Jibuni mapigo ya wapinzani -Pinda

Raia Mwema

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
535
79
VIONGOZI na wanachama wa CCM wametakiwa kujibu mapigo dhidi ya kauli za wapinzani, zinazobeza mafanikio ya Chama na serikali katika kuwahudumia wananchi. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alitoa msimamo huo jana, alipozungumza kwenye hafla ya kuwapongeza wabunge wapya wa CCM, Dk. Dalaly Kafumu (Igunga) na Mohamed Said Mohamed (Baraza la Wawakilishi) na madiwani 17, walioshinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni. Pinda alisema kuachwa kimya bila kujibiwa kwa baadhi ya kauli zinazotolewa na viongozi wa upinzani kunawafanya wananchi kuamini yanayozungumzwa na kwamba, hakuna sababu ya kukaa kimya, huku baadhi ya viongozi hao wakiendelea kusambaza maneno ya kubeza na ya uongo dhidi ya CCM.
“Ninyi mmekuwa kimya mno, kila mtu akibeza mnakaa kimya, hapana mkipata mwanya mjibu ili wananchi wajue ukweli,” alisema Pinda na kuongeza, uongo ukirudiwa mara kwa mara, huku CCM ikikaa kimya wananchi wataamini uongo huo ni ukweli. Kwa upande wa serikali, alisema itaendelea kujibu tuhuma ambazo zitaelekezwa kwake kutoka kwa viongozi hao kwa kadri hali ilivyo.
Aliwataka wana -CCM kujitahidi kadri ya uwezo wao kutetea amani na utulivu uliopo nchini, ili usije ukatoweka na kwamba, wasiruhusu viashiria vyovyote vya uvunjivu wa amani vikapata nafasi, kwani amani ikitoweka wananchi watailaumu CCM. “Chonde chonde wana -CCM, nawaomba tutetee na kung’ang'ania kwa nguvu zote hali ya amani na utulivu iliyopo, kwani iwapo amani na utulivu vitaondoka Watanzania watakuja kutulaumu,” alisema.
Kwa mujibu wa Pinda, kuna baadhi ya wanasiasa wanataka kufika wanakotaka kwa kutumia vurugu, jambo ambalo linahatarisha amani.
UPOTOSHAJI UCHAGUZI IGUNGA
Awali, akimkaribisha waziri mkuu, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati, alieleza kusikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari vinavyopotosha umma kuhusu gharama zilizotumiwa na CCM katika uchaguzi mdogo wa Igunga.
Chiligati alisema si kweli kwamba CCM ilitumia zaidi ya sh. bilioni tatu, kwani fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya kampeni zilikuwa chini ya sh. milioni 400.
Alisema habari kuwa CCM inakufa kutokana na mgawanyiko uliopo ndani ya Chama si za kweli, kwani matatizo ya mtu mmoja si ya Chama.
Chiligati alisema yeyote atakayekuwa na matatizo katika Chama atashughulikiwa na kama atatoka, CCM itaendelea kuwepo na
kamwe haitakufa.
“Hata kama Chiligati ametoka CCM, bado itaendelea kuwepo na ipo imara, kamwe hakuna mtu atakayeweza kukiharibu Chama,” alisema.
MWIGULU ALIA NA WATENDAJI
Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, amewataka watendaji wakuu wa serikali kufuatilia hujuma zinazofanywa na baadhi ya watendaji na watumishi wa umma dhidi ya CCM.
Alisema baadhi ya hujuma hizo ni za makusudi, kwani serikali ya CCM imepanga majukumu yake kutokana na Ilani ya uchaguzi. Alisema hujuma hizo zinawafanya wanachama na wananchi kwa jumla kutokuwa na imani na CCM.
Nchemba alisema hujuma hizo zinafanywa katika miradi, ambayo mingine haitekelezwi kama ilivyopangwa, licha ya fedha kutolewa. Alisema ufuatiliaji ufanywe kwa makini ili asiwepo wa kuonewa.
“Tumepata malalamiko mengi katika sehemu mbalimbali kuhusu huduma, lakini ukifuatilia huoni tatizo bali ni mtumishi mmoja ameamua kwa ridhaa yake kuwanyanyasa wananchi, hili hatulikubali,” alisema.
Alisema kamati za siasa za ngazi zote ni vyema zikafuatilia utekelezaji wa miradi ya serikali, kwani wao ndio wenye Ilani ya uchaguzi.
Katika hatua nyingine, Nchemba alisema CCM ina mpango wa kumpeleka nchini India, kijana Mussa Tesha, aliyemwagiwa tindikali wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga.
Alisema hatua hiyo inatokana na Tesha kuendelea kupata maumivu usoni na jicho moja kutoona.
“Pia tunaangalia uwezekano wa kumuanzishia biashara ili aweze kujikimu, kwani ni yatima na ndiye mkubwa katika familia yao,” alisema.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Pinda alisema atalifikisha wazo hilo kwa Kamati ya Wabunge wa CCM na kwamba, Tesha hana sababu ya kujiona mnyonge, kwani Chama kipo kwa ajili ya kumsaidia.
 
Huyo Pinda naye ni mnafiki.Hana la maana kutueleza amegeuza mpiga tarumbeta kwa ajili ya kutetea mafisadi.Huyu Chiligati mhuni na mwongo hawezi kusema mtu mmoja akitoka chama hakitakufa.Mbona Rostam amaewatikisa, hadi wamemwita kuja kusaidia kampeni.na kwanini CCM hawakuzungumzia yale aliyoyatoa Rostam kwenye hotuba yake ya kujivua gamba?Chiligat alipaswa kusema kuwa ufisadi umemtoa Rostam CCM na hivyo hata kafumu akifisidi naye wamtoe.Lakini cha ajabu hili halikuzungumzwa kwenye kampeni zao.
 
Mboana amerudia maneno yaliyosemwa na ****** kitambo. Huyo naye anataka tu tumuumbue kwa tabia yake ya kunaniii watumishi wa jinsia ile mle mle ofisini mwake, loh!
 
VIONGOZI na wanachama wa CCM wametakiwa kujibu mapigo dhidi ya kauli za wapinzani, zinazobeza mafanikio ya Chama na serikali katika kuwahudumia wananchi. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alitoa msimamo huo jana, alipozungumza kwenye hafla ya kuwapongeza wabunge wapya wa CCM, Dk. Dalaly Kafumu (Igunga) na Mohamed Said Mohamed (Baraza la Wawakilishi) na madiwani 17, walioshinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni. Pinda alisema kuachwa kimya bila kujibiwa kwa baadhi ya kauli zinazotolewa na viongozi wa upinzani kunawafanya wananchi kuamini yanayozungumzwa na kwamba, hakuna sababu ya kukaa kimya, huku baadhi ya viongozi hao wakiendelea kusambaza maneno ya kubeza na ya uongo dhidi ya CCM.
"Ninyi mmekuwa kimya mno, kila mtu akibeza mnakaa kimya, hapana mkipata mwanya mjibu ili wananchi wajue ukweli," alisema Pinda na kuongeza, uongo ukirudiwa mara kwa mara, huku CCM ikikaa kimya wananchi wataamini uongo huo ni ukweli. Kwa upande wa serikali, alisema itaendelea kujibu tuhuma ambazo zitaelekezwa kwake kutoka kwa viongozi hao kwa kadri hali ilivyo.
Aliwataka wana -CCM kujitahidi kadri ya uwezo wao kutetea amani na utulivu uliopo nchini, ili usije ukatoweka na kwamba, wasiruhusu viashiria vyovyote vya uvunjivu wa amani vikapata nafasi, kwani amani ikitoweka wananchi watailaumu CCM. "Chonde chonde wana -CCM, nawaomba tutetee na kung'ang'ania kwa nguvu zote hali ya amani na utulivu iliyopo, kwani iwapo amani na utulivu vitaondoka Watanzania watakuja kutulaumu," alisema.
Kwa mujibu wa Pinda, kuna baadhi ya wanasiasa wanataka kufika wanakotaka kwa kutumia vurugu, jambo ambalo linahatarisha amani.
UPOTOSHAJI UCHAGUZI IGUNGA
Awali, akimkaribisha waziri mkuu, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati, alieleza kusikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari vinavyopotosha umma kuhusu gharama zilizotumiwa na CCM katika uchaguzi mdogo wa Igunga.
Chiligati alisema si kweli kwamba CCM ilitumia zaidi ya sh. bilioni tatu, kwani fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya kampeni zilikuwa chini ya sh. milioni 400.
Alisema habari kuwa CCM inakufa kutokana na mgawanyiko uliopo ndani ya Chama si za kweli, kwani matatizo ya mtu mmoja si ya Chama.
Chiligati alisema yeyote atakayekuwa na matatizo katika Chama atashughulikiwa na kama atatoka, CCM itaendelea kuwepo na
kamwe haitakufa.
"Hata kama Chiligati ametoka CCM, bado itaendelea kuwepo na ipo imara, kamwe hakuna mtu atakayeweza kukiharibu Chama," alisema.
MWIGULU ALIA NA WATENDAJI
Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, amewataka watendaji wakuu wa serikali kufuatilia hujuma zinazofanywa na baadhi ya watendaji na watumishi wa umma dhidi ya CCM.
Alisema baadhi ya hujuma hizo ni za makusudi, kwani serikali ya CCM imepanga majukumu yake kutokana na Ilani ya uchaguzi. Alisema hujuma hizo zinawafanya wanachama na wananchi kwa jumla kutokuwa na imani na CCM.
Nchemba alisema hujuma hizo zinafanywa katika miradi, ambayo mingine haitekelezwi kama ilivyopangwa, licha ya fedha kutolewa. Alisema ufuatiliaji ufanywe kwa makini ili asiwepo wa kuonewa.
"Tumepata malalamiko mengi katika sehemu mbalimbali kuhusu huduma, lakini ukifuatilia huoni tatizo bali ni mtumishi mmoja ameamua kwa ridhaa yake kuwanyanyasa wananchi, hili hatulikubali," alisema.
Alisema kamati za siasa za ngazi zote ni vyema zikafuatilia utekelezaji wa miradi ya serikali, kwani wao ndio wenye Ilani ya uchaguzi.
Katika hatua nyingine, Nchemba alisema CCM ina mpango wa kumpeleka nchini India, kijana Mussa Tesha, aliyemwagiwa tindikali wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga.
Alisema hatua hiyo inatokana na Tesha kuendelea kupata maumivu usoni na jicho moja kutoona.
"Pia tunaangalia uwezekano wa kumuanzishia biashara ili aweze kujikimu, kwani ni yatima na ndiye mkubwa katika familia yao," alisema.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Pinda alisema atalifikisha wazo hilo kwa Kamati ya Wabunge wa CCM na kwamba, Tesha hana sababu ya kujiona mnyonge, kwani Chama kipo kwa ajili ya kumsaidia.

Pinda!
Hao magamba wajibu mapigo yapi? kuwa hakuna ufisadi au mapigo yapi Pinda? kwa magamba hakuna cha kujibu kwani wanafaham kuwa wantuibia na wanakumbatia ufisadi na hivyo hawawezi kujibu maana wanachoambiwa ni ukweli mtupu.
 
kama waziri mkuu alitakiwa kuaw neutral. ccm kuna matatizo, tena mengi hata nchemba kasema. kujibu mapigo ni utoto, hoja hapa, nikushughulikia kero za watanzania na ustawi wa maisha ya watanzania na si kujibu mapigo, watanzania wamechoka ngojera
 
Back
Top Bottom