JK Vs SLAA: UNGEMCHAGUA NANI?

GIB

JF-Expert Member
Mar 2, 2012
336
92

Zaidi ya mwaka mmoja umeshapita sasa tangu Rais Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani katika muhula wake wa pili wa kuliongoza taifa hili. Ingawa mwaka mmoja sio muda wa kutosha kwa kiongozi kukamilisha malengo na ahadi zote,ni muda wa kutosha kutoa picha ya mfumo na mtindo wa ki-uongozi.
Je,mwaka mmoja baadae,uchaguzi ungefanyika unadhani kura yako ungempa nani katika ya Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa mpinzani wake mkuu katika uchaguzi uliopita,Dr.Wilbrod Slaa?
Kwanini?
Ninapoandika post hii,"madaktari wametangaza kuanza mgomo leo, wanaharakati nchini wamemtisha Rais Jakaya Kikwete kwamba endapo hatawaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Haji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, wataamua la kufanya"(Tanzania daima 7 march 2012).
Madaktari nao wasisitiza "Kama tulivyotaarifiana kwenye kikao chetu cha Machi 3, mwaka huu ni kwamba makubaliano yaliyofikiwa na hatimaye kutiliana saini kati ya madaktari na Serikali Machi 2, mwaka huu ni kuwa ili mazungumzo ya kujadili madai yetu yaweze kuendelea na hatua ya pili ni lazima, Waziri Dk Mponda na Naibu wake, Dk Nkya ama wawe wamejiuzulu au wamewajibishwa."

NB: Unaweza kutumia fursa hii kutoa maoni ya kujenga kwa maana ya kwamba kutoa maoni yenye tija na sio lawama na matusi.

Nawasilisha

Read more: JK Vs SLAA: UNGEMCHAGUA NANI? - BongoCelebrity
 
Hilo halina ubishi,maana mpaka mda huu na dakika hii rais wangu ni Dr SLAA!
 
Japokuwa hakutangazwa na tume iliyokuwa ya upande mmoja rais ni Dr SLAA jembe la ukweli.
 
jinsi ulivyotengeneza post yako inaonesha wazi unataka mchangiaji asimame wapi !
Haya nasimama unapotaka dr ametisha !
 
Unajua kuna maswali ya mtu mwenye busara kuuliza...ila kwa km akili zaitakuwa km za mkuu wa kaya utaweza kuuliza hadharani.
Hope Gab hapa umetukosea sana kuuliza swali km hili ambalo hata mtoto wa chekechea angesaidia kulijibu.
 
tunasema haya ni maswali mwongozo.jibu ni Dr.Slaa

WaTZ walimchagua Dr Slaa, akatangazwa kikwete, Wakamtaka Spika bora, Wakaletewa mwanamke. Ndo maana nchi imeyumba kiasi cha kutisha.

Kuna rafiki yangu aliniambia kuwa Tanzania ni nchi inaenda kama puto linaloelea angani bila kiongozi. Huna haja ya kwenda shule kuweza kubaini hili.

Kujibu swali lako: Kwa wakati kama huu mtu yeyote asingeweza kumchagua KIKWETE sio kwa sababu SLAA ni mtu makini no, kwa sababu KIKWETE ameonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye uongozi. Hata kama ungemlinganisha Sofia Simba.

JAmani tuchukue hatua, ombea nchi yetu. Pinga ukandamizaji kwa nguvu zote
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Chuo cha Polisi mjini Moshi leo Machi 6, 2012 tayari kwa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Shamsi Vuai Nahodha na kushoto kwake ni Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema.
 
'Ninge' 3times!

Watanzania tupewe shule ya kupiga kura.
Nadhani bado kuna kundi kubwa lina phobia au halioni umuhimu wa kupiga kura.
 
wakuu hivi ile kesi ya Dr wa ukweli kuhusu kupora mke wa mtu iliyopo pale manzese inaendeleaje????
 
Zaidi ya mwaka mmoja umeshapita sasa tangu Rais Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani katika muhula wake wa pili wa kuliongoza taifa hili. Ingawa mwaka mmoja sio muda wa kutosha kwa kiongozi kukamilisha malengo na ahadi zote,ni muda wa kutosha kutoa picha ya mfumo na mtindo wa ki-uongozi.
Je,mwaka mmoja baadae,uchaguzi ungefanyika unadhani kura yako ungempa nani katika ya Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa mpinzani wake mkuu katika uchaguzi uliopita,Dr.Wilbrod Slaa?
Kwanini?
Ninapoandika post hii,"madaktari wametangaza kuanza mgomo leo, wanaharakati nchini wamemtisha Rais Jakaya Kikwete kwamba endapo hatawaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Haji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, wataamua la kufanya"(Tanzania daima 7 march 2012).
Madaktari nao wasisitiza "Kama tulivyotaarifiana kwenye kikao chetu cha Machi 3, mwaka huu ni kwamba makubaliano yaliyofikiwa na hatimaye kutiliana saini kati ya madaktari na Serikali Machi 2, mwaka huu ni kuwa ili mazungumzo ya kujadili madai yetu yaweze kuendelea na hatua ya pili ni lazima, Waziri Dk Mponda na Naibu wake, Dk Nkya ama wawe wamejiuzulu au wamewajibishwa."

NB: Unaweza kutumia fursa hii kutoa maoni ya kujenga kwa maana ya kwamba kutoa maoni yenye tija na sio lawama na matusi.

Nawasilisha

Read more: JK Vs SLAA: UNGEMCHAGUA NANI? - BongoCelebrity

Unafanya comparisons ambazo sidhani kama zina maandiki. SLAA kaongoza lini tuone kama anaweza uongozi au kwa vile ni Mkurugenzi wa CCBRT? anaweza labda kuwa waziri wa Mambo ya Ndani.
Unapoongelea SLAA, MIGOMO YA MADAKTARI NA WANAHARAKATI, mimi nadhani unaongelea kitu kilekile kwa sababu hawa ni mapacha na wanasaidiana katika kupinga juhudi zote za serikali katika kuwahudumia wananchi.
 
Hizi Polls za mitandaoni huwa zinawadanganya sana Chadema, mnasahau wananchi walio wengi hawafiki huku.

Ndio maana watu wakitoa polls za ukweli huko mitaani kwa wananchi mnabaki kukandia, "ooh zimechakachuliwa".

Tafakari...
 
Rais wangu ni Dr slaa siku zote hadi mtoto wangu ukimuliza rais wako nani atakwambia Dr slaa! Kikwete mabangoni,Dr Slaa mioyoni mwetu.
 
usimwamshe aliyelala utalala wewe. Hawa wachache waliowezeshwa na Chadema humu JF waache watapetape wenzao wa CCM wanachapa mwendo.
 
Rais wangu ni Dr slaa siku zote hadi mtoto wangu ukimuliza rais wako nani atakwambia Dr slaa! Kikwete mabangoni,Dr Slaa mioyoni mwetu.

Inawezekana kabisa tunajua Dr. Slaa amewazalia watoto sana. Akina Joseph Mshumbuzi angekuwa mmoja bwana.
 
Back
Top Bottom