LE GAGNANT
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 1,241
- 251
Kwenye huu muungano wa kulazimisha, mengi tu yatashuhudiwa. Kisicho halali hakiliki, nyie mwalazimisha, mtatapika tu.
Barubaru,
Mjadala unaendelea, Nilishafafanua kama waafrika haswa kuanzia mashariki ya kati mpaka kusini wote ni wamoja. Kabla ya
wazungu kuweka mipaka na kuchora ramani ya kwanza ya Afrika na kujigawia makoloni. waafrika wa sehemu hizo
tajwa walikuwa wanaishi popote pale wanapotaka na wanapoona panawafaa. Sasa basi mpango huo wa kuanza kuzitenga
jamii barani Afrika , uliitwa "Berlin Conference" na ulifanyika kuanzia November, 1884 mpaka February 1885. katika mji wa
Berlin, Ujerumani. Nyuma ya hapo kulikuwa hamna mipaka. Ukiangalia Tanganyika baada ya michoro ya kuigawa Afrika
tayari ilishawafungia watu kwa kutokuweza kwenda wanapotaka kuhamia au kurudi kule walipotoka.
Makabila mengi ya Tanganyika yamekuja kutoka Kaskazini, Kusini na magharibi. Tuchulie mfano Wapare, Wamasai wametokea
" ABYSSINIA "yaani ETHIOPIA. Wangoni wametokea AFRIKA YA KUSINI . Wabembe, Wamanyema hao wametokea KONGO.
huo ni mfano mchache tu, na hayo makabila yote yalikuwa na sababu za kuhamia sehemu nyingine, aidha malisho ya mifugo,
aidha ardhi ya kulima, aidha kuvua samaki, aidha kushindwa vita na kukimbia na kuhamia sehemu nyingine.
Aina hiyo ya maisha ilikwama na kuwa mwanzo wa civilization kwa waafrika Waarabu wahindi waliokutwa katika sehemu husika.
Na ukazidi kuwa mgumu kwa watu kwenda na kuhamia sehemu nyingine,baadaya kuchorwa ramani ingine ya kiugawanya Afrika, ramani iliitwa " Political colonial africa, " 1916.
Turudi katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar. yaani " THE ARTICLES OF UNION BETWEEN TANGANYIKA AND ZANZIBAR "
ndio wenye matatizo madudu mengi ndani yake. kutokana na wakati wanatakiwa wakae mezani tena na ufanyiwe marekebisho.
kwa mapungufu na yote yanayohitajika muhimu yaingie humo, kwa sababu ulaghai upo. Baada ya hapo Articles mpya ya
muungano, yaani Union agreement inatakiwa ifanyiwe registrering katika secretariat ya UN, Legal Councel.
Na hapo Muungano ndio utakuwa umekamilika, Basi ikiwa kutakuwa na mwelekeo kutokuelewana kati ya nchi hizo mbili
mmoja wapo akipeleka mashtaka umoja wa mataifa, registered treaties to invoked. Kazi sasa imebakia kwa Watanganyika
na Wazanzibar kuuweka sawa Muungano, ilo ndio Darsa.
Tibaijuka uko sawa profesa wangu, ungekuwa hauko sawa basi ungeenda UN kuomba msumbiji na kenya ziongezewe eneo. Muungano haufai, watanganyika hatuutaki, na wazanzibari ndo kabisa hawautaki. Muungano umebaki kwa wana ccm na wacuf tu
​Zanzibar wanataka nini? uhuru wao au umbea?
Nitarudie tena kwa mara ya mwisho kama hutanielewa nitakufuata huko "nikuzabe vibao" maana kuna wanafunzi hawaezi kuelewa ila kwa viboko!
Sio kila jambo inaloamua SMT au SMZ lazima lipitie kwenye bunge la JMT au BLW. Vivyo hivyo wakati hili jambo EEZ linajadiliwa na kufikishwa UN halikupelekwa kwenye bunge la JMT au BLW (ni makosa ya katiba yetu mbovu).
Lakini hilo haliondoi ukweli kwamba Zanzibar haikushirikishwa. Hili jambo liliamulia kwenye baraza la mawaziri la SMT ambalo kuna wajumbe kutoka ZNZ nao VP Dr. Bilal, Dr. Shein (waziri asiye na wizara maalumu), Shamsi Vuai Nahodha (mambo ya ndani), Hussein Mwinyi (Ulinzi), Samia Hassan Suluhu (Muungano), Omari Nundu (Mawasiliano/Uchukuzi) etc.
Balozi Seif Idd kutojua kama kiongozi wa BLW, haina maana kwamba SMZ ilikuwa haifahamu. Ndiyo maana kwenye ule ujumbe ulio kwende UN kupeleka ombi walikuwepo wajumbe kutoka BLW, SMZ. Je, hawa wote walitoroka makazini kuapata ruhusa?! TAFAKARI
Tatizo kubwa la viongozi wa ZNZ wanapokuwa na wa wenzao wa muungano wanaongea lugha tofauti, wanapokwenda huko ZNZ wanaongea lugha nyingine, hii haikuanza leo tangia wakati wa Abood Jumbe Mwinyi na kitabu chake THE PARTNERSHIP. Matokeo yake Nyerere akamuweka kizuizuni Kigamboni.
This is the root causes ya maatizo yenu Wazanzibari, bila kuwa take into task viongozi wenu mtabaki kuwalalamikia Watangayika milele. Mfano mwingine ni sheria ya mabadiliko ya katiba mpya wabunge wenu (CCM na CUF) walivyoshadadia hiyo sheria inayominya uhuru wa kutoa maoni kwenye mambo yanahohusu muungano.
Mtajibaraguza huko kwenye masikani ya kahawa na kashata lakini we know finally mtafyata mkia na eno litaongezwa. Mark my words.
Tukiendelea kung'ang'ania huu muungano wa serikali mbili, matatizo hayatakwisha hata siku moja. Imefika wakati tuangalie moja kati ya options zifuatazo:-
1. Tuwe na serikali 3, ya Zanzibar, ya Tanganyika na ya Muungano.
2. Tuwe na serikali moja tu ya Muungano ili Wazanzibar nao wakubali kuipoteza serikali yao kama ilivyofanya Tanganyika
3. Tuuvunje Muungano ili kila nchi iangalie mambo yake yenyewe, Tanganyika ipate uhuru wake kwa mara nyingine na zanzibar pia iachane na "mkoloni" Tanzania.
Vinginevyo tuking'ang'ania sera za ccm za muundo wa serikali mbili, tujiandae kwa matatizo makubwa zaidi siku za mbeleni.