Mpigamsuli
JF-Expert Member
- May 24, 2012
- 3,885
- 575
Generalmwamunyange,shimbo na jesh zima sidhan kama wanafurahishwa na hilo la malaw kudai ziwa nyasa ni lao.
Kuna uzi mwaka jana ulitemebea hapa kuna mtu alielezea jinsi mipaka yetu inavyobadilishwa bim alisema pembe zote mpaka na Uganda ,Burundi,Ruanda,Kenya ,Zambia Malawi akaema upande wa malawi wamesogeza bim kwa mbali sana watu tulichangia lakini wengine wakasema mipaka yetu iko salama sijui kama kulikuwa na ufutiliajiMalawi inatoa wapi kiburi cha kutangaza sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni sehemu yake?hivi si kwamba sisi tumezembea mipaka yetu hadi jirani wameona udhaifu wetu?Hivi enzi za Mwalimu Nyerere Malawi wangethubutu?Kimsingi hata nchi jirani wameona udhaifu wa aina ya Uongozi tulio nao,uongozi hata kwenye mambo ya msingi unasema upepo utapita.
Serikali ya awamu ya nne chini ya utawala dhaifu wa JK,umeshindwa hata kulinda mipaka yetu,haingii akilini kuwa sasa nchi yetu imekuwa haina ulinzi wa kutosha kwenye mipaka hadi kusababisha mamia kama sio maelfu ya wahamiaji haramu kukamatia maeneo ya Katikati ya nchi,hii inaonyesha kuwa mipaka yetu haipo salama.
Sababu ya kuipiga Malawi tunayo,Uwezo tunao,na nia tunayo,JK peleka jeshi ziwa nyasa,angalau katika hili utakumbukwa kwalo kuwa ulisimama imara kuitetea mipaka ya Jamhuri yetu,kuendelea kukaa kimya kunawapa Malawi advantage a hivyo kuadhiri wananchi kwa ujumla kisaikolojia,ni lazima serikali yako ichukue hatua
Haaaaa haa Mkuu umenifurahisha sn! Hata mm nimeshawahi kukaona hako kaboti!!Tunacho kikosi imara pale Kyela tangia enzi za Nyerere. Huwa nawaona wanafyeka majani baadae wanacheza draft wakisubiri mtu akatishe uwanja wa jeshi wamsulubishe. Ukienda Itungi port utakuta kuna kaboat ka zamani sana hambako hurusiwi kukapiga picha eti ni kifaa cha kivita. Sina uhakika kama hata mafuta ya h
patrol yanatolewa na serikali maana sijawahi kuiona katikati ya ziwa.
Nafikiri huyu mama wa Malawi atatuamsha usingizini sasa.
JK kama utahitaji askari wa akiba, naomba unihesabu mimi, maana tangu nimetoka JKT sikamua triga wala kuosha mtutu kwa mdeki.
Jeshi la wananchi wa tz kwa ujumla linasubiri amri kutoka kwa jk,na tunawapiga kwa kikosi cha brigedi ya magharib tu.
Haya yaliwahi kuibuka awamu zilizopita?
huyu wa kwetu ni mdhaifu sana mbele ya kina mama,Angalieni isijeikawa kahonga ziwa nyasa anatuzuga tuu,kama sio mbona hajatoa kauli yoyote
Hili la Malawi kudai ziwa Nyasa lilishawahi kuibuka mwaka 1979 wakati ule Rais alikuwa Nyerere tena ilikuwa ni baada tu ya kumng'oa Iddi amin.
Alichofanya Nyerere ni kupeleka majeshi mpakani mwa Tz na Malawi cha ajabu Wamalawi hawakuendeleza chkochoko mpaka leo ndio wameamua kulianzisha tena.
Haaaaa haa Mkuu umenifurahisha sn! Hata mm nimeshawahi kukaona hako kaboti!!
na hapa ndo mahali J.K anatakiwa kurudisha heshima yake kwa kuwatandika Wamalawi angalau tuwe na kakumkumbukahapo ndo jeshi linatakiwa itumike,siyo kuzuia maandamano,na wananchi wanaodai haki zao,kama wana ubavu wapelekwe huko