Uovu ziwa Tanganyika. Lifungwe haraka

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
567
1,550
Kabla ya utekelezaji wa mkataba wa kufunga Ziwa Tanganyika, lazima tuyajue mambo kadhaa Kwa uhalisia wake.

Mwambao mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuanzia Kata ya Kagunga( Mpakani) Mpaka Kata ya Kalya Kigoma kusini hapo ndipo utakuta makundi ya wahamiaji/ wavuvi Haramu kutoka Burundi na Congo. Kuna sababu kadhaa ambazo zimepelekea wimbi kubwa la wavuvi Haramu toka Burundi na Congo. Katika tafiti niliyofanya ni kwamba wavuvi Haramu toka Congo sio kutoka mwambao wa ziwa Tanganyika Kwa upande wa Congo. Wengi wametoka umbali wa zaidi ya kilomita mia sita huko Kivu Kasakazini katika Mji wa Goma kwenye visiwa vya Idjwi. Hawa ni wakimbizi wa athali walizo zisababibsha wenyewe huko kwao katika ziwa Kivu.

Baada ya kuendesha uvuvi Haramu huko kwao na kumaliza samaki Wote, ilipelekea serikali ya Congo kuweka Sheria Kali sana ambapo ilibidi wavuvi hao Haramu kuhamisha mitego Yao kuja ziwa Tanganyika. Walipofika Ziwa Tanganyika walikuta Kuna Sheria Kali pia huko Upande wa Congo na Burundi. Hii ilipelekea wavuvi hao kuangalia nchi dhaifu na kugundua kuwa Tanzania ndio sehem pekee za kufanya uvuvi wao Haramu. Ili kujificha zaidi waliamua kuingia ndani zaidi mwa Mkoa wa Kigoma, Katavi na Rukwa.

Wakati wakiwasili waliungana na Makundi makubwa ya wavuvi Haramu toka Burundi. Mpaka kufika mwaka 2020 kulikuwa na zaidi ya wavuvi Haramu 4000 toka Burundi na Congo. Ukweli ni kwamba vyombo vingi vya uvuvi Haramu vinamilikiwa na Matajiri wakubwa toka Burundi na wengine ni viongozi wa Siasa na jeshi toka Burundi. Asilimia kubwa ya wavuvi katika vyombo hivyo ni walio wahi kuwa wanajeshi wa serikali au makundi ya waasi.

BIASHARA YA KU-EXPORT SAMAKI -BUJUMBURA
Hii biashara inafanywa na Matajiri ambao wamefungua makampuni ya kuuza samaki kwenda Marekani na Canada kutokea Burundi Bujumbura. Makampuni hayo ndio yanayo fadhili vyombo vya uvuvi mkoani Kigoma.

Ukwepaji Kodi
Katika kutelekeza kutorosha samaki bila kulipa Kodi stahiki, Warundi hutumia leseni za watanzania katika kusafirisha Samaki mpaka katika paka wa manyovu ambapo huvusha samaki bila kulipa Kodi stahiki.
Pia hupakia katika boti toka Bandari za Sibwesa na Mgambo. Boti huondoka kupita katika umbali ambao ni katikati ya ziwa Tanganyika na kutokezea Burundi.
Kila wiki husafirishwa zaidi ya Tani 200 kwenda Burundi Kwa ajili ya kuuzwa Ulaya.

Maeneo hatari Kwa uvuvi Haramu

Yapo maeneo hatari Kwa uvuvi Haramu. Warundi na wakongo wamekaa katika maeneo ya kimkakati, ambapo wameamua kuanzisha vijiji na kuweka uongozi wao. Maeneo haya ni kuzunguka hifadhi ya Taifa ya Mahale. Upande wa kaskazini wamekaa katika ameneo ya Rubengela, Mkuyu na Herembe.

Upande wa kusini wamenzia kwenye mpaka na hifadhi katika kijijini Cha Sibwesa ( Eneo linaitwa Nanga) Kisha wakaanzisha Kijiji Chao sehem inaitwa Kamakala na Rwega ( Mpakani kati ya Kigoma na Katavi)

Screenshot_20230512-094514.jpg
Katika maeneo hayo utakuta mpaka viongozi wa mitaa mi Warundi. Wameweka tozo, Kodi na malipo mbalimbali ambayo hupelekwa Burundi.

Pia hapo wanamfumo wa kupokea wageni bila serikali kujua. Katika ameneo hayo, Lugha kuu ni Kirundi na hata mauziano yanaweza kufanyika Kwa pesa za Burundi.

Hapo utakuta Mwenye chombo Cha uvuvi ni Mrundi au Mkongo, Wavuvi Wote ni Warundi au Wacongo. Wafanyakazi wa kusindika samaki lazima awe Mrundi na hata Mtanzania akiomba kazi hapewi.
Wanapovua samaki hao wa Tanzania wanahakikisha hakun Mtanzania ambaye amenufaika na samaki hao.

Huko kumejaa Visa vya Watanzania kuuwawa Kwa kuchomwa visu. Hii imepelekea vijana wengi kuogopa kwenda ameneo hayo. Mfano mwaka Jana mwezi November aliuwawa Binti Mtanzania Kwa kuchomwa kisu na Warundi na kutupwa ufukweni mwa ziwa na wauwaji kubaki wakitamba mtaani.

Hapo ukifika leo utauziwa kipande Cha Ardhi ambayo inamilikiwa na Mrundi muhamiaji haramu na Mtanzania Hauna mamlaka ya kuitumia. Hapo utakuta Mrudi kuanzia ukoo mzima Babu mpaka mjukuu wamehamia hapo.

Katika maeneo yote hayo kunafanyika uharibifu mkubwa wa misitu. Warundi hapo wamiliki mashine za kukata miti (chainsaw) Kwa ajili ya mbao na Kuni za kukausha samaki. Takribani hekari 50 za miti hukatwa Kila mwezi katika maeneo ya kuzunguka hifadhi ya Mahale.

Hapo utaona namna watu kutoka Congo na Burundi wanavyo ingia Tanzania kupitia Ziwa Tanganyika na kupokelewa na Uongozi wa Warundi na kuhifadhiwa bila mamlaka za uhamiaji kujua lolote. Hapo kuningizwa chochote kizuri au kibaya bila Serikali kujua. Jambo la kuishangaza ni pale viongozi wa serikali wanapo shirikiana na wageni.

Mfano mwaka Jana mwezi Oktoba kulifanyika Mkutano wa Diwani wa Kalya Mh. Mateso na kundi la Warundi hao wavuvi Haramu huku akiwa na agenda kuu ya kuwahamasisha kujenga makazi ya kudumu. Ililifikia hatua ya kugawa ameneo ya Ardhi katika Eneo Kando ya Hifadhi ya Mahale na kuwapa Warundi wajenge huku wakiahidiwa kutambuliwa kama kitongoji rasmi na ahdi za kupewa miundombinu ya shule na Baranara.

Namna uvuvi Haramu hufanyika
Kwa kawaida samahi huvuliwa katika Maji ya kina Cha juu Kwa kutumia mvuto wa mbanga wa taa. Hii hufanyika kipindi Cha Giza na ifikapo kipindi Cha Mabalamwezi wavuvi katika ziwa Tanganyika huginga uvuvi na kupumzika Kwa wiki mbili.

Katika kipindi hiki samahi hupata kuzaliana na utulivu wa mazingira kabla ya wavuvi kurejea kipindi Cha Giza.
Namna hii ya uvuvi imekua ni desturi iliyo rithiwa toka enzi na hata tafiti za kitaalam zinabariki mfumo huu Bora Kwa ikolojia ya ziwa Tanganyika.Mfumo huu Bora umefanya Eneo hasa Kigoma kusini kuwa pekee liliobakia na ifadhi ya samaki tofauti na sehemu zote katika Ziwa Tanganyika katika nchi zote. Na hii ndio iliwavuta Wavuvi Haram Toka Congo na Burundi kuja Tanzania baada ya Serikali zao kuchukua hatua Kali.

Kinyume na mfumo huo Bora, Walipovamua wavuvi Haramu toka Burundi, walikuja na mfumo hatari sana.
Nyavu zao ni maalum Kwa iunasa samaki wakubwa Kwa wadogo. Vyavu hizo Haram ambazo zimepigwa marufuku kutumika katika maeneo mengi Duniani, huuzwa Toka Congo na kuningizwa Tanzania kupitia mipaka isiyo rasmi. Nyavu hizo mara nyingi hukatika na kuzama chino ya Maji. Nyavu hizo huweza kukaa miaka 100 bila kuoza na wakati huo zikiendelea kunasa na kuua samaki. Nyavu hizo zenye urefu wa kilomita zaidi ya Kumi na upana mapaka wa mitaa 50 hudondokea ziwani Kila Mwezi.Inakadiliwa Kila miezi sita hasa kipindi Cha masika Kuna zaidi ya Nyavu 8000 kupotelea ziwani.

Wavuvi Haram wao wanaanza uvuvi katika Mabalamwezi. Wakati samaki walitakiwa kutulia na kuzalia, hapo ndipo hukumbana na mitego ya Warundi na Wacongo. Hivyo mbali na kuvua samaki wadogo Bado wavuvi hao huvuruga ikolojia ya ziwa Tanganyika. Hayo waliyafanya huko kwao Kwa miaka mingi mpaka walipo maliza samaki Wote na Kisha kukimbilia Tanzania.

Tunaomba serika mbali na kulifunga Ziwa Tanganyika pia Ifanyike Operation maalum kama Operation Tokomeza na Operation Kimbunga. Kiuhalisia kulifunga Ziwa Tanganyika kuna faida kubwa sana.Tunaamini kama sio uvamizi huu wa Wageni Toka nje, tusingeona athali wala utazima wa kufunga uvuvi.

Baada ya hapo nini kifanyike?
Baada ya kulifunga Ziwa Tanganyika.Tunahitaji kufanya mambo Kadhaa.

1. Kuondoka maafisa uvuvi Wote Mkoa wa Kigoma.
2. Kufanya usajili wa wamiliki wa vyombo vya uvuvi Kwa kutumia vitambulisho vya utaifa NIDA

3. Kuweka vyeti na vitambulisho maalum Kwa wavuvi Kwa kutumia NIDA

4.Kutunga Sheria maalum ya kufunga uvuvi katika ziwa Tanganyika Kila ifikapo Mbalawezi. Kwa kufanya hivi pekee itazuwia uvuvi Haramu Kwa asilimia 90 kwani wengi hutumia Mbalawezi badala ya mataa kama nyenzo ya kivuta samaki na wavuvi Haramu hawawezi kuvua katika Giza. Hivyo ni vema kuweka Sheria na adhabu Kali mpaka ya kuteketeza nyavu endapo mtua atakamatwa anavua Mbalawezi.
Hii inafanyika huko Congo ambapo nyavu hizihizi Haramu endapo zikikamatwa huchomwa moto na mitumbwi kitaifishwa. Na Sheria hizi ndizo zimewakimbiza huko na kukimbilia Tanzania kwenye shmba la Bibi.

Tumesikia Wanasiasa wakiongozwa na Zitto Kabwa wakijaribu kutete. Naamini hawahui uhalisia huu na hawajafanya utafiti wowote. Huko Congo pamoja na maandamano Bado amri imtoka Kwa maandihi na utekelezaji unaendelea.

IMG-20230512-WA0000.jpg
Screenshot_20230512-095820.jpg


Nchi kama Zambia walianza mapemba ambapo Kila ifikapo November mosi maziwa yote hugungwa na hata kusafirisha Samaki hairujusiwi mapaka ifike mwezi March.

TULINDE NCHI YETU NA RASILIMALI ZETU KWA FAIDA YETU.
 

Attachments

  • Screenshot_20230512-094514.jpg
    Screenshot_20230512-094514.jpg
    158.8 KB · Views: 10
Kwanini walifunge badala ya kuimarisha ulinzi ili mapato halali yapatikane na kuondoa uvuvi haramu?
 
Kabla ya utekelezaji wa mkataba wa kufunga Ziwa Tanganyika, lazima tuyajue mambo kadhaa Kwa uhalisia wake.
Mwambao mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuanzia ...
aseeh, umecho kiandika hapa ni ukweli mtupu. warundi na wa congomani wamesha ufanya mkoa wa kigoma kama wa kwao. Nimeshuhudia mara kadhaa watanzania wakinyimwa kazi za kivuvi kwa kisingizio cha uvivu.

Hatimae huleta wavuvi kutoka makwao kitu ambacho sio sawa kabisa na kinahatarisha usalama wa nchi. kuna wakati wanajifanya na wao ni raia wa Tanzania kisa wanaongea kiswahili cha mchongo.

Wanaanza kuvamia aridhi (mashamba na viwanja) kwa mabavu. serikali inatakiwa kuliangalia hili.

Wafuate sheria kwanza ya kufanya kazi na kukaa nchini kwa vibali
 
Kabla ya utekelezaji wa mkataba wa kufunga Ziwa Tanganyika, lazima tuyajue mambo kadhaa Kwa uhalisia wake.
Mwambao mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuanzia Kata ya Kagunga( Mpakani) Mpaka Kata ya Kalya Kigoma kusini hapo ndipo utakuta makundi ya wahamiaji/ wavuvi Haramu kutoka Burundi na Congo.
K
Tatizo la watu wa sehemu hizo ni kwamba wao ndo wanaowahifadhi hao wageni kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa,maafisa uvuvi na viongozi wengine wa ngazi za juu.mikoa hiyo mitatu kigoma,rukwa na katavi ina wageni wengi sana na wengine wamefanikiwa hata kupenya kwenye nyazifa za juu serikalini.kigoma wakazi wake wengi ni warundi na ndo wafanyabishara wakubwa mkoani hapo.

Na wengi wa hao walikaribishwa na wenyeji.pia watu wa kigoma ni vigeugeu na wanapotakiwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka huwa hawako tayari sababu wameingiliana sana.serikali inabidi ifanye juhudi za maksudi ya kuwatambua na kuwarudisha makwao vinginevyo kivu ya kaskazini itahamia kigoma,katavi na rukwa.
 
tatizo la watu wa sehemu hizo ni kwamba wao ndo wanaowahifadhi hao wageni kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa,maafisa uvuvi na viongozi wengine wa ngazi za juu.mikoa hiyo mitatu kigoma,rukwa na katavi ina wageni wengi sana na wengine wamefanikiwa hata kupenya kwenye nyazifa za juu serikalini.kigoma wakazi wake wengi ni warundi na ndo wafanyabishara wakubwa mkoani hapo.na wengi wa hao walikaribishwa na wenyeji.pia watu wa kigoma ni vigeugeu na wanapotakiwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka huwa hawako tayari sababu wameingiliana sana.serikali inabidi ifanye juhudi za maksudi ya kuwatambua na kuwarudisha makwao vinginevyo kivu ya kaskazini itahamia kigoma,katavi na rukwa.
nikweli wapo baadhi ya wamiliki wa mitego. niwatanzania lakini huwezi kukuta wameajiri mtanzania wanaajiri hao wageni
 
wa
Kabla ya utekelezaji wa mkataba wa kufunga Ziwa Tanganyika, lazima tuyajue mambo kadhaa Kwa uhalisia wake.
Mwambao mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuanzia Kata ya Kagunga( Mpakani) Mpaka Kata ya Kalya Kigoma kusini hapo ndipo utakuta makundi ya wahamiaji/ wavuvi Haramu kutoka Burundi na Congo.
Wale wabunge waliokuwa wanapiga kelele hadi kufikia kutaka kukwamisha bajet ya Uvuvi na Mifugo wametokea nchi hizo za Congo na Burundi? Huo mpaka wa Magharibi una matatizo makubwa. Inawezekana kabisa hao viongozi ni wahamiaji haramu wana ndugu zao Congo na Burundi. Rais km nchi imemshindakwa maana ya ukubwa ni bora waigawe, ingawa Tanzania ni nchi ya 13 kwa ukubwa Africa.

Siyo kwamba nchi ni kubwa vichwa vinavyoongoza nchi hii ni vidogo sana. Watu hawana uzalendo, hawana uchungu na nchi yao utafikiri kuna nchi tutahamia tukiharibu ya kwetu. Hebu jaribu kwenda nchi za watu na ufanye ujinga wako km huo, km haijarudi maiti au hata isizikwe, wenzetu hawana mchezo na nchi zao kwani wanajua hakuna sehemu nyingine hapa duniani ukaenda ukaishi kwa uhuru na amani. Inauma sana wahamiaji haramu wanajitengenezea kitongoji na wanahamisha mali zetu kupeleka kwao maana wanajua hapa si kwao, halafu eti wanawabagua mpaka kuwaua wenye nchi yao? JWTZ wanalindaga mipaka ipi? Uhamiaji wako wapi? Au nao ni wa kutoka nchi hizo?
 
wa

Wale wabunge waliokuwa wanapiga kelele hadi kufikia kutaka kukwamisha bajet ya Uvuvi na Mifugo wametokea nchi hizo za Congo na Burundi? Huo mpaka wa Magharibi una matatizo makubwa. Inawezekana kabisa hao viongozi ni wahamiaji haramu wana ndugu zao Congo na Burundi. Rais km nchi imemshindakwa maana ya ukubwa ni bora waigawe, ingawa Tanzania ni nchi ya 13 kwa ukubwa Africa.

Siyo kwamba nchi ni kubwa vichwa vinavyoongoza nchi hii ni vidogo sana. Watu hawana uzalendo, hawana uchungu na nchi yao utafikiri kuna nchi tutahamia tukiharibu ya kwetu. Hebu jaribu kwenda nchi za watu na ufanye ujinga wako km huo, km haijarudi maiti au hata isizikwe, wenzetu hawana mchezo na nchi zao kwani wanajua hakuna sehemu nyingine hapa duniani ukaenda ukaishi kwa uhuru na amani. Inauma sana wahamiaji haramu wanajitengenezea kitongoji na wanahamisha mali zetu kupeleka kwao maana wanajua hapa si kwao, halafu eti wanawabagua mpaka kuwaua wenye nchi yao? JWTZ wanalindaga mipaka ipi? Uhamiaji wako wapi? Au nao ni wa kutoka nchi hizo?
tatizo sio uhamiaji wala jwtz. hata sisi raia tunashida sisi ndio tunatakiwa kuwa walinzi namba 1 wa mipaka yetu
 
Back
Top Bottom