sir.JAPHET
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 699
- 133
[h=2][/h] Jumanne, Septemba 18, 2012 05:41 Na Oliver Oswald, Dar es Salaam
RAIS Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja, unaoendelea katika baadhi ya maeneo nchini.
Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango, alisema uzinduzi huo utahusisha miradi mitatu ambayo ni ya ujenzi wa madaraja, barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi pamoja na barabara za kawaida, ikiwamo Barabara ya Makofia-Msata.
Alisema kwa sasa Serikali ya awamu ya nne inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa yote.
Balozi Mrango alisema kuna barabara zenye urefu wa kilomita 11,154, ambazo zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Kwa mujibu wa Balozi Mrango, Rais Kikwete, ataanza na uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Makofia-Msata, iliyopo Bagamoyo, yenye urefu wa kilomita 64 na kwamba uzinduzi huo utafanyika katika Kijiji cha Kiwangwa kesho.
Kesho (leo), Rais atazindua ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam ambao mkandarasi wa mradi huu ni Strabag International.
Mradi huu unahusisha Barabara za Kimara kuelekea Kivukoni, Magomeni kuelekea Morocco na Fire hadi Kariakoo.
Septemba kesho kutwa (kesho), atazindua ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambapo sherehe zitafanyika Kurasini, alisema Balozi Mrango.
Alisema pia kwamba, daraja hilo la Kigamboni linajengwa na Mkandarasi wa China Railway Constrution Company Limited, kwa kushirikiana na China Major Bridge Engineering Company Limited.