Elections 2010 Jimbo la Karagwe kwenda CHADEMA

Acha ushabiki huu usio na data. Kwani Kahama ndie aliyempa Ubunge Blandes au wana Karagwe wenyewe ndo waliamua awe Mbunge? au upo kambi ya huyo Kijana uliyemsifia hapo juu Mkuu??.

Mambo mengine ni vizuri mkayaangalia kwa mapana yake na kuacha "bias". Hivi ni vipi Blandes anatumia fedha za Sir George ili kumpitisha Mwanae Joseph Kahama mwaka 2015??? Otherwise ni kutuambia kuwa huko Karagwe hakuna wapiga kura badala yake jimbo ni mali ya Kahama's family ambapo Blandes nae alipewa na Kahama kwa masharti ya kulirejesha mwaka 2015!!! (a joke!!).

...Do you mean kwamba Sir George Kahama nae anahusika kwenye tuhuma za rushwa ulizodai awali zinamhusu Blandes kwa maana ya kuwa anamsaidia Blandes kifedha???
======
Umesema yote, sina cha kuongeza Ngoshwe.
 
======
Umesema yote, sina cha kuongeza Ngoshwe.

MKuu, kesi ya rushwa dhidi ya Blandes ni ile iliyoripotiwa mwaka 2007 na Tanzania Daima au ipo nyingine katika uchaguzi huu ? na inakuwaje maelezo ya thread # 1 hapo juu inaonkena kama kuna hakika kuwa Mhe. huyu atahukumiwa kwenda jela kana kwamba tayari ana hatia ya kutoa rushwa??.



Mbunge Blandes apandishwa kizimbani kwa rushwa

blank.gif
blank.gif
11-blandes.jpg
blank.gif
Mheshimiwa Gosbert Blandes​
h.sep4.gif

na Mwandishi Wetu, Karagwe


MBUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Karagwe, Gosbert Blandes, na Katibu wake, Twaha Kifurebe, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Karagwe wakituhumiwa kutoa rushwa ya sh 52,000 kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wa Wilaya ya Karagwe.
Mbali na fedha hizo, aliwaahidi wajumbe kuwapatia sh 900,000 iwapo wangemchagua katibu huyo wa mbunge kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa kuwakilisha wilaya hiyo.
Mbunge huyo na katibu wake walifikishwa mahakamani hapo Jumatano iliyopita wakiwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa kadhaa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wa Wilaya ya Karagwe.
Akiwasomea shitaka lao mbele ya hakimu Velinace Kawiche, Mwendesha Mashtakla wa Takukuru, Eunice Masalu, aliiambia mahakama hiyo iliyokuwa imefurika wafuasi wa mbunge huyo kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo Agosti 27, mwaka huu.
Katika maelezo yake, Masalu aliiambia mahakama kuwa siku hiyo walikutwa washitakiwa hao wakiwa na 'mabulungutu' katika eneo la Nyakasana, Kata ya Bugarama.
Alisema kuwa waliwakamata wakitoa hongo ya sh 52,000 kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kama kishawishi cha kutaka katibu wa mbunge huyo achaguliwe.
Mwendesha Mashitaka huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa pia katika eneo hilo watuhumiwa waliwaahaidi wajumbe hao kuwa iwapo katibu huyo wa mbunge angechaguliwa, basi wangewapatia wajumbe hao fedha nyingine kiasi cha sh 900,000.
Hata hivyo, mbunge huyo na katibu wake walikana mashitaka hayo. Wameachiwa kwa dhamana ya sh 500,000 na mdhamini mmoja.
Hata hivyo, nusura mbunge huyo apelekwe rumande baada ya mdhamini wake, Thomas Mtabaza, aliyejitambulisha kuwa ni mfanyabiashara wa Karagwe, kushindwa kujua jina la balozi wake na kukosa kitambulisho.
Hakimu alikemea hali hiyo na kumtaka mdhamini huyo kuwasilisha kitambulisho chake baadaye. Hata hivyo, baada ya kuachiwa kwa dhamana, mbunge na katibu wake walikamatwa tena na kurudishwa ndani ya mahakama kwa madai kuwa hawakusaini baadhi ya nyaraka za mahakama kulingana na taratibu za kesi hiyo. Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 6, mwaka huu.


Mbunge Blandes apandishwa kizimbani kwa rushwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom