JK aitilia shaka maandamano na migomo.......ni kumn'goa yeye au?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Kikwete ashitukia maandamano, migomo

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 5th February 2011 @ 23:50

RAIS Jakaya Kikwete amesema amegundua kuwapo njama za makusudi za kudhoofisha Serikali yake ionekane haifanyi kitu.

Alisema hayo katika hotuba yake ya kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

“Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwaka 2010, nilidokeza taarifa ambazo vyombo vya usalama vinazo, kuhusu mipango ya makusudi ya uvunjifu wa amani kwa kutumia njia ya migomo na maandamano,” alisema Rais.

Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na maandamano na migomo katika taasisi mbalimbali hususan za elimu ya juu nchini. Alisema aliwatanabaisha wananchi kutambua njama hizo na kuepuka kushiriki maandamano au migomo ya aina hiyo.

“Wanaoandaa wana ajenda yao ya kisiasa iliyojificha nyuma ya jambo linalotangulizwa kama sababu. Wanataka kujitengenezea mazingira ya ushindi mwaka 2015 kwa vurugu,” alisema.

Rais alisema anakumbuka alihadharisha watu wajiepushe kugeuzwa mbuzi wa kafara kwa kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani fulani.

“Niliyoyasema yametokea Arusha na dalili zipo za mipango ya namna ile kuandaliwa kutokea sehemu nyingine nchini. Napenda kurudia kuwasihi Watanzania wenzangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hao.

“Wanawasakizia kwenye hatari ambayo mnaweza kuiepuka. Naomba muwakumbushe tena, kuwa wanayo fursa bungeni na kwenye majukwaa mbalimbali kutoa hoja zao, badala ya kuwagombanisha ninyi na vyombo vya Dola,” aliongeza.

Aliwataka wanasiasa wenzake kutumia fursa tele walizonazo badala ya njia ya uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha na mali za watu na kuharibu sifa ya Tanzania.

Hivi karibuni, viongozi na wafuasi wa Chadema, walifanya maandamano haramu mkoani Arusha na kukabiliana na polisi walipotaka kuvamia kituo cha Polisi cha Arusha, ili kuwatoa wenzao waliokuwa wamekamatwa.

Katika purukushani hiyo, wafuasi wao wawili na raia mmoja wa Kenya waliuawa na viongozi wa chama hicho hivi sasa wanakabiliwa na kesi mahakamani ya kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi.

Juzi, wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Ardhi, walijaribu kuandamana kwenda Ikulu kumwona Rais Kikwete kushinikiza Serikali iwaongeze fedha za kujikimu, lakini maandamano hayo yasiyo na kibali pia yalivunjwa na polisi.

Katika vurugu hizo wanafunzi wawili walijeruhiwa na mmoja kutoka mimba.
 
PHP:
RAIS Jakaya Kikwete amesema amegundua kuwapo njama za makusudi za kudhoofisha Serikali yake ionekane haifanyi kitu. 
 
Alisema hayo katika hotuba yake ya kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. 
 
"Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwaka 2010, nilidokeza taarifa ambazo vyombo vya usalama vinazo, kuhusu mipango ya makusudi ya uvunjifu wa amani kwa kutumia njia ya migomo na maandamano," alisema Rais. 
 
Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na maandamano na migomo katika taasisi mbalimbali hususan za elimu ya juu nchini. Alisema aliwatanabaisha wananchi kutambua njama hizo na kuepuka kushiriki maandamano au migomo ya aina hiyo. 
 
"Wanaoandaa wana ajenda yao ya kisiasa iliyojificha nyuma ya jambo linalotangulizwa kama sababu. Wanataka kujitengenezea mazingira ya ushindi mwaka 2015 kwa vurugu," alisema. 
 
Rais alisema anakumbuka alihadharisha watu wajiepushe kugeuzwa mbuzi wa kafara kwa kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani fulani.

Ni vyema JK akaelewa migomo na maandamano ni haki za kimsingi kabisa kwa raia kwenye nchi yoyote ile inayoendeshwqa kidemokrasia........................siyo njama kama yeye alivyodai..........................................
 
Taarifa kwamba maandamo ya Arusha yalikuwa HARAMU ni uchochezi wa makusudi.
Mwandishi ni lazima aombe msamaha chadema.
Mandamano yalipewa kibal.i Polisi Wilaya walikuwa na taarifa na hawakuwa na pingamizi, Lakini IGP Katili alitoa tamko katika TV kuyazuia jambo ambalo ni kinyume cha Sheria na taratibu za Kipolisi na zaidi Mwema aliingilia kazi ya Mkuu wa polisi wa wilaya.Haikuwa kazi yake MH Mwema kuzuia maandamano hayo hata kama madai ya ""Inteligensia"" yalikuwa ya kweli.

Kikwete ashitukia maandamano, migomo

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 5th February 2011 @ 23:50

RAIS Jakaya Kikwete amesema amegundua kuwapo njama za makusudi za kudhoofisha Serikali yake ionekane haifanyi kitu.

Alisema hayo katika hotuba yake ya kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

"Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwaka 2010, nilidokeza taarifa ambazo vyombo vya usalama vinazo, kuhusu mipango ya makusudi ya uvunjifu wa amani kwa kutumia njia ya migomo na maandamano," alisema Rais.

Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na maandamano na migomo katika taasisi mbalimbali hususan za elimu ya juu nchini. Alisema aliwatanabaisha wananchi kutambua njama hizo na kuepuka kushiriki maandamano au migomo ya aina hiyo.

"Wanaoandaa wana ajenda yao ya kisiasa iliyojificha nyuma ya jambo linalotangulizwa kama sababu. Wanataka kujitengenezea mazingira ya ushindi mwaka 2015 kwa vurugu," alisema.

Rais alisema anakumbuka alihadharisha watu wajiepushe kugeuzwa mbuzi wa kafara kwa kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani fulani.

"Niliyoyasema yametokea Arusha na dalili zipo za mipango ya namna ile kuandaliwa kutokea sehemu nyingine nchini. Napenda kurudia kuwasihi Watanzania wenzangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hao.

"Wanawasakizia kwenye hatari ambayo mnaweza kuiepuka. Naomba muwakumbushe tena, kuwa wanayo fursa bungeni na kwenye majukwaa mbalimbali kutoa hoja zao, badala ya kuwagombanisha ninyi na vyombo vya Dola," aliongeza.

Aliwataka wanasiasa wenzake kutumia fursa tele walizonazo badala ya njia ya uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha na mali za watu na kuharibu sifa ya Tanzania.

Hivi karibuni, viongozi na wafuasi wa Chadema, walifanya maandamano haramu mkoani Arusha na kukabiliana na polisi walipotaka kuvamia kituo cha Polisi cha Arusha, ili kuwatoa wenzao waliokuwa wamekamatwa.

Katika purukushani hiyo, wafuasi wao wawili na raia mmoja wa Kenya waliuawa na viongozi wa chama hicho hivi sasa wanakabiliwa na kesi mahakamani ya kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi.

Juzi, wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Ardhi, walijaribu kuandamana kwenda Ikulu kumwona Rais Kikwete kushinikiza Serikali iwaongeze fedha za kujikimu, lakini maandamano hayo yasiyo na kibali pia yalivunjwa na polisi.

Katika vurugu hizo wanafunzi wawili walijeruhiwa na mmoja kutoka mimba.
 
Huyu ndugu yetu mwehu nini!watu wanadai stahili zao yeye anasema wanatumiwa na wanasiasa!haya ni matusi makubwa watz,hivi wanapoandamana kupinga ongezeko la bei ya umeme,kudai nyongeza ya posho ya kujikimu vyuoni,kupinga malipo kwa dowans,kulalamikia ugumu wa maisha,kuporomoka kwa uchumi,matokeo mabaya ya kidato cha nne..watz hawana ufahamu wa madhira haya mpaka wanasiasa wawatumie?Ebu acha upuuzi mkuu,rekebisha hayo ili tusipate hoja ya kugoma na kuandamana,vinginevyo hautafika 2015!
 
Haya sasa, wale wanao sema bwana mkubwa anadanganywa watuambie. hapa anadanganywa au anaziba his critical thinking fuculties to favor his self course? Kama kila lalamiko la wanaolalama ni kisiasa, basi mku wetu hataki kusoma alama zilizo ukutani.
 
Nashiwishika kuamini kua huyu baba wa wenzetu sio RAIS
 
'CCM inahitaji upasuaji makini'

*Wasomi wadai bila hivyo watagawana mbao

Na Tumaini Makene

WAKATI Chama Cha Mapinduzi kikijiandaa kujivua gamba kama alivyoahidi mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imeelezwa kuwa
kinapaswa kuwa makini kwani 'kinahitaji upasuaji wa uangalifu' ili kurudisha imani ya Watanzania.

Uchunguzi wa Majira kwa siku kadhaa juu ya mstakabali wa chama hicho, umebainisha kuwa kwa hali kilipofikia chama hicho kinapaswa kufanya mabadiliko ya dhati, ili kiweze kuweka 'gamba jipya la kusimamia matakwa ya watu na jamii na kuuhisha miiko ya uongozi iliyopotea, vinginevyo mwakani au 2015 wanaweza 'kugawana mbao'.

Mmoja wa wabunge wa chama hicho akizungumza na Majira jana kuwa hata vikao vya CCM vinavyotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Dodoma vinaweza visikisaidie chama hicho iwapo watu 'wanaosema ukweli' ndani ya chama wataendelea kushughulikiwa na makundi fulani.

Mbunge huyo ambaye hakutaka kutajwa jina akizungumza na Majira jana katika semina ya wabunge juu ya usimamizi wa bajeti inayoendelea Dar es Salaam alisema kuwa vikao vya Dodoma havitaweza kuiponya CCM iwapo watu wanaosema ukweli, ndani ya chama hicho, kwa kukemea maovu na kushauri pale inapobidi 'wanashughulikiwa' kwa kupitia makundi ya umoja huo, hususan Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM).

Alisema kuwa vikao hivyo haviwezi kuisaidia CCM kwani imepoteza ushawishi kwa wananchi wa chini kwa kushindwa kusimamia na kuzungumzia kero zao, badala yake 'viongozi walafi na wabadhirifu' wamepewa nafasi na wale 'waadilifu wanaosimamia
uwajibikaji na uadilifu wanasakamwa au kuwekwa kando'.

"Nikwambie kitu chama hiki si kimoja tena. Hakipo. Kimeparanganyika mno na ushindi wake mwaka 2015 ni mfinyu sana, watu huko chini hawana imani nacho tena, hebu kaulize mikoani au wilayani, akina nani wanaofanya mikutano tena, ukiona mbunge
anafanya mikutano sasa si kwa sababu watu wanakitaka chama bali wanamkubali yeye, basi.

"Chama hakiwazungumzii watu tena, wala hakiwezi kupona kwa kufukuza watu pekee. Usishangae hata mimi kesho nikashughulikiwa na vijana kwa yale niliyoyasema hivi karibuni katika vyombo vya habari," alisema mbunge huyo.

Pia, Profesa wa masuala ya uchumi, Samuel Wangwe amelieleza Majira kuwa ili CCM iendelee kuwa salama hasa kuelekea uchaguzi wa ndani 2012 na ule mkuu wa mwaka 2015 haina budi kufanya marekebisho makubwa la sivyo itakuwa katika hali mbaya.

"Kwa hatua iliyofikia sasa CCM lazima ifanye mabadiliko makubwa, la sivyo hali itakuwa mbaya 2015, wanaweza kufanya mabadiliko...ikiji-organize inaweza, bado wana nafasi ya kujirekebisha, lakini kwa maumivu fulani. Haitaweza kufanya marekebisho bila kuumia, lazima ikubali kuumia, kama alivyoshauri mwenyekiti kuna haja ya kujivua gamba.

"Itachukua muda kwa CCM kufa kwa sababu bado iko vijijini, bado ina nguvu maeneo mengi ya nchi vijijini, lakini kama hali itaendelea kuwa hivi kuna hatari ya kupoteza ushawishi hata huko pia," alisema Profesa Wangwe.

Mchambuzi mwingine, Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Bw. Bashiru Ally alisema ili kujivua gamba kama afanyavyo nyoka, CCM inatakiwa kujifanyia upasuaji mkubwa, ili iendelee kuwasemea watu, wakulima na wafanyakazi ambao ndiyo wazalishaji wakuu wanaonyanyasika na mfumo mbovu.

Bw. Bashiru ambaye alisema kuwa bado anaamini kuwa maneno ya Hayati Babab wa Taifa kuwa 'bila CCM imara nchi itayumba', alisema kuwa chama hicho hakina budi kujifanyia 'upasuaji wa kitaalamu' ili kuondoa mfumo uliozalisha makundi ndani ya chama, yanayotumia matatizo ya watu kujihalalisha katika jamii.

"Sijui kama Mwenyekiti wa CCM alisema juu ya mageuzi makubwa ndani ya chama baada ya kufanya uchambuzi wa kina, gamba la CCM si sawa na gamba la nyoka ambalo linajivua naturally baada ya kufikia kipindi fulani, halina usumbufu katika kujivua na haliathiri maisha ya nyoka. Hili la CCM ni tofauti, hili limeganda haliwezi kutoka smoothly. CCM inahitaji zaidi ya hapo. Inatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kitaalamu.

"Maana upasuaji makini wa kitaalam lazima utagusa maslahi ya kakundi kalikoteka chama, kuweka gamba jingine litakalozingatia sera, matakwa ya watu na jamii, miiko ya uongozi na maadili ili kuwaondoa viongozi walanguzi na waporaji walioko katika
chama, kiongozi wa namna hiyo akijitokeza tena anashughulikiwa siku na saa hiyo hiyo. Hicho ni chama cha wafanyakazi na wakulima wazalishaji wakuu.

"Chama kinachopaswa kuwasemea wakulima wa pamba Shinyanga wanaolia kwa kuuziwa dawa ya kabeji badala ya pamba, hiki cha sasa kimegueka, hakilindi maslahi ya wakulima wala wafanyakazi tena...viongozi walanguzi wanatumia jasho la mkulima asiyekuwa na
mtetezi...upasuaji huu unapaswa kuhusisha maandalizi ya msingi, wasiende Dodoma kukatana mitama, bali wafanye upasuaji wa kitaalamu, kisha wanachama wazaliwe upya, wasioweza wajiondoe wenyewe," alisema Bw. Bashiru.

"CCM hakina budi kurejea katika misingi yake ya awali, badala ya kuendelea kukumbatia wafanyabiashara, wachuuzi, walanguzi, wababaishaji wanaojilimbikizia mali kupitia gamba la chama hicho, hao watafute chama chao katika mfumo kama huu wanaweza kabisa kuwa na chama chao cha walanguzi na wachuuzi, badala ya kuendelea kutumia jasho la wazalishaji na wavujasho."

3 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Tena waachane na hao wafanyabiashara wakubwa na kuwapa vyeo ndani ya chama hao ndiyo wanao fanikisha wizi nadhani wanafahamika pia wale viongozi ambao wameonekana ni mzigo kwa chama na kuwa na kauli za kupenda sifa pia waachane nao.Mawazo yao imekuwa kwamba wanamsadia Mwenyekti kumbe wanampotosha timua wote.
March 16, 2011 3:05 AM
blank.gif

Anonymous said... Watu wabaya wapo katika sehemu zote ndani ya jamii na si ndani ya CCM tu. Nasema hivyo nikimaanisha ya kwamba si wafanyabiashara wote wakubwa nchini mwetu waliomo CCM ni wabaya ila wapo kweli wanaojilimbikizia mali na umaarufu wa kuwatumia wananchi kwa manufaa yao. Hawa siwaungi mkono. Kama tutarudi nyuma ni jinsi Baba wa Taifa alivyokuwa mimi siwezi kusema ya kwamba alijilimbikizia mali kwa ajili yake na familia yake. Na kwa sasa sina habari za uhakika kama Kikwete amejilimbikizia mali; maana sijaibaini na kama nitapata ushahidi huo basi nitasema. Tuangalie pia wanachama wa kawaida wa CCM wenye mali nyingi. Je nao wamezipata wapi? Usafishaji wa chama utuguse sisi wote wana CCM ili tujipange sawa kwa manufaa ya nchi yetu. Jakaya hawezi peke yake bila nguvu ya umoja wa wana CCM wakiwemo vijana. Nawatakia UVCCM baraka na busara.
March 16, 2011 5:06 AM
blank.gif

Anonymous said... chama ccm ni kizuri isipokuwa kimepoteza malengo mila na desturi zake, hebu turejee katika misingi halisi ya chama hiki cha ccm, ilikuwa ni kulinda na kutetea maslahi ya wakulima na wafanyakazi, na ndiyo maana hata alama zilizopo katika bendela ya chama hicho ni jembe na nyundo, jembe likiwakilisha mkulima, na nyundo ni mfanya kazi. je viongozi wa sasa wa chama hicho wanajua hata maana ya hizo alama? au wanadhani ccm ni kuvaa nguo za njano na kijani? hiyo ni elimu ndogo ya awali ambayo nadhani viongozi wa chama hiki waliowengi hata hawajui. Nampongeza kiongozi mstaafu alitoa ushauri kuwa chama kina viongozi ambao hata hawakijui chama , hata historia yake. Mwalimu alikuwa anapeleka makada wake ktk chuo cha siasa ili wakapate elimu ya siasa. Leo siasa za ccm zimevamiwa na walanguzi, majambazi, watukanaji wenyeviburi wsiojua hata miiko ya ungozi. ushari kwa mwenyekiti wa ccm; kaka jitahindi kuondoa uswahiba na kujuana katika masuala ya msingi kama haya na ndipo utakinusulu chama kilichokuwa kinang'ara na kutia matumaini kwa watanzania walio wengi. usione haya wakati wa kujivua gamba mheshimiwa, kumbuka usipofanya hivyo watakuharibia mazuri mengi uliyopanga kuwafanyia watanzania.Pia washauri hao walanguzi waunde chama chao wasijichanganye kwenye chama hiki, wasitumie kivuli cha ccm kuleta uchafu katika nchi nzuri ya watanzani. Mungu ibariki Tanzania.
March 16, 2011 5:14 AM
 
Siasa hizi ni hatari

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
KWA masikitiko makubwa tunaandika tahariri hii tukiwa tumehuzunishwa na aina ya siasa zinazoendeshwa hivi sasa na viongozi wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tumejitahidi kwa muda mrefu na tutaendelea kukaa pembeni ya siasa za vyama hapa nchini lakini kamwe hatutaacha kushauri, kuonya na hata kukemea pale tunapoona waliopewa dhamana kubwa ya kuendesha siasa za nchi hii wanatoka nje ya mstari na kuanza kutupeleka kusiko.
Watanzania ni mashahidi wa aina ya siasa chafu ambazo zimekuwa zikiendeshwa na CCM kwa miaka mingi dhidi ya vyama vya upinzani.
Mashambulizi ya CCM kwa sasa yameelekezwa sana kwa CHADEMA bila shaka kwa sababu kwa viwango vyovyote vile chama hicho cha upinzani ndicho tishio kubwa kwa CCM.
Tulisikia miaka kadhaa huko nyuma baada ya CHADEMA kuzidi kukua kwa kasi, chama tawala kwa kutumia makada wake kikaanza kuwatangazia wananchi kwamba chama hicho ni cha kikabila.
Bahati nzuri CHADEMA walikuwa wepesi kujibu mashambulizi hayo na kufafanua kwa wananchi na hivyo wananchi wakaonekana dhahiri kutupilia mbali madai hayo ya chama tawala na kuendelea kuiunga mkono CHADEMA.
Baada ya kashfa hiyo, wakaja na hoja ya udini ambayo ilianzia kati kati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Ni baada ya mgombea wa CHADEMA Dk. Willibrod Peter Slaa kuonekana tishio kubwa kwa mgombea wa CCM ambaye hata wakati huo alikuwa ni rais wa nchi, Jakaya Mrisho Kikwete.
Kashfa ya CHADEMA kutumia udini kwenye kampeni zake ilipigiwa sana chapuo na Rais Kikwete kuliko mtu mwingine yeyote na ameendelea kuizungumza hata baada ya uchaguzi.
Na ikumbukwe kwamba awali wakati wa mwanzo wa kampeni hizo CCM walikuja na kashfa binafsi dhidi ya Dk. Slaa wakidai ameiba mke wa mtu, kashfa ambayo pia ilidharauliwa na wananchi.
Kashfa hiyo nayo ilipuuzwa na wananchi wanaoonekana kuiunga mkono CHADEMA hivi sasa, wanaongezeka kwa kasi na hali hiyo imejionyesha hata kwenye maandamano yaliyofanywa na chama hicho hivi karibuni katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Sasa makada wa chama hicho tawala wameibuka na kashfa nyingine. Safari hii wanadai kuna mataifa ya Ulaya yanaifadhili CHADEMA fedha ili kuandaa maandamano ya kuiangusha serikali iliyoko madarakani.
Sisi tunasema, hii sasa si siasa tena! Mataifa yanayosondwa kidole leo tena na baadhi ya mawaziri wa serikali iliyoko madarakani, ndiyo hayo hayo ambayo tunategemea yatupe misaada ya kujazia bajeti ya serikali kila mwaka kwa asilimia karibu 40.
Kashfa hizi zaweza kuharibu uhusiano wa kidipromasia kati yetu na mataifa hayo na kufanya wazuie misaada yao na hatujui serikali ya Kikwete itafanya nini bila hiyo misaada, kama tuna misaada na bado hali ya maisha ni ngumu namna hii!
Lakini pia mawaziri hawa wanaiaibisha serikali yetu! Wanakiri kwamba serikali haina mifumo ya kuhakiki usafirishaji wa pesa kutoka nchi za nje kuingia nchini mwetu.
Hii ni aibu kubwa mbele ya jumuia ya mataifa. Na ni bahati mbaya sana kwamba wote waliotoa tuhuma hizo hawakuonyesha ushahidi wowote wa tuhuma zao na hivyo tunaweza kujikuta katika uhusiano mbaya na mataifa rafiki kwa masilahi binafsi ya kisiasa ya watu wachache katika nchi hii.
Rai kwa CHADEMA, kama wana uhakika hawajawahi kupokea pesa za nchi za nje kwa ajili ya maandamano yao, basi wana kila sababu ya kuchukua hatua za kisheria kwa kuwapeleka mahakamani mawaziri waliohusika kusambaza tuhuma hizo za uongo.
 
Pinda awashangaa Sumaye, Lowassa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th March 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 1089; Jumla ya maoni: 5

Habari Zaidi: Pinda awashangaa Sumaye, Lowassa
Dawa ya Babu wa Loliondo ni salama
Wakala ‘akomba' mabilioni NHC
Serikali yaagiza walimu wapya walipwe
SMZ kuboresha maslahi ya wafanyakazi
Mrema ataka DCI kubeba maofisa wabadhirifu
JK akerwa na tatizo la watoto wa mitaani
Meneja mgodi wa Mollel wa Mererani mbaroni
Kamati ya Bunge yarejesha taarifa ya Fedha ya Tanesco
Wadau wazungumzia mtego Sheria ya Manunuzi
Wakala ‘akomba' mabilioni NHC
Afurahia kugeuzwa ‘shoga' mahabusu
Magereza watakiwa kuboresha huduma za tiba
Hakimu ajitoa kesi ya Mahalu
Wanahabari waaswa kuleta umoja
Barclays yasaidia ukarabati Gongo la Mboto
DC ahimiza mazao ya muda mfupi
Tunakazi ya kuandaa vijana waliobobea sayansi-Dk. Bilal
Arusha wapania kupanua eneo la kilimo
Wahakikishiwa utatuzi mgogoro wa ardhi

Habari zinazosomwa zaidi: Balaa lingine kwa Chenge
Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
‘Housigeli' anataka kuniharibia ndoa
Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
Vatican yamvua jimbo Askofu
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewashangaa viongozi waandamizi wastaafu serikalini na CCM kuacha kuzungumzia malalamiko yao katika vikao halali kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

"Vyama vina mifumo yao ya kuendesha shughuli zao … vina maeneo ya kusemea mambo yao na huko ndiko kusaidia chama na kuweka mikakati ya kukiendeleza," alisema Waziri Mkuu alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana.

Alikuwa akijibu swali kuhusu viongozi wa CCM wakiwamo wastaafu, kulumbana na umoja wa vijana wa chama hicho hadharani badala ya kutumia vikao halali vilivyopo.

Alisema kutoa madukuduku kwa kutumia magazeti kabla hata ya kukataliwa katika vikao halali vilivyopo, si dhamira nzuri.

"Kama malalamiko yako uliyatolea katika vikao halali na ukakataliwa kusikilizwa na hivyo ukaamua kutoka na kuyasema nje, hilo halina tatizo. "Na hasa viongozi wastaafu. Hawa wana fursa ya ziada, wana uhuru hata wa kumwona Rais na kusema naye, wakitumia uzoefu walionao kumsaidia hata yeye," alisema Pinda.

Aliasa kuwa si picha nzuri kuona kana kwamba viongozi hao wanakataliwa kusikilizwa katika vikao na hivyo kuamua kuyasema hadharani. "Msiwe waoga kusema ndani ya vikao halali kwani huko ndiko hasa pa kujenga na si kusemea kwingine … huko ndiko kukisaidia chama na kupanga mikakati zaidi ya kukiimarisha," alishauri Pinda.

Hivi karibuni, yamekuwapo malumbano baina ya viongozi wastaafu wa CCM na Serikali yake pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM), baada ya viongozi hao kuzungumzia hoja za Chadema na kuitaka CCM izijibu.

UVCCM ilitupa lawama kwa viongozi hao akiwamo Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Spika wa zamani wa Bunge, Samuel Sitta kuhusu kuzisema CCM na UVCCM hadharani badala ya kufuata vikao halali.

Wiki iliyopita, Sumaye akizungumza na vyombo vya habari kujibu tuhuma za UVCCM dhidi yake, alisema wanapotoka na kuwataka wajirekebishe, huku akiwatuhumu kwa kutoa kauli zinazoashiria kuwa wana mgombea wao wa urais wa mwaka 2015 wanamwandaa.

Kuhusu hali ya umeme, Waziri Mkuu alisema kuna unafuu kidogo kutokana na mvua zinazonyesha, ambazo zimeongeza kina cha maji katika mabwawa ya Kidatu na Kihansi, lakini Mtera hali bado si nzuri kutokana na Mto Ruaha kutokuwa na maji ya kutosha.

Akizungumzia Serikali kutotoa tamko lolote kuhusu Libya kushambuliwa na majeshi ya kigeni, Pinda alisema anatambua uhusiano na urafiki uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania, lakini akasema kwa sasa Serikali haiwezi kusema lolote ila itaheshimu uamuzi na msimamo wa pamoja wa Umoja wa Afrika (AU).

Kuhusu hali ya chakula, alisema bado kipo cha kutosha na kwamba kwenye maeneo yenye upungufu uliosababishwa na ukosefu wa mvua, Serikali imeshasambaza tani 13,000 na zimechukuliwa na halmashauri husika, na kuzitaka zenye matatizo ziseme ili zisaidiwe haraka.

Juu ya suala la matrekta madogo, Waziri Mkuu alisema si kwamba yana matatizo ila inategemea na aina na pia maeneo yanakopelekwa kufanya kazi.

"Matrekta haya ndio mbadala wa jembe la mkono, huwezi kumrusha mkulima mdogo kutoka jembe la mkono hadi trekta kubwa, ni aghali.

Lakini matrekta madogo yanastahili kilimo cha tambarare na si milimani … tuhakikishe tu
yamethibitishwa na vyombo husika," alisema.

Akizungumzia uhaba wa sukari, alisema ni jambo lililopangwa kwa makusudi na wafanyabiashara wa chini, kwa sababu sukari ipo ya kutosha na kuwataka maofisa biashara nchini kuingilia kati ili kudhibiti udanganyifu unaofanywa kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha.

Kuhusu foleni Dar es Salaam, Waziri Mkuu aliahidi kuyafanyia kazi mawazo aliyopewa na wahariri hao yakiwamo ya kuyapangia muda, malori ya mizigo yapitayo barabara ya Nelson Mandela, wa kuingia na kutoka bandarini asubuhi na jioni.

Jumla Maoni (5) Maoni Ni imani yangu kuwa yote yanayosemwa magazetini ni matokeo ya mrolongo wa matatizo ambayo serikali japo inayasikia na kuyajua lakini hakuna hatua zozote za dhati zinazochukuliwa. katika hali hiyo huwezi kutegemea haya kusubiri vikao anavyodai Waziri Mkuu Pinda. Je, wale ambao hawako CCM au UVCCM na hawana nafasi ya kumuona mkubwa wa nchi wafanyeje?. Majibu ya PM ni ya kisiasa zaidi kuliko hali halisi. Maoni Tunashukuru mheshimiwa Pinda kwa kuwakumbusha hao wenzetu.
Jamani fuateni taratibu za chama katika kutoa maoni. Maoni Kuhusu foleni Dar es salaam,Mheshimiwa Waziri Mkuu anatakiwa achukue na maoni haya hapa:

1.Waziri Mkuu waambie Sumatra watoe Elimu kwa madereva wa daladala juu ya jinsi ya kupaki mabasi yao kwenye vituo vya kupakia abiria.
2.Sumatra watoe elimu na kuwapanga abiria wajue namna ya kupanda daladala bila kupigania na wasipande basi ambalo halijapaki vizuri kwenye kituo.
3.Waziri Mkuu waambie Polisi watoe elimu kwa njia ya mabango na matangazo juu ya matumizi mazuri ya barabara.kila mwendesha gari ajue njia ya kupita na sio kujiendea tu.Tatizo la Dar es salaam ni kwamba watu wanajifunza udereva tu lakini hawajifunzi matumizi sahihi ya barabara(Highway driving)
4.watu wanaopanda daladala wapange mstari kituoni.Hata nchi zingine wanafanya hivyo.

USHAURI HUU UKIZINGATIWA FOLENI ITAKWISHA.bali mkijenga barabara nyingine mambo ni hayohayo! Wasalaam. Maoni Kuhusu foleni Dar es salaam,Mheshimiwa Waziri Mkuu anatakiwa achukue na maoni haya hapa:

USHAURI HUU UKIZINGATIWA FOLENI ITAKWISHA.bali mkijenga barabara nyingine mambo ni hayohayo! Wasalaam. Maoni Natumai Waziri mkuu ni kiongozi mwelewa sana! tena hatuna budi kumsifu juu ya hilo. Pia tuna heshimu sana mawazo yake.
Lakini nami pia nina haki ya kuchangia mawazo yangu kama jinsi yeye alivyotoa mawazo yake na ndiyo maana ikawekwa hii fursa. Asante kwa hili pia.
Kwanza, Hao viongozi waandamizi wastaafu wa CCM wana haki ya kusema/kukosoa/kukemea/kijitetea popote pale walipo, hata kama ikiwa ni barabarani ili mradi tu hawavunji taratibu/mwendo na desturi ya mtanzania. Lkn tunapotaka kuwafanya hao viongozi we2 wastaafu waongelee jambo/mambo/dukuduku lao sehemu maalum tu, basi tutambue kuwa tunawafanya washindwe kuwa na huru zaidi pia sisi ambao hatuna uwezo wa kufika huko ndani ya vyama husika hatutaweza jua ni kipi kinachoelea na badala yake tutakuja ambiwa lile lilochujwa na kuamuliwa hilo ndilo litakalosemwa kwa manufaa yao tu na si kwa watanzania wote.
Nasema/napendekeza kuwa kila mtu mwenye wazo lake, maadam haleti fitina/uchochezi/uvunjifu wa amani basi awe na huru huo wa kusema popote pale alipo ili wenginge nao waweze changia mawazo yake.

Asante.

Rahim
 
Pinda awashangaa Sumaye, Lowassa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th March 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 1089; Jumla ya maoni: 5

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewashangaa viongozi waandamizi wastaafu serikalini na CCM kuacha kuzungumzia malalamiko yao katika vikao halali kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Vyama vina mifumo yao ya kuendesha shughuli zao … vina maeneo ya kusemea mambo yao na huko ndiko kusaidia chama na kuweka mikakati ya kukiendeleza,” alisema Waziri Mkuu alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana.

Alikuwa akijibu swali kuhusu viongozi wa CCM wakiwamo wastaafu, kulumbana na umoja wa vijana wa chama hicho hadharani badala ya kutumia vikao halali vilivyopo.

Alisema kutoa madukuduku kwa kutumia magazeti kabla hata ya kukataliwa katika vikao halali vilivyopo, si dhamira nzuri.

“Kama malalamiko yako uliyatolea katika vikao halali na ukakataliwa kusikilizwa na hivyo ukaamua kutoka na kuyasema nje, hilo halina tatizo. “Na hasa viongozi wastaafu. Hawa wana fursa ya ziada, wana uhuru hata wa kumwona Rais na kusema naye, wakitumia uzoefu walionao kumsaidia hata yeye,” alisema Pinda.

Aliasa kuwa si picha nzuri kuona kana kwamba viongozi hao wanakataliwa kusikilizwa katika vikao na hivyo kuamua kuyasema hadharani. ”Msiwe waoga kusema ndani ya vikao halali kwani huko ndiko hasa pa kujenga na si kusemea kwingine … huko ndiko kukisaidia chama na kupanga mikakati zaidi ya kukiimarisha,” alishauri Pinda.

Hivi karibuni, yamekuwapo malumbano baina ya viongozi wastaafu wa CCM na Serikali yake pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM), baada ya viongozi hao kuzungumzia hoja za Chadema na kuitaka CCM izijibu.

UVCCM ilitupa lawama kwa viongozi hao akiwamo Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Spika wa zamani wa Bunge, Samuel Sitta kuhusu kuzisema CCM na UVCCM hadharani badala ya kufuata vikao halali.

Wiki iliyopita, Sumaye akizungumza na vyombo vya habari kujibu tuhuma za UVCCM dhidi yake, alisema wanapotoka na kuwataka wajirekebishe, huku akiwatuhumu kwa kutoa kauli zinazoashiria kuwa wana mgombea wao wa urais wa mwaka 2015 wanamwandaa.

Kuhusu hali ya umeme, Waziri Mkuu alisema kuna unafuu kidogo kutokana na mvua zinazonyesha, ambazo zimeongeza kina cha maji katika mabwawa ya Kidatu na Kihansi, lakini Mtera hali bado si nzuri kutokana na Mto Ruaha kutokuwa na maji ya kutosha.

Akizungumzia Serikali kutotoa tamko lolote kuhusu Libya kushambuliwa na majeshi ya kigeni, Pinda alisema anatambua uhusiano na urafiki uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania, lakini akasema kwa sasa Serikali haiwezi kusema lolote ila itaheshimu uamuzi na msimamo wa pamoja wa Umoja wa Afrika (AU).

Kuhusu hali ya chakula, alisema bado kipo cha kutosha na kwamba kwenye maeneo yenye upungufu uliosababishwa na ukosefu wa mvua, Serikali imeshasambaza tani 13,000 na zimechukuliwa na halmashauri husika, na kuzitaka zenye matatizo ziseme ili zisaidiwe haraka.

Juu ya suala la matrekta madogo, Waziri Mkuu alisema si kwamba yana matatizo ila inategemea na aina na pia maeneo yanakopelekwa kufanya kazi.

“Matrekta haya ndio mbadala wa jembe la mkono, huwezi kumrusha mkulima mdogo kutoka jembe la mkono hadi trekta kubwa, ni aghali.

Lakini matrekta madogo yanastahili kilimo cha tambarare na si milimani … tuhakikishe tu
yamethibitishwa na vyombo husika,” alisema.

Back
Top Bottom