JK mgeni rasmi uzinduzi wa barabara

Sehemu ya Barabara ya Bagamoyo - Msata iliyojengwa kwa kiwango cha lami ambayo ujenzi wake ulizinduliwa rasmi leo na Rais Dk Jakaya Kikwete, huko Kiwangwa, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani

Source:
http://issamichuzi.blogspot.com/2012/08/barabara-ya-msata-bagamoyo-sasa-mambo.html

Wenzake akina Kibaki wanazindua barabara za ukweli siyo hizi njia za ng'ombe!
 
Naona JK sasa ameamua kuingilia kazi za Bilali(Mzee mkasi),

maana tulishazoea sana kumwona Bilali akitembea na mkasi kwenye koti lake, ili kila anapofika kuzindua miradi asihangaike kutafuta mkasi wa kukata utepe.

Hizi si ndo atakuja kutudanganyia toto kuwa ni sehemu ya ahadi!!! Magamba bana....wizi mtupu.
 
Sasa yy anazndua then bilal afanye kaz gani? Mbna anaingilia kazi za mwezake
 
hakika kwa hili nampongeza sana jk, amejitahidi sana kuboresha barabra zetu.
Wenye roho za korosho wasokubalai kumsifia mtu hata anapopatia waendelee kuumia.
JK ni binadanamu kama mimi na wewe, anamazuri yake na mabaya.
Anapopata asifiwe, anapokosea akosolewe, huo ndo uungwana na ndio GT walivyo.
Kwa hili kapatia na apewe haki yake.

Hii ndo kazi yenu magamba!!!

Kupongezana...
 
Huyu rais wetu anapenda mno vitu vya weupe, nini imani miradi anayofungua ni mikubwa na ni hela za mkopo zenye riba kubwa...walipaji ni wananchi thru taxes. Angetuamsha tupambane na adui ujinga na maradhi angekuwa ametupa fadhila ya kutosha. Kwa hali hiyo miradi tungejenga sisi wenyewe sio wachina, wajerumani n.k.
 
tungekua na serikali makini kama mkakati wa punguza foleni ingekua inajenga barabara kuanzia njia nne kwenda na nne kurudi,ujenzi wanafanya sasa ni vichekesho kwa mtu mwenye akili!

Ni kichekesho kwa punguani; hizo njia nne unazoziongelea unataka nyumba ngapi zivunjwe? sai nyie ndio mnampiga vta Magufuli akitekeleza majukumu yake ?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hivi huu mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi haukuwahi kuzunduliwa mwaka 2010?
 
Hivi huu mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi haukuwahi kuzunduliwa mwaka 2010?

Mkuu watu wengi wamekuwa wakiulizza hili swali. Naambiwa kilichozinduliwa wakati huo ilikuwa ni Mradi wote ambao utakuwa na phase kadhaa. Kinachozinduliwa sasa ni ujenzi wa barabara za mradi huo phase one ambayo ni barabara ya kimara - Ubungo - Kivukoni na Magomeni - Morocco pia Msimbazi - Kariakoo. Naambiwa kutakuwa na phase nyingine baada ya hii phase.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Naona JK anapambana kutimiza ahadi zake safi sana hizi ndio zitakuwa fimbo kuelekea uchaguzi mkuu.

uchumi na maisha bora kwa kila mtanzania, haiwezi kuboreshwa kwa miundo mbinu ya ya mabarabara na daraja la kigamboni, bali ujumla wa vichocheo vyote vilivyowezeshwa na rasilimali za watanzania, vikasisismka na kusitawishwa, na hasa kwa kujitegemea na si blabla huku vichocheo hivyo vikidumaa na kukera jamii pana na kutoridhika na dhana ya uchumi kukua.JK Kutekeleza ahadi pekee yake ,huku maisha ya watanzania yakiwa hoi hukuna mantiki , bali ni kujenga msitakabali wa kuhahakikisha maisha hayo yanaboreshwa kwa nguvu zote hasa wakulima, wa Wafanyakazi wenye kipato kidogo na maisha duni, ili kulinda msilahi ya wanyonge.JK keshasahau wanyonge ;hata muasisi wa TANU na CCM ibrahimu kaduma kathibitisha kwenye kipindi cha jumanne cha "je tutafika "; kuwa ccm imewasahau wanyonge na kukumbatia matajiri.
 
Do acha wongo urafiki ,general tyre, kiwanda cha sukari moshi ,kiwanda cha zana za kilimo bicyle kiltex mwatex mutex ka uchache navitaja kwa uchungu nyerere aliacha watu walikuwa wanakula mzigo.

nikupe tu mahesabu kidogo ya general tyre ambayo imekufa 2005. staff 600 paye yake serikali imekosa.

Chakula aliye kuwa ana suply mchele maharaeg nyanya vitungu kwa siku milo 3 yaani plate 1200 per dy ,mayai 300.lita 300 za maziwa na aliekuwa analipwa kusafirisha hizo bidhaa amekosa na kodi serikali imekosa umeme na maji kama m200 per month ttcl yaani simu.

Internate provider aliyekuwa anauza yaani agent anesafirisha tyres aaaa napata na mshangao hilo wewe hulioni
.
 
Naona JK anapambana kutimiza ahadi zake safi sana hizi ndio zitakuwa fimbo kuelekea uchaguzi mkuu.

Mradi unaofadhiliwa kwa fedha zilizopatikana baada ya kutembeza bakuli !!
Yaani Tanzania na utajiri wake wote tunafadhiliwa hata kwa kujenga 'kabarabara' kama haka !!
Mimi naona afadhali tungemwambia 'mzee wa vijisenti' angeweza kujenga huo mradi kwa fedha zake mwenyewe ili aonyeshe uzalendo wake !!
 
Na zile million 183 za ruzuku alizokopa Babu hawara toka CDM inakuwaje au alishalipa?

Atalipa, si ni mkopo kama mikopo mingine tu.
Ila jiulize, vile 'vijisenti' na yale matrilioni yaliyoko Uswisi vipi ?? jamaa washayalipa, au watayalipa ??
Hapo vipi ??
 
Huyu anaitwa 'mzee wa uzinduzi wa miradi !!!


Mradi huu alishauzindua mwaka 2012 akiwa na waziri wake Kawambwa...
10/08/2010
8 Comments

Rais Jakaya Kikwete amezindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo kasi kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari katika Jiji na Dar Es Salaam. Mradi huo utahusisha barabara ya mabasi yanayotoka eneo la Ferry kuanzia Kivukoni hadi Kimara.

Raisi alisema kuwa Wizara ya Miundombinu ipo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi atakayejenga barabara hiyo yenye jumla kilomita 20.9 kwa awamu ya kwanza na kwamba ujenzi umepangwa kufanyika kwa kwa awamu sita. Mradi unatarajiwa kukamilika mwaka 2025.

"Ili kupunguza msongamano huo, maeneo ya Ubungo Mataa na TAZARA ndiyo yatakuwa ya kwanza kujengwa barabara za juu na kufuatiwa na Magomeni, Fire, KAMATA na Chang'ombe," alisema Rais Kikwete.

"Serikali inaangalia uwezekano wa kutumia treni kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri wa katikati ya mji kwa njia ya Ubungo, Buguruni, Mabibo, Tabata na baadaye Kimara hadi Tegeta."

241331.jpg
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam Bwana Cosmas Takule akionyesha mchoro wa ramani ya utekelezaji wa mradi huo jiji Dar es salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa, Waziri wa TAMISEMI Bi.Selina Kombani na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya dunia Bwana John McIntyre wakisikilza kwa makini wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu ya mradi huo zilizofanyika Ferry Kivukoni, jijini Dar es Salaam leo mchana.



Source: Raisi azindua ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo kasi - wavuti
 
Miaka 50 ya uhuru ni kuchelewa sana, na wa si vya kujisifia hata kidogo

Hakika. Kwa utajiri wa mali asili za Tanzania, tulitakiwa kuwa na maendeleo zaidi ya Afrika Kusini.
Lakini, jamaa humu JF wanasherehekea 'uzinduzi' wa kamradi kadogo kama haka !!
Angalieni maendeleo ya Afrika Kusini ambayo tunaizidi saaana kwa utajiti wa mali asili..
Uongozi uliooza wa serilaki ya CCM ndio kero hapa !!
Angalieni picha ya barabara za Afrika kusini...... Sio ninyi mnasherehekea ka-barabara kadogo huku mafisadi wakiwacheka, maana wao wangeweza kujenga barabara zaidi ya hizo kwa 'vijisenti' tu....!!
 

Attachments

  • south.jpg
    south.jpg
    27.2 KB · Views: 29
Mkuu hamna barabara hapa!!!!!!vipo vichochoro huwezi kabisa kulinganisha Rasilimali tulizonazo!!! barabara zipo Nairobi na Addis Ababa sitaki kutaja manchi makubwa kama huko uliko

Hakika,
Hebu angalieni South Africa kulivyo !! Tanzania inaizidi sana South Africa kwa utajiri ..
Leo hii jamaa zetu hapa wanasherehekea ka-barabara kadogo sana, huku wakificha ma-trilioni ya pesa Uswisi >>

Hii hapa ni Port Elizabeth, South Africa .. !! Lindi au Mtwara inatakiwa kuwa hivi !!!!
 

Attachments

  • barabara za juu.jpg
    barabara za juu.jpg
    106.4 KB · Views: 47
Hakika,
Hebu angalieni South Africa kulivyo !! Tanzania inaizidi sana South Africa kwa utajiri ..
Leo hii jamaa zetu hapa wanasherehekea ka-barabara kadogo sana, huku wakificha ma-trilioni ya pesa Uswisi >>

Hii hapa ni Port Elizabeth, South Africa .. !! Lindi au Mtwara inatakiwa kuwa hivi !!!!
Mkuu Mu-Israeli hebu waelezee hawa pro-ccm ni vichwa ngumu sana. wanasherekea vichochoro kwi! kwi! kwi! kwi! teh! teh! teh!
 
Ni kichekesho kwa punguani; hizo njia nne unazoziongelea unataka nyumba ngapi zivunjwe? sai nyie ndio mnampiga vta Magufuli akitekeleza majukumu yake ?

Chama
Gongo la mboto DSM

barabara za Kilwa, Nyerere, Morogoro, Bagamoyo,Mandela, Kawawa na Sam Nujumo zina maeneo ya kutosha ya kuwa na njia hata 6 kila upande,tatizo ni mipango ya watawala wako wanaoendekeza njaa! Kila siku utasikia barabara inakarabatiwa na kupanuliwa,kumbe inaongezwa njia moja,baada ya miezi michache foleni zinarudi pale pale! Akili za tope!
 
Back
Top Bottom