Tanzania ni nchi yenye maziwa makuu mengi barani Afrika, kwanini bado kuna shida ya maji hususani kwenye mikoa inayozungukwa na maziwa hayo?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,864
Tanzania ni moja kati ya Nchi zilizobarikiwa kwa rasilimali nyingi na ardhi nzuri Duniani.

Miongoni mwa rasilimali tulizonazo ni Maziwa Makuu ambayo ni Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa (Likifahamika kidunia kama Ziwa Malawi) na mengine kama Ziwa Rukwa, Ziwa Eyasi, Ziwa Natron, Ziwa Manyara, Ziwa Burigi, na maziwa mengine madogo madogo, mabwawa pamoja na mito.

Africa_(satellite_image).jpg

Mikoa inayozungukwa na Maziwa Makuu ni;
1. Mara (Ziwa Victoria)
2. Simiyu (Ziwa Victoria)
3. Mwanza (Ziwa Victoria)
4. Geita (Ziwa Victoria)
5. Kagera (Ziwa Victoria)
6. Kigoma (Ziwa Tanganyika)
7. Katavi (Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa)
8. Rukwa (Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa)
9. Mbeya (Ziwa Nyasa)
10. Njombe (Ziwa Nyasa)
11. Ruvuma (Ziwa Nyasa)

images (3).jpeg

Hii ndio mikoa inayozungukwa na maziwa makuu yenye uhakika wa maji kwa muda wote na mrefu zaidi.

images (2).jpeg

SWALI: Ni kwa nini Jiji kama Mwanza ambalo asilimia kubwa ya Wilaya zake ziko ukingoni mwa ziwa Victoria kuwe na shida kubwa ya maji. Mwanza ni miongoni mwa majiji yanayokuwa kwa kasi barani Afrika na kwa ukanda wa Ziwa Victoria, Jiji la Mwanza linatunishiana vifua na majiji kama Kampala, Uganda na Kisumu, Kenya.

Inasikitisha na ni aibu kuona Majiji mengine barani Afrika ambayo Nchi zao hazina hata Maziwa makubwa mfano Botswana, wanaweza kuwa na maji ya uhakika wakati jiji kama Mwanza lililoko pembezoni ya ziwa wananchi wake wakiwa bado wanatumia maji ya Visima au ya kuagiza kuchota umbali mrefu.

Hivyo hivyo kwa mikoa mingine inayopakana na Maziwa Makuu Nchini Tanzania nao wanapitia changamoto ya kukosa maji wakati wapo kwenye maziwa makuu. Tumepewa maji ya uhakika na Mungu ila tunayaangalia tu huku wananchi wakipata tabu, wakati nchi nyingine wanatumia mito tu na wanauhakika wa maji kwenye miji yao mikuu.
 
Mada fikiri itakayopata majibu ya kisiasa, huku lingusenguse mto Ruvuma wenye fresh water haupo mbali sana,ila maji Safi na salama ni shida
 
Tanzania ni moja kati ya Nchi zilizobarikiwa kwa rasilimali nyingi na ardhi nzuri Duniani.

Miongoni mwa rasilimali tulizonazo ni Maziwa Makuu ambayo ni Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa (Likifahamika kidunia kama Ziwa Malawi) na mengine kama Ziwa Rukwa, Ziwa Eyasi, Ziwa Natron, Ziwa Manyara, Ziwa Burigi, na maziwa mengine madogo madogo, mabwawa pamoja na mito.
Hakika🙏🙏🙏
 
Inafikirisha sana
 
View attachment 2757885
Mikoa inayozungukwa na Maziwa Makuu ni;
1. Mara (Ziwa Victoria)
2. Simiyu (Ziwa Victoria)
3. Mwanza (Ziwa Victoria)
4. Geita (Ziwa Victoria)
5. Kagera (Ziwa Victoria)
6. Kigoma (Ziwa Tanganyika)
7. Katavi (Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa)
8. Rukwa (Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa)
9. Mbeya (Ziwa Nyasa)
10. Njombe (Ziwa Nyasa)
11. Ruvuma (Ziwa Nyasa)

View attachment 2757886

Hii ndio mikoa inayozungukwa na maziwa makuu yenye uhakika wa maji kwa muda wote na mrefu zaidi.

View attachment 2757887

SWALI: Ni kwa nini Jiji kama Mwanza ambalo asilimia kubwa ya Wilaya zake ziko ukingoni mwa ziwa Victoria kuwe na shida kubwa ya maji. Mwanza ni miongoni mwa majiji yanayokuwa kwa kasi barani Afrika na kwa ukanda wa Ziwa Victoria, Jiji la Mwanza linatunishiana vifua na majiji kama Kampala, Uganda na Kisumu, Kenya.

Inasikitisha na ni aibu kuona Majiji mengine barani Afrika ambayo Nchi zao hazina hata Maziwa makubwa mfano Botswana, wanaweza kuwa na maji ya uhakika wakati jiji kama Mwanza lililoko pembezoni ya ziwa wananchi wake wakiwa bado wanatumia maji ya Visima au ya kuagiza kuchota umbali mrefu.

Hivyo hivyo kwa mikoa mingine inayopakana na Maziwa Makuu Nchini Tanzania nao wanapitia changamoto ya kukosa maji wakati wapo kwenye maziwa makuu. Tumepewa maji ya uhakika na Mungu ila tunayaangalia tu huku wananchi wakipata tabu, wakati nchi nyingine wanatumia mito tu na wanauhakika wa maji kwenye miji yao mikuu.
Aibu hii!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom