JK: Ni Marufuku kipengele cha Dini kwenye Sensa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Source Habari Leo na Jambo leo

Akiwa mjini Mbeya rais J. Kikwete kasema kuwa ni MARUFUKU kuweka kipengere cha dini kwenye hesabu ya sensa na makazi itakayo anza mwezi ujao na kusisitiza kuwa dhamila ya serikali ni kujua idadi ya watu wake sio idadi ya waumini wa Tanzania na kuainisha kuwa vitu vya msingi ni;

Kujua idadi ya watu kwa maendeleo ya mipango ya serikali tu hakuna cha ziada.

Concern

LIWALO NA LIWE
 
Mnafiki tu! Anawalea mwenyewe hao wanaopiga domo la kususia sensa kwa kipengele cha udini halafu anajifanya hayupo nao. Hipocrite!

Ni kweli kabisa hawa kina Sheikh Ponda walikufa naona ghafula wamefufuka wakati wake huu.
 
Source Habari Leo na Jambo leo

Akiwa mjini Mbeya rais J. Kikwete kasema kuwa ni MARUFUKU kuweka kipengere cha dini kwenye hesabu ya sensa na makazi itakayo anza mwezi ujao na kusisitiza kuwa dhamila ya serikali ni kujua idadi ya watu wake sio idadi ya waumini wa Tanzania na kuainisha kuwa vitu vya msingi ni;

Kujua idadi ya watu kwa maendeleo ya mipango ya serikali tu hakuna cha ziada.

Concern

LIWALO NA LIWE

Hapo amenena
 
Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kuwa kipengele cha dini hakitaingizwa kwenye maswali ya Sensa ya Watu na Makazi kwa sababu lengo ni kutaka kufahamu idadi ya Watanzania isaidie katika kupanga mipango ya maendeleo ambayo haipangwi kwa misingi ya dini.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa swali kuhusu dini halijapata kuwepo katika maswali katika sensa zote zilizopita.

"Halipo na halijawahi kuwepo," alisema.

Alisema hayo jana kwenye mkutano wa wananchi katika eneo la Swaya, nje kidogo ya Mji wa Mbeya wakati akizindua mradi mkubwa wa maji kwa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake.

"Nafahamu kuwepo madai ya baadhi ya watu kutaka swali la watu kuwa na dini gani liingizwe. Swali hili halipo na halikuwahi kuwepo kwa nia njema kabisa," alisema na kuongeza: "Hatupangi mipango yetu ya maendeleo kwa misingi ya dini au rangi za watu bali kwa kuzingatia maeneo na shughuli, mambo ambayo hunufaisha watu wa dini zote".

Alifafanua zaidi kwamba siyo kwamba serikali inapuuza dini za watu bali shabaha ya Sensa ni maendeleo ya wote.
 
Source Habari Leo na Jambo leo

Akiwa mjini Mbeya rais J. Kikwete kasema kuwa ni MARUFUKU kuweka kipengere cha dini kwenye hesabu ya sensa na makazi itakayo anza mwezi ujao na kusisitiza kuwa dhamila ya serikali ni kujua idadi ya watu wake sio idadi ya waumini wa Tanzania na kuainisha kuwa vitu vya msingi ni;

Kujua idadi ya watu kwa maendeleo ya mipango ya serikali tu hakuna cha ziada.

Concern

LIWALO NA LIWE

Hakuna Jipya, mwisho wa ck anayetaka atashiriki na asiyetaka atakaa pembeni.
Ila binafsi sioni tatizo kuweka kipengele cha dini ktk sensa, nchi nyingi duniani zinafanya
na wala hukuna tatizo. Inaelekea kuna watu wanahofu zisizo na msingi.
 
Serikali inaogopa nini? Anhaa inaogopa mfumokristo! Kama ndivyo basi aongeze magereza kwakuwa yaliyopo hayatatosha. Chukua mfano waislam ni nusu ya Watanzania! Robotatu ya waislam washiriki sensa na robo ambayo ni zaidi ya milioni tano wanagomea sensa! JK atawaweka wapi watu wote hawa? Serikali inakawaida ya kutisha na kutenda,lakini kwa hili mh! Amani mashakani.
 
J Kikwete anastahili sifa kwa mara nyingine tena amedhihirisha yeye ni Rais wa Tanzania na si mwakilishi wa dini yoyote.Hii ni mara ya pili Rais Kikwete anaeleza ukweli mweupe viongozi wa dini ya kiIslam wasiliingize taifa katika mvurugano wa udini.Nakumbuka mwaka jana mjini Dodoma nadhani katika sikukuu ya Maulid aliwaambia waIslam waanzishe na kuiendesha mahakama ya Kadhi wenyewe wasitegemee ufadhili wa serekali.

Utashangaa wapo baadhi ya wanaojiita viongozi wa taasisi mbali mbali bado wanashinikiza mambo yasiyowezekana,nampongeza Sheikh mkuu Mheshimiwa Simba kwa kuanza kuwateua makadhi wa mikoa mbali mbali ikiwa ni hatua ya kuitikia na kutekeleza mwito wa serekali wa kuanzisha na kuendesha mahakama ya kadhi.Naipongeza BAKWATA na wanazuoni wa kiIslam kwa kukubali kwamba sensa ni kwaajili ya maendeleo ya watanzania wote na si kwaajili ya dini yoyote.
 
Taratibu nchi inakariibia boiling point NSSF ,SENSA, mgomo Madkatari,......... etc. Jamani fungeni milango wanakuja!
 
Source Habari Leo na Jambo leo

Akiwa mjini Mbeya rais J. Kikwete kasema kuwa ni MARUFUKU kuweka kipengere cha dini kwenye hesabu ya sensa na makazi itakayo anza mwezi ujao na kusisitiza kuwa dhamila ya serikali ni kujua idadi ya watu wake sio idadi ya waumini wa Tanzania na kuainisha kuwa vitu vya msingi ni;

Kujua idadi ya watu kwa maendeleo ya mipango ya serikali tu hakuna cha ziada.

Concern

LIWALO NA LIWE

Asubiri mfungo uishe akawatangazie hayo kwenye sherehe za Idd kama kweli ana maanisha hayo anayoyasema!!
 
Asubiri mfungo uishe akawatangazie hayo kwenye sherehe za Idd kama kweli ana maanisha hayo anayoyasema!!

Mfungo ukiisha, hiyo Sensa itakuwa haijamalizika tu? Atawatangazia nini sasa wakati jambo lenyewe litakuwa limeshapita? Mimi naona ni sahihi alivyoamua kusema sasa, ingawa hata hivyo alichelewa sana kutamka hayo.
 
Kwenye nchi ya wengi compromise ni muhimu na kutambua kwamba hakuna kundi litakalo yote ya wanayotaka.
 
mambo ya dini anasubiri muda wa kampeni ukikaribia, kwangu mimi huyu jamaa ni mdini na ni mnafki tu. anaonge asicho maanisha. ni bahati mbaya sana watanzani hatujawahi kuwa na rais makini... sikjui kuhusiana na mwalimu jk. kazi tunayo
 
Ngongo Hakuna lolote ni usanii tu .
Hukusikia waziri mkuu akisema serikali ita wafathili mashea kwenda kujifunza ? je huo sio uthamini ?
JK nizaidi ya umjuavyo.

kila kiongozi ana laki Makamu warahisi alisema mahakam yakathi inashuhulikiwa na serikali kwahivyo waislamu watulie JK kasema waislamu waanzishe wenyewe na serikali haitawasaidia , Juzi waziri mkuu kasema serikali itawafathili mashee kwenda kujifunza namna yakuendesha hi mahakama .

wajinga ndo waliwao
 
Last edited by a moderator:
Kikwete alisimamia kuingizwa kipengele cha kadhi kwenye ilani nawe unasema si mwakilishi wa dini yoyote?

Huyo simba na Bakwata si ndio hao hao waliosema watainyima CCM kura, watasusia sensa - leo wamegeula vipi? Imani huwa inageuka. Askofu akikana imani yake inambidi aenguliwe na mwingine achukue nafasi yake. Sasa mufti leo nataka kesho sitaki.

vidini vingine bana?
 
Back
Top Bottom