JK mgeni rasmi uzinduzi wa barabara

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumanne, Septemba 18, 2012 05:41 Na Oliver Oswald, Dar es Salaam

RAIS Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja, unaoendelea katika baadhi ya maeneo nchini.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango, alisema uzinduzi huo utahusisha miradi mitatu ambayo ni ya ujenzi wa madaraja, barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi pamoja na barabara za kawaida, ikiwamo Barabara ya Makofia-Msata.

Alisema kwa sasa Serikali ya awamu ya nne inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa yote.

Balozi Mrango alisema kuna barabara zenye urefu wa kilomita 11,154, ambazo zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Kwa mujibu wa Balozi Mrango, Rais Kikwete, ataanza na uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Makofia-Msata, iliyopo Bagamoyo, yenye urefu wa kilomita 64 na kwamba uzinduzi huo utafanyika katika Kijiji cha Kiwangwa kesho.

“Kesho (leo), Rais atazindua ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam ambao mkandarasi wa mradi huu ni Strabag International.

“Mradi huu unahusisha Barabara za Kimara kuelekea Kivukoni, Magomeni kuelekea Morocco na Fire hadi Kariakoo.

“Septemba kesho kutwa (kesho), atazindua ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambapo sherehe zitafanyika Kurasini,” alisema Balozi Mrango.

Alisema pia kwamba, daraja hilo la Kigamboni linajengwa na Mkandarasi wa China Railway Constrution Company Limited, kwa kushirikiana na China Major Bridge Engineering Company Limited.
 
Dr Slaa akiona hivyo roho inamuuma sana yeye anatamani kila siku JK akwame tu yeye apate singo ya kutokea.

anachokifanya leo jk ni kama mtu mzima kutambaa ...miradi yote ni kwa hisani ya watu wa? na ni madeni kwa kwenda mbele deni la taifa linakuwa faster than ever......nakushauri angalia leo citzen tv saa moja jioni wataonesha jinsi kenya walivyo wanajenga mtambo mkubwa wa umeme wa makaa ya mawe sisi stiglers godge nihistory tangu imeanza kutalk

 
Ritz kumbe hujui kwa nini hatuwataki tena ccm si ahadi ni wizi mlioufanya miaka yote huko nyuma mliiba we eti leo unakisifu jk anatekeleza ahadi, wakati mafisadi wanakula bata tu na wezi wa kuku wanaozea segerea, mshachelewa baba m4c is larger than life itself
 
anachokifanya leo jk ni kama mtu mzima kutambaa ...miradi yote ni kwa hisani ya watu wa? na ni madeni kwa kwenda mbele deni la taifa linakuwa faster than ever......nakushauri angalia leo citzen tv saa moja jioni wataonesha jinsi kenya walivyo wanajenga mtambo mkubwa wa umeme wa makaa ya mawe sisi stiglers godge nihistory tangu imeanza kutalk

Huko na kutapatapa mkuu kwa hiyo Chadema wakichukuwa nchi pesa watatoa mfukoni kwa Dr Slaa.
[h=2]Tuesday, August 10, 2010[/h] [h=3]*JK AZINDUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI DAR[/h]
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia John Mc Intyre (watatu kulia),Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa (kushoto) na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selina Kombani (kulia) wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi zilizofanyika Kivukoni jijini Dar es Salaam leo mchana.
 
Ritz kumbe hujui kwa nini hatuwataki tena ccm si ahadi ni wizi mlioufanya miaka yote huko nyuma mliiba we eti leo unakisifu jk anatekeleza ahadi, wakati mafisadi wanakula bata tu na wezi wa kuku wanaozea segerea, mshachelewa baba m4c is larger than life itself

6.jpg
ub.jpg
DSCN4153%255B4%255D.jpg


10.jpg
 
Mkuu Ritz vipi utakuwepo manake nami nataka nihudhurie nisikie Waziri Magufuli akitoa data!!
 
Last edited by a moderator:
Navyomjua Magufuli atakuwa kanuna kweli(anatamani kupiga mbizi kuvuka kigamboni na kurudi) baada ya kuingiliwa kazi za Ufunguzi na Mwajiri wake.
 
anachokifanya leo jk ni kama mtu mzima kutambaa ...miradi yote ni kwa hisani ya watu wa? Na ni madeni kwa kwenda mbele deni la taifa linakuwa faster than ever......nakushauri angalia leo citzen tv saa moja jioni wataonesha jinsi kenya walivyo wanajenga mtambo mkubwa wa umeme wa makaa ya mawe sisi stiglers godge nihistory tangu imeanza kutalk

kwa hiyo ulikuwa unashauri aachee kujenga hizo barabara na mafaraja kwa kuwa amechelewa!??? Watu wa chadema kila kitu lazima mpinge duh
 
Back
Top Bottom