JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,022
Guys, smell the coffee. Wacheni kutumia jazba au kuwadharau wazanzibari. Kuwa ni nchi ndogo haimaanishi munaweza kuwaburuza munavo taka nyinyi. Wazanzibari wametaka referendum kuhusu muungano na nyinyi mumeng'ang'ania tu, hamutaki kuwapa nafasi kujiamulia. Munafurahi s.sudan walipopata uhuru wao hata Mkapa alikuwepo huko lakini likija sualla ka zanaibar, muanatafuta kila sababu ya kuwakandamiza.
Nimeoma hoja zenu ukumbini na ni wazi kabisa munazungumza kupitia mioyo yenu na sio akili zenu. Tanzania ni nchi ya kusadikika, haipo ni ndoto tu.
Falconer,
..madai ya Referendum yana taratibu zake.
..kwa kuanzia madai hayo yanapaswa kupelekwa mbele ya bunge la muungano.
..Mh.Jussa aliteuliwa na Raisi Kikwete kuwa mbunge mwaka 2009. Sikupata kumsikia akizungumza lugha anazozungumza sasa hivi wakati alipokuwa na nafasi hiyo.
..lakini fuatilia msimamo wa Wabunge wa ZNZ[CUF + CCM] wakati wa mjadala wa sheria ya kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Wabunge toka Zanzibar kwa ushabiki wao, huku wakimtukana matusi makubwa-makubwa Mh.Tundu Lissu, wamepitisha sheria ambayo inaweka vikwazo kwa mjadala wa kina kuhusu muungano wetu wakati wa mchakato wa katiba mpya.
..mwisho, CUF wamewasilisha rasimu ya katiba ya Jamhuri ya muungano ambayo inapendekeza serikali 3 ambako kutakuwa na Raisi mmoja wa muungano, na serikali za Tanganyika na Zanzibar zitaongozwa na magavana!! Sisi wengine tunaona kwamba wanasiasa wa Zanzibar wanaongea kwa "ndimi mbili."
NB:
..kama kweli Wazanzibari wako serious basi waanze na kugomea masuala yote ya muungano. Washinikizeni viongozi wenu wasusie shughuli za muungano na kuachia madaraka yao ktk serikali ya muungano.