Barabara ya Kibada mpaka Kimbiji kupigwa lami

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji yenye urefu wa KM 41 Wilayani Kigamboni, Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema hayo leo akiwa Kigamboni ambapo amesema hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi za Serikali za kuiwezesha Wilaya ya Kigamboni kuwa na barabara nyingi za lami na hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi wake.

"Mh.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amenituma nije nikague barabara hii ambayo ujenzi wake utaanza hivi karibuni, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Eng. John Mkumbo uendelee kuikarabati barabara hii ili ilipitike wakati wote wakati maandalizi ya kuijenga kwa lami yakiendelea”

Kufuatia ombi la Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo la kuiomba Serikali kujenga kipande cha KM 7, kutoka Kimbiji hadi Cheka ambacho ni mwendelezo wa barabara hiyo, Bashungwa amemuagiza pia Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam kufanya usanifu katika sehemu hiyo wakati yeye akifuatilia kibali cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuiwezesha barabara yote kujengwa kwa lami.

Waziri Bashungwa amehitimisha ziara yake ya siku tatu Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea Wilaya zote 5 za Mkoa huo ambazo ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni na kukagua athari za mvua za vuli na kutoa maelekezo kwa TANROADS, Wakandarasi na Wananchi hususan kutovamia maeneo ya hifadhi ya barabara na kuzilinda barabara ili zidumu kwa muda mrefu.
 
Weekend lazima nimtafute Dalali Msomi.
Kuna hawa wanaitwa Canan land au kingo. Wanauza maeneo mazuri tu square mita wanauza kwa buku 5 au 6500.

Lile eneo Lina maendeleo ya chapchap sana. Umeme umefika mapema zaidi ya ilivyokadiriwa. Kinachoviziwa Kule ni barabara tu ili Bei ya nauli ishuke tuanze kujenga
 
Back
Top Bottom