Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,056
Mkitaka kufanya maandamano ya aina yoyote ile yawe ya shughuli za kisiasa, kidini, michezo au yawayo yoyote, sheria inawataka kulitaarifu jeshi la Polisi. Japo polisi hawana mamlaka ya kuzuia maandamano lakini wanaweza kutoa ushauri hata wa kuahirisha au kubadilisha njia kutokana na mazingira ya siku hiyo au shughuli nyinginezo za siku hiyo hiyo. Kwa hiyo, kimantiki, Polisi ndio wanaojua maandamano yanapita wapi, yataishia wapi, na pia wanajua matukio mengine kama vile misafara ya viongozi kwa siku hiyo hiyo.
Kama hakuna dharula kama vile maafa, inatarajiwa kuwa aliyetangulia kupewa au kukubaliwa njia atakayoitumia, ndiye atapewa haki ya kuitumia njia hiyo, na shughuli nyingine ambazo taarifa zake zilifuata baadaye, watalazimika kupewa njia nyingine, maana watakapotaka kuitumia njia ambayo tayari inatumika na aliyetangulia kutoa taarifa, Jeshi la polisi litamwambia huyo mtoa taarifa wa baadaye kuwa tayari barabara hiyo ina tukio jingine.
Sasa kama ilikuwa inajulikana kuwa maandamano ya CHADEMA yalikuwa yanatumia barabara tajwa, ilikuwaje tena Jeshi hilo hilo la polisi kupitisha msafara wa Biteko kwenye barabara hiyo hiyo? Ikumbukwe kuwa Biteko ndiye waziri wa Wizara ya nishati, wizara inayohusika moja kwa moja na ukosefu wa umeme nchini, na moja ya malalamiko yaliyosababisha maandamano hayo ni pamoja na ukosefu wa umeme. Je, kwa tendo lile la msafari wa waziri anayehusika na umeme kuvamia msafara wa waandamanaji wanaolalamikia ukosefu wa umeme haikuwa tendo la kuwatia hasira zaidi wananchi ambao tayari walikuwa wamekwishakuwa na hasira? Je, tendo lile halikuwa linahatarisha usalama wa Biteko na msafara wake, na kwa upande mwingine kuhatarisha usalama wa waandamanaji kama kungetokea vurugu, na polisi kutaka kumwokoa waziri?
RPC wa Mbeya, kwa tukio lile anastahili kuwajibishwa. Labda aseme kuwa walimwelekezo Biteko an alternative road, lakini Waziri , kwa kiburi chake, alilazimisha kuwa angepita katikati ya waandamanaji ili awatie hasira zaidi. Na hilo likidhihirika, basi Biteko anastahili kuadhibiwa.
Wananchi wanaheshimu misafara ya viongozi kiasi cha kuwa tayari kuacha shughuli zao zote kuwapisha viongozi wapite bila usumbufu kwa sababu kuna sheria inayoelekeza hivyo. Sasa inakuwaje viongozi hao hao hawataki kuheshimu msafara wa maandamano ya wananchi, tena ambayo yanalindwa kwa sheria na kanuni?
Mwisho wa yote, Polisi au Biteko au wote kwa pamoja, wanatakiwa kuwaomba msamaha wananchi wa Mbeya kwa kufanya tukio lililokuwa limekusudia kuvuruga maandamano ya wananchi.