Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 81
- Thread starter
- #41
Hitimisho, Mheshimiwa Spika,
Waheshimiwa Wabunge:
nimesema Mengi. Kwa Leo Inatosha. Ninamalizia Kwa kuwahakikishieni Kuwa Nafahamu Vizuri Sasa Ukubwa Wa Heshima Na Uzito Wa Majukumu Niliyokabidhiwa Na Watanzania Wenzangu. Ninafahamu Matarajio Ya Chama Changu, Chama Cha Mapinduzi. Nitaongoza Kwa Dhati Utekelezaji Wa Ahadi Zetu Kwa Wananchi, Na Kwa Dunia. ninayajua Matarajio Ya Watanzania Wenzangu Walipoitikia Wito Wa Ari Mpya, Nguvu Mpya Na Kasi Mpya. Ninayajua Matarajio Ya Nchi Jirani, Bara La Afrika Na Dunia Kwa Awamu Ya Nne Ya Uongozi Wa Taifa Letu. Ninajua Wahisani Wetu Na Wawekezaji, Wa Ndani Na Nje, Wananisikiliza Kwa Makini, Wakitaka Kujiridhisha Iwapo Nitavijaza viatu Alivyoniachia Rais Wetu Mpendwa Wa Awamu Ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Nitajitahidi Ingawa Ni Vikubwa Kwangu.
Kwenu Nyote, Na Kwao Wote, Naahidi Kwa Msaada Wa Mwenyezi Mungu, Na Kwa Ushirikiano Na Bunge Hili Na Wananchi Kwa Ujumla, kuwa Naweza Kutimiza Matarajio Ya Kila Mmoja. Tanzania Yenye Neema Tele Inawezekana. Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania Yanawezekana. Kila Mmoja Wetu Atimize Wajibu Wake.
Mungu Ibariki Afrika. Mungu Ibariki Tanzania.
Ahsanteni Kwa Kunisikiliza.
na Hapa Ndipo Lilipokuwa Hitimisho La Sanaa,