JK: Vumilieni shida

Mahakama, Mheshimiwa Spika:

Serikali nitakayoiunda, pamoja na kuheshimu uhuru wa Mahakama, itatimiza ipasavyo wajibu wake na kuimarisha miundombinu ya kutoa haki kwa kuongeza idadi ya watumishi, kuwaendeleza kitaaluma, kukarabati majengo yaliyopo na kujenga mapya, na kupeleka huduma za utoaji haki karibu zaidi na wananchi.

Mapato na Matumizi ya Serikali, Mheshimiwa Spika:

Kusimamia vizuri mapato na matumizi ya Serikali nayo ni sehemu ya utawala bora. Isitoshe, utekelezaji mzuri wa jukumu hilo ndio unaipa Serikali uwezo wa kutekeleza mengine yote inayopaswa au inayokusudia kuyatekeleza. Serikali ya Awamu ya Tatu, chini ya uongozi shupavu wa Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, iliongeza mapato ya Serikali mara tano sambamba na kuweka mfumo mpya na wa kisasa wa kudhibiti matumizi, na kuongeza uwazi katika bajeti ya Serikali.

Hatutalegeza kamba hata kidogo. Hatutavumilia wanaokwepa kulipa kodi stahiki za Serikali au wabadhirifu wa fedha na mali za umma. Sheria ya Fedha, na Sheria ya Manunuzi ya Umma, lazima zifuatwe. Watakaokiuka wachukuliwe hatua za nidhamu. Wasiorejesha masurufu ya safari nao wasivumiliwe.

Kazi za Serikali kwenye Uchumi wa Soko, Mheshimiwa Spika:

Utawala bora ni pamoja na Serikali kufanya vizuri kazi zake nyingine muhimu katika mazingira ya uchumi wa soko. Jukumu la msingi la Serikali ni kutengeneza mazingira mazuri kwa uchumi kukua na biashara kustawi.
 
Kwa sababu hiyo, Serikali ya Awamu ya Nne itatekeleza mambo manane yafuatayo:

• Kwanza, kuweka sera na mazingira bora ya kuvutia uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi;

• Pili, kuweka sera nzuri zinazowezesha ukuaji wa uchumi wa kisasa;

• Tatu, kuweka mfumo mzuri wa usimamizi wa mazingira ili kulinda uhai wa binadamu na viumbe hai;

• Nne, kuweka mifumo bora ya kusuluhisha haraka migogoro ya kibiashara;

• Tano, kuweka utawala mzuri wa sheria na wa haki;

• Sita, kuwa na taasisi za kudhibiti na kusimamia viwango vya huduma na bidhaa;

• Saba, kuwa na sera nzuri za kifedha ili kuhamasisha uwekezaji na uzalishaji; na

• Nane, kutekeleza kwa dhati sera ya uwezeshaji wa wazawa.
 
JK: Vumilieni shida


TANZANIA DAIMA, 21ST JULY, 2008

na Anna Makange, Tanga



RAIS Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa, inayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani.

Rais Kikwete ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho Watanzania wengi, hasa wa kipato cha chini wamekuwa wakilia kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana, wilayani Muheza, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo, ikiwa ni siku ya tisa ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, mkoani Tanga.

Rais Kikwete alisema kupanda kwa bei ya mafuta, kumechangia kwa kiasi kikubwa kulipuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali duniani kote.

Alisema hali hiyo pia imechangia kuzorotesha kasi ya ukuaji wa uchumi hasa kwenye nchi zinazoendelea na hivyo watu wenye kipato duni kukabiliwa na hali ngumu ya maisha, hususan katika upatikanaji wa mahitaji muhimu, jambo ambalo aliongeza kuwa hata yeye limekuwa likimuumiza kichwa.

“Ndugu zangu Watanzania wenzangu…naelewa sana jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu siku hadi siku…na hali hii inasababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta hapa nchini, hivyo kila bidhaa kwa sasa gharama zake ni za juu sana, kuanzia vyakula hadi vitu vingine ambavyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku. Linatuumiza sana hasa wale wananchi ambao ni maskini wa kipato,” alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo alisema Watanzania wasikate tamaa kwa kuona kwamba maisha yataendelea kuwa hivyo, na kusisitiza kwamba yeye kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali duniani wanalishughulikia suala hilo.

Wakati Rais Kikwete akiwataka Watanzania kutokatishwa tamaa na hali hiyo, Chama cha NCCR- Mageuzi, jana kilisema wananchi hawana sababu ya kuilaumu Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kwa kupandisha bei ya nauli na badala yake lawama hizo zielekezwe kwa serikali ya Rais Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi, Faustine Sungura, alisema kutokana na matatizo hayo, kuna haja ya kuwepo kwa serikali mbadala, kwa madai kuwa serikali imeshindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi, hasa ya upandaji wa gharama za bidhaa mbalimbali.

“Watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na makosa, kwani muda waliowapa viongozi wa CCM kutawala unatosha na haujaonyesha mafanikio yoyote katika maisha zaidi ya kuzidisha ugumu wa maisha,” alisema.

“Watu wanakosea sana wanapoilaumu Sumatra badala ya kuilaumu serikali ambayo imeshindwa kudhibiti upandaji wa bei kwenye bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta,” alisema Sungura.

Alisema hata ziara anazofanya Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Ali Mohamed Shein ni dhihaka kwa Watanzania, kwani ahadi zao hazitekelezeki na wameshindwa kuwasaidia wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wanashinda Ikulu.

“Hivi hawa ni viongozi wa aina gani kama wameshindwa kuwasaidia wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshinda pale Ikulu, wataweza vipi kuwasaidia watu wa huko mikoani?” alihoji Sungura.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amesema serikali itahakikisha inafanya kila jitihada za kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwekeza kwenye kiwanda cha usindikaji wa matunda wilayani Muheza, kwa lengo la kuwatafutia wakulima wa machungwa soko la uhakika.

Alisema lengo la kujenga kiwanda hicho licha ya kumtafutia soko mkulima, lakini pia itakuza kipato cha wakulima sambamba na kupunguza kiwango kikubwa cha machungwa yanayoharibika mashambani kwa kukosa wanunuzi hasa nyakati za msimu.

“Serikali inaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumemsaidia mkulima kwa kiasi kikubwa kuwa na soko la uhakika sambamba na kukuza kipato chake ambacho hivi sasa kinapotea kutokana na kiasi kikubwa cha matunda kuharibika…nawaahidi kwamba hili tutalitekeleza haraka iwezekanavyo,” alisisitiza Rais Kikwete.

Miongoni mwa ahadi alizotoa rais wilayani Muheza ni pamoja na kupeleka darubini katika zahanati ya Kijiji cha Kicheba, kuchangia sh milioni mbili katika ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Mtindiro, sambamba na kutafuta magari ya wagonjwa katika wilaya zilizokosa huduma hiyo mkoani hapa.

HII SASA KALI, KAZI KWENU WADAU


Hopeless president
 
Uchumi Endelevu wa Kisasa Unaokua, Mheshimiwa Spika:

Serikali ninayoiongoza itatoa kipaumbele katika kujenga uchumi endelevu, wa kisasa, unaokua. Serikali ya Awamu ya Tatu imefanya kazi kubwa katika eneo hilo, na kutuachia msingi imara ambao sisi tutajenga juu yake. Hatutabomoa msingi huo bali Serikali itatumia mafanikio hayo kama nyenzo ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wetu.

Mheshimiwa Spika:

Sekta binafsi ndiyo mhimili wa uchumi wa nchi yetu hivi sasa. Serikali ya Awamu ya Tatu imeweka mazingira mazuri ya ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi wa Taifa. Aidha, Serikali ya Awamu ya Tatu imejenga mahusiano mazuri na sekta binafsi ambayo sasa imepewa fursa ya kushirikiana na Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini. Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza kazi hiyo nzuri. Tutajitahidi kuwa karibu na sekta binafsi kwa maslahi ya nchi yetu.

Kilimo, Mheshimiwa Spika:

Kilimo ndiyo sekta inayoajiri watu wengi na ndiyo inayotuhakikishia upatikanaji wa chakula, bidhaa za kuuza nje na malighafi za viwanda. Vilevile, uhai na maendeleo ya sehemu kubwa ya wananchi yanategemea kilimo. Hivi sasa, Serikali inatoa ruzuku kwenye mbolea na vilevile unafuu wa kodi kwenye pembejeo za kilimo na mifugo. Mpango huo utaendelezwa na kuimarishwa zaidi.

Aidha, Serikali itahakikisha kuwa Mpango Kabambe wa Umwagiliaji Maji unaongezewa fedha na wataalam. Tutahakikisha kuwa utaalam wa asili wa kilimo cha umwagiliaji unafufuliwa, pamoja na miundombinu yake. Huduma muhimu za ugani na masoko zitapewa kipaumbele na msukumo maalumu.

Mheshimiwa Spika:

Tutachukua hatua za dhati kuboresha ufugaji wetu. Hatuna budi tutoke kwenye uchungaji wa kuhama-hama na kuwa wafugaji wa kisasa. Tutachukua hatua za kuboresha malisho na huduma za madawa, majosho na minada.

Tanzania ina mifugo mingi sana, na tukiboresha ufugaji, itatoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa na maendeleo ya wafugaji. Serikali pia itawawezesha wavuvi wengi iwezekanavyo kupata zana bora na vifaa muhimu vya uvuvi wa kisasa ili waweze kutumia kwa ukamilifu eneo la bahari, maziwa na mito ambalo tumejaliwa kuwa nayo.

Viwanda Vidogo na vya Kati, Mheshimiwa Spika:

Katika maendeleo, uchumi wa taifa siku zote unaongeza mchango na viwanda katika pato la taifa. Nasi hatuna budi tufanye hivyo. Viwanda—vikubwa, vidogo na vya kati—vina uwezo mkubwa wa kukuza uchumi, kutoa nafasi za ajira, lakini vilevile vinasaidia kusindika mazao ya kilimo, kuyaongezea thamani na kuzuia yasiharibike wakati wa mavuno.

Serikali ya Awamu Nne itatengeneza mkakati kabambe wa kutekeleza sera ya viwanda nchini. Tutachukua hatua za makusudi za kukuza sekta ya viwanda nchini. Serikali itaendeleza na kuimarisha utoaji wa mikopo kwa viwanda vidogo na vya kati chini ya mpango wa mikopo, na dhamana kwa mikopo, kwa sekta hiyo ambao unasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania. Shirika la Viwanda Vidogo nalo litapewa uwezo zaidi wa kumudu kazi za kutoa elimu, ushauri, uwezeshaji na usimamizi.

Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Spika:

Serikali ya Awamu ya Nne itahimiza matumizi ya sayansi na teknolojia, na kuwekeza katika utafiti. Aidha, Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana kwa ajili ya taasisi na asasi mbalimbali zinazoshughulikia utafiti wa kiteknolojia. Mfuko wa Taifa wa Sayansi na Teknolojia utaimarishwa kwa kuongeza mchango wa Serikali na kuwahamasisha wadau wengine kuchangia.

Mheshimiwa Spika:

Teknolojia ya habari na mawasiliano imewezesha elimu, taarifa na habari kuvuka mipaka na hivyo kusaidia kupunguza pengo la habari na elimu lililopo kati ya nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, tutaongeza kasi ya kuandaa mazingira yatakayotuwezesha kutumia teknolojia hii.

Uchumi Unaoshirikisha Raia Wengi, Mheshimiwa Spika:

Mageuzi ya uchumi yameongeza tofauti ya mapato miongoni mwa wananchi. Tofauti hizo zisiposhughulikiwa zinaweza kuwa chanzo cha migogoro na mitafaruku katika jamii.
Jawabu si kuwanyang’anya walio nacho na kuwagawia wasio nacho. Jawabu sahihi ni kuwasaidia wasio nacho wajikwamue, na wainue hali za maisha yao. Changamoto kubwa ni jinsi gani tunaongeza fursa kwa wasio nacho, na kuchochea utayari wao kutumia fursa hizo.

Mheshimiwa Spika:

Kurekebisha na kutengemaza uchumi ni hatua ya mwanzo tu katika safari ndefu ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Serikali ya Awamu ya Nne itaendelea na hatua inayofuata ya kuongeza ushiriki wa Watanzania walio wengi katika uchumi wa Taifa lao. Wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza juhudi zilikuwa kuwafanya wananchi wamiliki uchumi wa Taifa lao kupitia mashirika ya umma. Leo tunataka kufikia lengo hilo hilo la wananchi kumiliki sehemu kubwa ya uchumi wa Taifa lao, moja kwa moja, au kupitia vyama huru
vya ushirika.

Mheshimiwa Spika:

Kwa kifupi Serikali ya Awamu ya Nne itaboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa ajili ya wafanyabiashara na wawekezaji wadogo wadogo, kwa kuchukua hatua zifuatazo:-

• Kwanza, kuandaa utaratibu mzuri zaidi wa kutoa leseni za biashara;

• Pili, kurekebisha mifumo ya udhibiti ili udhibiti usizuie sekta binafsi kukua;

• Tatu, kuandaa mazingira mazuri ya kufikisha taarifa muhimu kuhusu masoko, kuhusu ubora wa viwango vinavyotakiwa, na kuhusu masharti mengineyo kwa wafanyabiashara na hasa wafanyabiashara wadogo na wa kati;

• Nne, kuitaka mikoa ianzishe vituo vya kufanikisha biashara na uwekezaji mikoani, pamoja na Mabaraza ya Biashara ya Mikoa;

• Tano, kuboresha mazingira ya biashara na ujasiriamali, ikiwemo kutoa msaada na upendeleo maalum kwa mikopo midogo midogo na ya kati hasa kwa vijana, wanawake na Watanzania wanaohangaika kujikwamua kimaisha;

• Sita, kuboresha miundombinu inayogusa shughuli za wafanyabiashara wadogo na wa kati;

• Saba, kuhamasisha, kuhimiza na kutoa motisha kwa shughuli za usindikaji nchini ili kuongeza thamani ya mauzo nje; na

• Nane, kuhamasisha, kuhimiza na kutoa motisha kwa mafunzo ya ufundi ili kuongeza tija na ufanisi.
 
Mheshimiwa Spika:

Serikali ya Awamu ya Nne itaongeza kasi ya kupambana na umaskini. Tutawezesha Watanzania kwa makundi. Kundi la kwanza ni la Watanzania wasomi, walio ndani au nje ya nchi yetu. Zamani ilikuwa mtu ukitoka Chuo Kikuu, kazi ya Serikali inakungoja. Leo hali si hiyo. Wengi inabidi watafute kazi kwenye sekta binafsi, au wajiajiri wenyewe.

Napenda leo nitoe changamoto na ahadi kwa wasomi wetu hao, wenye fani mbalimbali kama vile kilimo, mifugo, uvuvi, uhandisi, ubunifu wa majengo, sheria, uhasibu na kadhalika. Katika dunia ya utandawazi na ushindani unaoambatana nao, Watanzania wasomi watabaki nje iwapo hawatakuwa wabunifu zaidi, wakaungana na kuanzisha kampuni kubwa za wazalendo.
Lakini wakikubali kuungana, na kuanzisha kampuni kubwa zinazoendeshwa kwa misingi halisi ya kibiashara, na sio ubabaishaji, Serikali, kupitia vyama vya taaluma zao, itawaunga mkono, itawasaidia na itawawezesha. Serikali ya Awamu ya Nne itakaribisha mawazo kutoka kwa vyama vya kitaaluma juu ya namna bora ya Serikali kufikia lengo hilo. Ninataka wasomi wetu wawe kiini cha wajasiriamali wasomi na wakubwa nchini.

Kundi la pili la Watanzania tutakaowasaidia na kuwawezesha ni la wenye miradi midogo sana, miradi midogo na miradi ya ukubwa wa kati. Mazuri mengi yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tatu, kama vile sera ya uwezeshaji wananchi, sera ya uwekezaji mdogo na wa kati, na mfuko wa udhamini kwa mikopo ya mitaji midogo na ya kati. Yote haya, na mengine mengi, tutayaendeleza kwa jitihada kubwa.

Kundi la tatu ni la wakulima wadogo, wavuvi wadogo na wafugaji wadogo. Hatuwezi kushinda umaskini bila kuwasaidia watu wa kundi hili ambao ndio wengi zaidi. Nitahitaji kuona ubunifu wa hali ya juu kutoka kwa nitakaowakabidhi kusimamia sekta hizi kufanikisha azma yetu hii.
Mheshimiwa Spika:

Yote haya yatawezekana tu iwapo Watanzania watabadili mtazamo wao kuhusu nafasi yao, na nafasi ya Serikali, katika kukuza uchumi wa Taifa na uchumi binafsi. Waswahili husema, ukibebwa na wewe shikilia. Maisha bora hayaletwi na Serikali peke yake; yanaletwa kwa ubia kati ya Serikali na wananchi. Naomba tuimarishe ubia huo katika Awamu ya Nne ya Uongozi wa Taifa letu.
 
Ajira na Viwanda, Mheshimiwa Spika:

Katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM tulijiwekea lengo la kuongeza nafasi za ajira milioni moja katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Nafasi hizi za ajira zinatarajiwa kupatikana Serikalini na katika sekta binafsi. Upanuzi wa sekta za afya, elimu, kilimo, ujenzi wa nyumba na barabara, usindikaji wa mazao na bidhaa asilia, samaki, na utalii ndilo tumaini kuu la ajira. Aidha, matarajio mengine makubwa ya ajira ni kutoka katika sekta isiyo rasmi, yaani ajira binafsi. Tunasisitiza ahadi yetu ya kuchukua hatua thabiti za kuwasaidia vijana, wanawake na Watanzania kwa jumla kupata mikopo na mitaji ya kuwawezesha kujiajiri. Lengo letu ni kuwa kila raia awe na chanzo cha uhakika cha kipato, na kuibua maeneo mapya ya kuwapatia ajira wananchi wengi zaidi.

Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza pia juhudi za kuhimiza, na kuwezesha, uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kama vile vya nguo na vya kuunganisha bidhaa za matumizi ya nyumbani vyenye uwezo mkubwa wa kutoa nafasi za ajira. Serikali ya Awamu ya Tatu ilibuni mradi uitwao Tanzania Mini-Tiger Plan 2020 ambao kwa kutumia maeneo maalum ya uchumi utaongeza mauzo nje ya nchi, na kuongeza haraka nafasi za ajira. Serikali ya Awamu ya Nne itautekeleza mradi huo kwa ukamilifu.

Ushirika, Mheshimiwa Spika:

Ushirika ni nguzo muhimu ya kuwawezesha wanyonge kuwa na sauti na hivyo kuweza kupambana na umaskini. Serikali ya Awamu ya Tatu imefanya kazi kubwa na nzuri ya kuunda upya ushirika nchini kwa kuhuisha sera na sheria ili kuweka mazingira yatakayochochea kujengeka kwa vyama huru vya ushirika vinavyomilikiwa na kuendeshwa na wanaushirika wenyewe. Serikali ninayoiongoza itaendeleza juhudi hizo pamoja na kuendelea kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kujiunga na vyama hivyo.

Huduma ya Jamii

Kuendeleza huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji na kadhalika itaendelea kuwa kipaumbele cha juu cha Serikali ya Awamu ya Nne.

Elimu, Mheshimiwa Spika:

Kazi kubwa ya kupanua miundombinu ya elimu nchini imefanyika katika miaka kumi iliyopita chini ya Serikali ya Awamu ya Tatu. Uandikishaji wa wanafunzi, wa kike na wa kiume, katika ngazi zote za elimu umeongezeka sana.
 
Elimu itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Nne, ambayo itafanya yafuatayo:-

• Kwanza, kuendelea kuandikisha watoto wote wa rika lengwa la kuanza shule;

Pili, kuboresha taaluma ili kuongeza viwango vya kufaulu;

• Tatu, kuongeza ajira ya walimu wa elimu ya msingi na sekondari;

• Nne, kushirikiana na wazazi na wadau wengine wa elimu kujenga vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maabara na vyoo;

• Tano, kuongeza ruzuku inayotolewa hivi sasa kwa ajili gharama za kuendesha shule;

• Sita, kuimarisha taasisi za kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa;

• Saba, kutoa fursa na motisha kwa sekta binafsi, taasisi za dini na mashirika binafsi yanayowekeza katika elimu;

• Nane, kuimarisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili iweze kutoa mikopo kwa wahitaji wengi zaidi;

• Tisa, kujenga angalau chuo kikuu kingine kipya; na

• Kumi, kuhakikisha kuwa mafunzo ya ufundi stadi yanaendelezwa na kuimarishwa kama mkakati wa kupambana na tatizo la ajira.

• Kumi na moja, kuboresha maslahi ya walimu katika shule na vyuo hapa nchini.

Maji, Mheshimiwa Spika:

Tatizo la maji ndicho kilio kikubwa cha Watanzania mijini na vijijini. Ndiyo kero nambari wani. Serikali za awamu zote zimefanya jitihada kubwa kukabiliana na tatizo hilo. Serikali ya Awamu ya Nne inakusudia kulikabili tatizo hili kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Ni makusudio yangu kuwa tuwe na Mpango Kabambe wa Maji kwa nchi nzima. Mpango ambao utajumuisha mikakati na mbinu mpya za kutekeleza kwa kasi Sera ya Maji na kutatua tatizo la maji. Aidha, tutakamilisha miradi mikubwa ya ukarabati na upanuzi wa Majisafi na Majitaka Dar es Salaam, na ule wa kupeleka maji katika miji ya Kahama, Shinyanga na vijiji vitakavyopitiwa na bomba kutoka Ziwa Victoria.
 
Afya, Mheshimiwa Spika:

Serikali ya Awamu ya Tatu imechukua hatua mbalimbali kuboresha sekta ya afya, na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi. Tutaendeleza hatua hizo. Huduma ya afya kwa kina mama na chanjo mbalimbali kwa watoto zitaendelea kutolewa na kuboreshwa zaidi. Tunataka kila mtoto wa Kitanzania apate chanjo zote zinazostahili.

Aidha, tutaimarisha mtandao wa kusambaza dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati, pamoja na kuendelea kuongeza bajeti ya ununuzi wa dawa na vifaa vya tiba. Ukarabati na ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati utaendelea. Kwa kutambua kuwa kinga ni bora kuliko tiba tutakazania pia elimu ya afya. Mapambano dhidi ya malaria na kifua kikuu yatapewa msukumo maalum.

UKIMWI, Mheshimiwa Spika:

Nchi yetu inakabiliwa na tatizo kubwa la UKIMWI. UKIMWI ni janga la kitaifa na dunia kwa ujumla. Janga hili limekuwa likiathiri utendaji na kupunguza nguvukazi ya Taifa. Tutaendeleza jitihada za kuhamasisha na kutoa elimu ya UKIMWI kwa wananchi wote ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anao uelewa sahihi wa janga hili. Aidha, Serikali itatenga rasilimali zaidi, na kushirikiana na wadau mbalimbali, kuongeza upatikanaji wa dawa za kurefusha maisha na kupunguza makali kwa watu wengi zaidi walioathirika na UKIMWI.

Makundi Maalum, Mheshimiwa Spika:

Katika jamii yetu yapo makundi maalum ambayo Serikali inao wajibu wa kuwasaidia. Kundi la kwanza ni la watoto yatima. Tunahitaji wadau mbalimbali wakae pamoja na kuandaa mipango endelevu ya kuwalea na kuwasaidia watoto hawa. Watoto yatima wanahitaji elimu, lishe bora, huduma za afya, makazi na upendo sawa na watoto wengine wa Kitanzania. Serikali ya Awamu ya Nne inaahidi kuwa yatima watapata elimu na huduma ya afya kwa kusaidiwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika:

Kundi jingine maalum ni lile la walemavu. Zipo hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa kuwapa fursa walemavu kutumia vipaji vyao ili kujitegemea. Changamoto kubwa kwetu kama Taifa ni kuwa tuache kuwanyanyapaa na tuwaone kuwa ni binadamu wenzetu. Serikali itachukua hatua za kuhuisha sera na sheria ili kutoa upendeleo maalum kwa walemavu katika utoaji wa huduma mbalimbali na vilevile katika kuweka mazingira yatakayowapa fursa ya kutekeleza majukumu yao kwa jamii.

Mheshimiwa Spika:

Lipo pia kundi la wazee wetu. Wazee ni hazina kubwa ya Taifa lolote. Jamii yeyote iliyostaarabika inalo jukumu la kuwaenzi na kuwatunza wazee, tukianza na wanafamilia na wanajamii wa karibu wa mzee anayehusika. Wasikwepe jukumu hilo asilia, na la mila za Kiafrika. Serikali itahakikisha kuwa kunakuwepo utaratibu na mipango itakayowawezesha wazee kupata huduma muhimu kwa wepesi zaidi na kwa gharama nafuu, kwa kuzingatia taratibu, mila na utamaduni wa jamii zetu.

Mheshimiwa Spika:

Serikali itazingatia nafasi ya wanawake katika maendeleo. Tutaongeza, awamu kwa awamu, ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi wa kisiasa, kiutendaji na nafasi nyingine za maamuzi. Kadhalika, tutatekeleza ahadi ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Utalii, Mheshimiwa Spika:

Serikali yangu inakusudia kuendeleza sekta ya utalii ili iongeze mchango wake kwenye pato na maendeleo ya taifa letu. Tunapaswa kuboresha huduma kwa watalii kama vile malazi, chakula, usafiri na bidhaa za kumbukumbu za kuwauzia watalii. Tunapaswa kukaribisha wawekezaji wa ndani na nje watakaojenga hoteli zenye hadhi ya kimataifa kuanzia nyota nne hadi tano. Tunahitaji kujenga miundombinu ya kuwafikisha watalii katika maeneo ya kitalii kwa urahisi.

Hifadhi ya Mazingira, Mheshimiwa Spika:

Serikali ya Awamu ya Nne itatoa msukumo maalum kwa hifadhi ya mazingira kwani athari zake pale tulipopuuzia zinaonekana wazi. Mvua haba, raslimali maji inazidi kupungua, na ukame unaongezeka. Serikali itaendelea kuthamini na kulizingatia suala hili, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza uelewa wao kuhusu hifadhi ya mazingira. Tutaiongezea Wizara inayohusika na mazingira uwezo na mamlaka ya usimamizi. Tutaendeleza kampeni ya upandaji miti na kuhimiza tabia ya kutokata miti ovyo, au kuchoma misitu ovyo. Ili kupunguza mahitaji ya kuni na mkaa tutaendeleza matumizi ya nishati mbadala.

Miaka arobaini tu iliyopita, Tanzania Bara ilikuwa bado na misitu mingi, chemchem na vijito vingi. Sehemu kubwa ya ardhi yake ilikuwa imefunikwa na majani. Leo hali ni tofauti, na kwenye baadhi ya maeneo hali inatisha.
Mheshimiwa Spika:

Uchomaji misitu na ukataji ovyo wa miti vimesababisha vyanzo vya maji kukauka, mito kupungua maji na baadhi ya viumbe kuathirika na kutoweka. Hatuwezi kuendelea kuwa watazamaji au washangaaji wa vitendo hivi vya hujuma dhidi ya misitu na uhai wa taifa letu. Na wala uhuru wa Mtanzania kuishi popote katika nchi yake haujumuishi pia uhuru wa kuharibu mazingira sehemu fulani na kuhamia sehemu nyingine.

Mheshimiwa Spika:

Yapo maeneo ambayo lazima zichukuliwe hatua maalum za kulinda na kuhifadhi mazingira kwani hali imeanza kuwa mbaya sana. Eneo mojawapo ni Bonde la Mto Ruaha ambalo linahusisha vyanzo vya mito yote mikubwa nchini. Tumeshuhudia hali ya bwawa la Mtera inavyoendelea kuwa mbaya. Aidha, mto Ruaha Mkuu umeanza kukauka katika baadhi ya maeneo. Itabidi uongozi wa Serikali katika ngazi zote uwajibike zaidi kuhakikisha kuwa uharibifu wa mazingira unaosababisha hali hii ya kutisha unakomeshwa.

Eneo jingine ni lile linalozunguka Ziwa Victoria. Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kuwa pamoja na umuhimu wa ziwa hilo, uchafuzi wake unaongezeka. Serikali itahakikisha kuwa uongozi wa mikoa yote inayozunguka ziwa hilo unashirikiana na taasisi za kitaifa na kimataifa na wananchi kuhifadhi ziwa hilo linalotegemewa na idadi kubwa ya wananchi wetu.

Uchumi Unaopaa, Mheshimiwa Spika:

Baada ya mafanikio ya Awamu ya Tatu, haitarajiwi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne italegeza kamba na kupuuza misingi iliyotuletea mafanikio tunayojivunia. Najua mengi yamesemwa na watu wanaodai wanamfahamu Jakaya Mrisho Kikwete na jinsi atakavyolegeza mambo. Napenda kuwahakikishieni kuwa watu hao wamepotea sana.

Wakati wa kampeni wapo baadhi ya wapinzani waliothubutu, kwa kukosa shukrani, kusema ati Serikali ya Awamu ya Tatu ilikuwa inatekeleza sera zinazobuniwa Washington. Serikali ya Awamu ya Nne haitaogopa kubuni na kutekeleza sera na mikakati ya maslahi kwa ukuaji wa uchumi na maisha bora kwa kila Mtanzania ati kwa vile zinaungwa mkono au kufadhiliwa na nchi tajiri na mashirika ya fedha ya kimataifa.

Hatutafanya lolote lisilo na maslahi kwa taifa letu kwa kuwaogopa au kutaka kujipendekeza kwa wakubwa hao. Lakini vile vile hatutaacha kufanya lolote la maslahi kwa taifa na Watanzania kwa vile tu linaenda sambamba na ushauri wa mashirika ya fedha ya kimataifa.

Mheshimiwa Spika:

Mbali ya kusukumwa na hoja ya kukuza uchumi haraka ili kupiga vita umaskini, tunasukumwa pia na ukweli wa nguvu za utandawazi na ushindani mkubwa katika masoko ya kanda na ya kimataifa. Hivyo basi, sote tuunganishe nguvu zetu ili tuongeze uzalishaji, tuongeze uwekezaji, tuongeze mauzo nje, tuongeze ubora wa mazao na huduma zetu na tuongeze kasi ya ukuaji wa uchumi wetu ili upae.

Michezo, na Burudani na Utamaduni, Mheshimiwa Spika:

Michezo ni furaha. Michezo ni muhimu kwa afya zetu. Watanzania wanapenda sana michezo, ila furaha imekuwa inawakwepa kwa timu zetu kutokufanya vizuri. Lazima tutoke huko na inawezekana. Tutahimiza maendeleo ya michezo shuleni na pale inapowezekana katika sehemu za kazi. Shule ziwe mahali pa kubaini vipaji vya sanaa na michezo na kuiendeleza.

Tutaviwezesha vyama mbalimbali vya michezo ili Tanzania iweze kuwa mshiriki vizuri, na siyo kuwa msindikizaji, katika mashindano mbalimbali ya michezo ulimwenguni. Pamoja na hayo nitaanzisha mjadala wa kitaifa wa kuendeleza michezo nchini. Wadau wote washiriki, na Watanzania, tukubaliane juu ya mstakabali wa michezo nchini mwetu.

Tutaendeleza sekta ya utamaduni na burudani kwa jumla. Miongoni mwa mambo ambayo tutayaangalia kwa karibu ni haki na maslahi ya wasanii ili kazi kubwa waifanyayo iwe na tija kwao.

Mheshimiwa Spika:

Lugha ya Kiswahili imeanza kupata umaarufu Afrika na duniani.
Umoja wa Afrika umekubali Kiswahili kuwa moja ya lugha zake kuu. Aidha Nchi za Kanda ya Maziwa Makuu zimekubali kutumia na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Serikali ya Awamu ya Nne itahakikisha kuwa juhudi hizi zinaendelezwa na kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakua nje ya mipaka ya Afrika.
 
Mipango Miji, Mheshimiwa Spika:

Kuendeleza miji ni jambo tutakalolipa uzito unaostahili ili tuwe na miji mizuri, safi na salama. Sote tumeona jinsi ambavyo dhana ya mipango miji inavyopuuzwa na kukiukwa na baadhi ya wananchi wetu, manispaa na halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika:

Tusipozuia hali hiyo, miji yetu itakuwa kama pori la majengo yasiyo na mpangilio wala huduma zinazohitajika. Serikali ya Awamu ya Nne itazitaka Halmashauri zote zishughulikie jambo hili haraka inavyowezekana.
Tutaangalia uwezekano wa kuanzisha upya chombo cha fedha kitakachotoa mikopo ya kujenga na kununua nyumba.

Huduma za Kiuchumi

Kuendeleza huduma za kiuchumi za barabara, nishati, simu na kadhalika itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Nne. Serikali za Awamu zilizotangulia zilisimamia ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikijumuisha barabara, vivuko na madaraja. Kwa kuzingatia hoja ya kuunganisha nchi na kuibua maeneo mapya yenye uwezo wa kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza kwa kasi upembuzi yakinifu, usanifu, na ujenzi wa barabara na madaraja yote yaliyoorodheshwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005. Tutauimarisha Mfuko wa Barabara ili uendelee kuwa nyenzo muhimu ya kuboresha huduma ya barabara nchini.

Nishati, Mheshimiwa Spika:

Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani. Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini.

Mheshimiwa Spika:

Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na hivyo ndivyo tutakavyofanya. Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua mipango ya umeme wa Mto Rusumo na Stigler’s Gorge. Vile vile tutaharakisha upatikanaji wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.

Mheshimiwa Spika:

Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne pia ni kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa, kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma katika gridi ya Taifa.
 
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Spika,

Awamu ya Kwanza ya uongozi wa nchi yetu iliweka misingi endelevu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Misingi hiyo ni ujirani mwema, ulinzi wa mipaka yetu, kuwasaidia wakimbizi na kuwa mtetezi wa wanyonge. Awamu zilizofuatia zimefanikiwa kuendeleza misingi hiyo. Serikali ya Awamu ya Nne nayo itaendeleza misingi hiyo pamoja na kusimamia utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje ambayo inalenga zaidi kwenye diplomasia ya kiuchumi.

Mheshimiwa Spika:

Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza kwa dhati mazungumzo ya kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki litakalotunufaisha sote sawia. Serikali ya Awamu ya Nne pia itaendeleza ushiriki wetu na uhusiano wetu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo Kusini mwa Afrika (SADC).

Tutahakikisha pia kuwa Tanzania inaendelea kushiriki kwa ukamilifu na kuwa mwanachama mwaminifu wa Umoja wa Afrika, inaendelea kushiriki kwa ukamilifu katika utatuzi wa migogoro Barani Afrika, na hususan katika mchakato wa amani na maendeleo kwenye Kanda ya Maziwa Makuu.
Mheshimiwa Spika:

Tanzania itaendelea kushiriki kwa ukamilifu kwenye shughuli za Umoja wa Mataifa. Hivi sasa nchi yetu ni mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuanzia kesho kutwa, Januari 1, 2006, Tanzania itashika nafasi ya Urais wa Baraza hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Katika kipindi hicho Tanzania inatarajia kuleta ajenda ya usalama na usuluhishi wa migogoro katika Eneo la Maziwa Makuu ili lijadiliwe na Baraza hilo. Kadhalika, tutaongeza ushiriki wa Jeshi letu katika Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Spika:

Amani na utulivu wa nchi yetu ni moja ya agenda kubwa ya Serikali ya Awamu ya Nne. Maendeleo ya uchumi pia yanategemea sana utulivu wa nchi. Pamoja na matukio ya hapa na pale nchi yetu kwa jumla imetulia, na ni wajibu wetu kuuendeleza utulivu huu, kwa kufanya yafuatayo:

• Kwanza, kujenga mazingira mazuri ya kazi kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama;

• Pili, kuendeleza juhudi za kuwa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama yaliyo imara yenye nidhamu ya hali ya juu na utii, na yenye utaalam na zana za kisasa;

• Tatu, kuongeza uwezo wa vyombo vya ulinzi na usalama kupambana na ujambazi na kuzagaa kwa silaha ndogondogo ambazo zinatumika kufanyia uhalifu dhidi ya raia wema. Tatizo hili tutalivalia njuga.

• Nne, kuanzisha na kutoa vitambulisho vya uraia; na

• Tano, kuongeza kasi ya urejeshaji wa wakimbizi makwao.

Hitimisho, Mheshimiwa Spika,

Waheshimiwa Wabunge:

Nimesema mengi. Kwa leo inatosha. Ninamalizia kwa kuwahakikishieni kuwa nafahamu vizuri sasa ukubwa wa heshima na uzito wa majukumu niliyokabidhiwa na Watanzania wenzangu. Ninafahamu matarajio ya Chama changu, Chama Cha Mapinduzi. Nitaongoza kwa dhati utekelezaji wa ahadi zetu kwa wananchi, na kwa dunia. Ninayajua matarajio ya Watanzania wenzangu walipoitikia wito wa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Ninayajua matarajio ya nchi jirani, bara la Afrika na dunia kwa Awamu ya Nne ya uongozi wa taifa letu. Ninajua wahisani wetu na wawekezaji, wa ndani na nje, wananisikiliza kwa makini, wakitaka kujiridhisha iwapo nitavijaza viatu alivyoniachia Rais wetu mpendwa wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Nitajitahidi ingawa ni vikubwa kwangu.

Kwenu nyote, na kwao wote, naahidi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na kwa ushirikiano na Bunge hili na wananchi kwa ujumla, kuwa naweza kutimiza matarajio ya kila mmoja. Tanzania yenye neema tele inawezekana. Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana. Kila mmoja wetu atimize wajibu wake.

Mungu Ibariki Afrika. Mungu Ibariki Tanzania.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
 
Jk na ccm yake wajue tu kuwa uvumilivu una kikomo. wananchi hawawezi kuendelea kuvumilia shida huku wanaona mafisadi na serikali wanaishi maisha ya Anasa kwa nguvu za wanyonge.
 
Kadhalika, hatuna budi kuchukua hatua thabiti za kuzuia watumishi wa umma kutumia nafasi zao kujitajirisha na kujilimbikizia mali. Sisemi kwamba ni haramu mtu kuwa tajiri au kuwa na mali. Ninachosema mimi kuwa ni haramu ni kutumia nafasi yako ya utumishi au uongozi wa umma kujipatia manufaa ya kujitajirisha au kujilimbikizia mali.

Jambo hili ndilo linalokera sana watu kuona mtu ambaye hana chochote lakini miezi michache tu baada ya kupata cheo anakuwa tajiri mkubwa. Ona majumba ya fahari, ona madaladala, teksi bubu, anaishi maisha ya kifahari na kadhalika. Wananchi wanayo haki kuhoji, na wanayo haki kupata majibu. Ndugu zangu, naomba tuwe waadilifu. Tusilaumiane. Nataka Tume ya Maadili ya Viongozi isione haya kutuuliza jinsi tulivyozipata mali tunazosema tunazo. Nitawasaidia kujenga uwezo wa kufanya hivyo kama tatizo lenu ni hilo.

Maneno mengi matendo hakuna kabisaaa, kumbe kila kitu anakijua!
 
JK: Vumilieni shida

TANZANIA DAIMA, 21ST JULY, 2008

na Anna Makange, Tanga



RAIS Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa, inayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani.

........watu wenye kipato duni kukabiliwa na hali ngumu ya maisha, hususan katika upatikanaji wa mahitaji muhimu, jambo ambalo aliongeza kuwa hata yeye limekuwa likimuumiza kichwa.

“Ndugu zangu Watanzania wenzangu…naelewa sana jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu siku hadi siku…na hali hii inasababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta hapa nchini, hivyo kila bidhaa kwa sasa gharama zake ni za juu sana, kuanzia vyakula hadi vitu vingine ambavyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku. Linatuumiza sana hasa wale wananchi ambao ni maskini wa kipato,” alisema Rais Kikwete. .......

Mhe Rais mbona unatuzidi kutuzuga tu...kama kweli unaelewa jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu je umeamua nini kuhus kuhusu hizi fedha za EPA?usituambie kuwa shida imeanza hapa majuzi tu baada ya kupanda bei ya mafuta.....wataalam wa Economics wanasema...Nanukuu

Asked to comment on the economic repercussions of the EPA scandal, the director of policy and research in the Confederation of Tanzania Industries (CTI), Hussein Kamote, told THISDAY that the resulting capital flight was detrimental to the national economy.

’’Society has been denied various social and economic services since the (stolen) monies have been put to personal use by the beneficiaries instead of benefiting the entire population,’’ he said.

Mheshimiwa hii shida haijaanza leo kama unavyodai....Hata hivyo shida ya mpasuko wa bei ya mafuta ipo .....je huoni kuwa na wewe kama kiongozi ni bora uanze kubana matumizi?....kuna sababu gani ya wewe kuwa na msafara wa magari zaidi ya 20 ambayo yanabugia mafuta kukulinda?..

Unaogopa nini?....viongozi wa nchi za magharibi, ambao ndio wanatusaidia kwenye bajeti yetu, misafara yao haizidi hata gari 3....wabunge wao hutumia public transport....je umeshaona hata mbunge mmoja wa nchi hii masikini ambayo unawaambia wananchi wavumilie shida wakipanda daladala?
 
Namshangaa sana JK kuthubutu kusema wazi kwamba tuvumilie, wakuu hapa JF nadhani haya ni matusi. Ni sawa na mtu anakuingizia kitu #*#$..ni halafu anakuomba uvumilie, ni kwanini ayaongee haya wakati shida zimeanza muda? nadhani ameona kelele zimezidi na alikuwa hana njia ya kujitetea maana ili watu waona anapigana angeshafanyia kazi tuhuma zilizoko. Sasa wananchi naona pressure yetu haoitoshi ama kwa utabiri nadhani imefikia mahala ambapo serikali imeshaamua kwamba liwalo na liwe hata ikibidi kuwatoa zaka wananchi. Kama serikali imefikia kwenda kuwakamata wahandishi wa habari wakawaacha watu majambazi wanaojulikana, serikali imeshakata shauri la kututoa sadaka, na kama alivyosema mkuu mmoja hapa JF basi wao pia ndio waliomwagia yule jamaa ile tindikali, HII IMESHAKUWA SERIKALI YA KIFEDHULI. Ni siku nyingi Dr. Slaa alisema bungeni kwamba ana nyaraka hizo wanazosema kwamba ni nyeti, Marmo akasema ni makosa na naibu spika akagongea msumari kwamba akikamatwa ni shauri yake. KWANINI SERIKALI (POLISI) HAIJAMKAMATA DR. ALIYEJITOKEZA MWENYEWE KWAMBA ANAZO HIZO NYARAKA?. Serikali ya kioga tena ya watu wasio na akili wala mwelekeo, ni upumbavu mkubwa uliofanywa na vyombo vya dola na aliyeidhinisha hilo AMEIDHALILISHA SERIKALI AMBAYO WALAU BADO WANANCHI WALIKUWA WANAISUBIRIA WAONE MATOKEO YAKE, NAWAOMBA WANANCHI WAJIKAZE MAANA KAMA HAWAJAJUA WAMESHAKAZWA HATA WASIPOJIKAZA WENYEWE. HAKUNA ATAYETUTOA KWENYE UFEDHULI HUU TUSIPOJITOA WENYEWE. Serikali imekasirika maana maovu yanayoandikwa yanawakosesha muda wa kukaa na kutafakari njia nyingine ya kuendelea kutudanganya tuliokwisha kujua tunadanganywa.
 
Huyu Mkulu naona sasa keshaishiwa kabisa.Eti tuvumilie shida? Kwa mfumo na utendaji wa serikali yake hawataweza kuleta mabadiliko yoyote yale kwa wananchi.
Serikali yake ni kama pakacha ambalo anatumbia tulijaze maji huku hali likiwa na matundu kibao.Inatakiwa kwanza yeye Mkulu kuziba matundu na nyufa kwenye pakacha hilo kabla ya kutafuta visingizio vya umasikini na hali ngumu kwingineko.

Ni dhahiri nchi imemshinda na amekosa dira na mwelekeo.

Wananchi tafadhali eleweni kuwa bila ya kuwa na uongozi bora hakutakuwa na suluhisho la matatizo yetu ya umasikini katika taifa letu.Hata huko Marekani nchi inayumba kutokana na uongozi mbovu na maamuzi yasiyo ya msingi,hivyo tusitafute visingizio vingine, hatuna uongozi bora period.
Ni bora 2010 kuchagua watu mathubuti kuliongoza Taifa letu ama sivyo msilalamike kuhusu hali ngumu ya maisha.
Waswahili walisema kufanya kosa si ....bali kurudia kosa!!

Wembe
 
JK: Vumilieni shida

TANZANIA DAIMA, 21ST JULY, 2008
na Anna Makange, Tanga

RAIS Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa, inayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani..........

Rais Kikwete alisema kupanda kwa bei ya mafuta, kumechangia kwa kiasi kikubwa kulipuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali duniani kote.

Hata hivyo alisema Watanzania wasikate tamaa kwa kuona kwamba maisha yataendelea kuwa hivyo, na kusisitiza kwamba yeye kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali duniani wanalishughulikia suala hilo.

Kama bidhaa zimepanda basi na dhahabu yetu imepanda.....kwa hiyo usitupe matumaini kuwa unaweza kuongea na waarabu wakapunguza bei ya mafuta....
kwa kuongezea,hapa kuna jibu zuri tu kutoka kwa mwandishi wa THIS DAY....


FINNIGAN WA SIMBEYE
DAR ES SALAAM
.........The Canadians want us to continue calling them as donors while receiving what Barrick and TRE have paid as taxes to Ottawa while not doing the same to Dar es Salaam. And some of our members of parliament think that is fine. It?s simply economic diplomacy, period! However, a situation that is meant to keep our country as a beggar is not very palatable.

I can imagine our ambassador to Saudi Arabia lobbying Saudi MPs to lower the price of oil for our country. The Saudis, because they are wise, will simply ignore whoever that envoy is and cash on spiralling oil prices which will earn them extra income to finance infrastructure development, pay civil servants better salaries and boost health and education budgets.

The Bomani committee report is a good opportunity for this country to ensure that foreign mining corporations which have made a staggering fortune out of our mineral deposits start paying back to the people of this country.

We cannot continue to be a country whose development budget is financed by net aid while allowing multinational corporations to make super profits from our mineral resources.

TRE?s Chief Executive and Chairman, James Sinclair, is predicting that an ounce of gold may soon hover around $1,000 which is good for the investor and certainly should be good for those unfortunate Tanzanians who are bearing the brunt of gold mining activities at Geita, Bulyanhulu, Mirerani and elsewhere
 
Mwalimu Juliasi alituambia tufunge mkaja kwa muda wa miezi kumi na nane ,sasa huyu anatuambia tuvumilie kwa muda usio julikana ,na hii naona imetokana na wafadhili kueka ngumu, Muungwana afahamu kuwa kuwafuga mafisadi ni kulimaliza Taifa na hakohako ka akiba kalikobaki ,tunataka WaTanzania siku moja wanaamka wanasikia mafisadi wote wamekamatwa operation ambayo ilikuwa na mafanikio kule Pemba walipokamatwa watu ambao eti walikuwa na njama za uhaini wakati kila hatua waliyoifanya waliiandika na kuipeleka magezitini ,sasa hawa wahujumu Uchumi ambao mambo yao ya ufisadi yalikuwa siri kubwa zisizojulikana kwa wanini wasikamatwe kama ni wahaini wa Uchumi ,Mh.Kikwete amuru watu hawa wakamatwe usiku mmoja tu,wewe ni Amiri Jeshi unayo nguvu hiyo , halafu ndio utuambie tuwe wavumilivu kwa muda usio julikana basi tutakuwa razi na tutakuunga mkono na mguu.
 
Tizama hadithi za Abunuwasi, baaada ya kuununua uchaguzi akasema hivii:-


Mheshimiwa Spika:

1. Yameanza kujitokeza mawazo kuwa uongozi unaweza kununuliwa kwa fedha.

2. Kama ni kweli, tusipokuwa waangalifu, nchi yetu inaweza kuwekwa rehani kwa watu wenye fedha za kununua uongozi au wanaoweza kupata fedha za kufanya hivyo.

3. Lakini, fedha kutumika kununua ushindi si halali. Ni vema sasa tuanzishe mjadala wa kitaifa na hatimaye kuelewana kuhusu utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutafuta fedha za uchaguzi;

4. na utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutumia fedha hizo. Na utaratibu tutakaokubaliana uwe ni sehemu ya maadili ya uchaguzi katika uchaguzi wa kiserikali na ndani ya vyama vya siasa. Katika mjadala huo suala la takrima nalo tuliangalie.
 
JK: Vumilieni shida


TANZANIA DAIMA, 21ST JULY, 2008

na Anna Makange, Tanga



RAIS Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa, inayosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani.

Rais Kikwete ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho Watanzania wengi, hasa wa kipato cha chini wamekuwa wakilia kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana, wilayani Muheza, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo, ikiwa ni siku ya tisa ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, mkoani Tanga.

Rais Kikwete alisema kupanda kwa bei ya mafuta, kumechangia kwa kiasi kikubwa kulipuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali duniani kote.

Alisema hali hiyo pia imechangia kuzorotesha kasi ya ukuaji wa uchumi hasa kwenye nchi zinazoendelea na hivyo watu wenye kipato duni kukabiliwa na hali ngumu ya maisha, hususan katika upatikanaji wa mahitaji muhimu, jambo ambalo aliongeza kuwa hata yeye limekuwa likimuumiza kichwa.

“Ndugu zangu Watanzania wenzangu…naelewa sana jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu siku hadi siku…na hali hii inasababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta hapa nchini, hivyo kila bidhaa kwa sasa gharama zake ni za juu sana, kuanzia vyakula hadi vitu vingine ambavyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku. Linatuumiza sana hasa wale wananchi ambao ni maskini wa kipato,” alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo alisema Watanzania wasikate tamaa kwa kuona kwamba maisha yataendelea kuwa hivyo, na kusisitiza kwamba yeye kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali duniani wanalishughulikia suala hilo.

Wakati Rais Kikwete akiwataka Watanzania kutokatishwa tamaa na hali hiyo, Chama cha NCCR- Mageuzi, jana kilisema wananchi hawana sababu ya kuilaumu Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kwa kupandisha bei ya nauli na badala yake lawama hizo zielekezwe kwa serikali ya Rais Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi, Faustine Sungura, alisema kutokana na matatizo hayo, kuna haja ya kuwepo kwa serikali mbadala, kwa madai kuwa serikali imeshindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi, hasa ya upandaji wa gharama za bidhaa mbalimbali.

“Watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na makosa, kwani muda waliowapa viongozi wa CCM kutawala unatosha na haujaonyesha mafanikio yoyote katika maisha zaidi ya kuzidisha ugumu wa maisha,” alisema.

“Watu wanakosea sana wanapoilaumu Sumatra badala ya kuilaumu serikali ambayo imeshindwa kudhibiti upandaji wa bei kwenye bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta,” alisema Sungura.

Alisema hata ziara anazofanya Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Ali Mohamed Shein ni dhihaka kwa Watanzania, kwani ahadi zao hazitekelezeki na wameshindwa kuwasaidia wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wanashinda Ikulu.

“Hivi hawa ni viongozi wa aina gani kama wameshindwa kuwasaidia wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshinda pale Ikulu, wataweza vipi kuwasaidia watu wa huko mikoani?” alihoji Sungura.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amesema serikali itahakikisha inafanya kila jitihada za kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwekeza kwenye kiwanda cha usindikaji wa matunda wilayani Muheza, kwa lengo la kuwatafutia wakulima wa machungwa soko la uhakika.

Alisema lengo la kujenga kiwanda hicho licha ya kumtafutia soko mkulima, lakini pia itakuza kipato cha wakulima sambamba na kupunguza kiwango kikubwa cha machungwa yanayoharibika mashambani kwa kukosa wanunuzi hasa nyakati za msimu.

“Serikali inaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumemsaidia mkulima kwa kiasi kikubwa kuwa na soko la uhakika sambamba na kukuza kipato chake ambacho hivi sasa kinapotea kutokana na kiasi kikubwa cha matunda kuharibika…nawaahidi kwamba hili tutalitekeleza haraka iwezekanavyo,” alisisitiza Rais Kikwete.

Miongoni mwa ahadi alizotoa rais wilayani Muheza ni pamoja na kupeleka darubini katika zahanati ya Kijiji cha Kicheba, kuchangia sh milioni mbili katika ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Mtindiro, sambamba na kutafuta magari ya wagonjwa katika wilaya zilizokosa huduma hiyo mkoani hapa.

HII SASA KALI, KAZI KWENU WADAU

Watanzania wavumilie shida wakati mama Salma anachezea pesa ya walipa kodi kwa shopping London, JK mwenyewe kwa misafara isiyokuwa na kichwa ughaibuni, pesa ya walipa kodi inakwapuliwa bila huruma kutoka kwenye BENKI ZETU. AKIANZA KWA MIFANO KUSAFISHA HAYO WTZ WATAMUUNGA MKONO.

JE, RAIS WETU AMEKUWA SULTANI KIPINGO?
 
Tizama hadithi za Abunuwasi, baaada ya kuununua uchaguzi akasema hivii:-


Mheshimiwa Spika:

1. Yameanza kujitokeza mawazo kuwa uongozi unaweza kununuliwa kwa fedha.

2. Kama ni kweli, tusipokuwa waangalifu, nchi yetu inaweza kuwekwa rehani kwa watu wenye fedha za kununua uongozi au wanaoweza kupata fedha za kufanya hivyo.

3. Lakini, fedha kutumika kununua ushindi si halali. Ni vema sasa tuanzishe mjadala wa kitaifa na hatimaye kuelewana kuhusu utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutafuta fedha za uchaguzi;

4. na utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutumia fedha hizo. Na utaratibu tutakaokubaliana uwe ni sehemu ya maadili ya uchaguzi katika uchaguzi wa kiserikali na ndani ya vyama vya siasa. Katika mjadala huo suala la takrima nalo tuliangalie.

FMES, Mkuu asante sana kwa kutuwekea hiyo hotuba hapa. Yaani ni upuuzi mtupu na dhihaka na fedhuli! Kumbe tulikuwa tunechoreka sana! Lakini ninaweza kusema kwa kujiamini kwamba sikumwamini JK tokea alipochukua fomu za kugombea in 1995! kwa hiyo mimi nilikuwa nasubiri watz wenzangu watakapoamka na kuona usanii wake na wanamtandao wake! This is just the beginning!
 
Back
Top Bottom