Kipimo cha UKIMWI kinavyotumika kama mbadala wa Kondomu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
hiv-oral-test.jpg

Hofu ya uwezekano wa ongezeko la maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kwa miaka ijayo inazidi kutanda mitaani kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya vipimo vya haraka (HIV Rapid test) vya kubaini maambukizi hayo kwa kupima damu.

Uchunguzi uliofanywa kwa zaidi ya wiki mbili katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam limebaini uuzwaji holela wa vipimo hivyo huku wengine wakivitumia kama mbadala wa kondomu kwa vijana na kinadada wanaojihusisha na ukahaba.

Desemba 2019, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema Bunge limerasimisha sheria ya wananchi kujipima wenyewe VVU huku akiweka angalizo kuwa, kujipima mwenyewe si majibu ya mwisho, hivyo kuwataka wananchi kuwa, baada ya kujipima wanatakiwa kwenda katika vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya kuthibitisha na ushauri zaidi wa jinsi ya kuishi.

Ummy hakupatikana alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, lakini Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Abel Makubi alipoulizwa alisema suala hilo ni la kitaalamu lipelekwe kwa mganga mkuu wa Serikali.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu alipotafutwa na Mwananchi naye alielekeza suala hilo lijibiwe na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP).

Meneja wa programu wa NACP, Dk Anneth Rwebembera alisema kuuzwa holela kwenye maduka ya dawa kwa vipimo hivyo “ni kinyume na utaratibu na hakiruhusiwi.”

“Ni kweli. Siyo utaratibu bidhaa hizo kuuzwa Pharmacy (maduka ya dawa) na tunashukuru kwa ushirikiano wa taarifa hiyo kwa jamii. Tunafuatilia ili tupate taarifa kamili kutoka maduka ya dawa hayo,” alijibu kwa njia ya ujumbe mfupi na kumuunganisha mwandishi na mfamasia mkuu wa Serikali.

Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi alisema kuuzwa kwa bidhaa hizo kwenye maduka binafsi ni kukiuka sheria na anayejihusisha na biashara hiyo anapaswa kuchukuliwa hatua.

Msasi alisema watalifuatilia suala hilo kwa makini ili wajue bidhaa hizo zinatokea wapi na maduka ya dawa yanayoziuza.

Hali ilivyo

John Mnanja (si jina halisi), mkazi wa Mwenge mpakani ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu jijini hapa, anasema kabla ya kujamiiana na mwanamke lazima ampime kwanza kwa kipimo hicho ili aepuke kutumia kondomu.

“Mimi navinunua kwa ajili ya kumpima mwenzi wangu kabla ya kujamiiana, binafsi siwezi kutumia kondomu,” alisema.

“Baada ya kumpima damu akiwa mzima nitakwenda naye. Bahati nzuri kwa niliowapima wote, wanafika sita, sijawahi kukutana na mtu mwenye maambukizi ya Ukimwi,” aliongeza.

Mkazi mwingine wa Dar es Salaam anayeishi Segerea, Tabata anasema aliwahi kulazimika kuachana na mwenzi wake kutokana na kukataa kupimwa Ukimwi kwa kipimo hicho cha haraka.

“Alinilazimisha kunipima Ukimwi kabla ya kujamiiana. Nilimkatalia na nilimwambia hana fani ya utabibu na hawezi kunipima Ukimwi kwa kuwa hawezi kunipa ushauri nasaha ikitokea nimekutwa na maambukizi,” alisimulia binti huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Lakini kwa upande wake Mwanamkasi Shabani mkazi wa Mbezi Beach anasema yeye amewahi kupimwa virusi hivyo na mpenzi wake kwa ajili ya kumridhisha na kulinda mahusiano yao yasiishe.

“Yule mwanaume vipimo alikuwa navyo ndani, kuna siku nimeenda nyumbani kwake akaniambia anataka tupime Ukimwi, niliingiwa na wasiwasi wakati akinitoa damuna nilijiuliza ananionaje mpaka atake kunipima?” anasema.

Mwanamkasi anasema alijiuliza swali lingine kama ikitokea ana VVU usiri wa matokeo hayo utakuwaje?

Hata hivyo, anasema alikubali shingo upande ili mwenza wake asimfikirie vibaya na wasigombane.

Zimekuwepo taarifa kuwa hata baadhi ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono hutembea na vipimo hivyo.

Yanayojiri mitaani

Katika kufuatilia zaidi taarifa hizo, mwandishi alifunga safari hadi kwenye maeneo ambayo dada poa hufanya biashara zao za ngono.

Katika maeneo, pamoja na wengineo, mwandishi alikutana na mmoja wa makahaba hao ambaye licha ya kumpa gharama za huduma yake, alidokeza suala la kutaka kumpima kwanza kujua kama ana virusi hivyo.

Uchunguzi uliofanyika na gazeti hili ulibaini dada poa huyo pamoja na wengine, hununua vipimo vya Ukimwi kwenye maduka ya dawa na kutembea navyo kwa ajili ya kuwapima wateja ambao hawataki kutumia kondomu, kwa masharti ya kuongeza bei ya huduma hiyo.

Wasemacho madaktari

Kuhusu watu kutumia vipimo hivi vya Ukimwi kama mbadala wa kondomu, Dk Juma Fea wa Zahanati ya Mbagala Kizuiani, alisema mtu akijipima na papo hapo kushiriki ngomo bado yupo hatarini kuambukizwa kwa sababu maambukizi ambayo mhusika ameyapata karibuni hayaonekani kwenye kipimo hiki.

“Kiitaalamu kuna kitu kinaitwa ‘window period’, ni kipindi toka mtu anapopata maambukizi hadi kinga mwili (antibodies) zinapozalishwa kwa ajili ya kupambana na maambukizi, kwa hiyo mtu akiwa katika kipindi hicho akipima majibu yanakuwa negative (yasnaonyesha hana virusi) hata kama anayo,” alisema.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Dk Zainabu Hussein, daktari katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi aliyesema mara nyingi VVU havionekani ndani ya wiki mbili tangu mtu apate maambukizi, hivyo kuna hatari ya kuambukizwa endapo mtu unayempima na kujamiiana naye wakati kapata maambukizi hayo ndani ya muda mfupi.

“Njia hii (ya vipimo vya haraka kabla ya kujamiiana) ni hatarishi na inaweza kusababisha maambukizi yaongezeke huko mbeleni,” alisisitiza Dk Zainabu.

Upatikanaji wa vipimo

Katika maeneo ambayo gazeti hili lilibaini vipimo hivyo vinauzwa holela ni maduka ya dawa, mojawapo likiwa katika eneo za Mabibo likiwa limeambatana na maabara.

Katika duka hilo, muuzaji alimtaka mwandishi azunguke nyuma ya maabara wanakoviuza.

Alipofika huko, baada ya kuhojiwa kidogo na kupewa ya matumizi, mwandishi alitakiwa alipe Sh5,000 kwa kipimo kinachotumia damu.

“Utaweza kupima? Una buffer solution? (kemikali inayowekwa kwenye kipimo kwa ajili ya kusoma matokeo). Hakikisha unasoma kipimo ndani ya dakika 20 na zisizidi hizo,” alisisitiza mhudumu.

“(ukishaweka damu) ikitokea mistari miwili hapo ni positive (una VVU) na ukitokea mstari mmoja ni negative (hauna VVU),” alielekeza.

Baada ya kumfungia kipimo kwenye bahasha, mwandishi aliomba risiti, jambo ambalo halikukubaliwa ikielezwa kuwa vipimo hivyo vinatolewa kwa siri.

“Hapana kwa vipimo hivi hatutoagi risiti maana haviruhusiwi kuuzwa,” aliongeza mhudumu huyo.

Katika eneo la Magomeni Mapipa, kwenye duka la dawa ambalo lilikuwa na dawa chache na baadhi ya makabati yakiwa wazi, mwandishi alipoviulizia aliambiwa “hapa vimeisha wiki iliyopita, mtu anayenileteaga amesema ataleta Jumatatu.”

Safari haikuishia hapo, katika duka jingine lililopo Tegeta Kibaoni, mwandishi aliambiwa asubiri vikafuatwe stoo na mhudumu aliingia chumba kingine na kurudi nacho kwenye kiufungashio. Muuzaji alimtaka mwandishi awe makini anavyotoka hapo ili watu wasijue amebeba nini.

“Kaka kuwa makini na hicho kipimo, tunauza kwa magendo sana,” alisisitiza.

Kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja ya wauzaji wa dawa alisema vipimo hivyo husambazwa na mtu ambaye hakumtaja kwenye maduka ya dawa na wanaovihitaji humpigia simu.

“Kuna mtu anayesambaza bidhaa hizi, huzunguka karibia Dar nzima, sijui kama naye ana duka,” alisema.

Hata hivyo, katika hilo, Dk Zainabu alisema vipimo hivyo vinaweza kuwepo kwenye maduka ya jumla kwa matumizi ya hospitali au zahanati lakini si kwa mtu mmoja mmoja.

“Kuna aina mbili za vipimo vya haraka, kuna kile cha mdomo (Oral Self-test) na cha kutoa damu (bioline), kwa sasa kitaalamu tunashauri watu kujipima kwa kutumia kipimo cha mdomo kwa sababu hakihusishi kutoa damu, suala ambalao linakuhitaji kutumia utaalamu kidogo,” alisema.

Makosa ya vipimo

Wakati matumizi ya vipimo hivyo yakiongezeka, Dk Zainabu anasema bado kuna kasoro zinazoweza kutokea endapo mtu atajipima mwenyewe bila maelekezo.

“Mtu ambaye hana utaalamu akijipima kwa kutumia vipimo hivi anaweza kukosea kusoma majibu, lakini pia anaweza kukosea jinsi ya kuweka damu kwenye kipimo na pia kunaweza kuwa na makosa katika kachanganya damu na kitendanishi (buffer solution),” alisema.

Dk Johnson Lyimo, ofisa anayeshughulikia programu ya kifua kikuu na Ukimwi Tanzania kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), alisema majibu wanayoyapata watu baada ya kujipima hayatakiwi kuwa ya mwisho, bali wanatakiwa kurudi hospitali kuthibitisha.

“HIV self-test ni mkakati muhimu kuyafikia makundi ambayo hayafikiki kirahisi lakini msisitizo mkubwa tunaoutoa kwamba unavyoyapata yale majibu usiridhike, si ya mwisho lazima uende kituoni ukahakikishe,” alisema.

Dk Lyimo alisema wanashauri waliojipima kurudi hospitali kwa ajili ya kujiridhisha na kuweka takwimu za maambukizi sawa.

“Lengo kubwa ya kufanya hivyo ni kuongeza uimara na uhakika wa Takwimu za Ukimwi na kwa sasa sisi WHO na Serikali tunaunda Community unified Solution, mfumo unaoimarisha Takwimu kwenye ngazi ya jamii na kituoni,”alisema

Vinatoka wapi?

Etty Kusiluka, ofisa mahusiano na mawasiliano katika Bohari ya Dawa (MSD) baada ya kuulizwa aliomba atumiwe picha ya mfano wa vipimo hivyo na aweze kubaini kama vinatoka kwenye bohari hiyo.

“Tumeiangalia hiyo bidhaa, batch number (namba ya mzigo) yake tumegundua si ya kwetu. Sisi hatujapokea mzigo huo, kikawaida huyo supplier (msambazaji) yupo ni Mtanzania. Msambazaji sio kwamba anatengeneza bidhaa zote kwa ajili ya MSD, anaweza pia kutengeneza kwa ajili ya wateja wake wengine,” alisema.

“Utaratibu wa MSD kupeleka bidhaa nchini upo na bidhaa zote tunazipeleka kwa mgao uliochanganuliwa na Wizara ya Afya,” aliongeza.

Kujipima bila ushauri

Naima Omary ambaye ni mwanasaikolojia wa kujitegemea alisema kujipima magonjwa nyeti yanayohitaji ushauri nasaha kunaweza kusababisha matatizo ya kisaikolojia na afya ya akili.

“Ikitokea mtu amejipima mwenyewe bila kupata ushauri nasaha na akaonekana ana maambukizi hali ile inaweza kumsababisha hisia zinazoumiza (trauma). Hiyo trauma inaweza kumsababisha mtu kujiua au kutumia dawa za kulevya,” alisema.

Takwimu Za UKIMWI

Sakata hili linaibuka ikiwa ni siku chache zipite tangu Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) iseme maambukizi mapya ya Virusi vya UKIWMI (VVU) yamepungua nchini kutoka watu 110,000 mwaka 2016/17 hadi 54,000 mwaka 2020/2021, sawa na pungufu ya asilimia 50.9.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk Leonard Maboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Novemba 15 mwaka huu kuelekea kilele cha Siku ya Ukimwi Duniani alisema theluthi ya maambukizi yanatokea, inapatikana kwa vijana.

Alisema Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri katika kupunguza maambukizi mapya na kuwa sasa asilimia 89.7 wanajua hali zao ikilinganishwa na asilimia 61 mwaka 2016 /2017.

MWANANCHI
 
Ukijipima ukikutwa unao nicheki nikupe dawa yaasili ya kuondoa virus
 
[mention]denicy [/mention] sitaki kukupoteza tajiri yangu njoo uchukue elimu uku
 
Back
Top Bottom