania tunatakkwa kuamka kutoka usingizini. Hii nchi ina mambo mengi sana ya kipuuzi yanayofanywa na watawala; hawalafu wananchi tunawaangalia tu wafanye wapendavyo.
 
Wastaafu wengi wamependeza baada ya kustaafu.

Waliojipanga wakiwa kazini wanamelemeta.

Tatizo, wengi wanastaafu wakiwa na madeni, mizigo ya watoto wa kusomesha na kuwapa mitaji, hawana nyumba Wala mashamba.

Suruhisho,
Watumishi mlioko kazini zaa mtoto wa mwisho ukiwa pungufu ya miaka 45, kuwa na makazi Yako ukiwa na pungufu ya miaka 40, Fanya biashara au kilimo au ufugaji ili kujiongezea kipato.

Somesha wanao kwenye shule au vyuo unavyomudu, usikope ili mtoto akasome lakini mwanao akope heslb ili asome.

Ongeza vitega uchumi Leo.
 
Jibu rahisi, wana POWER ya kuamua wanachotaka.

POWER
POWER
POWER

Hata uwe na pesa kibao ama elimu kubwa, mwenye power huwezi kumpangia, ni yeye ndie atakupangia.
 
Mtoa mada hii sio rocket science, sheria za nchi yetu zipo za wao na nyie!,ndio maana mwanajeshi mshenzi anapiga raia na watu wanakuja kulalama humu, fikiria mazishi ya chief wa kizulu, inatokea mwanajeshi kumpiga raia ile ngumi,nakuhakikishia kungetokea push back pale ya kufa mtu, Tanzania mtu amechukua video, na watu wanalalama ndani ya JF, kesho issue mpya
 
Kazi ya mbunge ni ya mkataba wa miaka mitano, sio 'permanent and pensionable'.

Hoja ya msingi ni wafanyakazi wote wa mikataba walitakiwa kupewa chao na mifuko ya hifadhi za jamii baada ya mikataba yao kuisha kama wanavyofanya kwa wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya N.K

Na sio kuletewa sarakasi za sijui thibitisha kuwa hauna kazi, mara tutakuba moja ya tatu hiyo nyongine mpaka ufikishe miaka 60. Ni wizi na upumbavu kabisa.
Wanaozungushwa ni wanaocha kazi kinyemela bila kufuata utaratibu. Au mwajiri alikuwa hapeleku MiCHANGO.

Kama unamdau alichishwa kazi GGM, crdb au nmb hakulipwa na nssf ajitokeze.

Wanaosumbuka wengi wao chanzo ni mwajiri kutopekeka MiCHANGO.

Hata serikalini Huwa Kuna magepu, mtumishi hushauriwa kulipa mwenyewe ili kwenye mfumo pakae sawa na mwajiri atamfidia.

Wanaokuwa wakaidi ndo hucheleweshwa.

Unashauriwa kuanza michakato ya uhakiki mwaka mmoja kabla.
 
Wastaafu wengi wamependeza baada ya kustaafu.

Waliojipanga wakiwa kazini wanamelemeta.

Tatizo, wengi wanastaafu wakiwa na madeni, mizigo ya watoto wa kusomesha na kuwapa mitaji, hawana nyumba Wala mashamba.

Suruhisho,
Watumishi mlioko kazini zaa mtoto wa mwisho ukiwa pungufu ya miaka 45, kuwa na makazi Yako ukiwa na pungufu ya miaka 40, Fanya biashara au kilimo au ufugaji ili kujiongezea kipato.

Somesha wanao kwenye shule au vyuo unavyomudu, usikope ili mtoto akasome lakini mwanao akope heslb ili asome.

Ongeza vitega uchumi Leo.

ni sawa kabisa .lakini wapewe hela zao zote au 50%
 
Kawa wewe ni mtumishi wa umma ingia psssf portal uangalie MiCHANGO Yako.

Mtumishi aliyeajirea 1992, hajachangia milioni 89,000,000 anazotarajia kupata. Huyu ni Maza angu anastaafu mwakan na Mimi ndo namjaxia pepmis, na nyaraka zote. Lazima aniache na 30!
 
Kazi ya mbunge ni ya mkataba wa miaka mitano, sio 'permanent and pensionable'. Pia viwango vya pensheni havifanani, kuna watu wao ni makundi maalamu, au tuseme wameamua kujiweka wawe makundi maalumu. Hao wabunge ni miongoni mwao. Mshahara wao ni wa kawaida tu, kama milioni nne hivi, lakini wamejiwekea posho ya karibu milioni kumi na moja isiyokatwa kodi!! Alafu wakimaliza muda wao wanapewa hayo mafedha yote kwa mkupuo.

Hoja ya msingi ni wafanyakazi wote wa mikataba walitakiwa kupewa chao na mifuko ya hifadhi za jamii baada ya mikataba yao kuisha kama wanavyofanya kwa wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya N.K

Na sio kuletewa sarakasi za sijui thibitisha kuwa hauna kazi, mara tutakuba moja ya tatu hiyo nyongine mpaka ufikishe miaka 60. Ni wizi na upumbavu kabisa.
hii ndio hoja
 
Chukua hii.

1. Viongozi wakuu wa nchi, viongozi wakuu wa vyombo vya usalama na maafisa wakuu hupata 80% ya mishahara yao wakistaafu na stahiki 80% za aliyeko madarakani.

Pension zao za mkupuo ni mzigo wa maana Toka hazina. Mzito hasa.

NB. Mtumishi wa kundi hili alifariki mwenza anahudumuwa Hadi Umauti.

2. Viongozi wa kisiasa, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na madiwani. Hupata 40% ya jumla ya mishahara yao. Muda wao ukiidha au utenguzi, anapewa Hela yake.

Mfano mbunge analipwa 12,000,000 *60*04 jibu unalopata ndo anapata.

Hataendelea na malipo yoyote.

Ndiyo maana Hawa ni machawa hasa, kila sentensi mama amesema na ukunguni wote.

3. Kundi la watumishi wa umma.
Kuna formula yenu. Mtapata 33%. Na utaendelea kupata malipo Kwa miaka 12½ Toka ustaafu. Unashauriwa ustaafu ikiwa na 60.

Ukifa kabla, mwenzi wako ataliopwa Kwa miaka mitatu mfululizo, atahudumiwa na nhif, na kama una mtoto mnufaika wa nhif pia atahudumiwa Hadi afikishe 18 yrs.

4. Watumishi wa sekta binafsi ni kama na3 hapo juu isipokuwa bima.

Mnaopindea kikokotoo wengi ni watumishi wenye miaka 50+ au watoto wao Kwa kuwa wamejazwa taarifa zisizo sahihi.

Serikali iwaelimishe.
Sio kweli kwamba viongozi wote wa juu kwenye namba moja wanalipwa 80% ya mshahara na stahiki zote za aliyepo madarakani.

Ni nafasi ya Rais pekee ndiyo hulipwa 80% ya mshahara wa aliyepo madarakani. Viongozi wengine waliosalia wanapata stahiki zingine ingawaje ni kubwa ila sio kuendelea kulipwa asilimia ulizotaja wanapostaafu.
 
Back
Top Bottom