Mhagama Awataka Viongozi Kuwapatia Wenyeviti wa Mashina ya CCM Taarifa Muhimu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama ametoa wito viongozi kuhakikisha wanawapatia wenyeviti wa Mashina wa Chama cha Mapinduzi taarifa muhimu za utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ili waweze kuzielezea vyema kwa Wananchi.​

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo Wakati wa ziara yake ya kutembelea Wenyeviti wa Mashina Katika Kata ya Magagula;Mbingamwalule, Kizuka, Liganga, na Litisha zilizopo Jimbo la Peramiho lilopo katika Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

Ameongeza kusema kwamba siasa za sasa zinalenga katika kujenga hoja hivyo ni muhimu wenyeviti wa Mashina kuwa na maelezo muhimu yatakayosaidia kukielezea Chama vyema kwa wananchi.

"Utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM inategemea Mafiga Matatu kwa maana ya Rais, Mbunge na Diwani Jambo ambalo linarahisisha katika utekelezaji wa shughuli za serikali na heshima hiyo mnatupatia nyie wenyeviti wa Mashina," alisema.

Aliongezea kuwa Wenyeviti mwendelee kuwa na uelewa mzuri wa miradi inayotekelezwa na Serikali kwani itasaidia kusemea Chama, na Rais ikiwa ni sambamba na kusaidia kusukuma Gurudumu la maendeleo pamoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Thomas Masolwa amesema ziara ya Mhagama kutembelea Wenyeviti Mashina inasaidia kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Ameongeza kusema kuelekea uchaguzi ujao ni vyema Wenyeviti wa Mashina wakajua kwamba Uchaguzi ni hesabu za namba, ukiwa na namba nyingi lazima utakuwa umemshinda mpinzani wako.

" Ni vyema tuhamasishe wananchi waende kukipiga Kura Chama Cha Mapinduzi, tutengeneze wapiga Kura kwa kuhakikisha wanasajiliwa ili watambulike na Chama," alisema.

WhatsApp Image 2024-02-28 at 08.10.14 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-02-28 at 08.10.14.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-28 at 08.10.15 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-02-28 at 08.10.15.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom