JF ladies mnaweza?

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Ni kwamba wanawake wa Rwanda na Burundi ambao waume zao ni madereva wa malori ya masafa marefu, wamebuni utaratibu mpya. Wakijua wazi waume zao wako katika mazingira hatarishi kupata VVU, kabla ya waume zao kuanza safari, huwafungia shehena ya kutosha ya condoms.

Wanajua wazi huko waendako wanalala na wanawake lukuki. Siku mume akirudi nyumbani, may be baada ya wiki 2, 3 au hata mwezi na nusu, mwanamke akigundua zile condoms zimetumika, hufurahi sana, kwani anajua mumewe anajilinda.

Vp akina dada wa JF, mumeo anaenda safari ya muda mrefu.

Je waweza mfungia shehena ya 'zana' ndani ya begi lake la safari?

source, BBCswahili
 
Siwezi hata kidogo, sitakua na amani hata kidogo maana nitahisi ana do ovyo hivyo hata mapenzi kwake yatapungua. Yataka moyo....
 
Haiwezekani kuhalalisha uzinzi kwa kiasi hicho, akishindwa kuvumilia atanunua mwenyewe hukohuko sio mie nimbebeshe
 
Ishu ya condoms
sio watu hawapendi kutumia

ishu ni kuwa baada ya pombe watu husahau

huku condoms zipo mifukoni mwao.....

Ishu ni pombe
 
Ni vigumu ila inahitaji moyo kwani wanaume wanaoendesha malori wengi wao sio waaminifu kwa ndoa zao na anaweza akakaa safarini hata miezi miwili na kuendelea na sio wanaume wa rwanda tu au burundi hata watanzania wapo wanaoenda drc.
Kweli akina mama tuna kazi kwa sisi tunaofanya kazi za barabani unaweza usiolewe kabisa na wanume wa aina hiyo make percent yao ni wadhindhi na wanavituo vyao wanavyosimama ukisikia majina wanavyoviita utashangaa na huwezi kuwa na imani na mwanaume anayelala pale mfano kuna sehemu moja inaitwa Runzewe wao wanaiita shamba la nyenge.Naomba mniwie radhi kwa kutumua maneno makali namna hiyo.
 
Ukimfungashia mwanaume kondom, tafsiri yake ni kuwa huyo si mumeo tena...basi!
Hapo kati yenu hakuna mapenzi!...nikuishi kwa mazowea tu na kusukuma siku.
 
Ni kwamba wanawake wa rwanda na burundi ambao waume zao ni madereva wa malori ya masafa marefu,wamebuni utaratibu mpya.Wakijua wazi waume zao wako katika mazingira hatarishi kupata VVU,kabla ya waume zao kuanza safari,huwafungia shehena ya kutosha ya condoms.Wanajua wazi huko waendako wanalala na wanawake lukuki.Siku mume akirudi nyumbani,may be baada ya wiki 2,3 au hata mwezi na nusu,mwanamke akigundua zile condoms zimetumika,hufurahi sana,kwani anajua mumewe anajilinda.Vp akina dada wa JF,mumeo anaenda safari ya muda mrefu,je waweza mfungia shehena ya 'zana' ndani ya begi lake la safari?(source,BBCswahili)
<br />
<br />
Ushauri wangu:kama akizipunguza baadhi na kurudi nazo pungufu,si still ataonekana kazitumia?nadhan ni vizur wakashaur wanaume zao wawe waaminif kuliko kuwapa silaha ambazo hata akitumia au asipotumia huwez kua na uhakika kama alituia silaha izo kupambana na Adui.
 
Mimi kama mwanaume,mambo mengine kama mtu unajua thamani yako na ya mkeo,pamoja na utu wako na namna unavyomjua Mungu huwezi kufanya ujinga huo,huyo mkeo atakuwa na thamani gani kwako?Umemuoa wa nini?Na pia utakua na tofauti gani na mbuzi?
 
You know what? Because truck drivers wanajua kwua wakirudi nyumbani wake zao wanafurahi kuona condoms zimetumika kuna uwezekano mkubwa kabisa wa hao truchers kuzitupa njiani ili kuwafurahisha wake zao!

By the way, marriage life is about making your partner happy!
 
Ishu sio kumfungashia condom ishu ni je atazitumia?mm siwezi kufanya upumbavu huo wa kuvunja nyumba yangu kwa mikono yangu mwenyewe je na mm nikiwa ni mfanya biahsara nasafiri safiri na mm atanifungashia CARE?
 
Ishu sio kumfungashia condom ishu ni je atazitumia?mm siwezi kufanya upumbavu huo wa kuvunja nyumba yangu kwa mikono yangu mwenyewe je na mm nikiwa ni mfanya biahsara nasafiri safiri na mm atanifungashia CARE?
wao si wamejihalalishia kama vile ni halali na sie ni haramu
 
Watu wanakuwa nazo kwenye wallet lakini zinashindikana kutoka sembuse kwenye begi!!!Kuvaa kondomu ni wito na wala siyo kipaji!!
 
Ishu ya condoms
sio watu hawapendi kutumia

ishu ni kuwa baada ya pombe watu husahau

huku condoms zipo mifukoni mwao.....

Ishu ni pombe

kitafunio cha chai ni mkate,andaz ,chapati and other type of bite's WHILE KITAFUNIO cha bia ni mwanamke..
 
Vishindo vya ndani ya ndoa noma,vinahitaji 'shock absorber',ndo maana wanandoa ni victims wakubwa wa VVU!
 
Back
Top Bottom