Jirani yangu anafanya kazi gani?

Kuishi maisha mazuri kunahitaji sacrifice .

Unaweza kuta anafanya mishe za mitandaoni ambazo kupata au kupoteza ni njee njee kitu ambacho hata leo akikushirikisha utagoma either kwa hofu ya kupoteza ulichonacho au unaweza kumuita tapeli.

Kumbuka hakuna pesa rahisi
Umeongea jambo zito sana.Hakuna pesa rahisi na haitokuja kutokea pesa ikawa rahisi.Mkuu much respect.
 
Unajikuta mzungu sana, nimeuliza tu
Hawa ndo Watanzania sasa, kwa namna ulivyo, wewe ni Mswahili hasa, sahau kufanikiwa, endelea tu kuishi kwa sababu umeamka unapumua....!
 
Sio kwamba namchunguza, ila natamani namimi niishi life style kama yake, mana wengine tunachapika na maisha huenda kuna watu wana shortcut.

Ni miaka miwili tangu amalize nyumba yake na kuhamia,
1. Amejenga ndani ya miezi miwili au mitatu.

2. Tangu ahamie, muda wote yuko ndani, mara kadhaa hutoka au husafiri na ananiaga ila hakai hata wiki anarudi.

3. Anaagiza mahitaji kwa boda au mara nyingine anatoka, (hii sio ajabu sana).

4. Kuna mdada/ wadada wanakuja ila hawakai sana wanaondoka, jamaa yuko mwenyewe

5. Hana kufulia, au aje aombe kitu, mimi ndo niliwahi kwama nikamfata aniazime kiasi cha pesa.

6. Kusema ni jambazi anatoka usiku hapana, mana hata usiku yupo, na ni mpole sana hana shida na mtu.

Je, anaishije?
Digital Economy
 
Wakuu nitawaambia kitu huyu jamaa mnamshambulia bure tu...
Mfano mzuri ni mimi...
Sina hela nyingi hapana...ila kuna lifestyle naishi naona kabisa inawakera majirani na watu wote wanaonizunguka...ratiba
Saa tano asubuhi hadi saa sita natoka home( na mguuu)
Saa nane naenda kijiweni ni baa flani hv napiga wali nyama 2500
Nakunywa maji ya hill 1000 na soda water
Saa tisa maji tena
Saa kumi maji tu
Bado nipo kijiweni ila natoka sana kuongea na simu
Saa kumi na moja naanza bia...mpaka saa nne usiku
Na washkaji siku moja moja wanapata....
Kwahiyo in average bia tu huwa natumia si chini ya 25k per day...
Sasa huku bar hawaulizi sana ila kila siku ikifika saa 12 na nusu lazima niende tigopesa ambayo ukiwa hapo bar unaiona..halafu narudi bar....

Nyumbani majirani kinachowachanganya nina watoto watatu wanasoma ada ni 3m tu per kila mtoto per year
Na home nina wawili wadogo kama 4 and 3yrs
Wanakula,wanavaa wanasoma na mengineyo wakati wengine wanahustle sana ila hata ada ya mtoto naona kabisa inawazingua...
Ambacho hawajui nina vibiashara ambavyo viko active na navifatilia kwa karibu...na nauza kila siku sio hela nyingi ila sikosi gross profit ya 70-100 per day...

na kuna siku kila baada ya two weeks sionekani saana kumbe nakua nafanya stock na kuagiza mizigo..kiufupi mm ni mmoja ya watu wavivu na natumia sana ila..

Nachomshauri huyo jamaa hapa mjini..ukiweka racket yako vizuri...unakula hela hata kama ni 20k daily na hakuna atakaejua just shut your mouth tu!
 
We ni tajiri
 
We ni tajiri
Hapana mkuu sina gari sema kuna siri flani za biashara ukizijua hela itakusumbua kidogo sana mi napata ya kula tu...kwa mfano ukiweza kuwa na biashara ya peke yako au soko la peke yako au ukatatua changamoto ambazo watu wengi zinawasumbua hutalala njaa

Mfano: fungua kampuni ya kukata tu ukoka na majani nyumbani kwa watu kama hujawa tajiri....
Njoo inbox nikupe nyingine bure
 
Sio kwamba namchunguza, ila natamani namimi niishi life style kama yake, mana wengine tunachapika na maisha huenda kuna watu wana shortcut.

Ni miaka miwili tangu amalize nyumba yake na kuhamia,
1. Amejenga ndani ya miezi miwili au mitatu.

2. Tangu ahamie, muda wote yuko ndani, mara kadhaa hutoka au husafiri na ananiaga ila hakai hata wiki anarudi.

3. Anaagiza mahitaji kwa boda au mara nyingine anatoka, (hii sio ajabu sana).

4. Kuna mdada/ wadada wanakuja ila hawakai sana wanaondoka, jamaa yuko mwenyewe

5. Hana kufulia, au aje aombe kitu, mimi ndo niliwahi kwama nikamfata aniazime kiasi cha pesa.

6. Kusema ni jambazi anatoka usiku hapana, mana hata usiku yupo, na ni mpole sana hana shida na mtu.

Je, anaishije?
Atakuwa ni amata huyo
 
Mbona kama unanisema mimi? Majirani kumbe huwa mnaumiza vichwa hivyo, kwanini huwa hamtuulizi?
 
Ukiwa bado una mind ya kwamba mtu lazima atoke asubuhi na kurudi jioni ndo apige hela basi una safari ndefu sana kimafanikio maana maisha yashabadilika watu wanaishi kisasa
 
Back
Top Bottom