Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

Du, mambo ya kosoma kukariri na kuibilizia!, ...kaazi kweli kweli!.

Mhe. Godbless Lema, katika hili la Kafulila.... Bure Kabisa!.
Maisha ya mwanaadamu yame base kwenye ku copy n`paste kutoka kwenye natural principles kama huwezi/hutaki kwenda hivyo. Then you are not worth live
 
...anauma na kupuliza! nimeipenda "huwezi kumsaidia mkeo kubeba mimba hata kama unampenda sana" Ushauri mzuri, hongera kamanda lema.
 
Namuunga mkono Lema,yuko sahihi kumwambia Kafulira "ajitafakari na kuomba msamaha", Zitto aliyesema anamkaribisha CDM namshangaa,anataka kusema kufukuzwa kwake ni kaonewa??if kaonewa kwann yeye mwenyewe alilia machozi na kuomba asamehewe? Tuwe na jadi wakati flani ya kujiangalia wapi tumekosea c kukimbilia kuhama chama! Mkuu Pasco pia kwa hapa naona umeonyesha only personal hatred dhidi ya Lema
 
Du, mambo ya kosoma kukariri na kuibilizia!, ...kaazi kweli kweli!.

Mhe. Godbless Lema, katika hili la Kafulila.... Bure Kabisa!.

daima najua unaakili za wastani/pungufu lakini kwa kauli hii inaonesha Masaburi ni rafikio na Unaugua Upunguani.
 
Nadhani lazima tukili kwamba wapo binadamu wa aina mbalimbali na Mungu amefanya haya kwa makusudi ili utukufu wa Mungu ujulikane kama Pasco anapewa keki anaona ni kinyesi basi yafaa apewe kinyesi ndicho atakachoona ni keki. Ujumbe wa Mr Godbless Lema una content tena with empirical evidences, mimi ninadhani Bwana mdogo Kafulila anataka always kutaka kuanza kukimbia wakati kukaa hajaweza,nilidhani alipofukuzwa Chadema he learned something,mbona kuku anayetaga ukihamisha mayai yake hataendelea kutaga hapo anakuwa amejifunza kwamba hapo si salama tena na wapi aende ambapo ni salama zaidi.Ukiacha wizi mpaka watu waje waamini kwamba ni kweli umeacha hivyo wakuamini oh parefu !!By Fidelis Mawona "KIFULUFUMBI"
 
Du, mambo ya kosoma kukariri na kuibilizia!, ...kaazi kweli kweli!.

Mhe. Godbless Lema, katika hili la Kafulila.... Bure Kabisa!.

Tunataka Mtu awe na sifa Gani tuseme ana nidhamu mbovu?
Hapa tuache Majungu ,Kafulila hana nidhamu na ana tamaa ya kupaa kiuongozi. Mfano mzuri ni kwenye ndoa, kama kila baada ya Muda mfupi unavunja ndoa this means una udhaifu fulani. Tukubali au tusikubali ukweli uko pale pale Kafulila hana Nidhamu na ana Tamaa na uroho wa sifa na Madaraka , ndiyo maana wazee wanamshikisha adabu! Huu ni mwiba tena mwiba kama wenye pini nyingi kama mkia wa Octopus- Kokote atakakohamia kuweni Makini!

Lazima tuache tabia za Kimonduli za Lowasa kujiudhuru kwa Ufisadi halafu wanamsukumia gari lake na kumbeba juujuu. Huo ndo ninaouita ufukara wa fikra!
 
Soma kisha tafakari........*

*Nimesoma taarifa mbali mbali juu ya kufukuzwa uanachama kwa Mbunge**David**Kafulila na nilipata fursa**ya kutoa maoni yangu pale vyombo vya habari vilipotaka hivyo kutoka kwangu, nimefuatilia kwa makini sana mijadala mbali mbali haswa katika mtandao wa Jamii Forum na kuona mawazo ya**Watanzania mbali mbali juu ya jambo hili .Na ninafikiri ninao wajibu**kama kijana tena Mbunge kutoa maoni yangu na mtazamo wangu kwa kina juu ya jambo hili ambalo limemkuta Mbunge mwenzetu na rafiki yetu kijana Bwana David Kafulila.  Kwanza kabisa Bwana David Kafulila pole sana lakini kikubwa zaidi jipe moyo kwani changamoto katika siasa mara nyingi ni matukio yasio ya kawaida ambayo yanaweza kushusha heshima ya mtu au kupandisha heshima ya mtu, lakini tambua kuwa matatizo sio msingi mkuu wa kuharibu ndoto ya mtu makini aliyekusudia kutimiza jambo ambalo wajibu wake ni upendo , utu na ukweli katika jamii ni imani yangu kuwa**changamoto hii inaweza kukufanya uwe kijana mwenye**hekima zaidi**kwani katika kila changamoto kubwa Duniani hapo ndipo ukombozi ulipotokea Duniani.

*Ninatambua wakati unaopitia kwa sasa wewe na familia yako na wapiga kura wako , lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako , chama chako cha NCCR-Mageuzi**kimechukua hatua muhimu katika maisha yake ya siasa na kwamba** Nidhamu katika Chama itakuwa ni msingi mkuu katika kutafuta ukombozi wa kweli katika Taifa,**Binafsi**sifurahi wewe kufukuzwa katika Chama lakini nimefarijika na jinsi Chama**kinachukuwa**taratibu kama NCCR kinavyoweza kuchukua maamuzi magumu ya kulinda nidhamu na heshima ndani ya Taasisi ya Chama cha Siasa, Watu wengi hata mimi ningependa usamehewe , lakini David katika maisha ya siasa na Nyanja nyingine , uvumilivu na nidhamu katika kufanikisha maono au ndoto ni vitu ambayo ni msingi mkuu wa mafanikio**na hauwezi kuviepuka**ndio maana , Mtu mmoja mwenye hekima aliwahi kupata kunena kuwa  huwezi kupata kifaranga cha kuku kwa kuvunja yai bali kwa kusubiri yai liatamiwe kwa siku kadhaa na**baadae vifaranga watatotolewa ,
Lakini vile vile Mtu huyu mwenye hekima akasema tena** haijalishi**unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia  kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda**sana , hivyo malengo makubwa katika siasa ni jambo muhimu kwa kijana makini kama wewe kufikiria lakini uvumilivu na kusubiri ni*muhimu katika kufikia malengo makuu , Mimi binafsi ninatofautiana na watu wengi kwamba kupoteza jimbo ni jambo gumu na baya , hapana kupoteza jimbo kwa sababu ya kulinda nidhamu ni jambo jema linalopaswa kufanyiwa hata sherehe , hivi kweli tunaweza kupima nidhamu**na ni kitu gani katika maisha ya mwanadamu**? na vile vile tufikirie kama leo Mbunge au Diwani akifukuzwa kwa utovu wa nidhamu na sisi tukafikiri ni makosa , je ni halali sasa vyama vya upinzani kutafuta kuunda dola kama vitashindwa kusimamia tu**nidhamu ndani ya vyama vyao**,je*vitaweza kweli kusimamia nidhamu ya dola pindi vitakapochukua madaraka ?
NCCR Mageuzi wamefanya maamuzi ya msingi na ya uhakika kulinda nidhamu ndani ya chama ambaye yeyoye atakayethubutu kulaani basi ajiulize swali hili ? Kama nafasi ya Ubunge inathamani kubwa kuliko nidhamu ndani ya chama na jamii , je mtakuwa na ujasiri kweli wa kupinga dhambi**dhidi ya utu wa mwanadamu ambapo hivi karibuni mlipewa masharti ya ndoa ya jinsia moja kama mnataka misaada ?**sasa mkisema nidhamu ipuuzwe dhidi ya nafasi moja ya Ubunge , mtawezaje sasa kuvumilia**njaa ,mateso na dhiki dhidi ya kutetea utu wenu ? nina wasi wasi kuwa**siku moja pengine mtakubali yale mashariti mliyopewa**na**waziri Mkuu wa Uingereza ili muweze**kula lakini**kwa kudhalilisha utu wenu , kwani nafasi ya nidhamu katika maisha ya binadamu haupaswi kupigiwa kura .
Hivyo tukifahamu msingi mkuu wa mafanikio**kuwa ni**pamoja na**nidhamu ya kweli , nafikiri maoni ya wachangiaji**yatajikita katika kuutukuza ukweli na wala sio nafasi au cheo cha mtu,**Na ni hatari**wasomi wakifikiri kwamba lengo la vyama vya upinzani ni kushinda viti vya ubunge , madiwani bila kuzingatia maadili na nidhamu basi ni ukweli kuwa hatutakuwa na sababu ya msingi ya kuwaondoa madarakani chama tawala , kwani ugomvi wetu**vyama vya upinzani na chama tawala hausababishwi na tofauti ya rangi za bendera**bali ni msingi katika maadili, nidhamu na uwajibikaji usiozingatia haki na kweli ndio maana kwa sababu hiyo ufisadi,wizi na ubabaishaji umekuwa ukiongezeka kila wakati na kuletea Taifa madhara makubwa.
*Aliyekosa akiwa muungwana anaomba radhi na ndio ushauri wangu kwa David , lakini jambo hili limeshitua lakini pia limefundisha**na jambo la kushangaza hapa,**ni kwanini watu wameshituka sana Mbunge kufutiwa uanachama na sio kwanini Mbunge amekuwa mtovu wa nidhamu**, hata hivyo sifahamu mgogoro huu kwa kina sana , lakini najua**sihitaji ruhusa kuingia chumbani kwangu , mgogoro huu na malumbano yalikuwa wazi tena wazi sana ,
Sasa nimalizie kwa kusema**David bado unayo nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuwa kiongozi mzuri , wako waliopata matukio magumu ya kisiasa kuliko wewe lakini waliweza kurudi kwenye nafasi zao kwa utumishi**kama,**Martin Luther King Jr.**alivyopata*kunena****The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort, but where he stands at times of challenge and controversy.
Naibu Katibu mkuu wetu Mh Zitto nimesoma habari mbali mbali kuwa amekukaribisha Chadema ,**lakini mimi kwa sasa**nakukaribisha**Arusha kama utapenda kupumzika huku ukitafakari ili upate kujua kuwa unapaswa kuhama Chama au unapaswa kuomba radhi na kujirekebisha ? Mfano ,ukiuguua ugonjwa wa zinaa pamoja na kutubu dhambi kwa mwenyezi Mungu lakini**pia itakupasa kwenda Hosipatalini kutafuta dawa, sioni kama ni muhimu sana kuhama Chama isipokuwa kuomba radhi hata kama wewe sio Mbunge tena
*Jipe moyo David Kafulila na Hongera NCCR-MAGEUZI. . Sasa ningekushauri utafute kitabu kinachoitwa** THE 21 MOST POWERFUL MINUTES IN A LEADERS DAY  Kilichoandikwa na na mwandishi maarufu  John C. Maxwell.
*
If you are a leader , its not enough to know what to do . You have to know when to act.  John C. Maxwell.
Godbless Lema . (Mb)
Asante Lema. Umezungumza mambo yanayoua taasisi yoyote ikuwemo serikali. Sula la nidhamu lisipoangaliwa tutaangalia personalities na individualistic ideas. Nchi yetu iko hapa kwa sababu ya kukosekana kwa nidhamu. Hakuna wa kumwajibisha mwingine. Sifurahii Kafulila kufukuzwa, lakini sifurahii utovu wa nidhamualiouonyesha kwa chama na viongozi wake kwa misingi ya freedom of expression. Tutakubaliana kuwa Mbatia ana tuhuma za kununuliwa na ccm. Sina ushahidi juu ya hilo, lakini haimfanyi mwana nccr yeyote kukosa nidhamu kwake kama kiongozi. Nimeshatamka tena kuwa nadhani Kigoma kuna tatizo la either cheap popularity au kutaka sana madaraka. Zitto amelionyesha hilo, Kafulila naye mkondo huohuo. Lazima tujiulize, can such people be true leaders? Kafulila na Zitto na wengine wanaodhani wanaweza kupanda juu kwa kutumia ngazi za barafu wakati jua linawaka wafikiri tena. Kafulila is just a young man, anaweza kurebounce na kurudi victorious ila aangalie ni wapi ameanguka akarekebishe ndipo arudi.namkaribisha tulime kuku huku akitafakari
 
lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako
Mtu gani anaandika kitu kama "kwa mtu makini kama mimi"? Jamaa anajifagilia mwenyewe, ndio hawa makada wa CHADEMA ambao nimekuwa nikisisitiza kwamba chama kiwekeze zaidi katika kuwapeleke masomoni waongeze elimu.
 
kweli lema ame prove beyond reasonable doubt ni philosopher wa hali ya juu!! I appreciate the way he could narate the whole issue clearly.Kilichofikisha taifa hapa lilipo ni ukosefu wa nidhamu na kulindana na kulinda vyeo!!waziri anafanya ufisadi wizi chama kinaogopa kumfukuza kwa kuogopa nafasi yake na ubunge wake
Code:
[B]!!eti tukifukuza mafisadi chama kitapasuka?? shame!![/B]ona kwa kulindana hata wale wabunge walioshindwa kutumikia wananchi wanahongwa ukuu wa mikoa na ubalozi!! tukiwa makini na ku observe discipline yeyote anayeshindwa kutekeleza majukumu yake hana nidhamu anapaswa kuchukuliwa hatua, nakubalina na Lema kuwa lazima tushangae na kujiuliza kwa nini rais, mbunge waziri, katibu mkuu, mwenyekiti wa chama n.k hana nidhamu na sio kushangaa kwa nini hatua za kinidhamu zinazolenga kumrekebisha zimechukuliwa dhidi yake!!Jasiri gani unapiga magoti na kulia kama mtoto?? you have to remain firm on your stands!![B] viva Lema' viva Arusha 'viva CDM!!!!![/B]
 
Du, mambo ya kosoma kukariri na kuibilizia!, ...kaazi kweli kweli!.

Mhe. Godbless Lema, katika hili la Kafulila.... Bure Kabisa!.

I can smell kawivu kwa mbaali!!!
Mimi nimependa uchambuzi wake kuliko zako nyingi sana!
 
msiangaike na Pascal sio mzima kiakili kabisa kwanza uwa anavaa skin jinz mtaani na uku mtoto wa kiume,msamehee bure.....lema be blcd my bro!!
 
Lema ndio kaandika ule upupu? Hivi kiwango cha elimu ya Lema ni kipi kabla sijachangia nataka kujua...sijuhi kwa nini umeweka hizi dot***
 
Wanasiasa wetu jamani yaani hata sielewi kabisa wamejifunza wapi siasa hizi.. Sasa huyu Lema maswala ya NCCR yanamhusu nini hadi kuingilia kati na kuchagua upande wakati hajui undani wa haya maswala na Pilipili asiyokula inamwasha nini?.. Ni kihelele kipi kilichomkumba Lema au ana beef na Kafulila?..
 
Du, mambo ya kosoma kukariri na kuibilizia!, ...kaazi kweli kweli!.

Mhe. Godbless Lema, katika hili la Kafulila.... Bure Kabisa!.

Pasco wa jf au mtu kakwibia? I do respect your contribution ila hapa umepotoka as per your caliber
 
Lema ndio kaandika ule upupu? Hivi kiwango cha elimu ya Lema ni kipi kabla sijachangia nataka kujua...sijuhi kwa nini umeweka hizi dot***

Najua Lema bado ni mwiba kwa magamba, na wengi mnajitahidi sana kutaka kujua elimu yake. Hao wenye DR4 wanawasaidia nini sasa hivi???

Lema hongera kwa ushauri wa bure kwa Kafulila, nazipenda siasa za Lema ni aina ya siasa inayotakiwa Tanzania, magamba mnatudanganya na amani kumbe mnalinda matumbo yenu, hizo mirija mlizoegesha kwenye rasilimali za nchi yetu zitawaponyoka tu hasa ninyi jamii ya watz kama ritz

 
Back
Top Bottom